ecolizer baba
Member
- Sep 29, 2010
- 88
- 310
Wasalamu ndugu zangu. Poleni na majukumu.
Nimekaa na kutafakari sana juu ya mwenendo wa Sasa za Kenya kwa hivi Sasa hasa baada ya kuonekana dhahiri kuwa mhimili wa Mahakama na ule wa Serikali wana uhasama. Yote haya ni kwa sababu ya kufutwa kwa matokeo ya Urais.
Jana tumeona Haki Mkuu David Maraga akilalamika hadharani huku akilituhumu jeshi la polisi kwa kushibdwa kutoa ulinzi kwa Majaji wa Mahakama ya juu.
Lakini pia tumeona kile kinachoitwa kuwa ni shtaka la kutaka DCJ Mwilu na Isaack Laneola wachunguzwe kwa kile kibachodaiwa kuwa ni kuwa na mawasaliano kati yao na watu wa NASA ikihusishwa na suala zima la kesi ya matokeo ya urais.
Maoni yangu juu ya hayo mambo mwili:
1. CJ David Maraga anazidi kufanya makosa. Yule ni Mwanasheria tena nguli. Ndiye reference ya mambo yote ya kisheria kwa Kenya sahivi. Hakupaswa kufanya press ya aina ile ya kulituhumu jeshi la Polisi na serikali. Haya ni makosa makubwa. Alipaswa kuongea na Rais Uhuru Kenyatta na kumueleza juu ya uhitaji wao wa ulinzi na kumuambia kuwa IGP ameshindwa kutekekeza maombi yao. Rais Kenyatta akishindwa kuwapa ushirikiano ndio angetoka before the public. But kile alichokifanya sio sawa. Amegeuka kuwa mwanasiasa badala ya kusimamia professionalism.!!
2. Tuhuma dhidi ya DCJ na Laneola kama ni za kweli huenda Mahakama ya nchini Kenya ikaingia kwenye tope zito. Na hii huenda ikafanya wananchi wakapoteza imani nayo. Lakini pia heshima ambayo ilikuwa imejijengea hivi karibuni kimataifa huenda ikafutika.
Sasa kutokana na malalamiko ya Maraga huenda watu wenye nia ovu wakatumia mwana huo kuwadhuru Majaji halafu Jubilee na serikali yake wakahusishwa. Hii ikitokea, believe me hali ya kisiasa itachafuka kwa sababu akina Raila watapata loop hole ya kulazimisha serikali ya nusu mkate.
Tuendelee kuwaombea wakenya katika kipindi hiki kigumu.
Naomba kuwasilisha.