Uteuzi: Rais Samia, afanya uteuzi wa Makamishna wa Jeshi la Polisi Desemba 9, 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
784
1,661
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Makamishna wa Jeshi la Polisi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:

Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais


  1. Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Kombo Khamis Kombo amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Atachukua nafasi ya CP. Hamad Khamis Hamad, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
  2. Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Tatu Rashid Jumbe amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu katika Jeshi la Polisi. Atachukua nafasi ya CP. Suzan Kaganda, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Snapinsta.app_469641756_18262325491258462_1930813542163919633_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom