Utafiti usio rasmi kuhusu mitandao ya kijamii na watumiaji wake

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
27,205
65,599
UTAFITI USIORASMI; KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII NA WATUMIAJI WAKE TANZANIA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Leo nitaleta kautafiti kadogo nililokafanya ambako sio rasmi.

Mitandao ya kijamii Kwa hapa Nchini ambayo ni Maarufu ni Facebook, Instagram, WhatsApp, Jamii forum, Twitter's, Tiktok, ambayo hii ni Maarufu na inawafuasi wengi.

Ingawaje ipo mitandao ya Siri ambayo inahusu masuala ya Mahusiano ambayo sio Maarufu Kwa nchi yetu ingawaje inawafuasi.
Mitandao hiyo ni pamoja na Badoo, Eris, CDFF, miongoni mwa mingine.

Hata hivyo wapo wanaotumia Blog kama mitandao ya kijamii. Yapo makundi Kama Mashoga na Wasagaji ambayo mara nyingi hutumia Blog Maarufu kutafuta marafiki wapya wa karba yao.

Mitandao au Blog Maarufu Tanzania Kwa Mashoga na Wasagaji ni pamoja na blog ya The guest books, Black wa Ukwee, Tanzania Guys networks miongoni mwa zingine. Hata hivyo Kwa uchunguzi wangu blog hizi zilidorora Kama sio kufa kabisa baada ya mwaka 2015 alipoingia Hayati Magufuli. Hii kusema kundi Hili ndani ya jamii licha ya kujificha katika blog za Siri lakini bado likaathiriwa vikali na Utawala wa awamu ya tano.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa blogs hizo zimefufuka hasa kuanzia mwezi May mwaka huu, pengine ningeulizwa sababu ningefikiri huenda ni baada ya JPM Kufariki.

Nikirudi kwenye mitandao ya kawaida.

Mitandao ya Facebook, Instagram, Twitter na Jamii forum.

Kundi kubwa lililojiunga na mitandao hii ni Vijana wenye umri wa miaka 17-45.

Hata hivyo ili ujiunge mitandao hii yakupasa uwe na simu Janja.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa, katika umiliki wa simu Janja, wakazi wa mjini ndio wenye kumiliki simu Janja kuliko wakazi wa vijijini.

Niliendelea kubaini kuwa, Vijana wa mjini pia ndio waliojiunga kwenye mitandao ya kijamii ukilinganisha na wakijijini.

Pia nilibaini kuwa, Asilimia 80% waliojiunga Facebook Kama mtandao wa Kwanza kabla ya mitandao mingine.
20% ndio walijiunga mitandao mingine Kwa mara ya Kwanza.

Sababu kubwa ya watu wengi kujiunga Facebook Kwa wingi na Kama mtandao wa Kwanza ni kutokana na mambo makuu matatu niliyoyabaini:

1. Urahisi wa kujisajili
2. Simu nyingi zinanunuliwa zikiwa tayari zina app ya Facebook
3. Gharama ya mtandao kuwa rahisi

Hii ni tofauti na mitandao mingine ambayo kujisajili tu inawapa mtihani watu wengi kutokana na elimu duni. Baadhi ya app huhitaji email ili kujisajili. Hii huwafanya watumiaji hasa wenye elimu duni kushindwa kujisajili.

Pia suala la kupakua App ni changamoto, na gharama ya kutumia Facebook ni nafuu kwani kuna Facebook ya bure.

MAJINA NA USERNAME
Uchunguzi wangu umebaini kuwa, watumiaji wa mitandao ya kijamii Asilimia 80% hawatumii majina Yao halisi wengi hujiita Nickname(AKA) zao. Na wachache huyaboresha majina yao Kwa kuyaongeza au kuyapunguza

Kwa mfano:
Mtu Kama anaitwa Robert Heriel.
Basi Mtandaoni atajiita Taikon wa Fasihi Hilo ndilo username yake.

Kwa upande wa kuboresha majina Yao,
Mtu anaitwa Andrew Joseph
Basi atajiita Andrew Da Silva

Nilipouliza ni Kwa sababu gani wanaotumia majina ambayo sio halisi au wameboresha majibu yao yalikuwa;

1. Wanapenda tuu kujiita hivyo 70%
2. Wameamua na hawajui Kwa nini wamejiita hivyo 30%

Hata hivyo uchunguzi wangu ulibaini kuwa wengi huyaboresha majina Yao Kwa kutumia majina ya watu mashuhuri wanaowapenda, aidha ni watu HAO mashuhuri ni wanamuziki au wachezaji wa mpira.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa, Asilimia 20 ndio hutumia majina halisi. Na hawa wengi ni Wale watu wazima ambao ndio wengi wao, viongozi WA nchi, na baadhi ya wasomi kidogo.

Nilibaini kuwa, watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wao hawapendi kutumia majina ya kikabila hasa majina ya ukoo.
Uchunguzi wangu unaonyesha 76% majina yao hayana majina ya ukoo. Yaani huwezi jua huyu ni kabila gani au ukoo gani kwani wameficha majina ya ukabila.

25% ndio hutumia majina ya Ukoo.

PICHA NA MAUDHUI YA POST
Uchunguzi wangu ulibaini kuwa, watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Facebook na instagram, wameweka profile picha Kama hivi:

1. 60% waliweka picha zenye taswira zao wenye
2. 40% Waliweka picha zenye taswira za wahusika wengine au maandishi.
Wahusika wengine ni Kama wanyama, wachezaji mpira, Wanafalsafa, Wanaharakati, viongozi mashuhuri wa Kisiasa na Kidini, wanamuziki NK.
Wengine waliweke Profile picture zenye maandishi Kama vile Aya za Quran, Biblia, memes za mapenzi, Maua yenye jumbe za mapenzi NK.

Utafiti wangu baadaye utaelezea mahusiano ya Profile picture na Mhusika.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii waliotuma picha Nusu(passport zilizoishia kwenye mabega au kiunoni) wengi wao 90% ni wafupi kimaumbile.
Hii ipo upande wa jinsia zote mbili.

Nilibaini kuwa 90% za watumiaji wa mitandao ya kijamii picha zao walipiga na wanapendelea kuzipiga wakiwa Maeneo yenye mandhari nzuri, wakila vyakula vizuri, wakiwa wamevaa vizuri.

Nilibaini kuwa sababu ya watu kutumia picha nzuri ni kutokana na tabia ya kujitunisha kuonekana nao wamo.

10% nilibaini wao wapo tayari kupiga picha hata Kama mazingira au hawajavaa vizuri.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa, picha zinazotumwa Mtandaoni 90% lazima zieditiwe ndipo zipostiwe.
Pia editing hizo nilibaini zililenga kuwatakatisha na kuwafanya wahusika kuwa weupe.

Nilipouliza baadhi ya watumiaji kuwa Kwa nini huwezi kupost picha bila kuediti wengi wao wakisema kuwa picha haipendezi pasipo kutiwa vionjo vya editing.

95% ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamejisajili Kama watu waliohitimu elimu ya vyuo vya Kati na chuo kikuu.
5% Wameishia Kidato cha nne. Huku walioshia darasa la Saba wakikosekana.

Maudhui yanayopostiwa na watumiaji wa mitandaoni yamegawanyika kama ifuatavyo;

1. 50% Hutoa maoni jinsi wayaonavyo maisha na kumhusisha na Mungu.
Maoni Kama " Kila hatua Dua" ipo siku yangu"
Usimdharau mtu hujui kesho"
Maudhui ya Aina hii wengi huyachapisha Kama sehemu ya kujifariji

2. 25% matambo, vijembe, mafanikio.
Hawa wengi hupenda kutuma maudhui kuwajibu na kuwarushia vijembe adui zao. Hawa hurusha matambo, huonyesha mafanikio yao, na kuwazingua mahasimu wap.

3. 5% Vituko, vichekesho, memes, vioja
Hili ni kundi linalochapisha maudhui yenye memes mbalimbali, vichekesho, vioja, na mambo yote yenye kufurahisha jamii.

4. 10% Watuma Matangazo ya biashara
Kundi hili huchapisha maudhui ya biashara. Biashara za nguo, nafaka, udalali, Huduma za kijamii, biashara ya Umalaya nkm

5. 5% Waandika mafundisho, Makala na mambo yote yenye kujenga.
Kundi hili ni Wale wanatumia mitandao kuweka maudhui yenye kujenga, kufundisha jamii na kuionya.
Kundi hili wapo waandishi wa Makala, Wanaharakati, watunzi wa kazi za Fasihi, wachungaji, masheikhe, Wataalamu wa elimu na Afya NK.

5. 5% hutuma maudhui yasiyojali Mila na desturi za jamii.
Hawa huposti jumbe na picha za utupu, utapeli, ushoga, ulaghai, uzushi, na maudhui yenye kuleta taharuki.
Kundi hili wapo wengi wasanii hasa wanamuziki na waigizaji. Ila wapo pia Malaya na watu waliovurugwa au kujivuruga.

INBOX/ MESSENGER/PM
Uchunguzi wangu ulibaini kuwa,
Wanaume ndio wanaoongoza kuwafuata wanawake kwenye PM au inbox zao.

Asilia 99% za wanaume wanaotumia mitandao ya kijamii wameshaingia na kutuma jumbe kwenye inbox za wanawake au watu waliojisajili Kwa majina ya wanawake. Lengo kuu likiwa kuwataka kimapenzi

Nilibaini kuwa 99% wamefuatwa inbox na wanaume.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa sababu kuu inayowafanya wanaume waingie kwenye inbox au PM za wanawake au waliosajili majina ya wanawake ni;

1. Profile picture yenye taswira ya mwanamke mrembo.
Nilibaini kuwa wanaume wengi hutuma ujumbe inbox Kwa wanawake Kwa kuvutwa na uzuri WA picha za mwanamke husika.
Picha za mwanamke mwenye matako makubwa, mweupe, na mwenye Sura nzuri huvutia wanaume wengi.

2. Jina zuri/Username
Nilibaini kuwa uzuri WA jina huchangia wanaume kuwafuata inbox kinadada.
Katika mtandao wa Jamii Forum ambao watumiaji wake wengi hutumia majina bandia, niliweza kufanya uchunguzi Kwa wahusika ninaowafahamu tunaotumia JF.
Kisha niliweza kuunda Account 5 zenye majina mazuri ya kike kisha account 5 zingine zenye majina ya kawaida au Mabaya ya kike.
Katika account 5 zenye majina mazuri zote zilitumiwa ujumbe na baadhi ya members wa JF huku zenye majina mabaya ni account moja tuu iliyotumiwa.

Nilibaini kuwa inbox za Wanawake au zenye majina ya wanawake hasa WA Facebook, hutumiwa jumbe na wanaume au Vijana wengi wenye Asili ya Asia, kutoka Pakistan, India, Indonesia NK.
Wanaume au Vijana hao huwaomba wanawake mahusiano ya ngono, na pia huwatumia picha na video za uchi.

Nilibaini kuwa account nyingi zenye picha za wanawake wazuri hazimilikiwi na wanawake isipokuwa wanaume ambao ni Matapeli.

Kwenye account 10 zenye username na picha za wanawake basi 7 ni watu bandia, watatu ni halisi.

Kundi hili unapolitumia ujumbe inbox, usitarajie kujibiwa na hayo ndio matokeo chanya kwako.

Lakini endapo utajibiwa basi jua utapata matokoe hasi.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa wasichana halisi warembo waliopo Facebook, Jamii forum au Instagram ukiwatumia ujumbe inbox hawatajibu.

Na endapo watajibu, hasa Kwa haraka ujue huyo Mrembo bandia.

Na itachukua dakika chache kukutaka pesa ambazo huwa ni elfu mbili mpaka elfu kumi.

Uchunguzi ulibaini kuwa, maudhui watu wanayoshare ni Yale yenye ukaribu na ngono na mtazamo mbaya.

Maudhui yenye kujenga ni vigumu kutumwa huku na huku, labda yawe ya watu mashuhuri.

Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa,
Watumiaji wenye Followers wengi mitandaoni ni Wale mashuhuri Kwa Mambo ya hovyo Kama kutuma picha au hadithi za matusi.

Pia watumiaji wanaotetea haki za wanawake nilibaini wanawafuasi wengi ukilinganisha na wenye mtazamo wa mfumo dume.

Uchunguzi wangu ulibaini kuwa 80% ya Vijana wasomi walipata simu na kujiunga na mitandao ya kijamii walipomaliza Kidato cha sita au walipoingia chuoni.

Uchunguzi wangu, ukiweza baini athari za mitandao ya kijamii miongoni mwa Vijana.

1. Moja wapo ni Vijana kuwa addicted katika mitandao.

2. Sonona na misongo ya mawazo.
Inayotokana na Yale wayaonayo Mtandaoni.

3. Utapeli unaofanywa na Matapeli wa biashara na wanajifanya wanawake kumbe ni wanaume.

4. Taharuki na hofu Kwa baadhi ya taarifa zipatikanazo Mtandaoni.

5. Kihoro Kwa kuona picha na video za matusi.

Hata hivyo uchunguzi wangu ulibaini manufaa Yafuatayo kwenye mitandao ya kijamii

1. Kupata habari Kwa wepesi.

2. Kurusha Matangazo ya biashara

3. Sehemu ya kutoa maoni na kujua maoni ya wengine

4. Kupata marafiki wapya na wakati mwingine kupata wenza wa maisha.

5. Kujua Duniani kunaendeleaje.

6. Sehemu ya kupata elimu.

Kwa leo tuishie hapa
Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro.
 
Umechambua vizuri Sana ndugu mleta mada.
Kwa upande wangu nimeanza kutumia mtandao wa kijamii mwaka 2010 na nimejiunga nayo rasmi 2012.

Ukweli Ni Kama ulivyoeleza wengi wetu huanza na Facebook, kwa sababu fb imepewa promo kwa kiasi kikubwa kwamba kila mtu anajua Kuna Facebook, na anapo pata kitu kitakachomuwezesha kufika Facebook basi ndio huwa ya kwanza kujiunga.

Na kwa vile wengi wanakua na uchanga wa internet na social network basi maudhui yao mengi huwa Ni kitoto hata Kama Ni watu wazima.
Kiasi ikifika mbele maarifa mapya yakiingia huikimbia ile account na kuanzisha nyingine.

Lakini wengine tulibadilika kulingana na nyakati hivyo maudhui tunayowasilisha nayo hubadilika.

Ila kusiko na utoto mwingi Ni hapa jamii forum, kwangu Mimi Ni mwaka wa nane jamii forum, japo nilianza na ujinga lakini kila leo naimarika kimtazamo, ingawa members wengi wa nyakati hizi haswa kuanzia ile 2015 kidogo mabadiliko Ni makubwa.

Miaka yangu yote sita kwa user name hii na miaka miwili kwa aser name nyingine nimewahi ku pm mtu mmoja tu tena hivi karibuni na Ni kwa Salam tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utafiti wa twaweza huu

Sisi wadau wa JLW,
Mitandaoni yetu ya kijamii Kama xnxxforums mbona umetutenga.
 
Siku moja nilikaa nikaanza kusoma inbox upya nilizokuwa nawatumia watu wakati ndio naingia Facebook , nikajishangaa hivi ndio Mimi kweli huyu?

Niliachaa kupost chochote Facebook siku hiyo na nikaanza kufuta baadhi ya post maana nilikuwa kituko.
 
Siku moja nilikaa nikaanza kusoma inbox upya nilizokuwa nawatumia watu wakati ndio naingia Facebook , nikajishangaa hivi ndio Mimi kweli huyu?

Niliachaa kupost chochote Facebook siku hiyo na nikaanza kufuta baadhi ya post maana nilikuwa kituko.

😃😃😃😃😃
 
Back
Top Bottom