Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Wanabodi,

Hili ni swali, Jee, huu Utumbuaji Majipu wa Rais Dr. John Pombe Magufuli: Which is which?!
A: Is He Doing The Right Thing, at The Right Time, And Doing It Right?
B: Is He Doing , The Right Thing, at the Right Time but in a Wrong Way?.
C: Is He Doing The Right Thing, at The Wrong Time, But Does It Right?,
D: Is He Doing The Wrong Thing, at The Wrong Time, And Doing It Wrong?.

Tangu rais Magufuli aanze utumbuaji, amekuwa akishangiliwa sana na watu, kuna maeneo ambayo amefanya utumbuaji sahihi, katika muda sahihi na kwa usahihi, yaani doing the right thing, at the right time and doing it right!. Kwa utumbuaji huu, rais amefanya kitu sahihi, na anastahili pongezi!.

Lakini pia kuna utumbuaji ambao amefanya kitu sahihi, katika muda sahihi lakini alivyokifanya amekifanya vibaya!. Hii ni doing the right thing, at the right time, but in a wrong way!, yaani not doing it right, lakini pia kuna utumbuaji ambao ni right thing, at the wrong time and doing it right,
lakini pia kuna utumbuaji, amefanya a wrong thing, at the wrong time, and does it wrongly, na mfano hai wa hili ni huu utumbuaji wa leo wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ewekezaji, TIC, Bibi Julliet Kairuki, kwa mujibu wa sababu zilizotolewa, huu ni utumbuaji wa wrong thing, umefanywa at the wrong time and in a wrong way!.

Kwa mliofuatilia media jana mliona Julliet ametayarisha mikutano mikubwa miwili ya uwekezaji ambayo yote inafanyika leo. Asubuhi tulikuwa na mkutano wa uwekezaji katika Tanzania na Singapore pale Kilimanjaro Hotel, na mchana huu tuko ukumbi wa JNICC kwenye mkutano wa wawekezaji kutoka Urusi, Juliet ndiye alikuwa moderator, hivyo hata kama ilikuwa ni kumtumbua, why umtumbue leo?!, kwa nini asingesubiri angalau mikutano hii ikapita ndipo akamtumbua!, utumbuaji wa aina hii ni very unfair!.

Naunga mkono juhudi za rais Magufuli katika utumbuaji wa baadhi ya majipu, anafanya kazi nzuri, lakini siungi mkono huu utumbuaji ambao sio utumbuaji sahihi, kwa muda sahihi na bado unafanyika in a wrong way!. Japo rais wetu ni binadamu na sio malaika, hivyo anaweza kufanya makosa, lakini yeye kama mkuu wa nchi, macho yetu wote yako kwake, hivyo we have very high expectations on him to be perfect, it is not only about doing the right thing at the right time, but he got to do it right!.

Nimeguswa sana na hili!. Just imagine mko kwenye international investment forum, imechelewa kuanza kwa sababu Juliet anasubiriwa kuja ku modarate, no one tells us anything, ndipo Waziri wake kaja na kusema tuendelee tuu bila yeye!, kumbe....keshatumbuliwa!, huu ni utumbuaji gani?, kulikuwa na urgency gani?!.

Kiukweli Magufuli ni noma!, ni hatari sana!. Akiendelea hivi, hatuwezi kuwa na mwisho mzuri kutoka na pile up ya negative forces zitakazoweza kutengeneza a bad 'karma', na kiukweli 'karma' ni karma tuu, haina mswalie mtume!. Nasisitiza mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!, hata mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa, japo atanyongwa ila shurti atendewe haki!, haki sio favor ni right!.

NB. Mimi nimejibainisha wazi humu kuwa mkweli daima, nitasema kweli no matter what, sasa wasio upenda ukweli, wataona kama namkosoa sana Magufuli, ninakosoa pale ninapoona kuna makosa, lakini pia huwa ninapongeza kwenye mazuri.

Hebu msikilizeni, Mtoto wa Mkulima, anasema nini kumhusu mtu huyu?.

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize
Kauli za Vitisho na Kidikiteta za Rais Magufuli "Hana Ma
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'u

Pasco.
Definitely B
 
Nnamuunga mkono sana rais wetu ni kwa kipindi kifupi amefanya kazi kubwa sana ila kwa ili la mkurungezi wa TIC ata mimi limenigusa ni ukweli hakutendewa haki Bibi Julliet Kairuki ana uwezo mkubwa sana kiutendaji.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
Anamzidi Chenge?
 
Wanabodi,

Hili ni swali, Jee, huu Utumbuaji Majipu wa Rais Dr. John Pombe Magufuli: Which is which?!
A: Is He Doing The Right Thing, at The Right Time, And Doing It Right?
B: Is He Doing , The Right Thing, at the Right Time but in a Wrong Way?.
C: Is He Doing The Right Thing, at The Wrong Time, But Does It Right?,
D: Is He Doing The Wrong Thing, at The Wrong T, e, And Doing It Wrong?.

Tangu rais Magufuli aanze utumbuaji, amekuwa akishangiliwa sana na watu, kuna maeneo ambayo amefanya utumbuaji sahihi, katika muda sahihi na kwa usahihi, yaani doing the right thing, at the right time and doing it right!. Kwa utumbuaji huu, rais amefanya kitu sahihi, na anastahili pongezi!.

Lakini pia kuna utumbuaji ambao amefanya kitu sahihi, katika muda sahihi lakini alivyokifanya amekifanya vibaya!. Hii ni doing the right thing, at the right time, but in a wrong way!, yaani not doing it right, lakini pia kuna utumbuaji ambao ni right thing, at the wrong time and doing it right,
lakini pia kuna utumbuaji, amefanya a wrong thing, at the wrong time, and does it wrongly, na mfano hai wa hili ni huu utumbuaji wa leo wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ewekezaji, TIC, Bibi Julliet Kairuki, kwa mujibu wa sababu zilizotolewa, huu ni utumbuaji wa wrong thing, umefanywa at the wrong time and in a wrong way!.

Kwa mliofuatilia media jana mliona Julliet ametayarisha mikutano mikubwa miwili ya uwekezaji ambayo yote inafanyika leo. Asubuhi tulikuwa na mkutano wa uwekezaji katika Tanzania na Singapore pale Kilimanjaro Hotel, na mchana huu tuko ukumbi wa JNICC kwenye mkutano wa wawekezaji kutoka Urusi, Juliet ndiye alikuwa moderator, hivyo hata kama ilikuwa ni kumtumbua, why umtumbue leo?!, kwa nini asingesubiri angalau mikutano hii ikapita ndipo akamtumbua!, utumbuaji wa aina hii ni very unfair!.

Naunga mkono juhudi za rais Magufuli katika utumbuaji wa baadhi ya majipu, anafanya kazi nzuri, lakini siungi mkono huu utumbuaji ambao sio utumbuaji sahihi, kwa muda sahihi na bado unafanyika in a wrong way!. Japo rais wetu ni binadamu na sio malaika, hivyo anaweza kufanya makosa, lakini yeye kama mkuu wa nchi, macho yetu wote yako kwake, hivyo we have very high expectations on him to be perfect, it is not only about doing the right thing at the right time, but he got to do it right!.

Nimeguswa sana na hili!. Just imagine mko kwenye international investment forum, imechelewa kuanza kwa sababu Juliet anasubiriwa kuja ku modarate, no one tells us anything, ndipo Waziri wake kaja na kusema tuendelee tuu bila yeye!, kumbe....keshatumbuliwa!, huu ni utumbuaji gani?, kulikuwa na urgency gani?!.

Kiukweli Magufuli ni noma!, ni hatari sana!. Akiendelea hivi, hatuwezi kuwa na mwisho mzuri kutoka na pile up ya negative forces zitakazoweza kutengeneza a bad 'karma', na kiukweli 'karma' ni karma tuu, haina mswalie mtume!. Nasisitiza mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!, hata mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa, japo atanyongwa ila shurti atendewe haki!, haki sio favor ni right!.

NB. Mimi nimejibainisha wazi humu kuwa mkweli daima, nitasema kweli no matter what, sasa wasio upenda ukweli, wataona kama namkosoa sana Magufuli, ninakosoa pale ninapoona kuna makosa, lakini pia huwa ninapongeza kwenye mazuri.

Hebu msikilizeni, Mtoto wa Mkulima, anasema nini kumhusu mtu huyu?.

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize
Kauli za Vitisho na Kidikiteta za Rais Magufuli "Hana Ma
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'u

Pasco.
kamanda tulia hivyo hicyo.. mambo haya hujayazoea! inabidi uwe mvumilivu. jipu bwanalikishaiva tu huwa halisubiriwi eti mpaka libadilike rangi sijui nini. ni kulibinya tu kwa nguvu zote liishe. lazima kuna mazingira ambayo yamefanya haya yatokee. kwa sababu maamuzi anayochukuaga nadhani huwa anashauriana na Makamu na PM kabla ya kuyatekeleza. utaratibu ni huu. inawezekana kabisa kongamano lingesubiriwa liishe inawezekana lingekuwa na negative impactbkwa taifa huwez jua. tumwachie mkuu wa nchi hayo
 
Pasco juzi ulipokuwa pale clouds tv nilipenda ulivyojibu swali uliloulizwa la ..unaionaje awamu ya tano...tv ile inatumiwa kwa propaganza za kumtukuza magufuli..ulivyojibu swali lile wale watangazaji hawakutegemea kupata jibu na maelezo yale...kwa kifupi mimi nisema wazi tu kuwa tangu siku ile ya kampeni huyu magufuli alipopita juu ya roof ya gari nilihisi tatizo..nikajua ana maamuzi ya kukurupuka sana...na leo ndo yanayotokea...iko shida mahali kwenye ubongo wake
 
Sijaisoma posting yako yote,lakini,I get the drift of it,I got the gist. Wageni wanakuja,Warusi,Wasingapora,Magufuli anatumbua majipu kuwaburudisha wageni. Kama wakati ule alipokuja Rais wa Vietnam,Magufuli strolled to the Central Bank and someone got fired. Mimi sijaona tatizo lolote. Hawa watu wote wanaofukuzwa kazi,they seem to me to be very bad people. Naona focus inakuwa kubwa katika kuokoa hela,lakini hatusikii zilivyookolewa zinakwenda wapi.
 
Pasco juzi ulipokuwa pale clouds tv nilipenda ulivyojibu swali uliloulizwa la ..unaionaje awamu ya tano...tv ile inatumiwa kwa propaganza za kumtukuza magufuli..ulivyojibu swali lile wale watangazaji hawakutegemea kupata jibu na maelezo yale...kwa kifupi mimi nisema wazi tu kuwa tangu siku ile ya kampeni huyu magufuli alipopita juu ya roof ya gari nilihisi tatizo..nikajua ana maamuzi ya kukurupuka sana...na leo ndo yanayotokea...iko shida mahali kwenye ubongo wake
Anakurupuka vipi? Huyu mtu ni scientist. Anatumia scientific method. Science ndiyo inamwezesha mtu kufahamu kwamba mbinu ninayotumia sasa,itaniwezesha kufikia malengo niliyokusudia. Bila scientific training,you will just grope in the dark. Mafisadi walikuwepo toka zamani lakini there was no scientist to remove them in scientific way.
 
Bila experiments kuna science? We all know sio experiments zote ni successful.

Madudu ni mengi mno. Kusema atakuwa makini kwa kila situation ni kujidanganya. Na kusema anajua anakokwenda ni sawa na kuweka vichwa vyetu kwenye mchanga Kama ostrich. Anachofanya hapa ni kupambana na ukweli ni kwamba hana choice. Kwa hilo wengi tunamuunga mkono, tunachotofautiana ni njia anazotumia. Kwa scientists (aka robots) black is black na white ni white, shades za grey in between hana habari nazo. Non scientists tunaongozwa na instinct (gut feeling/machale) na emotions.
 
JF imejaza makanjanja,unaweza kukuta yupo Kigoma ila anaripoti mambo ya dar kama yupo,na kuna watu hodari unaweza kufikiri wanafanya kazi ikulu....ila muda ukipita utapata ukweli.Maanake too much!...Si dhani kama angekuwa kwenye forum angechelewa kuileta hii mada.Propaganda at its best.

Mpaka wanatia kinyaa. Ujuaji mwingi...
 
Mi nnacho jua haija wahi toka mtu aka waridhisha binadam wotee, malalamiko na ukosoaji uendelee tuu ni mzuri.

Lakin pia mi nnacho msifia Rais ana malengo mema, anaweza asi tu please kila siku ila kujua kuwa rais ana ifikira nchi yake na maendeleo na kuchapa kazi ni vizuri.

Na wenye mawazo mbadala waruhusiwe, wenye kupinga waruhusiwe pia, ila nao malengo yao yawe nchi, isije kuwa hisia za kuhurumia watumbuliwaji, au kupinga tuu.

Pia uyu mama kisheria na kikatiba haja onewa kwa kuwa ni nafas ya uteuzi. Rais ana haki ya kumtoa muda wowote, infact TIC yenyewe haikuwa na jipya chini yake

Exactly
 
Haya uliyoandika unahakika nayo?..negotiations miaka mitatu?...mbona negotiations NHC,TPB hazikuchelewa?...yaani Raisi aagize ulipwe 35 M halafu bodi icheleweshe 3yrs?....nani kakuambia kachongewa?..kwa hiyo unaamini raisi kaamua kwa kuambiwa leo asubuhi?...hivi wewe unaweza kuwa na taarifa zaidi ya Raisi?.....ulishawahi kumhoji Julieth au habari za wasap?Tumia akili zako usiwe mbayuwayu.

Analeta habari za whatsapp kabisa. Wanataka Rais atoke mbele ya waandishi aeleze yoooote kuhusu huyu mama?!!! Mwacheni mama akae pembeni.
 
Unafikiri nchi itapiga hatua kwa kufukuzana daily bila Sera za kuvusha nchi ni wastage of time matatizo ya haya nchi ni ccm wala sio wafanyakazi. Wanasiasa wezi ndo wametufikisha hapa sasa hasira zinahamishiwa kwa workers

My sister...ccm in watu na Watu ndo hao wanaokataa mishahara "midogo" Halafu wanajilipa posho za millions. Ccm in Watu na Watu ndo haoooo......tusidanganyane..in wachache waliotegemea kuona wanayoyaona. Whether we like it or not Tz has changed and changed for good. Hela ya serikali inabidi iogopwe Kama ukoma!
 
uongozi wa haki, wafaa kwa mafundisho, na kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili watu wawe kamili, wakamilishwe wapate kutenda matendo ya haki
 
Hatuwezi kuwa Taifa la namna hii, Taifa lililojaa matukio ya kufukuzana na kusimamishana tu huku taarifa za mambo ya maendeleo zikiwa chache.
Naona imekuwa kama sehemu ya kujipatia sifa laini kutokana na mkuu kuona watu wanapenda kusikia kutumbuana kuliko kusikia bei za bidhaa muhimu kushuka.
Kweli, tulihitaji kusikia zaidi taarifa za maendeleo kuliko huku kutimuana kila leo. Inachosha.

Ova
 
Nimeshangazwa na aina ya busara ya mtoa hoja,kwa sababu,mtu ati akituhumiwa leo,unasema ngoja amalizie hii kazi ni mhimu sana hahaha,sijapata kuona,polisi anamkuta jambazi anavunja kisha anasema ngoja amalizie kuiba kwanza.Kwa ufupi kazi anayofanya JPM sasa ni mhimu na ipo kwa wakati na tuliisubiria sana tu,shime na aendelee bila kuangalia ni nani ndicho kilio cha miaka mingi kupata kiongozi mwenye uwezo wa kumeza jongoo Tanzania.
 
Back
Top Bottom