Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,491
- 7,027
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatangaza kuufunga uwanja wa Benjamin Mkapa kwa muda kuanzia leo tarehe 9 Aprili 2025 ili kupisha marekebisho ya eneo la kuchezea (Pitch) lililopata athari kubwa kufuatia mvua zilizonyesha na kufuatiwa na mchezo wa Robo Fainali wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba SC na Al Masry ya Misri.
Timu ya Wataalamu itaanza mara moja kufanya tathmini ya kina ya madhara yaliyojitokeza na tarehe ya kufunguliwa kwa uwanja huo itatangazwa hapo baadaye.
Kufuatia uamuzi huu, timu zote ambazo zilipanga kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa zikiwemo zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa zinaombwa kutafuta uwanja mbadala wakati Serikali ikifanya marekebisho ya eneo la kuchezea kwa dharura.
Wizara inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na kufungwa kwa uwanja huu kwa sasa.