mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
Asante kwa elimu mkuu.
Ndio uwezekani wa kufanya ivyo upo tena mkubwa, ikiwa haujafata masharti tajwa pale juuMkuu ikitokea wakafanya ivo kwenye computer yangu nikaamua kubadilisha window na nikaweka window mpya. Je nitaweza kufanya ivo, again after doing so i will be safe?
Jana usiku nimetoa taadhari kwenye moja ya taasisi za umma juu ya Global Cyberattack - Uvamiszi wa kutisha wa udukuzi wa mifumo ya kompyuta - uliotokea jana nikiwataka wachukue hatua za haraka kujilinda. Hata hivyo nimeona niweke maelezo na ushauri wangu kwenye public maana jambo hili ni utishio kubwa kwa usalama wa taifa na hadi ninapoandika ujumbe huu udukuzi huu unaendelea kusumbua mifumo ya computer duniani kote nanimepata taarifa waathirika toka Tanzania. Kwa kifupi huu ni udukuzi wa kimtandao ambao umeathiri nchi takribani 100 duniani kwa siku ya jana tu. Nchi zenye wataalamu wa hali ya juu, mifumo ya kisasa, na uwezo mkubwa wa ulinzi na udukuzi wa mitandao kama Uingereza, Urusi, Ujerumani, na Ukrain wameathiriwa sana. Kama hawa wamedhurika ni wazi kwamba sisi tuko kwenye hatari kubwa na tunalazimika kuchukua hatua za haraka kama nchi na kama mtu mmoja mmoja.
View attachment 508699
Pamoja na kwamba hakuna taarifa nyingi kutoka Tanzania na Afrika kwa ujumla juu ya uvamizi huu, ukweli ni kwamba nchi za kiafrika zimeshavamiwa.asubuhi ya leo nimeshatapa taarifa za watu walikumbwa na kadhia hii nchini. Mfumo huu mpya wa udukuzi unaendeshwa na majangili wenye utalaamu mkubwa wa mitandao na wamejificha nyuma ya pazia la chuma lisilopenyeka kirahisi.
Udukuzi wa kimtandao (Cyberattack)
Udukuzi wa mifumo ya computer uliozoeeleka kama hacking ni kitendo cha wavamizi kuingilia mifumo ya computers hufanya mojawapo ya haya:
Hata hivyo udukuzi huu ulioivamia dunia jana ni wa ujambazi wa aina yake kwani wahusika pamoja na malengo mengine ambayo wanaweza kuwa nayo, kikubwa wanchotaka ni fedha. Wanapoivamia computer yako wanaitawala wao kwa kufunga programme na mafaili yote (encrypting your computer). Unapojaribu kuifungua unapata ujumbe wa kitendo walichokifanya ambacho hukupa maelezo kwamba njia pekee ya kuirudisha computer yako katika hali ya kawaida ni kulipa kiasi cha dola 300 za kimarekani ($300) ndani ya muda maalum waliokupa. Usipolipa ndani ya muda huo, dau linaongezeka au wanafuta mafaili yote kwenye computer yako.
- Kuiba taarifa toka kwenye mifumo kwa malengo ya kwenda kuzitumia kudanganya, kuiba, kazi za kiusalama, ugaidi, nk.
- Huingilia mifumo kuratibu mawasiliano ya watu ambayo wana interest naoi li kufuatilia mienendo yao.
- Kuingilia mifumo kwa lengo la kuharibu tu kama aina ya ukorofi, ubaya, ubabe, nk.
- Kuingilia mifumo kwa lengo la kufuta ushahidi fulani.
Udukuzi wa huu Unaitwaje?
Mfumo huu wa udukuzi unaitwa Ransomware kwa sababu umelenga kushambulia mifumo kwa madhumuni ya kujipatia fedha. Njia ya kujikomboa kwa mauathirika ni kulipa fedha pekee (you get back access to your computer after paying a sum of money demanded –ransom – hence the name Ransomware). Kirusi anayefanya shambulio hili la sasa anaitwa WannaCry na uharibifu aliofanya kwa siku moja tu ya jana ni mkubwa kuliko yote ambayo imewahi kutokea. Pamoja na kukutisha kufuta maifaili yako iwapo utashindwa kulipa fedha wanayotaka, wadukuzi hawa pia wanakutisha kutumia picha na mafaili waliyoyamiliki kwenye computer yako kukuaibisha kwa maana ya kukuanika mitandaoni. Wanachukua taarifa za siri kam amafaili, picha, na video ulizonazo na kuziweka hadharani ili kukudhuru au kukudhalilisha. Hivyo wanakupa chaguo dogo sana la kulipa au vinginvyo.
View attachment 508698
Nini kimetokea?
Mamlaka ya Usalama wa Taifa ya Marekani (National Security Agency – NSA) ni taasisi yenye nguvu kubwa ya intelligence kuliko zote. Pamoja na kazi zingine, taasisi hii ina kitengo maalumu cha cybersecurity chenye wataalamu wa hali ya juu kabisa. Pamoja na kazi za kujilinda dhidi ya uvamizi wa kimtandao, kitengo huki hutengeneza tools/software za kushambulia au kujipenyeza kwenye mifumo mingine duniani kwa lengo la kutafuta taarifa, kujua watu wanafanya nini kwenye computers zao, na kuwafuatilia wale wanaowashuku kiusalama kama vile magaidi, wezi, wauza madawa, na kuingilia mifumo ya nchi maadui. Mwezi wa nne mwaka huu, mifumo ya taasisi ya NSA ilivamiwa na wadukuzi (hackers) wasiojulikana ambao waliwaibia taarifa nyingi sana ikiwa ni pamoja na software yao walioyoitengeneza kwa lengo nililolitaja hapo juu. Software hiyo inaitwa Eternal Blue na ina uwezo wa kupenyeza knye Microsoft Windows computers (Windows XP, Windows 8, Windows 10) na kumruhusu muhusika kutizama unachokifanya na taarifa zako. Kwa kifupi, software hii inafungua mlango wa nyumba na vyumbai na kuiacha wazi kwa aliyefungua kufanya atakacho.
Majambazi hao wa kimtandao ambao hawajajulikana bado, walipoipata software hii inasemekana walioiweka Eternal Blue kwenye website moja iliyofichika tarehe 4 mwezi wan ne. baada ya kufanya hivyo, kundi linguine la kijambazi wa kimtandao wakaipata na wakaanza kuitumia kupenyeza kwenye computers za watu duniani kote walizokua (huend ana yako wameiingilia). Baada ya wao kuiona wana uwezo wa kuingilia computer za watu bila wao kujua, wakatengeneza kirusi aitwaye WannaCry ambaye ndiye anayefanya kazi ya kuiteka nyara computer yako. Hivyo Eternal Blue akishafungua milango ya computer yako, WannaCry anaingia na kuiratibu hivyo anafunga maifaili na programme zote usiwe na uwezo wa kufanya lolote. Njia pekee unayoachiwa ni kufuata maelekezo ya majangili hawa kwamba ni lazima ulipe ($300) ili waweke kukurudishia funguo za milango na madirisha ya nyumba yako (computer). Kwenye taasisi nyingine WannaCry amehitaji kulipwa kwa mamilioni ya dola ili arudishe access. Huu ni utekaji nyara wa kiwango cha juu sana kwani huna njia nyingine kwa vile uwezo wa kumtoa virusi mtu anakua nao tu pale ambapo computer inafanya kazi na sasa huna. Iwapo hutalipa kiwango wanachotaka kwa muda waliokupa, fedha inongezeka na wanaanza kudelete mafaili yako.
Unalipaje na kwa nini wameshindwa kufunga njia ya malipo?
Njia pekee ya kuwalipa hawa wadukuzini kupitia mfumo wa malipo wa siri ujulikanao kama BitCoin. Bitcoin ni mfumo wa malipo wa kielekroniki kama ilivyo PayPal ila mlipaji halipi gharama za huduma hiyo kwa kuwa mfumo huu unakwepa mifumo ya kiserikali inayotoza kodi. BitCoin iluitengenezwa na mtu alijitambulisha kama Satoshi Nakamoto mwaka 2008 na aliuweka mtandaoni mwaka 2009. Hata hivyo biidi zote za kumtambua Satoshi ni nani hazijafanikiwa hadi leo. Mfumo wa malipo wa BitCoin una uwezo wa kufanya mchakato wa malipo bila mifumo ya kibenki na serikali kutoza tozo (charges) hivyo hutumiwa sana na watu wanaoficha utambulisho wao kama magaidi, wauza madawa ya kulevya, na wengine wanaoendesha magenge ya kiuhalifu. Kwa kuwa mfumo huu unafanya kazi kwenye layer ya ndani/giza ya mtandao wa internet (Dar Web), imekua vigumu kuwakamata wahusika n ahata kufuatilia malipo yanayofanywa yanakwenda wapi. Hata hivyo wataalamu wanaonesha kwamba kuna uwezekano wakaanza kuweza kujua malipo yanapokwenda na hivyo kuwakamata wahusika.
Unawezaje kujilinda na udukuzi wa Ransomware?
Ushauri kwa Serikali na taasisi zake
- Moja, usifungue kabisa email yoyote ambayo humjui mwandishi ni nani wala hukua unasubiri ujumbe wa aina hiyo. Emails zinazokuja na kirusi huyu zina ushawishi mkubwa wa kukufanya uone imetoka kwenye taasisi au mtu unayemjua hivyo umakini mkubwa unatakikana haya kwa kutokudownload file lolote au kubonyeza link itakayoonekana kwenye email hiyo.
- Pili, hakikisha umefanya windows updates kwenye kompyuta yako haraka iwezekanavyo. Mifumo iliyoshambuliwa zaidi ni za computer za Microsoft windows hivyo kila anayetumia windows XP, Windows 8, Windows Vista, na Windows 10 yuko kwenye hatari hii. Hata hivyo kwa kuwa Microsoft walishajulishwa na NSA baada ya tool yao kuibiwa mwezi wa tatu, wametengenza update patches za windows ambazo zinamzuia Eternal Blue kupenyeza na hivyo kujikinga na WannaCry. Watu wote waliofanya windows updates siku za karibuni wamejikinga na udukuzi huu kwa sehemu kubwa.
- Tatu, kirusi huyu anakuja kama pop-ups kwenye browser yako hivyo usiruhusu pop-ups (don’t unblock pop-ups). Zikijika wakati una-browse zikatalie (Block them)
- Ukiona dalili ya computer yako kushambuliwa, ondoa computer yako mara moja kwenye internet ili uwe salama bila kujali chanzo cha internet unachotumia.
- Hakikisha computer yako ina antivirus imara na thabiti. Kumbuka free antivirus software wanazotumia watu wengi, hazina uwezo kabisa wa kupambana na udukuzi huu.
- Zingatia kwamba uvamizi huu sio kwa computer na mifumo ya computer tu bali unahusu vifaa vyote vinavyotumia internet ikiwa ni pamoja na simu yako ya mkononi, tablets, PDAs, nk.
- Hakikisha umefanya backup ya mafaili yako yote kwenye computer ili ukishambuliwa n ahata usipolipa bado uwe salama kwa maana ya taarifa zako.
Ninaishauri serikali hasa vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama wakiongozwa na usalama wa Taifa na TCRA wachukue hatua madhubutu na za haraka kulinda nchi yetu na uvamizi huu. Jambo hili ni la hatari sana kuliko maelezo na hasara yake ni kubwa. Vyombo husika vilipe tatizo hili status ya tishio la usalama wa taifa na tusingoje hadi tusikie mifumo ya BOT, TRA, Polisi, Usalama na mingine imeingiliwa ndio tuanze kutafutana. Nini wafanye?
Imeandikwa na Mathew Mndeme (Mwalimu MM)
- Wataalamu wa cybersecurity wa taasisi zote za serikali na mashirika ya umma wafanye kazi ya ziada kuhakikisha serveres ziko salama na ulinzi umeimarishwa
- Wataalamu wote wa ICT wa taasisi wahakikishe computers zaote kwenye ofisi na za watu bianfsi zinazotumika kwenye network zao zimefanyiwa windows updates haraka iwezekanavyo. Ninashauri serikali ichukue hatua kuwaita wataalamu wake wote wa ICT kwenda makazini kuanzia leo na kesho ili kufanya kazi hii na kusaidia mifumo kuwa salama Jumatatu watu wakiingia kazini
- Computers au mifumo ambayo sio lazima kuunganishwa kwenye internet, itolewe mara moja wakati jambo hili la kiusalama linashughuliwa
- TCRA wakishirikiana na vyombo vingine na media houses, watoe elimu kwa umma kwa haraka iwezekanavyo ili watu wachukue taadhari husika.
MM ni Mchambuzi wa mifumo ya kompyuta na Mtafuiti wa mifumo ya TEHAMA katika huduma za afra
Brua Pepe: mmmwalimu@gmail.com
Kwa taarifa za kiifundi nilizopata , hadi sasa taasisi kadhaa (tena nyeti) zimeshavamiwa na udukuzi huu. Nasisitiza ushauri wa taasisi zote kuzima internet kwenye mifumo ambayo haina ulazima wa kuwenye internet muda wote. Hi ni hatua ya muhim na ya haraka kuepuka hasara kubwa itakayojitokeza
Mkuu umeshuka vina vya hatari...swali langu ni kwamba kwa nini hawajafanikiwa China, Marekani na Israeli? au na zenyewe zimeathirika?
Pia kama kweli ni wababe kwa nini wasifanye hvyo kwa Raisi wa Marekani ili wajipatie dau nono?
Nitarudi badae! Maana sasa hivi sina mood ya kusoma maelezo marefu.
Dah! kiukweli nakushukuru sana kwa tahadhari uliyotupa, wewe ni mzalendo binafsi wala sipotezi muda naanza kufanyia kazi ushauri wako wa kitaalam.Asante!
Marekani imevamiwa pia. Ila taasisi zao hasa za umma zitakua zilichukua taadhari mapema zaidi maana NSA walipoibiwa hii tool yao waliwaambia Microsoft ... hivyo huenda taasisi zao zisiumie sana. Kwa kifupi nchi nyingi makini zimeathirika ila viwango vya athari ndio zinatofautina
Mkuu ikitokea wakafanya ivo kwenye computer yangu nikaamua kubadilisha window na nikaweka window mpya. Je nitaweza kufanya ivo, again after doing so i will be safe?
Nazidi kupokea taarifa nyingi za taasisi, makampuni, na watu binafsi waliovamiwa Tanzania. Leo watu wengi hawako makazini na wengine hawana access na Internet. Tafadhali chukua hatua kuwasiliana na unaowajua waambie wafuatile mifumo ya taasisi zao... ni janga hili na linahitaji attention inayolingana na ukubwa wake. Tusaidiane kujilinda na kuikoa nchi yetu na uvamizi huu
Hili ni swali la msingi sana na wataalamu wa security wamelijadili leo. Kwamba hawa jamaa wakishaingia kwenye computer wanaweza kubadilisha codes hivyo hakuna uhakika wa usalama sana hata baada ya kuwalipa. Ila kama ukafanikiwa kufuta windo na kuweka upya hakikisha umechukua taadhari zote ambazo nimeorodhesha kwenye hapo juu huenda ikakusaidia
Wakati mwingine watanzania baadhiyetu tuna shida ya uelewa na hatujipi muda kuelewa kabla ya kuongea. Pia tu wepesi sana kuacha issue na kumshambulia mtu. Una hakika ulichosema ndicho nilichomaanisha? Sijasema mimi ndio chanzo cha taarifa ndugu yangu bali nimesema baada ya kuona hili tatizo jana niliamua kuwasiliana na taasisi mojawapo nchini zichukue taadhari maana huenda hawakuwa wamelipa uzito unaotkakina. Wala sikusema niliowaambia walikua hawalijui. hakuna ugunduzi wowote nimeutoa hapa zaidi tu ya kuelewesha na kushauri.
Ni kweli habari hizi zimejaa mitandoani dunia nzima lakini sio kila mtanzania alikua amezipata kwa lugha na kuzielewa. Ni wewe tu unayetoa lugha hii lakini wenye walionielewa wanachukua hatua na wameanza kuokoa mifumo. Hata wewe una nafasi ya kutoa habari mitandaoni na kuitafsiri ukafaidisha wengine kama mimi nilivyofanya.
Ndio maana nimekushukuru kwa kutafasiri kuja kiswahili
Hayo mengine achana nayo na sita yafanyia editing
Usije ukawa unatumika kutuletea propaganda ili kesho mseme tunazima huduma za internet Tanzania kujiepusha kumbe ni mkakati!
Anyway, kama kweli, nashukuru kwa tahadhari
Wala sikuhitaji kufanya editing ndugu yangu. Sisi wengine kuelimisha ndio majukumu yetu bila kujali nani anajua nini hivyo lugha za dharau tumezoea kukutana nazo. Huoni kwamba kwa kuwa watu hawako maofisini au limetokea wengi wakiwa hawako maofisini ndio inatupa sababu kubwa zaidi kutoa taarifa kwa wingi iwezekanavyo? Ningejua lugha yako ningekuomba nawe utafsirikama ni kipare, kichaga, kisukuma, kimakonde, nk..ili wengi tuelewe.
I rest my case
MM
Du.. Ninatumika? Hebu jieongeze kidogo kufuatilia links hizi ili ujue wanaonituma:
1. Massive ransomware attack hits 99 countries
2. Government under pressure after NHS crippled in global cyber attack as weekend of chaos looms
3. NHS seeks to recover from global cyber-attack as security concerns resurface
4. Massive ransomware cyber-attack hits nearly 100 countries around the world
5. Russian-linked cyber gang blamed for NHS computer hack using bug stolen from US spy agency
6. NHS cyber-attack: Amber Rudd says lessons must be learnt - BBC News
Mkuu tunashukuru kwa taarifa hii muhimu sana. Naomba pia utupe ufafanuzi wa kitu hiki kinachoitwa D9.ambacho kinavuma sana hasa hapa jijini Dar kama unakifahamu. Maana watu wengi sasa hivi ndo habari na malipo yake nayo hufanyika kimtandao na nimekusoma umetaja kitu kinaitwa Bitcoin ambayo nao waliitumia kupitia bank moja hapa nchini lakini wakasitisha.
Em tupe mwanga kidogo ili kama kunawana JF wako huko wajue wako katika sehemu sahihi au lah, isijekuwa ni DESI "in second generation"
Kiasi kikubwa cha kumputa zilizo athirika ni zile zenye OS ambazo developer wameacha kutoa mainstream support (security updates n.k) kama vile windows xp, windows 8 (sio 8.1) na windows server 2003. Tujitahidi ku upgrade kwenda kwenye OS zenye usalama zaidi kama windows 8.1 na windows 10. Vile vile usipuuzie security updates kutoka kwa developer (microsoft kwa windows.. )
Aisee we jamaa leo ndo umemjua huyu mdudu baada ya kuona kwenye habari... Mbona wengine tulishakuwa attacked na tuka resolve vizuri tu toka 2014 na wala sio malware mpya huyo.
Pitia hii thread Cryptowall malware
Screenshots hizi hapa mkuu
View attachment 508735 View attachment 508736 View attachment 508737 View attachment 508738
Best of luck na usiombe ukakutana na huyu malware nashukuru ni resolve na hao jamaa in a polite way na wakanipa decryption key for free.
Halafu tatizo la hawa jamaa wakisha encrypt hawaachi key kwenye system yako bali inakua uploaded kwao na inajifuta kwenye computer yako. Ila early version ya huyo malware ilikua inaacha key na watu waliweza kurudisha files baadae wakaona isiwe tabu, wakaanza mfumo ambao hauachi key
Ishort kama wewe sio target hawa jamaa wapo fair sana.
mkuu hili ni shambulio la dunia nzima, mbona kuna uzi unaelezea toka jana, na ndio habari ya dunia kwa sasa?
Siyo lazma uwe unatumia net mkuu......
Ngoja niwasiliane na James Comey kwanza......
MKuu achana naye huyo binafsi nilikua nasikia sikia tu ila sasa umenifungua macho kiundani!
Wehu kama huyo huwa hawakosekani!
Ahsante kwa taarifa mkuu
Nimekusoma kaka. Ila kuna concept 2 hapa nilizogusia huku moja ikiwa ndio focus... moja ni Ransomware kama aina ya cyberattack... hii hiajaanza leo kama ulivyosema na wako virus wengi wanaofanya uharibifu wa aina hii.. lakini hata hivyo hakujawa na shambulizi lenye sura ya global crisis.
Ya pili ni Shambulizi hili la kirusi Wannacry kwa kutumia huo mfumo wa Ransoware. Hii ndio issue ya discussion ila niliona ni vema nitoe background ya Ransomware maana sio kila mtu ana uelewa wa kutosha .
Asante kwa elimu mkuu.
Usalama wa Taifa wa nchi gani?
Ndio uwezekani wa kufanya ivyo upo tena mkubwa, ikiwa haujafata masharti tajwa pale juu
Maandalizi ya kuhack na kuzima JF.
Wewe jamaa huna hata mshipa wa aibu kuquote mada yote hii?!!!!!Mkuu umeshuka vina vya hatari...swali langu ni kwamba kwa nini hawajafanikiwa China, Marekani na Israeli? au na zenyewe zimeathirika?
Pia kama kweli ni wababe kwa nini wasifanye hvyo kwa Raisi wa Marekani ili wajipatie dau nono?
UMejisikia raha ulivyo quote 'habari yoteMkuu umeshuka vina vya hatari...swali langu ni kwamba kwa nini hawajafanikiwa China, Marekani na Israeli? au na zenyewe zimeathirika?
Pia kama kweli ni wababe kwa nini wasifanye hvyo kwa Raisi wa Marekani ili wajipatie dau nono?
Wanaboa sana watu wa namna hiiUsiwe unaquote uzi wote...duh!
Mkuu, unahisi malaika wanashushwa na sizonje nini?Isije kuwa Ni plan ya kutuzimia mtandao..Utaona tu Magazeti..(System Ya TCRA Yavamiwa na kirusi wenda Tanzania nzima Internet Ikazimwa kwa siku Kadhaa.ndo Ikawa Mwisho Wa kutumia mitandao ya kijamii)
Aya ngoja Tusubili tuone demand Ya redio/Magazeti/Tv Ikipanda.
Si kweli,Maandalizi ya kuhack na kuzima JF.
Wee jamaa mbona unakuwa Mpumbavu sana.... Umesha ambiwa kuwa ni tatizo la dunia nzima... Siyo kuwa litaikumba Tanzania peke yake we unaingiza ushabiki wa siasa....Isije kuwa Ni plan ya kutuzimia mtandao..Utaona tu Magazeti..(System Ya TCRA Yavamiwa na kirusi wenda Tanzania nzima Internet Ikazimwa kwa siku Kadhaa.ndo Ikawa Mwisho Wa kutumia mitandao ya kijamii)
Aya ngoja Tusubili tuone demand Ya redio/Magazeti/Tv Ikipanda.