Utubora mkulima by Shaaban Robert

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
9,100
15,989
utuboraa.png

KUACHA KAZI​

Baada ya kutoka Burma, siku moja, Utubora alisimama katika ofisi mbele ya tajiri wake kumwambia kuwa alitaka kuacha kazi. Kazi yake ilikuwa ukarani katika ofisi kubwa ya biashara ya karafuu. Mshahara wa Utubora ulikuwa simulizi karibu katika Unguja nzima; ilisemwa pia kuwa uliwatia wivu watu wengi sana. Alianza kazi kwa mshahara wa shilingi 100 kwa mwezi. Baada ya miaka mitano tu, alifikia mshahara wa shilingi 500 kwa mwezi kabla ya kwenda Burma. Aliporudi Unguja, alishika tena kazi yake kwa mshahara wa shilingi 1,000 kila mwezi. Hata katika ofisi za serikali hapakuwa na karani aliyekuwa anapata mshahara mkubwa kama huo.

Utubora alistahili sana ajira kubwa kama hiyo kwa sababu ya sifa alizokuwa nazo. Alikuwa mtu imara mbele ya telezi nyingi, kama vile hiana na mengine; mvumilivu mbele ya majaribu magumu, kama rushwa; hodari mbele ya mashaka mazito, mfano wa kushika amana au dhima kubwa; mwaminifu kama mchana; na msiri kama usiku. Kwa kushika majira alikuwa kama saa; na mahudhurio yake mema katika kazi hayakuwezekana kushindwa na watumishi wengine. Kila siku yeye alikuwa mtu wa kwanza kuhudhuria kazini, wakati wenziwe walipokuwa wamechelewa; na wa mwisho kuondoka kazini, wakati wengine walipotangulia kwenda zao. Kwa matendo haya ya sifa Utubora alikuwa kama pumzi ya maisha kwa tajiri wake ambaye alikuwa hana mtu mwingine bora wa kutegemea.

Laiti watumishi wote wangekuwa kama Utubora, ugumu katika mioyo ya matajiri ungalilainika. Tajiri ye yote mwingine angalipenda mtumishi kama alivyokuwa mtu huyu. Kazi nyingi sasa zimetokea katika maisha siku hizi; Lakini ni jambo la kusikitisha mno kwa kuwa mpaka sasa ulimwengu umewateua watu wachache tu kuwa kama Utubora. Watu wachache wenyewe kama yeye hukutani nao katika dunia katika kila hatua. Ukipishana naye mmoja, hukutani na mwingine ila labda baada ya muda mrefu sana.

Basi, tajiri mzee wa Utubora, ambaye moyoni alikuwa na nia ya kumfanya Utubora kuwa mshirika na mwongozi wa kazi yake siku moja, baada ya usemi wa Utubora, alituhumu kwa fadhaa kubwa kuwa yamkini karani wake alikuwa amerukwa na akili, akasema, “Lakini, Utubora, kwa hakika unatupa kazi iliyo njema sana. Sina haya ya kujipendekeza kwa njia yoyote; bali mimi na wewe twajua kwamba kazi hii ni bora ambayo huwezi kupata badala yake pahali po pote

Usemi huu ulipotoka kinywani mwa tajiri, sauti yake ilizuia kila onyesho la dalili ya kite. Maongezi haya yalihusu kazi tu kati ya bwana na mtumishi wake, na kama yalimchoma vingine, hilo lilikuwa shauri lake mwenyewe. Wakati ule palikuwa hapana uhusiano mkubwa baina ya watu wawili hawa zaidi ya ule wa bwana na mtumishi wake tu.

Utubora alijibu, “Najua hayo yote, Bwana Ahmed. Mimi sina nia ya kujaribu kutafuta kazi nyingine kama hii, bali kweli ni kuwa nimechoshwa sana na mji huu.”

Tajiri alisaili, “Kama naweza kunena bila ya kuwa fedhuli, tafadhali nambie wanuia kufanya nini baada ya kuondoka hapa?”

Utubora alicheka, lakini alijua kwamba tajiri wake alizoea maisha ya mjini utadhani kuwa alikuwa mwehu, kisha alijibu,

“Nakusudia kwenda Mrima nikakae shamba, Bwana. Nadhani haya ni matokeo ya vita yanayonizuia kuishi katika mji nikafanya kazi tena katika ofisi, kwa sababu najiona sina raha hapa Unguja. Nataka wasaa, hewa ya wazi, jua na makonde ya nyasi mbichi; nataka kusikiliza ndege wakiimba na ng’ombe wakiroroma. Yamkini, mimi mjinga bali hivyo ndivyo fikira yangu inavyoniongoza.” Baada ya kusema hivi, bubujiko la shauku yake mwenyewe lilimtahayarisha.

Ndipo tajiri alipozidi kusema, “Lazima niseme kuwa shauri lako la kuacha kazi halionyeshi faida, na kama laonyesha sioni aibu kuungama kuwa mimi siioni. Sauti za ndege na miroromo ya ng’ombe sivyo vitu vilivyoko Mrima tu. Kuna ngurumo za simba na mivumo ya chui vile vile ambayo hutisha pengine. Kama nilivyokuajibia wakati uliponiaga kwenda vitani, nafahamu kuwa wewe si mwoga, lakini kusema nijuavyo juu ya ghasia zilizoko Mrima, nadhani si vibaya. Nisingejaribu kuvuta akili yako kujua hali ya Mrima kabla hujaondoka hapa kama si kwa ajili ya manufaa yako mwenyewe. Tena sidhani kuwa Mrima hufaa kwa mtu aliyezoea maisha ya mji wa anasa na starehe kama Unguja. Ungechukua wakati wa kufikiri mambo haya kabla ya kufanya haraka ya kutimiza nia yako.”

Utubora alitoa kauli, “Naelewa kuwa shauri langu halionyeshi faida, na hiyo ndiyo haja yangu. Nia ya kupata faida sinayo. Nimechoshwa na kazi. Sitaki kuwa tajiri, wala fedha siijali. Ukiwa na fedha utajuta, ukiwa huna utajuta pia. Cha nini kitu kama hiki!

“Siwezi kubisha kuwa Unguja si mji wa anasa na starehe, bali kunradhi, Bwana, nikisema kuwa anasa na starehe hutosa watu pengine. Binafsi nimepata kutumbukia ndani yake. Nikijaliwa nataka kutoka sasa kabla kichwa changu kuzama vile vile katika gharika ya anasa na starehe.”

Utubora alijiona alikuwa fidhuli kidogo kwa tajiri wake mzee. Hakupenda kufidhulika kwake hata kidogo, lakini palikuwa hapana jingine la kusema isipokuwa kweli. Alishikwa na nguvu ya kweli.

Tajiri alieleza sasa, “Labda ni kweli kuwa hujali fedha, bali vitu vipatikanavyo kwa fedha vina manufaa pengine. Nasadiki pia kuwa anasa na starehe hupoteza mara kwa mara, bali kumbuka kuwa vitu hivi ni pepo ya dunia.”

Utubora alisema maneno machache, “Taibu, lakini haja zangu mimi si nyingi, kisha sina Makuu.”

Baada ya hayo palikuwa na kimya kidogo. Ahmed alikuwa anajaribu kugundua sababu iliyomshawishi mtumishi wake kuwa katika nia ile mpya. Aliwaza isije kuwa nia ile ilitokana na binti yake, Sheha, aliyechumbiwa na kijana huyu zamani! Alifahamu kuwa Sheha alitenda jambo la kuchukiza kwa sababu ya kuvunja ahadi aliyotoa mwenyewe baada ya kufikiri sana. Halafu alianza kusema tena, “Nadhani kuwa Sheha hahusiani na kusudi lako la kuacha kazi hii!”

Utubora alijibu kwa haraka, “La, nia yangu ya kuacha kazi hii haihusiani na Sheha hata kidogo, ingawa kama tungalioana nisingaliazimu kuacha kazi yangu, lakini upande huo wa maisha yangu imekwisha. Sheha aliponikataa, niliona kwanza kama dunia ilikoma kwenda, nikabaini dhahiri kuwa hapana mwanamke mwingine atayekuja katika maisha yangu, au kuwa kwangu hodari kama alivyokuwa yeye katika moyo wangu; lakini fadhaa ya vita ilinisaidia kupona: ilinifundisha kwamba yalikuwako mambo mengine ya kuangalia. Yeye alichagua mtu mwingine, basi mwisho wetu ulikuwa huo.”

Baba yake alitoa kauli kwa makini. “Nadhani kwamba Sheha alishawishika na kitu kingine kuliko yalivyokuwa mahaba yake,”

Kwa kuwa Utubora alikuwa amekwishajiingiza katika mazungumzo yale na bwana wake, moyo wake ulikuwa hauna hofu tena, kama ilivyo desturi ya mdogo kwa mkubwa wake akasema kwa kicheko, “Mimi sikutambua kama ni hivyo ulivyosema sasa.”

Ahmed alimkazia macho akanena, “Wadhani mama yako angalikubali kusudi lako kama angalikuwa mzima?”

Macho ya Utubora yalilengalenga machozi, yalifanya hivyo sikuzote kila alipofikiri habari za mama yake aliyempenda sana. Alikuwa na imani kubwa moyoni kuwa mauti yaliweza kuondoa wapenzi wa mtu machoni pake, lakini hayakuweza kuwafuta katika moyo wake. Kisha alijibu,

“Naam, kwa hakika, mama angalikubali; naona kuwa yu radhi huko aliko, hasa katika hali yangu ya sasa. Kwa kweli, laiti angalikuwa hai, nisingalifikiri habari ya kuacha kazi yangu, ingalinipasa kumsaidia na kumkimu; lakini kwa kuwa nimebaki peke yangu sasa, naweza kutenda nipendavyo bila ya lazima ya kufikiri habari za mtu ye yote mwingine.”

Ahmed ingawa aliguna, alitabasamu kidogo akasema, “Jambo unalokusudia naliona kama choyo, lakini hata hivyo, nafikiri kuwa ni kweli. Unajitawala mwenyewe, bali juu ya hayo, mimi siwezi kujizuia kufikiri kuwa utaishi mpaka siku ya kulijutia tendo lako la sasa, kama umekusudia hasa kutimiza nia uliyo nayo.”

Utubora alitikisa kichwa chake; na baadaye kidogo tajiri wake aliendelea kusema, “Tazama, kijana, mimi sitafikiri maneno usemayo leo asubuhi kuwa ndiyo ya mwisho. Nimekutana na vijana wengi waliotoka vitani wenye mawazo makubwa na ya ajabu. Sisemi kwamba vita vimewaharibu, lakini nadhani kuwa akili zao si timamu.”

Utubora alisema polepole, “Hivyo sivyo, Bwana, ila tulijifunza mambo mengi sana huko ambayo habari zake hatukuzifikiri zamani; miongoni mwa mambo hayo tulijifunza thamani za vitu vilivyo vya lazima kabisa katika maisha.”

Kwa uvumilivu mwingi Ahmed alitabasamu akanena, “Sifu jambo ulipendalo kwa sifa upendayo, lakini matokeo yake huwa mamoja sikuzote. Jambo niazimulo kutenda ni hili. Chukua mwaka mmoja wa mapumziko, katafute hayo mambo yaliyo ya lazima, na kwa muda huo wa kupumzika, nitakuwekea wazi nafasi ya kazi yako. Nasema shauri hili kwa sababu ya manufaa yangu mimi mwenyewe na yako wewe; Sijasahau pia urafiki wangu wa zamani na marehemu baba yako. Mimi na baba yako tulikuwa vijana pamoja. Sitaki uondoke katika maisha yangu. Maungano ya nikahi niliyotazamia zamani baina ya binti yangu na wewe hayakuwa. Sheha hakushinda jaribu lake kama anavyostahili mwanamke aliye bora, lakini mimi nilitazamia kustaafu na kukuacha wewe kazini kama mshiriki wangu sikuzote.”

Utubora aliingiwa na huruma kwa maneno haya akasema, “Ahsante sana, Bwana, nami sipendi kuonekana kama kwamba sioni wema wako, lakini kwa kweli sitarudi. Nina hakika kuwa sitarudi tena.” Ahmed alitamka, “Kama ni hivyo, vema! Kwa kila hali nitakupa ruhusa. Nadhani huna kusudi la kuondoka leo au kesho?”

Utubora alijibu upesi, “La, sivyo kabisa, lakini nitakuwa tayari kwenda zangu wakati wowote ambao utaweza kunipa ruhusa, Bwana.”

Ahmed aliposimama wima ili atoke afisi, saa saba ilikuwa inagonga Bet-el-Ajaibu. Motokaa yake ilikuwa inamngoja nje tayari, lakini mazungumzo yake na Utubora yalivunja kawaida yake ya sikuzote. Aliona mambo yamemkulia, akasema kwa huzuni,

“Nasikitika sana. Nadhani kuwa hutaniona kuwa mkavu wa macho nikisema kwamba mshahara wako nitauzidisha, lakini mwisho wa mwaka tutafikiri jambo hili.”

Alishikana mikono na Utubora wakaagana kwa furaha. Utubora na tajiri wake walikuwa marafiki sikuzote, na wakati Utubora alipomposa Sheha, urafiki halisi kati ya Ahmed na Utubora ulitokea.
 
Sura ya 2.

Nuru Kidogo​

Nia Utubora haikugeuka. Mrima ilikuwa inamwita. Hamu makonde ya kijani ilimtopea. Uzito wa Unguja ulikuwa mwingi kwake kuliko alioweza kuvumilia. Alasiri alipokuwa anakwenda zake kwake furaha ilimjaa tele moyoni. Alikwisha sema nia yake. Alikuwa hana wasiwasi tena. Alichukia mji pamoja na kazi yake, akawa anaona kuwa mambo yale yatakuwa karibu kama mapito yaliyopita. Alishangazwa na namna alivyoweza kuvumilia dhiki ile siku nyingi, na alivyochelewa kuvunja pingu zilizomfunga tangu wakati ule wote.

Katika njia aliyokuwa anapita aliona umati wa watu mbalimbali. Matajiri na maskini, wazima na wagonjwa, watembezi na mahamali na sura zote nyingine mbalimbali, lakini kila mtu alionekana kama alishughulika kupata kitu kilichokuwa mbali naye - mbali kabisa kama zilivyokuwa nyota mbinguni. Alifikiri moyoni mwake kwamba karibu hatawaona tena.

Alipita kando ya majengo mazuri na karibu ya eneo la makumbusho, akafahamu kuwa aliweza kutengana na fahari ile yote bila ya sikitiko. Katika akili yake ilikuwamo ramani ya Mrima, makonde ya kijani, milima mirefu, mito iliyotiririka mabondeni na barabara pana sasa.

Alishangaa, Bihaya atasema nini atapomwambia mambo aliyotenda, akabahatisha tu kuwa atafurahi. Siku za kuchukiza na kuchosha hazitakuwako tena kwa kukaa katika nyumba ndogo. Nyumba aliyokuwa anakaa Utubora ilikuwa si ndogo kweli, ila sasa ndivyo akili yake ilivyokuwa inaona. Alitazamia wakati wa kuamka asubuhi na mapema na kutazama mapambazuko ya jua, hapana kulala tena kitandani wakati wa sehemu bora ya siku ilipopita bila ya kuiangalia. Kupoteza bure wakati bora kwa kufanya hesabu za watu wengine na kuharibu afya yake kwa kutazama madaftari yasiyo na faida ye yote kwake

hakutakuwako tena. Hasa katika wakati ujao alikusudia kuwa huru, kuishi maisha yake mwenyewe katika ulimwengu wa Mungu kama babu yake Adamu alivyoishi. Basi, alikuwa na mawazo namna hii njiani mpaka akafika nyumbani kwake.

Bihaya alikuwa mtumishi wa nyumbani. Alimlea Utubora tangu alipokuwa mtoto mikononi. Ndiye mtu aliyemtunza na aliyemwuguza kwa wema mama yake Utubora. Wakati mauti yalipokuwa karibu kuchukua roho yake mbinguni, Bihaya alimfariji, akapokea salamu zake za mwisho ili kuziwakilisha kwa mwanawe mpendwa wakati wa kurudi toka vitani.

Utubora alianza maisha vizuri sana. Alikuwa mwana wa dalali mkubwa. Alikusudiwa kuhitimishwa katika vyuo vikubwa vilivyopatikana duniani. Lakini kabla ya siku zake za kuhitimu kwisha baba yake alifariki dunia ghafula, ikaonekana wakati ule kuwa alikuwa amefilisika. Mkewe na mwanawe walibaki bila ya rasilimali isipokuwa fedha kidogo tu iliyookoka katika maangamizi.

Ndipo Ahmed, tajiri wa karafuu, Unguja, alipomchukua Utubora akampa kazi katika ofisi yake, ambayo kwa ajili ya mama yake, kijana huyu alifurahi sana kuipokea, wala hapakuwa na mtu hata mmoja aliyepata kukisia mawazo yaliyokuwa yamejificha moyoni mwa kijana huyu. Ni kweli kuwa moyo wa mtu ni msitu mkubwa.

Utubora alifanya kazi kwa bidii sana hata akapendwa na tajiri wake, ambaye halafu alimjulisha kwa Sheha. Utubora na Sheha walisalitika katika mapenzi wakafunga uchumba. Kabla ya arusi kuwa, Utubora aliitika mwito wa Serikali ya Kiingereza kwa hiari yake mwenyewe, akaenda vitani. Baada ya miaka miwili tu, huku nyuma, Sheha alichagua mchumba tajiri akaolewa. Labda Sheha aliona kuwa asiyekuwako na lake haliko, lakini Utubora alipopata habari hizi alihuzunika mno. Kwa muda mrefu sana alitamani mauti yamwokoe katika huzuni hii.

Alikuwa na bunduki na singe katika mikono yake kama ilivyo desturi ya askari. Aliweza kujiua kwa risasi na shindo la bunduki likawa ndiyo buriani yake, au kwa singe kimyakimya makusudi afute aibu ya kukataliwa. Subira ya Utubora ilikuwa nyingi sana. Kwa hivi, baadaye kidogo, fikira bora ilimwingia akaona kuwa ndoa hufunga mbinguni. Kwa wazo hili, huzuni ilitoweka polepole akaona kwamba palikuwa hapana faida kwa mtu ya kujiua mwenyewe kwa sababu ya kukataliwa.

Alishukuru alipoona waziwazi kuwa mfalme huchukua raia kuwa malkia wake; na malkia huchagua raia akawa mumewe. Matajiri huoa maskini; na maskini huolewa na matajiri. Kukataliwa hutia uchungu, huzuni hata msiba moyoni, lakini kufikiri kuwa fidia yake ni kujiua mwenyewe ni upuuzi.

Wazazi wa mabinti warefu na wafupi wangaliko, na wale wa wana wanene na wembamba wangaliko pia. Hapana mwanaume mbaya kwa wanawake wote; wala mwanamke mzuri kwa wanaume wote. Ukikosa huyu, utapata yule. Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kijana huyu ya kuangalia na kupima mambo sikuzote, na kwa desturi hii aliweza kushinda taabu nyingi sana katika maisha yake kila siku.

Utubora alivuka salama vitani, na kwa kuwa alikuwa kijana bado, alitazamia kwa furaha kurejea tena katika maisha yake ya zamani. Walakini, palitokea ghafula pigo jingine la huzuni. Pigo lenyewe lilikuwa kifo cha mama yake. Sasa mkono wake wa kulia uliponyokwa na mchumba aliyemwamini, na mkono wake wa kushoto ulipotelewa na mama aliyempenda. Ilionekana kuwa hakubakiwa na jamaa tena ila Bihaya, mtumishi wake mzee. Kwa kweli, huyu alikuwa hatoshi kwa kumkaribisha mtu aliyetoka katika mashaka ya vita.

Baada ya kutolewa jeshini alishika kazi yake ya zamani, alirejea katika Ofisi ileile, aliketi juu kiti kilekile, akaandika katika madaftari yaleyale; lakini hakuwa nayo tena fikira ile ile, wala matumaini yaleyale

Siku moja alikuwa afisi ameketi pahali pa sikuzote. Dirisha lililozungukwa pande zote na majengo yaliyosongana sana lilipenyeza ndani nuru ndogo ya jua. Kuona vile alifikiri kuwa hata jua lilikuwa haling’ai vema Unguja. Fikira hii ndiyo iliyoamsha hamu ile iliyokuwa moyoni mwake ya kutaka hewa na uhuru.

Hamu iliyoamshwa na cheche ile ya nuru ya jua ilianzisha mwendo wa fikira iliyoongoza katika mabadiliko makubwa katika maisha ya Utubora. Aliona ghafula kuwa alichukia Unguja na mambo yake, kuwa hakupenda kuketi kitako katika ofisi kutwa, na kuwa hakujali fedha aliyokuwa anapata kwa malipo ya mshahara. Alijiona kuwa kama mfungwa pale. Tokea wakati ule alijiona hawezi kuvumilia tena, na tokea pale, gurudumu la fikira yake likawa linazunguka namna hii.

Hushangaza pengine kuwa kitu kidogo huwezaje kufanya na kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya mtu! Walakini, hivi ndivyo dunia ilivyo sikuzote. Kwa mfano, ufunguo mdogo hufungua kufuli kubwa; na mlango mkubwa komeo lake ni dogo. Kadhalika, ubongo wa wakia chache katika kichwa cha mwanadamu ni kitabu cha kurasa zilizohifadhi fikira zisizo na mwisho.
 
Sura ya 3
Bihaya​

Utubora hakutazamia mgogoro wowote kwa mtumishi wake wa nyumbani juu ya shauri lake, ila alikuwa na matumaini kuwa mara likifika katika masikio yake litakubaliwa bila ya majadiliano, Walakini, majadiliano yasiyotazamiwa yalizuka jioni aliposema ghafula, “Keti kitako, Bihaya, nataka kusema nawe.”

Bihaya aliyekuwa amesimama aliuliza kwa mshangao, “Una habari gani kubwa mno, Bwana?”

Utubora alisema, “Siwezi kukwambia mpaka uketi kitako. Habari niliyo nayo kubwa sana kwa kuisimulia mara moja.”

Bihaya alipoketi kitako kitini, Utubora alitamka, “Ungependaje kwenda kukaa Mrima! Nadhani kuwa huko kutakuwa bora kuliko Unguja,” Bihaya aliitikia. “Naam, bara ni bora tena ku wazi zaidi, Je, wafikiri kwenda kupumzika huko?”

Utubora alisema, “Naam, nataka kwenda kupumzika. Kazi nimeiacha, yaani, kazi yangu ya ukarani hapa unguja, nasi tutakwenda Mrima, mimi na wewe, tukakae kama Adam alivyoishi, kwa kazi ya mikono na jasho la vipaji vyetu wenyewe.”

Bihaya alikuwa hana uhakika kama Utubora alikuwa anafanya mzaha au anasema kweli, akahoji, “Lakini Adamu hakufanya kazi hiyo vema, kisha alitoka jasho alipotolewa Aden kwa kufukuzwa.”

Utubora alinena, “Labda nami nitafukuzwa vilevile, bali sifikiri kuwa nitashindwa kufanya wajibu wangu. Nitajaribu niwezavyo mpaka nifaulu kuliko Adam. Tena sioni kuwa ni akili nzuri kuwaza kuwa neno fulani haliwezekani kwa sababu watangulizi wetu walishindwa kulitenda. Kusema kweli, Adam alikuwa mfano wa majaribu yetu ya sasa ambayo yamelazimu kushindwa na sisi watoto wake. Kama twataka kuishi maisha yaliyo kamili, imetupasa kujistahilisha kuwa washindi juu ya kila jambo lililowashinda watangulizi wetu, ama sivyo, hatutastahili kuwa warithi wao.”

Bihaya alitamka,” Tafadhali nifahamishe madhumuni hasa ya maneno usemayo nipate kuelewa vema.”

Utubora alisema, “Nasema habari za maisha yangu wakati ujao. Waonekana kama kwamba hufahamu kuwa kazi niliyokuwa nikifanya kwa Bwana Ahmed nimeiacha. Karibu nitakuwa kama watu wengi wengine wasio na kazi wala baadhi.”

Bihaya alinena, “Kama ni hivyo, basi nambie jinsi utavyopata riziki yako? Mimi sina neno, naweza kufanya kazi ya upishi na kushona.” Utubora alionya, “Lakini mimi nawe, Bihaya, lazima tuogelee au tuzame pamoja. Nimelifikiri sana shauri hili. Nitakwenda kujenga nyumba moja nzuri huko Mrima katika pahali ambako mama yangu alizaliwa, na kazi yangu itakuwa ukulima.”

Bihaya alistuka akasaili, “Lakini wajua kitu gani juu ya ukulima, nambie nifahamu?”

Utubora alieleza sasa, “Hivi sasa sijui mengi. Lakini naweza kulima chenge - kukata miti msituni na kuichoma moto pahali ilipokatwa nikapata weu wa kupanda mimea. Naweza pia kupiga matuta nikapanda mboga. Kama hapana budi, naweza kuajiriwa kwa kazi ya kulima sesa hata kufyeka magugu katika bustani. Nitakuwa navyo vitabu vyangu, nawe utaweza kufuga kuku ili tupate mayai, kisha utanadhifisha maskani yetu mapya.”

Yaliyosemwa yote hayakumtua Bihaya akasema, “Mimi sijasikia habari za upuzi kama hizi katika maisha yangu.”

Utubora alijibu, “Si vizuri kunung’unika, Bihaya. Shauri hili limekwisha. Nimesema sana na Bwana Ahmed leo asubuhi. Lakini kama wewe waona shauri lenyewe kuwa upuuzi nitakupa furaha kidogo; tajiri wangu asadiki kama wewe kuwa nimeingiwa na wazimu au maradhi mengine mabaya, naye atumaini kuwa kukaa kwa muda wa mwaka mmoja Mrima kutaniponya maradhi yangu, kwa hivi nafasi ya kazi yangu ataniwekea wazi. Mzee yule mwema sana, bali kwa kadiri nijuavyo sitaki tena ukarani. Basi, furahi sasa Bihaya kwamba itakuwa heri pengine, na labda huko Mrima wewe utaposwa uolewe!”

Bihaya alikunja kipaji chake kikawa kama kwamba hakitakunjuka, tena kilikuwa na makunyugu kama ngozi ya kifaru. Alimkasirikia sana

Utubora, akasema kwa sauti kali, “Sijapata kusikia habari za ujinga kama hizi katika maisha yangu yote. Mama yako angalikuwa mzima angalionaje juu ya jambo kama hili!”

Utubora alijibu polepole, “Nitakwambia neno moja, Bihaya. Mimi nina wazo fulani nisiloweza kulieleza vema kuwa mama yu radhi juu ya habari hizi. Nina hakika kabisa kuwa hana kinyongo, ingawa kama tungalikuwa naye mpaka sasa nisingaliweza kuwaza kuacha kazi. Lakini kwa nini nizidi kujisaga mwenyewe kila siku katika kazi niichukiayo, wakati ninapoweza kuwa katika ardhi ya Mungu iliyo wazi nikafanya kazi ninayopenda?”

Bihaya aliguna akanena, “Jambo lililo bora kwa mtu ni kutenda kazi afahamuyo. Wewe umekuwa karani tangu ujana wako. Nashangaa mno kusikia kuwa wataka sasa kuwa mkulima.”

Utubora alisema, “Nakusudia kujifundisha zaraa. Sitakuwa mkulima stadi, lakini hapana shaka natumaini kuwa mkulima wa kutosha baada ya juma au siku chache.”

Baada ya kuwaza kidogo, Bihaya alisema, “Bwana Utubora, waungwana hawana haja ya kuwalimia watu wengine. Kama huna budi kuwa mkulima, mimi nitakuwaje! Yamkini hutahitaji tena mtumishi wa nyumbani.”

Utubora alishtushwa sana sasa na maneno ya mwisho ya Bihaya, akasema upesi, “Tabaradi, Bihaya! Bila ya shaka nitahitaji mtumshi wa nyumbani. Ukinitoroka sitaweza kabisa kutenda nikusudiavyo.”

Bihaya alitamka, “Lakini, Bwana Utubora, hutaweza kujikimu wewe mwenyewe, acha mbali kumkimu mtumishi!”

Kama kwamba alikuwa akicheka, Utubora alisema, “Nitaweza kukukimu wewe. Nimefikiri shauri hili lote kwa uangalifu mwingi. Ninayo akiba ya fedha; kiasi cha shilingi ishirini na tano kwa matumizi ya juma moja. Natazamia kuwa karibu nitaweza kupata shilingi ishirini na tano nyingine, na kwa uwekevu itatulazimu kuweza kujikimu kwa fedha hii. Lakini, Bihaya, nimesahau kukupa malipo yako ya mwezi uliopita. Wasemaje nikikulipa sasa hivi!”

Bihaya alijibu, “Usifanye wasiwasi juu ya malipo yangu, Bwana. Mimi nina akiba ya kutosha kumaliza wakati wangu uliobaki, bali shauri lako naliona kama wazimu mtupu.”

Jambo hili lilikuwa huzuni kubwa kwa mwanamke huyu mzee kwa kuona kuwa bwana wake kijana ilimlazimu kutupa ukarani wake kwa kazi asiyoijua kama ya ukulima. Huku ndiko “Kuacha mbacha kwa msala upitao.” Alisema alivyoweza lakini Utubora hakujali neno hata moja, isipokuwa alishikilia kumshauri Bihaya kuondoa wasiwasi, na kuwa tajiri wake akimpa ruhusa, watakwenda zao Mrima.

Bihaya alifanya hila yake ya mwisho kwa kusema sasa, “Lahaula! Bwana Utubora hutaweza kuwa na mke huko Mrima.”

Utubora kama kwamba alikuwa amefumwa kwa mshale alisema, “Mimi sitaki mke. Mtu aliyeumwa na nyoka akiona gamba hustuka, kwa hivi sitaoa.”

Bihaya alitamka, “Waweza kufikiri hivyo sasa, bali moyo wako ni mwema sikuzote, na yamkini utataka kuoa halafu.”

Utubora alishikwa na kicheko. Alisadiki sana kuwa shauku yake ya ujana ilikwisha. Dhana yake ilimwongoza kufikiri kuwa mtu huerevuka akiwa na umri wa miaka thelathini. Hili ni jambo la kweli kabisa, lakini alisahau kuwa hakuna roho kongwe.

Bihaya alipatwa na huzuni kubwa sana juu ya ujinga wa bwana wake kijana. Huzuni hii ilipozoea moyoni mwake, alianza kupima faida na hasara zake. Aliona kuwa bwana wake alikuwa hana nyumba Unguja isipokuwa ya kupanga, alikuwa hana shamba, kiwanja wala mali yoyote nyingine, na kuwa huko Mrima bwana wake atakuwa na shamba dogo, na yeye atakuwa na kuku wachache wa kufuga na kukusanya mayai yake mwenyewe bila ya hofu ya kuvunja yai moja. Kwa hivi, shauri alilolidhani kuwa baya kwanza, lilikuwa si baya kama alivyoliwaza sasa.

Kadhalika, Utubora alijiona kama aliyekuwa anatembea kwa miguu angani. Wakati wa kuwa macho alitunga mashauri mbalimbali, na wakati wa kulala aliota ndoto kadha wa kadha. Usiku mmoja aliota habari za kijiji alichozaliwa mama yake na alikokaa wakati alipokuwa msichana. Alipoamka asubuhi alikuwa na mawazo ya ajabu kwamba alipata kufika hasa katika kijiji cha mama yake wakati alipokuwa amelala. Hadithi zilizosahauliwa zilirudi waziwazi katika akili y Jina la kijiji cha mama yake alilikumbuka usingizini kuwa kiliitwa Busutamu, akakiona kuwa kilikuwa katika njia panda na kando yake, mto ulikuwa unapita. Katika ndoto yake alikwenda hata akaona kiwanja kilichokuwa cha nyumba ya mama yake katika miaka arobaini iliyopita, Alitamani sana kununua kiwanja kile chote, lakini alizinduka usingizini ghafula. Hakupendezewa na kukatilizwa ndoto yake. Walakini, alikusudia kwamba wakati ukiwadia, atakwenda kukaa katika kijiji kile kile ambacho mama yake alikuwa anakaa wakati wa usichana wake.

Baada ya siku chache Utubora aliabiri chomboni akaenda Mrima. Alipofika Busutamu alistaajabu sana kwa kupaona kwa macho yake mwenyewe. Palikuwa pamesitawi kwa maendeleo ya miaka. Alibaini kwamba ile ndoto yake ya ajabu kama ile ya miujiza ya Miraji ilikuwa kama darubini ya kuthibitishia kuwako kwa kitu kisichoonekana kwa macho matupu kwa sababu ya udogo, au kwa sababu ya kuwa ng’ambo ya upeo wa mwanadamu. Kwa maulizo mengi, Utubora alipata kuona kiwanja alichokiota katika usingizi. Juu ya kiwanja hiki aliazimu kujenga nyumba yake.

Aliporudi Unguja aliweza kumshawishi hata Bihaya kwa shauku yake kwamba Busutamu palikuwa pazuri sana ambako hata Bihaya atapenda kukaa mara akipaona. Aliona maskani ya zamani ya mama yake, bali kulikuwa hakuna mkulima. Aliona kuwa huko kutamfaa kwa kujaribu kufanya kazi yake ya kwanza.

Karibu ya kiwanja alichochagua palikuwa na nyumba moja kubwa ya bimkubwa mmoja. Gugu lilikuwa limeota mpaka mlangoni pake. Palikuwa na kiunga kimoja kikubwa kilichojaa minazi, miembe, mikorosho, mikomamanga, mifenesi na miti yote mingine ya matunda na maua mazuri pia; Lakini kwa kuwa bimkubwa mwenyewe alipotelewa na mjukuuwe katika vita, hakujali kabisa kunadhifisha kiunga chake, wala kutaka kuonana na mtu ye yote. Utubora alisema kuwa akijaliwa atajaribu awezavyo kumshawishi bimkubwa yule kutunza tena kiunga chake. Maneno haya aliyasema kwa furaha kama mtoto.

Ingawa Utubora alikuwa na umri wa miaka thelathini lakini moyoni mwake alikuwa kama mtoto aliyekuwa hajui bughudha. Shela alipovunja uchumba wake bure, Utubora alipatwa na huzuni iliyochukua muda mrefu kutoweka kwa sababu alimwamini sana, lakini tangu sheha alipovunja ada ya mapenzi, imani ya Utubora juu ya wanawake iliharibika. Walakini, kumbukumbu ya mama yake ilimwokoa katika kuingia katika kosa lile kubwa la kulaumu wanawake wote kama ilivyo desturi ya baadhi ya wanaume wenye malezi mabaya. Si kweli kabisa kuwa samaki mmoja akioza, wameoza wote. Samaki wengine huogelea na huzama baharini bado; hawajavuliwa wala hawajaletwa sokoni kuuzwa.

Vita vilimfundisha Utubora mambo mengi sana, vikamwonyesha vile vile maana mbalimbali za thamani ya maisha. Aliona dhahiri kuwa maisha yalikuwa si kitu cha biashara, alifahamu kuwa yalikwenda mbio, na kuwa hayakudumu. Alisadiki kuwa miji mikubwa ilikuwa maangamizi ya maisha ya watu ambao kwa haraka ya kujitafutia fahari na vyeo vyao wenyewe walikuwa hawaoni kusudi la Muumba, kuwa watu walilazimu kuishi katika ulimwengu kwa kula matunda ya ardhi, na kuwa wakati wote uliotumiwa hapa ulikuwa wa kujiandaa tu kwa maisha ya wakati ujao. Utubora alipofikiri kuwa maisha yake yajayo yatakuwa kama vile ya babu yake wa kwanza, alifurahi kuliko alivyokuwa zamani. Asili yetu ina nguvu katika mioyo yetu.
 
Hadithi nzuri sana
 
Sura ya nne
Kama Uyoga​

Heri huenda mara kwa mara kwa wajasiri, nadra sana kwenda kwa walegevu, Usipojaribu kutenda neno, utaishi, na uzikwe kabla ya kutenda kitu cho chote katika dunia. Jambo hili la hasara lilikimbiwa sikuzote na Utubora hata akawa mtu wa matendo mengi mema. Kwa hivi, baada ya siku chache tu nyumba nzuri ya matofali ya kuchomwa, paa la vigae, milango ya nakshi, madirisha makubwa, na sakafu ya seruji ilizuka kama uyoga juu ya kiwanja alichochagua kule Busutamu. Mafundi waliochukua mkataba wa kujenga nyumba hii walipeleka habari za maendeleo yao Unguja. Habari hizi zilimpeleka Bihaya Mrima kutazama ukubwa wa jiko na mambo mengine.

Wakati Bihaya alipokuwa anashughulika na kazi iliyomleta, mwanamke mmoja mashuhuri aliyekuwa anapita barabarani alisita, akatazama kwa mshangao jengo jipya. Bibi huyu alikuwa Mke wa Liwali wa Busutamu. Yeye alikuwa si mtu peke yake aliyevutwa na uzuri wa jengo lile. Watu wengine wengi walivutwa vilevile, Walakini, wengine walipotosheka na kuona tu, yeye alitaka kudadisi ili amjue mwenye nyumba ile. Basi alikwenda hata mlangoni, lakini kabla ya kubisha hodi, Bihaya alitokea. Mke wa Liwali alipendezewa sana na bahati yake njema ya kuonana na mtu aliyemdhani kuwa mwenye nyumba, akaamkia kwa madaha.

“Subalheri, Bibi. Nilikuwa ninapita macho yangu yakavutwa na uzuri wa nyumba yako. Wewe ndiye uliyekuja kukaa katika upande huu wa ulimwengu pamoja nasi? Nafurahi kusema kuwa hewa ya hapa njema sana.”

Bihaya aliitika, “Subalheri, Bimkubwa,” Kisha aliendelea kunena kwa hadhari sana, “Mimi nimetangulia kuja kutazama ukubwa wa jiko na nafasi iliyomo nyumbani tu. Mwenyewe atafuata halafu. Kwa habari za hewa, mimi na Bwana Utubora hatuna afya mbaya.”

Mke wa Liwali alitamka, “Kuwa na afya ni bahati njema kabisa. Tafadhali niamuru kuuliza kazi ya mtu umsemaye. Jina lake laonekana kama kwamba si la kawaida. Mwenyewe hakosi kuwa mtu bora kama jina lake lilivyo.”

Bihaya alijibu, “Hajawa na kazi maalum hivi sasa, bali nadhani kuwa itakuwa ukulima. Akija hapa atakueleza zaidi yeye mwenyewe. Kwa machache juu ya jina lake, ningependa kusema kuwa sijaona mtu aliyefanana mno na anavyoitwa kama mtu huyo.”

Mke wa Liwali alieleza, “Ukulima ni kazi moja katika kazi bora za dunia. Hapana shaka twataka sana mkulima hapa. Isitoshe, nimefurahi kabisa kusikia kuwa mtu huyo amefanana ajabu na jina lake. Nadhani hutaniona mjuba nikisema kuwa hapana jambo baya duniani kama kuona kiumbe mwenye umbo la mtu amebadilika kuwa kama mnyama kwa uovu wa matendo yake. Wa miguu miwili huwaje wa minne!”

Sasa Bihaya alisema, “Ningependa kujua wewe ni nani, Bimkubwa?” Swali hili lilizuia mfuriko wa maneno ya Mke wa Liwali, kwa sababu kusaili na kusailiwa ni vitu mbalimbali. Kisha kwa sauti ya makuu kama aliyekuwa akijitangaza kuwa yeye alikuwa malkia wa malkia alisikiwa kutamka,

“Mimi ni mke wa Liwali wa Busutamu. Tunakaa katika Bet-el-Busu. Bila shaka, neno la sifa litokalo kwangu mimi huwa msaada mkubwa kwa mkulima hapa. Sisi tuna watumishi wetu, lakini baadhi ya marafiki wetu hawana, na kwa bahati mbaya mtu mmoja wa makataa apatikanaye hapa amekuwa mlevi mkubwa. Natumaini kwamba mtu uliyemtaja wewe si mlevi.”

Bihaya alipokanusha kuwa alikuwa hajamwona Utubora kujishughulisha na vileo, Mke wa Liwali alisema kuwa kama alikuwa halewi atafaa sana kwa sababu kazi nyingi ziwazi duniani kwa mtu asiyelewa; kuwa Mke wa Liwali binafsi yake, atakuwa tayari kumwajiri kama atataka mtu mwingine wa kazi, na kuwa alipenda sana kusaidia mtu ye yote aliyekuwa na adili na uaminifu.

Juu ya maulizo yake yote, Mke wa Liwali hakupata kujua pahali walikotoka watu hawa. Basi aliagana na Bihaya akaenda zake. Alipokuwa njiani alishangazwa sana na jinsi mwanamke aliyekuwa anazungumza naye alivyokuwa mtu wa siri na adabu nyingi kabisa. Alitazamia kuwa Utubora alikuwa mfano uleule.

Bihaya alipomaliza kazi yake alikwenda bandarini kutafuta chombo cha kuabiri apate kurudi Unguja. Aliajabia sana maskani yake mapya. Kufika kwake Unguja alimkuta Utubora amejaa wasiwasi wa kuhama kama kijana wa miaka kumi na mitano badala ya kuwa mtu mzima wa miaka thelathini. Ingawa umri wake ulikuwa mkubwa kidogo, lakini alikuwa na mazoea ya kushughulika na mambo mengi kwa bidii kama kijana mdogo.

Utubora alikuwa kijana wa kutamanisha sana. Alikuwa na wastani wa kimo na wa gimba chini ya futi sita, si mwembamba si mnene. Kichwa chake kilikuwa kimekaa vizuri juu ya mabega ya mraba. Alikuwa na macho ya nili yenye kopi fupi zilizokuwa nene; kipaji kipana na kikubwa chenye mikunjo miwili ya kulala juu yake; pua ya kusimama kama upanga wa chuma; kinywa kikubwa kilichokuwa imara. Karibu kila kiungo cha mwili wake kilikuwa kizuri. Walakini labda kitu cha kupendeza kabisa alichokuwa nacho kilikuwa kicheko chake. Yule mwanamke aliyemvunja uchumba alijuta mpaka siku yake ya kufa.

Nyumba ilipokuwa tayari, Utubora alianza kujiandaa kuhama. Jambo la kwanza alilofanya lilikuwa kuchagua vitu vilivyopaswa kuachwa. Jambo hili lilimhuzunisha kidogo. Mara alijiona kuwa hakuweza kutengana na kitu cho chote kilichokuwa katika miliki yake. Karibu kila kitu kilikuwa na ukumbusho wa mama yake. Vitu hivi vilikuwa na thamani kubwa sana katika moyo wake, akaona mhali kutengana navyo.

Zaidi ya vitu hivyo, maktaba ya Utubora yalikuwa na vitabu vingi vya thamani. Vitabu vya dini tangu zilipokuwa dhaifu hata zikawa maarufu duniani; tangu zilipokuwa mali za watu wachache wanyonge hata zikawa mali za watu kadha wa kadha wa hali mbalimbali. Aidha maktaba hayo yalikuwa na vitabu vingine vya elimu na sanaa zilizodharauliwa, lakini zilizoweza kuokoa watu katika ulimwengu wa uharibifu na maangamizi. Robo ya mshahara wa Utubora ilikuwa inatumiwa sikuzote kwa kununua vitabu hivyo. Kwa kuwa maktaba yenyewe yalikuwa kama hazina, mshauri na rafiki kwake, aliona huzuni kubwa kuyaacha nyuma.

Kwa bahati njema Bihaya alikuwa mwanamke mwenye busara, lakini ilimpasa kutumia akili na rai nyingi kwa Utubora au huyu wa pili angalihamisha vitu vyote walivyokuwa navyo Mrima ambako, ingawa nyumba yao iliweza kuviweka vyote, bali wao wenyewe ingaliwapasa kusimama na kulala vizingitini kwa kukosa nafasi ya kuingia ndani!

Nyakati za kuhuzunisha zilimkabili Utubora sasa alipokuwa anamtazama Bihaya alivyokuwa anaingia na alivyotoka chumba hiki na kile kutia alama vitu walivyokusudia kuuza. Alitamani kutambaa nyuma yake akafute alama zote. Wakati mmoja alisema kuwa badala ya kuuza kitu cho chote, atavipakia chomboni vyote aende navyo Mrima. Bihaya alimwuliza kama alikuwa anaelewa habari zo zote za nauli ya kupakilia vitu vilivyotosha kuwa shehena katika chombo. Aliungama kuwa alikuwa hana habari zozote alizojua juu ya nauli ya kupakilia vitu chomboni. Alipoambiwa kuwa itataka fedha nyingi sana, kwa manung’uniko, Utubora alighairi kuchukua vitu vyote. Bihaya alianza tena kumzuia Utubora kwenda Mrima akasema sasa,

“Bwana Utubora, achilia mbali shauri hili la kwenda Mrima. Wewe hukuumbwa kuwa maskini. Usitupe bahati yako Unguja. Karibu utakuwa tajiri kama utazidi kukaa na Bwana Ahmed. Ana mapendeleo mengi sana juu yako; hata wewe mwenyewe wafahamu; ukikaa hapa labda utaweza kudumu na vitu vyako vyote unavyovipenda. Hapatakuwa tena na haja ya kufunganya huku kote na kuuza kitu cho chote, Bwana.”

Utubora alitikisa kichwa chake tu. Hakuwa tayari kushawishiwa vingine, akasema, “Usinishawishi, Bihaya. Kama hatuna nauli ya kupakilia vitu hivi chomboni, haidhuru. Hatutavichukua. Kazi yetu si ngumu tena sasa. Kila kitu tukikiona kuwa kigumu maendeleo yatakuwa machache, na utu wetu utakuwa duni.

“Na tukaze mioyo yetu tupate kuendelea na kazi hii. Mimi si tayari kuvunja safari yangu kwa ushawishi wo wote duniani. Tumekula ng’ombe mzima, tusishindwe na mkia.” Aliishiliza maneno haya kwa kicheko cha kupendeza. Basi kazi ya kufunganya ikaendelea, na mwisho walichukua kiasi cha vitu vilivyowezekana kuwekwa katika nyumba yao mpya kwa nafasi, na vingine vyote vikauzwa mnadani.
 
Sura ya tano
Bet-El-Busu​

Jengo la Bet-el-Busu lilikuwa juu ya kilima kilichokuwa na majabali mawili yaliyofanana na watu wawili; mwanamume na mwanamke waliokumbatiana wakabusuana. Hapo palikuwa pahali ambako maarusi wengi walitumia fungate zao. Chini ya kilima hiki ndipo palikuwa na kijiji alichohamia Utubora. Kijiji hiki kiliitwa Busutamu kwa sababu watu waliotumia fungate zao huko kilimani walifuatwa na heri katika maisha yao ya ndoa. Bet-el-Busu ilikuwa nyumba yafahari na nzuri sana. Liwali wa Busutamu na mkewe walikuwa wanakaa hapo.

Nyumba hii ilikuwa na mtoto mmoja tu. Mtoto mwenyewe alikuwa mwanamke aliyeitwa Radhia. Umbo lake lilikuwa linapendeza mno machoni. Alikuwa mrefu na mwembamba, aliyenyoka mfano kama mwanzi. Uso wake ulikuwa mduara, mashavu kama waridi, pua nyembamba kama kitara, nyusi za pembe kama mwezi mchanga, macho ya kung’ara, meno meupe, kicheko cha kutamanisha, sauti ya kinanda, na moyo mwema uliochukia kudhuru kiumbe cho chote kizima.

Msichana huyu aliposwa na mchumba aliyeitwa Makuu. Posa hiyo ilipendeza wazazi wa Radhia. Kadhalika, Radhia mwenyewe hakuichukia ila alikuwa hana haraka ya kuolewa. Mambo yaliendelea vema kama yalivyokuwa, bali kila Makuu alipotaka kuoa, Radhia aliingiwa na wasiwasi bila ya kujua sababu yake, na mchumba wake akawa anachelea sana kuhimiza arusi yao. Alifikiri kuwa labda baadaye Radhia ataridhika mwenyewe kuolewa, lakini haikuwa. Kila Radhia alipohojiwa wazo la uchumba wake, aliona giza la usiku mbele yake.

Liwali na mkewe walipenda kuona binti yao ameolewa. Wakashangaa kwa kuona kuwa Radhia hakulifanyia haraka shauri hili. Jambo la ajabu lilikuwa kwamba Radhia alipendezewa na mchumba wake wakati alipokuwa peke yake. Lakini walipokuwa pamoja, alizoea kumcheka mchumba wake tu kila alipombembeleza kumwoa.

Siku moja walikwenda kutembea pamoja. Walipokuwa wanarudi Bet-el-Busu, walipita karibu na nyumba ya yule Bimkubwa aliyekuwa hataki kuonana na mtu ye yote.

Hapa Radhia alisema. “Namsikitikia Bimkubwa huyu sikuzote, hata kupita karibu na nyumba hii hunihuzunisha kabisa?”

Makuu alisaili, “Kwa nini wahuzunika? Hayumo katika dhiki ya kusikitikiwa. Ana fedha nyingi, na kama ataka kukaa maisha ya upweke, mimi nafikiri ni kwa sababu anapenda upweke. Bimkubwa huyu ana kiranga; na mwenye kiranga hasikitikiwi, wala akifa hawekewi matanga.”

Radhia alitamka, “Hawezi kutaka upweke ila hana furaha hata kidogo. Husemwa kuwa tangu mjukuu wake alipouawa vitani, hajacheka hata mara moja. Ana uchungu mwingi juu ya jambo hili kama kwamba vita vilifanywa makusudi kumtesa yeye.

“Tazama kiunga hiki chote amekiacha kuangamia katika magugu. Kweli ana fedha nyingi, lakini haina faida kwake. Ana huzuni na uchungu. Nataka ningeweza kumletea faraja na furaha kidogo katika maisha yake.

“Fikiri jinsi alivyopatwa na hasara, amepotelewa na mume wake na mwanawe, na kifo cha mjukuu wake juu ya misiba hiyo yote kimemaliza nguvu yake! Kiranga ni tendo lisilo sababu njema. Huzuni ya Bimkubwa huyu ina sababu ya kutosha.”

Makuu alifikiri maneno yake ya kwanza yalikuwa si wazi akaeleza, “Jambo lililo jema ni kuwa wanawake wengine wote katika dunia hawakutia moyoni mashaka yao kama atendavyo Bimkubwa huyu.”

Radhia alinena, “Labda usemavyo ndivyo, lakini yeye ni mzee sana na sisi sote hatukuumbwa namna moja. Naamini kuwa yeye hatoki nje hata kidogo, hata haendi katika kiunga chake, alizoea sana zamani kutoka nje; kiunga hiki kilikuwa kizuri ajabu, bali kitazame kilivyo sasa, magugu yameota mpaka mlangoni pake! Nahuzunika sana kwa kuona hali hii.”

Makuu alishauri, “Mpenzi wangu, usitie sana moyoni mashaka ya watu wengine. Jambo hili halina faida yoyote, bali hufadhaisha mtu tu. Ulipata kwenda kumtazama, sivyo?”

Radhia alitoa kauli, “Taibu, nilikwenda pamoja na mama, bali hakutaka kuonana na ye yote katika sisi. Juu ya hivyo, mimi nafikiri kuwa kuishi bila kujali mashaka ya watu wengine si maisha kamili. Tumeumbwa na furaha ya kushangilia mafanikio yetu na ya wengine; na tumetiwa huzuni mioyoni ya kuhuzunikia misiba yetu wenyewe na ya wenzetu. Nasadiki kuwa tumeumbwa kusaidiana na kushirikiana katika kila hali, mpenzi.”

Maneno ya msichana huyu yalikuwa hayakanushiki. Yalipenya masikioni mwa Makuu yakazizimisha damu yake mishipani, lakini kwa kuwa hakutaka kuungama kwamba ilikuwa kweli tu alionya kwa

nguvu,

“Mimi sioni kama lipo neno uwezalo kutenda juu ya habari hizi, na kwa kweli huna haja ya kujishughulisha mwenyewe juu ya hili. Kwa kila hali, Bimkubwa huyu aelewe namna bora apendayo kwa kuishi maisha yake.”

Sasa wachumba hawa walipokuwa wanakwenda zao, macho ya Radhia yalivutwa na sura ya aliyekuwa anakuja mbele yao. Mtu mwenyewe alikuwa Utubora. Kwa kuwa ile ilikuwa siku yake ya kwanza katika maskani yake mapya. Utubora alijiona kama aliyekuwa amemiliki dunia nzima. Macho ya Radhia na ya Utubora yalikutana mara moja walipokuwa wanapishana njiani. Walakini, kwa kuwa Utubora alikuwa amefurahishwa na mambo yake mwenyewe, hakujishughulisha na kitu cho chote kingine kama mwanamke. Radhia hakuweza kujizuia akamwuliza mwenziwe, “Nani yule?”

Makuu alijibu, “Mimi sikumtazama vema tulipopishana naye. Wageni wengi sana hapa siku hizi.”

Walakini alipogeuka nyuma kumtazama mtu yule aliyekuwa amevuta macho ya mchumba wake, shani ya kutatiza ilikabili macho yake sasa. Shani yenyewe iliamsha kumbukumbu ya siku za chuoni alipotazama mgongo wa mtu yule aliyekuwa anakwenda zake nyuma yao; na namna alivyokuwa ameinua kichwa chake akasema,

“Sijui ni nani! Nakumbuka kuwa nilipata kuona mtu kama yule zamani; najua sana mwendo wake, lakini sikumbuki pahali nilipomwona. Labda sasa anakaa Busutamu.”

Radhia aliitikia, “Yamkini anakaa katika nyumba ile mpya. Niliona moshi unatoka jikoni tulipokuwa tunapita pale, na tazama yule anaingia ndani ya nyumba ileile!”

Kwa kuwa Makuu hakuweza kukusanya pamoja kumbukumbu yake yote, aliacha kufikiri habari hizi wakenda zao.

Utubora alipoingia nyumbani mwake alisema kwa shauku, “Bihaya, pahali hapa pazuri. Wanaonaje, Wapapenda? Mimi nadhani kuwa hapa ni pahali pamoja katika mahali bora duniani, nami nina hakika kuwa patatufurahisha. Uchawi wa uzuri wake wateka moyo.”

Bihaya alijibu, “Naamini kuwa tutafurahia, Bwana. Furaha ni kitu wabarikiwacho watu waitafutao. Tutatenda kila tuliwezalo mpaka tupate fungu letu la furaha ya kutosha.”

Bihaya alipokwenda zake kulala usiku ule, Utubora aliketi kitako katika maktaba yake kuvuta tumbaku.

Kitabu kilikuwa pajani pake lakini mawazo yake yalizungukazunguka, na nje kulikuwa kimya kabisa.

Aliona palepale udhahiri wa ajabu kwamba alikuwa katika maongezi na mama yake aliyependezewa na mambo aliyoyatenda mwanawe. Aligeuza upesi kichwa chake kama aliyetazamia kumwona mama yake amesimama karibu naye, akanong’ona polepole,

“Mama, najua kuwa upo hapa ingawa sina macho ya kukuonea!”

Aliona kama mkono mwembamba wa mama yake ulikuwa unampapasa taratibu juu ya nywele zake, lakini ilikuwa si mkono. Ilikuwa upepo wa usiku ndiyo ulikuwa unampepea polepole. Upepo huo ulikuwa umejaa manukato ya maua. Moyo wa Utubora ulikuwa unatuta kwa amani na furaha ya maisha mapya. Alitoka katika maisha ya ghasia; ameingia katika maisha ya shwari. Hakuwa na masikitiko moyoni juu ya mambo yaliyopita, wala hofu ya wakati ujao, ila hamu tu ya mtu wa kushirikiana naye amani na furaha iliyokuwa moyoni mwake. Moyo mwema hupenda ukarimu, masilahi na ushirika sikuzote.
 
Muendelezo tunaomba
 
Ama kama unacho nakala laini nisaidie pdf
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom