Uwezekano wa Vita Vikuu vya Tatu (WW III) vya Dunia ni mdogo sana

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,273
47,497
Pamoja na purukushani zinazoendelea sehemu mbalimbali za dunia za kuchokozana, kuvamiana na kubutuana siku za hivi karibuni uwezekano wa kutokea vita vikuu vya tatu vya dunia bado ni mdogo sana.

Kwanza tukumbuke katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambavyo chanzo chake kilikuwa ni ulaya mataifa mengi yaliswagwa tu kama mifugo kuingia katika hivyo vita yakiwa kama makoloni. Kwa sasa mataifa yote ya dunia ni huru kuamua yenyewe.

Pili, mengi ya mataifa ukiacha machache kama Urusi, USA, Israel, Iran, Pakistan na Korea Kaskazini hayapendi sana vita na nchi nyingine na hayajakaa kishari.

Tatu, kutokana na maendeleo makubwa ya utandawazi (globalisation) itakuwa ni vigumu sana kwa mataifa mengi kuchagua upande. Leo hii India inayotegemea gesi kutoka Urusi, mafuta kutoka uarubuni na mtaji kutoka magharibi itachagua upande gani? China inayotegemea soko la magharibi na nishati ya Urusi itachagua upande gani?

Madhara yanayotegemwa, vita vya kwanza na vita vya pili vya dunia vilitumia silaha nzito lakini ukilinganisha na sasa ubora na wingi wa hizo silaha ni kama mbingu na ardhi. Hata hao waliokaa kivita na kishari wanaelewa ukubwa wa madhara yatakayotekea kipindi hiki vita vikiwa vikubwa vya mataifa mengi, wao wenyewe wanaparuana lakini kuna mstari wanachora wanajitahidi wasivuke kusababisha wengine kuwehuka na kujitoa mhanga bila kujali.

Haya ni baadhi ya mambo tu yanayofanya uwezekano wa kutokwa vita vya tatu vikubwa vya dunia kuwa finyu sana.
 
Kwa jinsi Marekani anavyo jaribu kulinda 'hegemony' yake na kukataa ushindani wa kibiashara, kiuchumi na kijeshi ni Kama anawabananisha kwenye kona washindani wake kuwalazimisha waingie vitani.
 
Pamoja na purukushani zinazoendelea sehemu mbalimbali za dunia za kuchokozana, kuvamiana na kubutuana siku za hivi karibuni uwezekano wa kutokea vita vikuu vya tatu vya dunia bado ni mdogo sana.

Kwanza tukumbuke katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambavyo chanzo chake kilikuwa ni ulaya mataifa mengi yaliswagwa tu kama mifugo kuingia katika hivyo vita yakiwa kama makoloni. Kwa sasa mataifa yote ya dunia ni huru kuamua yenyewe.

Pili, mengi ya mataifa ukiacha machache kama Urusi, USA, Israel, Iran, Pakistan na Korea Kaskazini hayapendi sana vita na nchi nyingine na hayajakaa kishari.

Tatu, kutokana na maendeleo makubwa ya utandawazi (globalisation) itakuwa ni vigumu sana kwa mataifa mengi kuchagua upande. Leo hii India inayotegemea gesi kutoka Urusi, mafuta kutoka uarubuni na mtaji kutoka magharibi itachagua upande gani? China inayotegemea soko la magharibi na nishati ya Urusi itachagua upande gani?

Madhara yanayotegemwa, vita vya kwanza na vita vya pili vya dunia vilitumia silaha nzito lakini ukilinganisha na sasa ubora na wingi wa hizo silaha ni kama mbingu na ardhi. Hata hao waliokaa kivita na kishari wanaelewa ukubwa wa madhara yatakayotekea kipindi hiki vita vikiwa vikubwa vya mataifa mengi, wao wenyewe wanaparuana lakini kuna mstari wanachora wanajitahidi wasivuke kusababisha wengine kuwehuka na kujitoa mhanga bila kujali.

Haya ni baadhi ya mambo tu yanayofanya uwezekano wa kutokwa vita vya tatu vikubwa vya dunia kuwa finyu sana.
Mkuu vita kuu ya tatu inaweza tokea bila kutegemea ingawa tofauti na ya kwanza na ya pili, hii ya tatu inaaminika itakuwa ndio mwisho wa human civilization, kumbuka ya kwanza ni Marekani pekee alikuwa na Nuclear, ila leo hii zaidi ya nchi 10 wana nuclear war head.
 
Albert Einstein is often quoted as having said: "I know not with what weapons World War III will be fought, but World War IV will be fought with sticks and stones".
 
Mkuu vita kuu ya tatu inaweza tokea bila kutegemea ingawa tofauti na ya kwanza na ya pili, hii ya tatu inaaminika itakuwa ndio mwisho wa human civilization, kumbuka ya kwanza ni Marekani pekee alikuwa na Nuclear, ila leo hii zaidi ya nchi 10 wana nuclear war head.
Zitaje tuone.
 
Pamoja na purukushani zinazoendelea sehemu mbalimbali za dunia za kuchokozana, kuvamiana na kubutuana siku za hivi karibuni uwezekano wa kutokea vita vikuu vya tatu vya dunia bado ni mdogo sana.

Kwanza tukumbuke katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambavyo chanzo chake kilikuwa ni ulaya mataifa mengi yaliswagwa tu kama mifugo kuingia katika hivyo vita yakiwa kama makoloni. Kwa sasa mataifa yote ya dunia ni huru kuamua yenyewe.

Pili, mengi ya mataifa ukiacha machache kama Urusi, USA, Israel, Iran, Pakistan na Korea Kaskazini hayapendi sana vita na nchi nyingine na hayajakaa kishari.

Tatu, kutokana na maendeleo makubwa ya utandawazi (globalisation) itakuwa ni vigumu sana kwa mataifa mengi kuchagua upande. Leo hii India inayotegemea gesi kutoka Urusi, mafuta kutoka uarubuni na mtaji kutoka magharibi itachagua upande gani? China inayotegemea soko la magharibi na nishati ya Urusi itachagua upande gani?

Madhara yanayotegemwa, vita vya kwanza na vita vya pili vya dunia vilitumia silaha nzito lakini ukilinganisha na sasa ubora na wingi wa hizo silaha ni kama mbingu na ardhi. Hata hao waliokaa kivita na kishari wanaelewa ukubwa wa madhara yatakayotekea kipindi hiki vita vikiwa vikubwa vya mataifa mengi, wao wenyewe wanaparuana lakini kuna mstari wanachora wanajitahidi wasivuke kusababisha wengine kuwehuka na kujitoa mhanga bila kujali.

Haya ni baadhi ya mambo tu yanayofanya uwezekano wa kutokwa vita vya tatu vikubwa vya dunia kuwa finyu sana.
Mungu atuepushe!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom