UTEUZI: Rais Samia afanya uteuzi na uhamisho wa Naibu Makatibu Wakuu. Dkt. Msonde kulamba asali TAMISEMI (Elimu)

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,229
4,554
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho kwa Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo:

Amemteua Dkt. Charles Enock Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI (Elimu). Bwana Msonde amechukua nafasi ya Bw. Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Msonde alikuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Dkt. Kazi amechukua nafasi ya Bwana Ramadhani Kailima aliyehamishiwa TAMISEMI. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kazi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Bwana Ramadhan Kailima Kombweyi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amechukua nafasi ya Dkt. Switbert Zakaria Mkama ambaye amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano).

Bwana Gerald Mweli, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo.

Dkt. Switbert Zakaria Mkama, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, amechukua nafasi ya Bwana Edward Gerald Nyamanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.

20220511_211520.jpg

20220511_211522.jpg
 
Mimi nilita kuuliza tu, lengo hasa la hizi teuzi holela za kiuhamisho ni nini hasa?
Mantiki hasa ni nini?
 
Alizaliwa ndani ya Necta ?!!!
Mbona kama una hasira! Watu wanasifia tu utendaji kazi wake mzuri na ulio tukuka! Na hasa kudhibiti udanganyifu kwa sehemu kubwa, lakini pia kuitoa NECTA kutoka kwenye mfumo wa kusahihisha mitihani kwa kutumia kalamu, mpaka kwenye kutumia computer!

Kwa mafaniko haya machache, watu wana haki ya kuulizana maswali ya hapa na pale.
 
Hapana kabisa kumuondoa Charles Msonde NECTA ni kuua uadilifu kabisa. Boss huyu aliiweza NECTA. Heshima ya mitihani ikajitokeza. Mifuko ya kidigitali kusahihisha mitihani.

Matokeo kwa haraka mno tena yakiwa perfect kabisa. Leo hii anapekekwa Tamisemi kusibiri maekekezo. Not fair. Au ndiyo Yale malalamiko ya upande wa pili kuwa Mkristo anakandakiza?

Hakuns Katibu wa NECTA ambaye hakuwahi kulalamikiwa na hao Jamaa. Sasa tunasubiri jina litakaloteuliwa ndiyo tutapima ukweli.
 
Back
Top Bottom