Utulivu wa watanzania baada ya pause ya vitendo vya utekaji ni meseji kubwa kwa taifa .

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,876
5,665
- Japo kuna makumi ya watanzania wenzetu walotekwa na hawajulikani walipo, wako hai au wamekufa. Na reaction Kali ya hamaki na hasira ya raia wakati vitendo husika vikiendelea, Utulivu ulipo wa watanzania baada ya vitendo husika kukoma unatoa somo kubwa;
-kwamba, watanzania ni wastaatabu, wasio na nongwa, ila hutibuliwa ili walete nongwa.
-watekaji pia wampata somo hilohilo kwani kama wangeendelea kuteka na kuua Japo walowateka hawajawaachia au wamewaua, walikua wanaenda kuondoa utulivu na amani ambayo ndo tunu kubwa inchi yetu imejaliwa.

  • pamoja na kwamba watawala ndo wamepewa ( nasisi) dhamana ya kutuongoza na kutumia vyombo vya dola. Hii inchi si Mali ya watawala na dola. Japo majority hawana kipato na nguvu ya dola, inchi hii ni Mali ya wenye inchi, watanzania.
  • Naomba kila mtu alimize majukumu yake kwa haki tuendelee kuitunza amani.
-Taifa hai litakua na wakosoaji acha wakosoe serikali ipate changakoto na kurekebisha palipo toboka.

- ukiambiwa hujafunga zipu ya suruali, humteki na kwenda kumuua alokutonya, unafunga zipu maisha yanaendelea.

Tatizo nikwamba huko kwenye dola huko kuna watu wachache conservative .wamekua brainwashed kwamba wao ndo wenye inchinna yeyote anayekosoa ni adui wao.
 
Upinzani wamerudi wametulia wako busy na uchaguzi..
Wanaharakati ndio sauti ya wananchi.

Upinzani kulalamika wanaweza lakini kuchukua hatua stahiki ni mtihani.
Waliopotea ni wanachama wao lakini wameacha kuwatafuta wanasubiri uchaguzi.

Tuna safari ndefu sana.
 
Hii ni pause tuu kusubiri kelele zipungue, halafu yule 'chinja chinja' bado ana dunda dunda bila tashwishi yoyote
Hivi ile Range Rover iliyokuwa hairuhusiwi kuegeshwa kwenye mabenki zamanigani je kuna mdau anaikumbuka ni model gani?
 
Maandamano yamezimwa, utekwaji ume-pause: Utadhani Maandamano na utekwaji vilikuwa vinaratibiwa kumoja 🤔
 
- Japo kuna makumi ya watanzania wenzetu walotekwa na hawajulikani walipo, wako hai au wamekufa. Na reaction Kali ya hamaki na hasira ya raia wakati vitendo husika vikiendelea, Utulivu ulipo wa watanzania baada ya vitendo husika kukoma unatoa somo kubwa;
-kwamba, watanzania ni wastaatabu, wasio na nongwa, ila hutibuliwa ili walete nongwa.
-watekaji pia wampata somo hilohilo kwani kama wangeendelea kuteka na kuua Japo walowateka hawajawaachia au wamewaua, walikua wanaenda kuondoa utulivu na amani ambayo ndo tunu kubwa inchi yetu imejaliwa.

  • pamoja na kwamba watawala ndo wamepewa ( nasisi) dhamana ya kutuongoza na kutumia vyombo vya dola. Hii inchi si Mali ya watawala na dola. Japo majority hawana kipato na nguvu ya dola, inchi hii ni Mali ya wenye inchi, watanzania.
  • Naomba kila mtu alimize majukumu yake kwa haki tuendelee kuitunza amani.
-Taifa hai litakua na wakosoaji acha wakosoe serikali ipate changakoto na kurekebisha palipo toboka.

- ukiambiwa hujafunga zipu ya suruali, humteki na kwenda kumuua alokutonya, unafunga zipu maisha yanaendelea.

Tatizo nikwamba huko kwenye dola huko kuna watu wachache conservative .wamekua brainwashed kwamba wao ndo wenye inchinna yeyote anayekosoa ni adui wao.
Hata hivyo ni vema Watanzania tuendelee kuwa na tahadhali kwa kupata uhakika wa wale wanaokuja kutukamata wakidai ni polisi.
Lazima kwanza tuhakikishe wamefuata taratibu zote za ukamataji.
 
Wengina tulishajiapiza kufia eneo la utekaji huku nikifa na mmoja wao Japo hii inahitaji uwe na some fighting skills. Ila kumbuka raia walianza kuzingira gari za polisi wanaotimiza Sheria maana imekua ngumu kuwatenganisha na wale wengine ( rogue killing for money)
 
Back
Top Bottom