ulishaona wapi mtu akapewa cash? ni kuchagua offer au usipewe kabisaNakuomba sana Dadaangu hio hela ya offer, mpatie Cash aache harakati za kukimbizana na abiria aandike story vizuri😅😅
hebu fikiria huo muda anaokula na kunywa, hela ya boss anaitafuta saa ngapi?ulishaona wapi mtu akapewa cash? ni kuchagua offer au usipewe kabisa
Hana boss huyo, chombo ni yake mwenyewhebu fikiria huo muda anaokula na kunywa, hela ya boss anaitafuta saa ngapi?
Boss ni yeye mwenyewe Umughakaahebu fikiria huo muda anaokula na kunywa, hela ya boss anaitafuta saa ngapi?
Sawa kipenzi!!Akiendelea naomba uwe unanitag mwaya coz naweza kosa mtiririko
Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
Saii masta anakula kuku kwa mrija na mrembo matraaatraaaaa sanaaaa Nakadori! Let them enjoyyyyyy the moment✌️✌️✌️✌️ misukule ngoja tusubirie tu hakuna namna!🙇
Lol kumbe hajafika??? Niliona ameitikia hapo msubirie atakuja tu !sijamuona hapa bado
me sitakaa siti ya mbele bwana mwambie asiogopaHahahaaa keshakua na uzoefu wa kutosha master hawezi ogopa buana he will come msubirie!!
Ukute una tako kubwa hatariUMUGHAKA ameoa halafu anapenda traako kubwa sana wakati me langu la kawaida
ngoja tu aje nimpoze poze amalizie story haha
hahahaha we shauri yako muulize Iblis Bin Shetan akwambie kama lipo au halipo. ila me me nakwambia halipooUkute una tako kubwa hatari
Asante bossUtajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani - 26
Maisha yaliendelea kuwa matamu sana kwa wakati huo na hakuna aliyefahamu kile tulichokifanya mimi na Ally kwenye ule mgahawa,watu wengi walikuja kujipatia chakula na kuondoka,kiukweli tulikuwa tunauza sana,kuna muda tulikuwa tunauza hadi tunachoka wenyewe.
Mimi kwa upande wangu maisha yangu yalininyookea na nilikuwa nikisevu fedha kwa ajili ujenzi wa nyumba tena,pamoja na kulipwa na Ally Mshahara kama msimamizi wa ule mgahawa lakini pia nilikuwa nikipitisha panga kubwa kwenye mauzo ya siku,kiukweli nilikuwa ninapiga sana pesa na ukizingatia kila mwisho wa mwezi nilikuwa nikijipatia fedha kwa njia ile ya Pete.
Mwanamke wangu Rehema alipokuja nyumbani,mambo ni kama yakaanza kubadilika,alikuwa mkali sana baada ya kuona nikiwa mkononi nimevaa Pete na akahisi uenda nilivishwa na mwanamke mwingine,kitu ambacho haikuwa kweli.
Rehema "Unadhani naweza kukuamini kama unavyodhani?"
Aliendelea "Niliwahi kukwambia nyie wanaume huwa mnatamaa sana,sasa umeona ushanitumia vya kutosha ukaona kabisa uvishwe Pete na mwanamke wako"
Aliendelea "Basi hata ungeniheshimu tu kwa kuivua na kuificha ili nikiondoka ndipo uivae!"
Mimi "Hayo ni mawazo mfu mpenzi wangu,siwezi kuvishwa Pete na mwanamke mwingine,inapaswa uniamini!"
Rehema "Usidhani kunisomesha ndiyo kigezo cha kunifanyia ujinga wako,tunaweza kuachana vile vile!"
Mimi "Kwani Ray siwezi kununua Pete na kuivaa tu?"
Rehema "Usinifanye mimi mtoto mdogo,wewe ungekuwa wa kununua Pete nadhani mimi ndiye ningekuwa wa kwanza kuvalishwa,sasa mimi hujawahi nivalisha Pete halafu unaniambia madudu gani sijui!"
Usiku mzima ulikuwa wa kupigizana kelele na Rehema na kiukweli hakuelewa kitu pamoja na kumueleza,siku hiyo kiukweli Rehema aligoma kabisa kunipatia maji ya kunywa ijapokuwa nilikuwa nina kiu ya kufa mtu,kila nilipokuwa nikajaribu kumgusa anigeuzie mtungi nichote maji ninywe yeye alidai niende nikanywe kwa mwanamke aliyenivisha ile Pete.Kiukweli usiku ule sikufanikiwa kabisa kuchota maji ya kunywa na nilikesha na kiu hadi asubuhi.
Sasa ilipofika asubuhi wakati mimi najiandaa kuelekea kazini na yeye aliamka akasema anarudi nyumbani kwao na nikimhitaji tena nihakikishe hanioni na hiyo Pete kwenye kidole.Nilijaribu kumtuliza lakini akawa mkali sana akawa ameondoka akaelekea kuoanda daladala.
Nilifunga mlango nikaondoka zangu kazini;Ilipofika usiku baada ya kutoka hapo kazini nilijaribu kumpigia simu Rehema lakini ilikuwa inaita tu haipokelewi,basi niliondoka hadi Ubungo msewe kwao Rehema na nilipofika nilivua ile Pete nikaiweka mfukoni kisha nikampigia simu,alipopokea nikamwambia nipo nje atoke tuzungumze!.Nilimbembeleza na nikamwambia ile Pete isije kuleta ugomvi kwani nimeivua na kuitupa,japo alinielewa lakini aligoma kabisa kuondoka na mimi akasema angekuja kesho yake,sikuwa na namna ilibidi niondoke zangu kurudi nyumbani,sasa wakati narudi nyumbani nikawa nimesahau kuivaa tena ile Pete na nilipofika nyumbani nikawa nimeingia kuoga na kulala,sasa ilipofika asubuhi wakati navaa ile jeans nilikuwa nimeivaa jana yake nilijaribu kuitafuta ile Pete mfukoni ili niivae lakini sikuweza kuiona,nilijitahidi kuitafuta sana hadi kukung'uta ile jeans lakini wapi !.
Niliamua kuondoka hivyo hivyo kuelekea job,sasa nikiwa kwenye gari Rehema akawa amenipigia simu ya kwamba anaenda nyumbani hivyo akawa anaulizia funguo nimeziweka wapi,nilipofika pale kituo cha Ngozi niliamua kushuka na kuingia upande wa pili ili nipande gari lingine nirudi nyumbani kumsubiri Rehema aliyekuwa njiani nimpatie funguo.Nilipofika nyumbani kuna hali nilianza kuhisi ambayo haikuwa nzuri,nilianza kuhisi baridi kama mtu ambaye alikuwa na malaria,kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndipo hali yangu nayo ilikuwa mbaya sana.
Rehema alipofika nyumbani alikuta nimelala na aliniuliza kama ninamwa lakini nilimkatalia,alijaribu kunishika shingoni akakuta homa imekuwa kali,alikwenda pharmacy kuninulia dawa za kutuliza homa lakini nilipotumia bado hali haikuwa nzuri,sasa kwakuwa nilikuwa tayari nishafahamu kilichokuwa kinaendelea,nilichukua simu yangu nikawa nimempigia Ally Mpemba lakini simu ikawa inaita tu jamaa hakupokea.Baada ya muda kupita jamaa akawa amenitumia sms iliyosomeka "Wewe huna akili na utakufa kifo kibaya sana!".
Baada ya kuisoma ile sms niliifuta kabisa ili Ray atakaposhika simu yangu asije kuiona;Niliona ningeendelea kukaa kimya ningekufa kipumbavu kama alivyoniambia Ally Mpemba,nilichukua simu yangu nikampigia mama yangu Tarime pamoja na Dada yangu mkubwa wa Mwanza na nikawa nimewajulisha hali yangu haikuwa nzuri,sasa mama aliona mpaka nimempigia simu kiukweli hali yawezekana haikuwa nzuri,yeye alimpigia simu Anko wangu kitu ambacho sikutaka kabisa yeyote kutoka upande huo afahamu,na nilijua anko akifahamu ataanza ngonjera zake.Niliamua kuzima simu kabisa ili yeyote atakayenitafuta asinipate.
Hali yangu ilikuwa mbaya sana hadi Rehema akaamua kunipeleka dispensary pale Gongo la mboto kwa ajili ya kuchukua vipimo,majibu yalipotoka sikuonekana na tatizo lolote lakini kiukweli nilikuwa naumwa,sasa wakawa wameniambia ninywe maji mengi kwasababu hali kama hiyo huwa ni kawaida.
Wakati Rehema anadhani ni ugonjwa wa kawaida mimi nilikuwa nimeshafahamu tatizo ilikuwa ni ile Pete niliyoivua na kupotelea kusiko julikana,niliona nikiendelea kuzubaa naweza kupotea kabisa,tulivyorudi nyumbani mimi niliondoka nikawa nimerudi pale Msikitini Gongo la mboto(Masijid ijumaa),kuna Sheikh mmoja nilikuwa nafahamiana naye nikawa nimefika kumuulizia lakini nikaambiwa siku hiyo hajaonekana hapo,sasa kuna Sheikh mmoja sikutaka kumficha kitu chochote kwasababu niliona kabisa nikiendelea kupuuzia naweza kupoteza maisha.
Nilimwambia kuna Pete nilikuwa ninayo lakini haikuwa nzuri ilikuwa ikinisaidia kwenye mambo yangu ya biashara na baada ya kuivua tu nikaanza kuugua,yule Sheikh aliniambia nimsubiri amalize swala kisha tuondoke.Kweli,nilivumilia hadi akawa amemaliza kuswali na alipotoka nje nilimuwahi nikamwambia nilikuwa namsubiri,alinichukua tukaondoka tukawa tunapiga stori za hapa na pale hadi tulipofika kwake mitaa ya mzambarauni,tulipofika kwake namshukuru Mungu Sheikh akaanza kunisomea dua za kufa mtu,alinisomea sana na hatimaye akawa ameniambia kuna mafuta ninapaswa nikayanunue kwenye maduka ya kisuna ambayo nitakuwa ninayaweka kwenye maji kabla ya jua kuchomoza kisha nakwenda kuoga.
Yule Sheikh aliniandika jina la yale mafuta nikaenda kuyanunua na kiukweli baada ya ya kutoka pale hali yangu ikawa nzuri kiasi.
Asubuhi baada ya kupambazuka niliyatumia yale mafuta na hali yangu ikawa nzuri japo si sana lakini kiukweli nilimshukuru sana Sheikh.
Baada ya kuwa nimepata japo ahueni,niliondoka nikaelekea Kkoo kwenye mgahawa wa Ally Mpemba ili kama nikimkuta nijaribu kuzungumza nae maana nilikuwa nampigia simu zangu jamaa hapokei,nilipofika pale kuna mwanamke mmoja mwenye asili kama ya Ally nilimkuta nikawa nimeambiwa na wale wafanyakazi wa pale kwamba yeye ndiye alikuwa msimamizi wa pale.Niliwaza sana laikini sikupata majibu kwasababu haiwezekani mimi kutokuonekana siku moja tu Ally Mpemba akaamua kuniweka pembeni.
Niliondoka hadi kwenye duka lake la pale Aggrey lakini sikumkuta,nilijaribu tena kumpigia simu hakupatikana kabisa.Niliamua kwenda hadi pale kwenye duka la Gerezani kujaribu kumtafuta lakini nilipokwenda nilikuta lile duka limefungwa,sikutaka kukata tamaa kirahisi nikaona nielekee kwake Magomeni.Nilipofika Magomeni nilikuta geti limefungwa na nilipojaribu kugonga hakuna aliyekuwepo ndani,niliamua kuondoka na kurudi zangu nyumbani mdogo mdogo nikiwa nimekata tamaa kabisa.
Rehema alikaa kwangu takribani wiki moja kisha akawa amerudi kwao ili akajiandae aweze kurudi chuo.
Baada ya Rehema kuondoka mimi pia niliondoka kuelekea Sumbawanga huko Namanyere kwa mtaalamu ambaye hapo awali Mwakisaka alikuwa amenielekeza na kunipa mawasiliano yake.
Itaendelea..............
utakuwa unanisomea story mimi naandika tuWewe niandalie offer wikiendi hii watoto wakishalala,ni mwendo wa bakacha tu!