RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 150
- 520
MHADHARA (89)✍️
Kitu pekee utakachokula/utakachomeza bure mjini ni mate yako tu. Lakini vingine vyote ni gharama. Hakuna cha bure, ni lazima ulicholishwa utalipia kifedha, kiroho, kimwili, kihisia, kiakili, n.k - kama hutolipia leo utalipa hata baadae.
Punguza au acha kabisa tamaa, uzembe, uroho, na shida zisizokwisha mbele ya jasho la wenzako.
1. Hujawahi kubeti wala kucheza mchezo wowote wa bahati nasibu. Unatumiwa ujumbe wa simu (SMS) kuwa umeshinda shilingi milioni 50, hivyo ili kupata hela yako tuma kianzio cha pesa kiasi fulani au piga simu namba "hii", na wewe unaingia mkenge 👁️Umerogwa au una wazimu?
2. Unaishi kwenye nyumba yako uliojenga. Unatumiwa ujumbe wa simu (SMS) isemayo "hiyo hela ya kodi ya nyumba tuma kwenye namba hii" - na wewe unatuma hela halafu baadae unalalamika umeibiwa 👁️Umerogwa au kuna michepuko umeipangishia nyumba?
3. Umetumiwa ujumbe wa simu (SMS) ya huduma za mikopo ya fedha. Kwasababu ya tamaa au shida unafuata maelekezo yao, lakini baadae unaambiwa tuma kwanza kianzio cha hela ili uingiziwe hela uliyokopa. Unachukua hela ndani kwako unatuma ili ukopeshwe hela 👁️Huo ni ukichaa au umerogwa?
4. Unakutana na watu wanakwambia kuwa wanauza madini (dhahabu) yenye thamani ya shilingi milioni 500, lakini wanataka kukuuzia wewe kwa shilingi milioni tatu (3) ili wewe ukauze upate hizo hela, na wewe unaingia mkenge mchana kweupe.
RIGHT MARKER
Dar es salaam.