SoC04 Utawala bora, chanzo cha Tanzania tuitakayo kwa miaka 10 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Eddy the broker

New Member
Feb 14, 2015
3
2
TANZANIA ilitajwa kuwa miongoni mwa nchi nzuri duniani na Bara la Afrika kwa ujumla, kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na tovuti ya money.co.uk kutokana uzuri wa asili wa Taifa hilo lenye vivutio vya aina yake(madini ya kipekee kama Tanzanite, Dhahabu, Almasi), vivutio vya utalii kama vile mlima Kilimanjaro, na hifadhi za taifa.

Tanzania ambayo ilitajwa kuwa nchi nzuri kwa kutalii ilipata alama 6.98 kati ya alama 10 zilizotumika kupima uzuri wa nchi huku ikiongoza kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni kutokana na utalii kwa kukusanya dola bilioni 2.6 kwa mwaka 2019 na kutembelewa na watalii milioni 1.5.

Uzuri wa Mlima Kilimanjaro, mbuga ya wanyama ya Serengeti zinazoongoza Afrika ambayo imeshinda tuzo za hifadhi za Taifa ‘World Travel Awards’.

Kwa mujibu wa chama cha kutangaza utalii wa Afrika (APTA) na mtandao wa UK Travel, Tanzania imetajwa kuwa nchi ya nne duniani kwa kuwa na vitutio na uzuri wa asili. Maeneo yaliyotajwa kuwa na uzuri wa asili ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, Hifafadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Zanzibar, Pemba, Mafia, Tarangire, Ziwa Manyara, Ziwa Victoria, Gombe na Mahale, Selous na hifadhi ya Nyerere pamoja na hifadhi ya Ruaha.

Lakini bado ni miongoni mwa nchi masikini Duniani kutokana na mfumo mbovu wa viongozi wenye tamaa ya madaraka, na kutaka kujinufaisha wenyewe na familia zao. Mara kadhaa pia tumesikia makontena yanakamatwa nje ya nchi yakiwa na nyara za serikali. Ni jambo la kushangaza kuwa nyara hizo husafirishwa ndani ya nchi na kupita hadi zinapovushwa huku kukiwa na ulinzi kwenye mipaka yetu. Vijana weengi wamesoma lakini bado hawana ajira, na wengine wakipata ajira kwa kujuana, hili ni tatizo kubwa sana.

Kwa upande wa mapato ya kila mtu, Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani.

Nini kifanyike kutengeneza TANZANIA mpya(TANZANIA TUITAKAYO).

1. Kubadilishwa muundo wa utawala kwa kuleta katiba mpya ambayo itapunguza mamlaka makubwa aliyo nayo Rais(Utawala na uteuzi wa wasaidizi wake watumie njia ya kuchaguliwa),. kwa mfano; Mashirika ya umma ya kibiashara 14 yalipata hasara katika mwaka wa fedha 2021/2022, miongoni hayo ni shirika la ya Ndege la Tanzania ATCL iliyopata hasara ya Tsh. Bilioni 35.2 na Shirika la Reli TRC limepata hasara ya Tsh. Bil 31.2, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kichere, lakini hakuna uzito mkubwa wa hatua kisheria uliochukuliwa kwa sababu wengi wao ni watumishi wa kuteuliwa waliosababisha hizo hasara kubwa.

2. Kubadilishwa kwa muundo wa ufundishaji mashuleni. Wanafunzi wajifunze kwa njia ya vitendo zaidi, na wafundishwe uzalendo kuliko kukariri maandiko bila vitendo(kwa sayansi).
Hata hivyo, inaelezwa wazi katika Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) kwamba elimu ya juu nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa usawa katika uandikishaji wa wanafunzi huku wanafunzi wengi wakijiunga na masomo ya binadamu na programu za sayansi ya jamii tofauti na sayansi na teknolojia.

3. Kuongeza udhibiti mahususi katika kupambana na Rushwa, na utawala wa mabavu.
Rushwa kiserikali ni usaliti kwa umma, kwasababu rasilimali za umma zinaweza kutumiwa vibaya kwa lengo la kumnufaisha mtoaji rushwa na mpokeaji. Mnamo septemba 2016 serikali ilianzisha mahakama kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu uchumi ili kushughulikia kesi kubwa za rushwa.

Rushwa huhatarisha utawala bora na haki za binaadamu, mfano kununua kura wakati wa uchaguzi na kutishia mchakato wa kidemocrasia. Rushwa pia Hupelekea kutoa nafasi za upendeleo chini ya huduma mfano huduma za afya, elimu, siasa vitu ambavyo ni kipaumbele cha maendeleo kwa nchi yoyote duniani.

Kuhusu Matumizi mabaya ya Madaraka na ukaidi kwenye usimamizi wa sheria, unaofanywa na asilimia kubwa ya viongozi wa serikali za vijiji, kwenye usimamizi wa Rasilimali ardhi ndio kiini cha migogoro ya kila mara kumekwisha ripotiwa mauaji, Uharibifu wa mali ikiwemo Mifugo na mazao ya kilimo, baadhi ya watu kusalia na ulemavu wa kudumu hayo yote yakisababishwa na misimamo binafsi ya viongozi bila kufata sheria.
Ugawaji wote wa ardhi ya kijiji lazima uthibitishwe na Mkutano Mkuu wa Kijiji, Suala ambalo halifanyiki katika maeneo mengi ikishuhudiwa mauziano yanayofanyika kinyemela baina ya mnunuzi na baadhi yao viongozi.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa katika moja ya hotuba zake aliposema “Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne kuchangia maendeleo vitu hivyo ni Ardhi, Siasa safi, Uongozi Bora na Watu”.Huenda Mwalimu alimaanisha ardhi ni miongoni mwa misingi Madhubuti ya maendeleo ambayo endapo viongozi wakiongozwa na siasa safi, kutakuwa na utumiaji mzuri wa ardhi hiyo kwa ajili ya yetu na vizazi vijavyo.

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo yakifanyika na kuchukuliwa hatua ndani ya miaka 10 tutakua na Tanzania tuitakayo. TANZANIA ni tajiri lakini watu wake ni masikini.
#Tanzania tuitakayo

1000040029.jpg
1000040030.jpg
1000040031.jpg
1000040032.jpg

Picha zikionyesha utajiri na uzuri wa Tanzania chanzo cha picha:globalpublishers.co.tz
 
Back
Top Bottom