Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,339
120,854
Wanabodi,

Hili ni swali, Jee, huu Utumbuaji Majipu wa Rais Dr. John Pombe Magufuli: Which is which?!
A: Is He Doing The Right Thing, at The Right Time, And Doing It Right?
B: Is He Doing , The Right Thing, at the Right Time but in a Wrong Way?.
C: Is He Doing The Right Thing, at The Wrong Time, But Does It Right?,
D: Is He Doing The Wrong Thing, at The Wrong Time, And Doing It Wrong?.

Tangu rais Magufuli aanze utumbuaji, amekuwa akishangiliwa sana na watu, kuna maeneo ambayo amefanya utumbuaji sahihi, katika muda sahihi na kwa usahihi, yaani doing the right thing, at the right time and doing it right!. Kwa utumbuaji huu, rais amefanya kitu sahihi, na anastahili pongezi!.

Lakini pia kuna utumbuaji ambao amefanya kitu sahihi, katika muda usio sahihi na alivyokifanya amekifanya vibaya!. Hii inaitwa doing the right thing at the wrong time and doing it wrongly. Hii ni doing the right thing, at the wrong time, and doing it in a wrong way!, yaani not doing it right, lakini pia kuna utumbuaji ambao ni right thing, at the wrong time and doing it wrongly, kutasababisha karmic consequences. Pia kuna utumbuaji, rais Magufuli anakuwa amefanya a wrong thing, at the wrong time, and does it wrongly, na mfano hai wa hili ni huu utumbuaji wa leo wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ewekezaji, TIC, Bibi Julliet Kairuki, kwa mujibu wa sababu zilizotolewa, huu ni utumbuaji wa wrong thing, umefanywa at the wrong time and in a wrong way, na amini usiamini, mwisho wa siku utakuja kuwa na bad consequences!.

Kwa mliofuatilia media jana mliona Julliet ametayarisha mikutano miwili mikubwa miwili ya uwekezaji ambayo yote inafanyika leo. Asubuhi tulikuwa na mkutano wa uwekezaji kati ya Tanzania na Singapore pale Kilimanjaro Hotel, na mchana huu tuko ukumbi wa JNICC kwenye mkutano wa wawekezaji kutoka Urusi, Juliet ndiye alikuwa moderator, hivyo hata kama ilikuwa ni kumtumbua, why umtumbue leo?!, kwa nini asingesubiri angalau mikutano hii ikapita ndipo akamtumbua!, utumbuaji wa aina hii ni very unfair!. Sisi wanaume tukifanyiwa kitu unfair tunaweza kujikaza kisabuni tusilie kama Wilson Kabwe alivyofanyiwa siku ile ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni, but we all knows what happened, and it was not right. Lakini kwa wanawake, it's not that way, wanawake wakikosewa hulia machozi. Siku zote chozi la mwanamke lina consequences.

Naunga mkono juhudi zote za rais Magufuli katika utumbuaji wa baadhi ya majipu, anafanya kazi nzuri, lakini siungi mkono huu utumbuaji ambao sio utumbuaji sahihi, kwa muda sahihi na bado unafanyika in a wrong way!. Japo rais wetu ni binadamu na sio malaika, hivyo anaweza kufanya makosa bila yeye kujijua kuwa anachofanya ni makos. Walio mzunguka wanajua he is not doing the right thing lakini wanamuogopa, hawamwambii ukweli, lakini yeye kama mkuu wa nchi, macho yetu wote yako kwake, hivyo we have very high expectations on him to be perfect, it is not only about doing the right thing at the right time, but he got to do it right!.

Nimeguswa sana na hili!. Just imagine mko kwenye international investment forum, imechelewa kuanza kwa sababu Juliet anasubiriwa kuja ku modarate, no one tells us anything, ndipo Waziri wake kaja na kusema tuendelee tuu bila yeye!, kumbe....keshatumbuliwa!, huu ni utumbuaji gani?, kulikuwa na urgency gani?!.

Kiukweli Magufuli ni noma!, hii ni hatari sana kwa huko tuendako!. Akiendelea hivi, hatuwezi kuwa na mwisho mzuri kutokana na pile up ya negative forces zitakazoweza kutengeneza a bad 'karma', na kiukweli 'karma' ni karma tuu, haina mswalie mtume!. Nasisitiza mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!, hata mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa, japo atanyongwa ila shurti atendewe haki!, haki sio favor ni right!.

NB. Mimi nimejibainisha wazi humu kuwa mkweli daima, nitasema kweli no matter what, sasa wasio upenda ukweli, wataona kama namkosoa sana rais Magufuli, ukwe ni kuwa lengo la ukosoaji huu ni kumsaidia rais Magufuli pale ninapoona kuna makosa ambayo rais wetu anayafanya yatakayo kuja kumsabishia bad karma, na kwa vile sio watu wote wanajua karma ni nini na inafanyaje kazi, ukosoaji huu ni kusaidia kumuokoa rais wetu na consequences za karma.

Hebu msikilizeni, Mtoto wa Mkulima, anasema nini kumhusu mtu huyu?.

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize
Kauli za Vitisho na Kidikiteta za Rais Magufuli "Hana Ma
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'u

Paskali.
 
Magufuri alipoanza kutumbua hukujua ww majipu ni yepi Na yako wapi na hujui atamaliza kuyatumbua lini , sasa sisi kujifanya tunajua kutathmini kazi anayofanya ni uswahili mtupu , mwacheni Rais akatumbue yy ndo mwenye nyenzo kibao za kujua jipu liko wapi na atalitumbuaje,
 
Pasco mbona utenguzi umefanyika tokea tar.24.4.2016 kwa mujibu wa PS!...nafikiri kuna tatizo moja kubwa la ujuaji kwa watu wengi,na kila anayeripoti anasema alikuwa na Kairuki...Naweka akiba ya maneno kesho lazima ifike.

Unaweza kuta Raisi alikwisha saini hiyo 24/4/2016 watu wakawa wanasubiri amalize kumobilize huu Mkusanyiko anao uzungumzia Pasco!
 
Najiuliza Kitu kimoja!
JK akiwa South Afrika kamuona Mtanzania mwenye potential ya kutusaidia kuvuta Investments

Kamshawishi mama kurudi nyumbani

Mama kaacha Milioni 35 , akakubali kusettle just for 18

Badala ya Kumpa 18 wao wakalazimisha apewe 5 per month

Mama akaona This is Unfairly treated ila akawa na Subira ya kusubiri negotiations na mamlaka

Ili isije ikahesabika kuwa karidhia huo mshahara wa milioni 5 akaacha kuchukua pending majadiliano

Ninavyoona, wachoma jungu wakampikia jungu eti hataki kuchukua mshahara

Mama Katumbuliwa huku akiinadi nchi yake.

Halafu eti kwenye barua ya tangazo la kumuachisha ikaandikwa eti kama yupo tayari kufanya kazi na serikali atapangiwa kazi nyingine. Jamani kazi gani tena mtampa wakati mmeshamtilia mashaka?
 
Unaweza kuta Raisi alikwisha saini hiyo 24/4/2016 watu wakawa wanasubiri amalize kumobilize huu Mkusanyiko anao uzungumzia Pasco!
JF imejaza makanjanja,unaweza kukuta yupo Kigoma ila anaripoti mambo ya dar kama yupo,na kuna watu hodari unaweza kufikiri wanafanya kazi ikulu....ila muda ukipita utapata ukweli.Maanake too much!...Si dhani kama angekuwa kwenye forum angechelewa kuileta hii mada.Propaganda at its best.
 
Najiuliza Kitu kimoja!
JK akiwa South Afrika kamuona Mtanzania mwenye potential ya kutusaidia kuvuta Investments

Kamshawishi mama kurudi nyumbani

Mama kaacha Milioni 35 , akakubali kusettle just for 18

Badala ya Kumpa 18 wao wakalazimisha apewe 5 per month

Mama akaona This is Unfairly treated ila akawa na Subira ya kusubiri negotiations na mamlaka

Ili isije ikahesabika kuwa karidhia huo mshahara wa milioni 5 akaacha kuchukua pending majadiliano

Ninavyoona, wachoma jungu wakampikia jungu eti hataki kuchukua mshahara

Mama Katumbuliwa huku akiinadi nchi yake.

Halafu eti kwenye barua ya tangazo la kumuachisha ikaandikwa eti kama yupo tayari kufanya kazi na serikali atapangiwa kazi nyingine. Jamani kazi gani tena mtampa wakati mmeshamtilia mashaka?
Tuelezane ukweli , uteuzi wake tangu mwanzo ulikuwa zaidi ya ujuzi kwa aliyemteua , taasisi siyo MTU mmoja , haya mambo ya teuzi za kishikaji hayana nafasi kwa serikali ya Magufuri. Utatumbuliwa hats ukiwa unaendesha kikao ukumbini
 
Najiuliza Kitu kimoja!
JK akiwa South Afrika kamuona Mtanzania mwenye potential ya kutusaidia kuvuta Investments

Kamshawishi mama kurudi nyumbani

Mama kaacha Milioni 35 , akakubali kusettle just for 18

Badala ya Kumpa 18 wao wakalazimisha apewe 5 per month

Mama akaona This is Unfairly treated ila akawa na Subira ya kusubiri negotiations na mamlaka

Ili isije ikahesabika kuwa karidhia huo mshahara wa milioni 5 akaacha kuchukua pending majadiliano

Ninavyoona, wachoma jungu wakampikia jungu eti hataki kuchukua mshahara

Mama Katumbuliwa huku akiinadi nchi yake.

Halafu eti kwenye barua ya tangazo la kumuachisha ikaandikwa eti kama yupo tayari kufanya kazi na serikali atapangiwa kazi nyingine. Jamani kazi gani tena mtampa wakati mmeshamtilia mashaka?
Haya uliyoandika unahakika nayo?..negotiations miaka mitatu?...mbona negotiations NHC,TPB hazikuchelewa?...yaani Raisi aagize ulipwe 35 M halafu bodi icheleweshe 3yrs?....nani kakuambia kachongewa?..kwa hiyo unaamini raisi kaamua kwa kuambiwa leo asubuhi?...hivi wewe unaweza kuwa na taarifa zaidi ya Raisi?.....ulishawahi kumhoji Julieth au habari za wasap?Tumia akili zako usiwe mbayuwayu.
 
Magu naunga utumbuaji ila kumtumbua MTU anayeongoza mkutano wa kimataifa siku hyo hyo bana sio fair naye aisee hata kama ni makosa mama ukute alizirai huko yani ni mbaya Mpaka basi.
Makongamano Na maforum mmefanya kibao wakati wa JK mmeleta tija hipi ? Wacha kwanza Magufuri asawazishe uwanja alafu haya maforum yatakuja kibao , huwa hayaishi hayo ndugu zangu hata ukienda marekani bado wanatafuta wawekezaji, uwekezaji ni kazi ya kudumu
 
1461851358215.jpg
 
Kuna jambo huwa sikuelewi #pasco,hivi kuna ulazima gani wa wewe kila uzi wa kusifia au kuponda utendaji wa JPM kuweka link za nyuzi za nyuma?Kama hoja yako ina mashiko,wasiwasi na kujihami kwa nini?
Unasababisha uzi kuwa mrefu kusoma bila sababu ya msingi!
Pili,uzi wako ungeandika kwa kiswahili tupu usingeeleweka?Sasa unaandika kiingereza halafu unatafsiri kiswahili,hii inaleta kero flani kwa msomaji.
 
Hii nchi inahitaji katiba mpya ile ya Warioba, vinginevyo tutaendelea kubishana kila siku kama yuko sahihi au hayuko sahihi. Raisi ni binadamu, anahitaji second amendment imsaidie kufanya maamuzi. Sio kumtumbua Kairuki na kumuacha Lugumi na Charles Kitwanga na hakuna wa kuhoji
 
Back
Top Bottom