Decemba mwaka 2015 nilikuwa miongoni mwa waandishi takribani saba kutoka vyombo mbalimbali nchini tulikwenda kutembelea baadhi ya sehemu za kibiashara katika Jimbo la Guangzhou Nchini China. Tulikwenda kwa hisani ya Ubalozi wa China nchini Tanzania.
Ziara yetu ilituchukua siku kumi tukiwa katika Jimbo hilo, ambalo kwa wakati huo tuliambiwa lilikuwa lina idadi ya wakazi milioni 107, idadi mbayo ilikuwa ni kubwa karibia ya mara mbili ya wakazi wa Tanzania kwa wakati huo.
Tukiwa na wenzangu tuliweza kutembelea sehemu mbali mbali za viwanda na sehemu za biashara. Tulifika pia kwenye kampuni ya kutengeneza simu ya Huawei, tulipofika hapa tulitarajia walau kupata simu moja moja lakini tulitoka kapa! Wachina bahili sana!
Tulipotembelea Bandari kubwa ya Shenzhen tuliona utalaamu mkubwa katika kupakia na kupakua mizigo kwa haraka sana. Ni wakati huo huo kulikuwa na tetesi kuwa shirika lao la Taifa -The State-run China Merchants Holdings International (CMHI) lilikuwa lije kuwekeza katika Bandari ya Bagamoyo.
Tulipokuwa hapo niliwauliza swali chokonozi, kuwa “Nasikia mnakuja kuwekeza katika Bandari yetu ya Bagamoyo, mbona hamuji?”
Mmoja wa maafisa wao katika Bandari hiyo ambaye ndiye alikuwa msemaji akanijibu kuwa “Sisi kila kitu tunacho na fedha tayari imetengwa lakini sisi tunacho subilia ni Serikali yenu kusema, tumekubali njooni muendelee na uwekezaji.”
Baada ya kuona utalaamu na ujuzi katika Bandari hiyo nilivutiwa sana nao na nikatamani hawa jamaa waje kuwekeza hapa kwetu.
Kwa ujumla ‘frankly speaking’ wale jamaa wana maendeleo makubwa sana. Kwa mujibu wa maelezo yao wamewezafika hatua hiyo baada ya wananchi na hasa viongozi waliopewa dhamana ya uongozi kutoweka maslahi binafsi mbele, badala yake wakatanguliza maslahi ya taifa [nation interests] mbele. Wamefika mbali sana kimaendeleo.
Kwanini nilibadilisha gia angani juu ya wao kuto pewa ujenzi na umiliki wa Badari ya Bagamoyo?
Wazanaki, wa zamani waliwahi sema kuwa “Ukitaka kujua njia ulizia wanao rudi.”
Na kama jinsi Wasukuma wasemavyo “Nguzo inayoshikiria nyumba huwa haipengewi makamasi,” nami pia niliamini maneno aliyosema aliyekuwa Mkuu wangu wa Nchi na Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli [Pumzika kwa amani], wakati akiongea na jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania Jijini Dar es Salaam nakunukuliwa na vyombo mbali mbali nchini, alisema makubaliano yaliyokuwa yanaendelea kati ya Serikali ya Tanzania na China juu ya ujenzi wa Bagamoyo yalikuwa ya hovyo sana!!
Nionavyo, Urais, ni Taasisi yenye vyanzo [reliable sources/impeccable sources] zenye uhakika]. Wengine wamezoea kusema serikali ina mkono mrefu! Na huo ndiyo ukweli.
Nionavyo, beyond doubt Rais hawezi kukurupuka na kudai wawekezaji wanakuja na masharti ya ajabu. Akasema “Ni kichaa tu ndiye atayakubali masharti hayo.”
Rais Magufuli aliyataja masharti hayo ni pamoja na: Wawekezaji walisema wakisha wekeza pale, sis kama nchi haturuhusiwi kuendeleza bandari yoyote toka Tanga hadi Mtwara Kusini. “You are not allowed to construct any port.”
Masharti mengine: TRA hawataruhisiwa kwenda pale kukusanya kodi! Walitaka wapewe guarantee ya miaka 33 bila kuwa uliza uliza; waliomba wapewe land lease ya miaka 99 tofauti na sheria za nchini kwetu.
Na kwamba hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kwenda kumuuliza mtu yeyote atakaye wekeza pale. Walitaka wapewe mandate ya kuchukua hiyo ardhi iwe kama ardhi yao!!!
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, ili kuhakikisha jambo hili lina materialise, kulikuwa na watu wanazunguka huku na huku kufanya lobbying [personal interests].
Rais alisisitiza “Najaribu kuzungumza haya ili sasa watanzania wajue kuwa, tumechezewa mno miaka mingi. “We are supposed to change.”
Nionavyo, kwa maneno haya ya mkuu wa nchi, pamoja na kwamba leo hatunaye ametangulia mbele ya haki, hatupaswi kuyatupilia mbali, tuyafanyie kazi. Kama wasemavyo wadau mabli mbali, wameiomba serikali ya sasa ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, isikurupuke kuwapatia Wachina kujenga hiyo Bandari.
Ni kweli kwamba fedha [financial muscles wanayo] lakini haya masharti yao hayafai kabisa na ni mwiba kwa vizazi vyetu vijavyo.
Tusiingia mikataba hii kwa mashinikizo na kuhongwa fedha lukuki, lakini tukumbuke kesho sisi hatutakuwepo lakini tutakuwa tumewaweka watoto, wajukuu na vitukuu wetu katika utumwa wa Wachina!!! Hawa jamaa ni wengi sana wanatafuta ardhi kwa nguvu na kwa gharama yoyote!
Huu ni wakati ambao Serikali yetu inapaswa kuamka na kuwapatia wawekezaji wazawa wa ndani [Private sector] kuwekeza katika Bandari hii ya Bagamoyo, hata kama watashirikiana na wawekezaji wengine kutoka nje ya nchi lakini wao ndiyo wanapaswa kuwa na umiliki mkubwa.
Ni ukweli usiopingika, sisi kama nchi tunahitaji wawekezaji katika nyanja mbali mbali lakini hatutaki wawekezaji watakao tumia nguvu na fedha zao kama super power [China], kuingia mikataba ya kinyonyaji na kikandamizaji. Lazima iwe ni mikataba ambayo ni win-win.
Wazee wetu wa zamani walizoea kusema asiye sikia la mkuu huvunjika guu.
Rais wetu Hayati Magufuli aliliona hili kwa kupitia vyombo vyake mbali mbali, kwa maslahi mapana ya nchi na kwa kutanguliza uzalendo mbele na wala siyo personal gain/interests, aliamua kuliweka wazi. Kwamba tulikuwa tunaingizwa mkenge.
Kama jinsi Serikali ilivyo amua kuwakaribisha sekta binafsi wazawa kuwekeza kwenye Mabasi ya Mwendo kasi, haina budi kufanya vinyo hivyo kuwakaribisha wawekezaji wazawa na wazalendo kuwekeza katika Bandari ya Bagamoyo.