Uteuzi: Suleiman Abubakar Mombo Ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Siwa amestaafu

Rais Samia afanya uteuzi wa Mkurugenzi Wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ambapo bwana Abubakar Mombo Ateuliwa baada ya ndugu Siwa kustaafu.
View attachment 3039745

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Mululi Majula Mahendeka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua na kumuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mombo alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu. Bw. Mombo amechukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Pia Soma
- Tetesi: - Mombo Seleman kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS). Aliyepo anafukuzwa muda wowote
Huyu mama tangu aingie huyu ni DG wa nne hapa yeye ndio matatizo sasa sio wateule huyu Siwa alikuwa NSSF juzi tu alimteuwa wa nini wakati akijua hana hata mwaka kazini very silly

USSR
 
Kula siku uteuzi mpya nafasi moja, hivi hata wewe Samia sisi tungekuwa kama wewe Kila siku tunabadili Rais, Leo upo wewe, kesho tunamuweka makamba, keshokutwa Halima mdee, nchi haiwezi kwenda. Halaf kama hao unaoteuwa unasemaga vitatu haviwatoshi, je wewe umejipima na kuangalia viatu kama vinakutosha.

Kama unajua wewe mwenyewe hutoshi, basi acha kutumbua tumbua bianadamu c wakamilifu
🤣😃😃😃😃😃😃😃😃😃
 
Rais Samia afanya uteuzi wa Mkurugenzi Wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ambapo bwana Abubakar Mombo Ateuliwa baada ya ndugu Siwa kustaafu.
View attachment 3039745
View attachment 3039759

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Mululi Majula Mahendeka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua na kumuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mombo alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu. Bw. Mombo amechukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
View attachment 3039754

Pia Soma
Tetesi: - Mombo Seleman kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS). Aliyepo anafukuzwa muda wowote
Ni jambo jema
 
Umenikumbuka miaka ile DgTiss akiwa Yule bwana mlokole aliyekuaga Nida.
Sasa almost mwezi hiv kabla ya kutumbuliwa, kuna mwamba mmoja humu alitambulika kwa id ya My Son Drink Water (sijui kapotelea wap sikunhiz), huyu jamaa alifululiza sana kuandika thread za kumtahadharisha yule bwana kwamba soon atatumbuliwa hivyo achukue hatua mapema, bas na mimi nikawa natumia zile nondo naenda kupigia soga ofisin enz hizo nimeajiriwa.

Bas siku ilipofika kwel akatumbuliwa, mkurugenz wangu ofisin aliniogopa sana, akawa anauliza wewe ulijuaje? 😂😂😂.
Maana zile story nilikua nazipiga kama mimi ndio za kwangu vile .

Kwani Mombo iko Wilaya ya Korogwe au Lushoto ?
 
Back
Top Bottom