Uspika wa Dkt. Tulia Ackson umedhihirisha yeye ni mtu wa namna gani

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,304
46,118
Ukipewa nafasi ya uongozi iwe kwa kuchaguliwa, kuteuliwa au kwa kudra za Mwenyezi Mungu, inatoa nafasi nzuri na halisia ya watu unaowaongoza kukufahamu kiuhalisia wewe ni mtu wa namna gani. Nafasi utakayokuwa nayo inaweza kukuinua au kukuporomosha.

Tukirudi kwa kilichotokea baada ya Spika Ndugai kujiuzulu, na kisha wabunge kumchagua mwenzao mmoja, Dr. Tulia kuwa Spika, matarajio ya wengi ilikuwa pengine mabadiliko haya ya kumleta spika mpya, pamoja na Bunge kujaa wabunge wengi batili kwa mujibu wa katiba na sheria, kulikuwa na matarajio kuwa huenda Dr. Tulia angekuwa bora zaidi kuliko mtangulizi wake, kwa maana binadamu siku zote, kwenye mabadiliko, hutarajia kupata kilicho bora zaidi.

Bahati mbaya, nchi ilikuwa kwenye ubaya, kisha ikaenda kwenye ubaya zaidi.

Dr. Tulia, akiwa spika akatangaza wazi kuwa Bunge linapofanya kazi ni lazima lifuate matakwa ya Serikali. Na akatamka wazi kuwa Rais na Serikali ndiyo maboss wa Bunge.

Kama vile ilikuwa imepangwa, naye Jaji mkuu akawaambia majaji kuwa wakati wote wanapotoa hukumu wazingatie matakwa ya Serikali. Kauli hizi za wakubwa wa mihimili miwili, zikaufanya mhimili wa mahakama na mhimili wa Bunge kuwa idara za Serikali.

Kilichofuatia wote tumeshuhudia kazi ya Bunge na kazi ya kila mbunge akiwa bungeni ikawa ni kumsifu tu Rais na Serikali. Serikali na Rais iwe wametenda mema au mambo ya hovyo, Bunge chini ya Dr. Tulia kazi yake kubwa ikawa ni kusifu na kupitisha kila kitu kinacholetwa na Serikali Bungeni; na Dr. Tulia akizuia hoja zinazoonekana zinahoji utendaji wa Serikali. Wananchi wanakumbuka jinsi Spika Tulia, hivi karibuni, wakati watu wakitekwa na kupotezwa, alivyozuia Bunge lisijadili jambo hilo.

Na hiyo ilifuatia baada ya Rais Samia kudai kuwa utekaji haupo, na wanaotekwa ni drama. Hivyo Dr. Tulia kama mtu ambaye kazi yake ni kulifanya Bunge kuwa kama idara tu Serikali, alichokifanya ni kuisistiza kauli ya mkuu wake, hivyo naye akarudia maneno ya mkuu wake kwa lugha tofauti kuwa, kusiwe na hisia kuwa kila anayepotea ametekwa na Serikali. Baada ya kauli hiyo akazuia mjadala juu ya Watanzania wanaoikosoa serikali kutekwa na kupotezwa.

Lakini hayo yalifuatia tukio baya kabisa kwenye historia ya nchi yetu ambapo, Bunge chini ya Tulia, lilipitisha mkataba wa hovyo kabisa wa IGA unaopora sovereignity ya nchi. Mkataba ambao hata mtu asiyejua sheria, aliona wazi kabisa ni mkataba mbaya.

Mkataba huo ambao taasisi mbalimbali independent kuanzia TLS, watu binafsi wataalam waliobobea katika masuala ya kisheria na mikataba, taasisi za dini, baadhi ya viongozi wa kitaifa wastaafu, wote walitamka kwa uwazi kuwa IGA ile ilikuwa ya hovyo kabisa. Lakini Tulia, bila ya kujali maoni ya na hisia za wananchi, alihakikisha mkataba huo unapita, na mpaka sasa ni janga ambalo Taifa linaisha nalo, kwa sababu IGA hiyo haijabadilishwa hata nukta moja.

Walichofanya ni kwenda kutengeneza HIGA ambayo inaweza kumpumbaza mtu kuona mambo ni mazuri, wakati IGA imesimama vile vile, na wakati wowote DPW inaweza kuitumia. Kufuatia IGA hiyo, kuna kila dalili, huko mbeleni, Tanzania ikapatwa na yale yaliyoipata nchi ya Djibout, ambayo viongozi wake baada ya kupewa rushwa, nchi ikaingia kwenye mkataba wa kishenzi na DPW, baadaye wazalendo wakachachamaa, wakaamua kuvunja mkataba, DPW wakaenda mahakama za UK, kulingana na mkataba waliousaini, Djibout ikahukumiwa kuilipa DPW zaidi ya dola za Marekani milioni 700.

Hata sisi kwa ubaya wa IGA iliyopo, kuna siku tutafika huko. Na hilo likitokea, mmoja wa wahusika muhimu watakaokuwa wameliletea hasara hiyo Taifa, ni Spika wa Bunge Dr. Tulia.

Matukio haya mabaya, ambayo yamelifanya Bunge kuwa chawa wa Rais na Serikali, yametupatia nafsi ya kufahamu kwa ukaribu na usahihi kuwa tuna Spika wa Bunge wa namna gani.

Na kwa haya aliyoyafanya Spika kwa Taifa hili, kuna haja kweli kuendelea na mtu huyu kwenye nafasi hiyo? Au kwa vile anaoenda sana kazi ya upambe, ingefaa akawa huku ikulu ambako kazi yake kubwa ingekuwa ni kumteyea Rais na Serikali?

Pia soma: Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin
 
matarajio kuwa huenda Dr. Tulia angekuwa bora zaidi kuliko mtangulizi wake, kwa maana binadamu siku zote, kwenye mabadiliko, hutarajia kupata kilicho bora zaidi.
naunga mkono hoja Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!
Dr. Tulia, akiwa spika akatangaza wazi kuwa Bunge linapofanya kazi ni lazima lifuate matakwa ya Serikali. Na akatamka wazi kuwa Rais na Serikali ndiyo maboss wa Bunge. Kama vile ilikuwa imepangwa, naye Jaji mkuu akawaambia majaji kuwa wakati wote wanapotoa hukumu wazingatie matakwa ya Serikali. Kauli hizi za wakubwa wa mihimili miwili, zikaufanya mhimili wa mahakama na mhimili wa Bunge kuwa idara za Serikali
Huu ni ukweli mchungu and this is not right, asante sana kulisemea hili, hili nami pia sio tuu nimelisemea, bali nimeliandikia Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?
Lakini hayo yalifuatia tukio baya kabisa kwenye historia ya nchi yetu ambapo, Bunge chini ya Tulia, lilipitisha mkataba wa hovyo kabisa wa IGA unaopora sovereignity ya nchi. Mkataba ambao hata mtu asiyejua sheria, aliona wazi kabisa ni mkataba mbaya. Mkataba huo ambao taasisi mbalimbali independent kuanzia TLS, watu binafsi wataalam waliobobea katika masuala ya kisheria na mikataba, taasisi za dini, baadhi ya viongozi wa kitaifa wastaafu, wote walitamka kwa uwazi kuwa IGA ile ilikuwa ya hovyo kabisa. Lakini Tulia, bila ya kujali maoni ya na hisia za wananchi, alihakikisha mkataba huo unapita, na mpaka sasa ni janga ambalo Taifa linaisha nalo, kwa sababu IGA hiyo haijabadilishwa hata nukta moja. Walichofanya ni kwenda kutengeneza HIGA ambayo inaweza kumpumbaza mtu kuona mambo ni mazuri, wakati IGA imesimama vile vile, na wakati wowote DPW inaweza kuitumia. Kufuatia IGA hiyo, kuna kila dalili, huko mbeleni, Tanzania ikapatwa na yale yaliyoipata nchi ya Djibout, ambayo viongozi wake baada ya kupewa rushwa, nchi ikaingia kwenye mkataba wa kishenzi na DPW, baadaye wazalendo wakachachamaa, wakaamua kuvunja mkataba, DPW wakaenda mahakama za UK, kulingana na mkataba waliousaini, Djibout ikahukumiwa kuilipa DPW zaidi ya dola za Marekani milioni 700. Hata sisi kwa ubaya wa IGA iliyopo, kuna siku tutafika huko. Na hilo likitokea, mmoja wa wahusika muhimu watakaokuwa wameliletea hasara hiyo Taifa, ni Spika wa Bunge Dr. Tulia.
Hili la IGA, hatukunyamaza ,tumesema sana
Kilichotokea behind the closed doors, waligundua ile IGA
ni batili hivyo they abandoned it kimya kimya bila kutangaza,ile HGA ni safi nzuri na legit ila ni siri。Walitekeleza ushauri huu Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?
Na hii sio mara ya kwanza Bunge letu kupitisha madudu ya ajabu wakiisha shtuliwa ni madudu, wanayasokomeza uvunguni kimya kimya
na kuyafuta kwenye hansard as if nothing happened !
baada ya kuwastua hapo waliufyata,azimio lao batili wakalisokomeza uvunguni kimya kimya wakaipokea ripoti ya CAG。
asante kwa hoja mujarab
P
 
Siku watu wakiamka kutoka kwenye huu usingizi mzito, tutapiga hatua kubwa. Nina hofu siku tukija kupata kiongozi ambaye yupo serious na maendeleo ya nchi, atakuta rasilimali zote muhimu zipo mikononi mwa mabeberu chini ya mikataba migumu ambayo haivunjiki.
Sijui kama hiyo siku itafika,inavyoonekana moshi wa mwengu unaozunguka nchi nzima ndo unaleta usingizi huo.
watu wote wamelewa moshi
 
UNYUMBU WA KISIASA, unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanao pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), a.k.a kujizima data, tuseme, kuahirisha kufikiri kizalendo
 
Kuna wazee wa hekima kama Jaji Warioba amewahi pia kulisemea hilo la wakuu wa mihimili kugeuka kuwa machawa wa Rais. Na akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa leo hii kila tukio analofanya Rais, spika na jaji mkuu utawakuta na wenyewe wapo. Sasa kama hilo tukio analolifanya Rais lilikuwa la hovyo au lipo kinyume cha katiba au sheria, spika atawezaje kwenda kuligomea Bungeni wakati na yeye alikuwepo kwenye tukio, na alipewa nafasi ya kuongea, ukalisifia jambo hilo?

Uchawa wa Spika na Jaji Mkui, unazidi kuliangamiza Taifa. Na Rais ili kuwamaliza nguvu kabisa, akaamua kuongeza muda wa Jaji mkuu kinyume cha sheria. Sasa kama jaji mkuu yupo kwenye nafasi hiyo kinyume cha sheria, muhimili wake utaweza kuhoji makosa ya Serikali?
 
Kuingia kwa Tulia kuwa Spika baada ya Ndungai ni sawa na ile kauli mbiu ya Simba Sorts Club ya UBAYA UBWELA. Ni sawa na kuruka mkojo na kukanyaga uharo.
Hakika. Umenena ukweli. Ni aheri angeendelea Ndugai kuliko huyu aliyeamua kuwa chawa wa Rais na Serikali. Chawa huwa hafikiri, anachojua ni kusifia tu, na kutumika. Dr. Tulia yupo bungeni kutumika na siyo kutathmini utendaji wa Serikali, na kuchukua hatua kwa maslahi ya umma. Anatumika kama kibaraka wa wenye nia mbaya ndani ya Serikali.
 
Kuna kitu watu nadhani wanakichanganya sana. Kufanya Tafsiri ya Kingereza ya neno Governement kuwa ni Serikali

Governement ipo na Pillars tatu:
1. Executive = Kwetu tunaita Serikari
2. Legislature = Bunge
3. Judiciary = Mahakama

Mkuu wa Gorvernment ni Rais wa Jamhuri ya muungana

Huu hapa mchoro unaonesha Three Pillars of the Givernement

1729489785244.png

Pascal Mayalla Ukiusoma mchoro huu na kuuelewa hautakuwa na shida sana. Mkuu wa nchi yeye ndiye kiongozi wa Serikali. Lakini Bunge na Mahakama zipo chini yake. Bams
 
Kuna wazee wa hekima kama Jaji Warioba amewahi pia kulisemea hilo la wakuu wa mihimili kugeuka kuwa machawa wa Rais. Na akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa leo hii kila tukio analofanya Rais, spika na jaji mkuu utawakuta na wenyewe wapo. Sasa kama hilo tukio analolifanya Rais lilikuwa la hovyo au lipo kinyume cha katiba au sheria, spika atawezaje kwenda kuligomea Bungeni wakati na yeye alikuwepo kwenye tukio, na alipewa nafasi ya kuongea, ukalisifia jambo hilo?

Uchawa wa Spika na Jaji Mkui, unazidi kuliangamiza Taifa. Na Rais ili kuwamaliza nguvu kabisa, akaamua kuongeza muda wa Jaji mkuu kinyume cha sheria. Sasa kama jaji mkuu yupo kwenye nafasi hiyo kinyume cha sheria, muhimili wake utaweza kuhoji makosa ya Serikali?
Kuhusu kuhoji, tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukivihoji utaambiwa kama umekua uondoke, hata kaka na dada yako, walimu, wachungaji, hawataki wahojiwe, matokeo yake jamii imeamua kuishi nayo kwenye ngazi zote za maisha, kuna wadau walihoji kuhusu tozo waliambiwa waende Burundi.

Washika tonge ndiyo hao wana tabia za unyumbu, ukiwa na hoja za kuwanyang'anya matonge utakipata cha mtema kuni, zama hizi uta tekwa na kupotezwa tena mchana kweupe kwa maana wanao kuteka wanajitambulisha tena mbele ya ndugu zako, majirani ama washikaji, watekaji ni kikosi maalum, wameshiba wengine wamejazia Minofu ya mwili, na wana magari mazuri.

Cha ajabu tume nyingi zinaundwa nyuma ya mikamera majibu ya hizo tume nyuma ya pazia, tume zikiundwa mnapiga makofi na waandishi wanaziiandika kwenye magazeti lakini majibu ya tume wanasahau kuandika
 
Kuna kitu watu nadhani wanakichanganya sana. Kufanya Tafsiri ya Kingereza ya neno Governement kuwa ni Serikali

Governement ipo na Pillars tatu:
1. Executive = Kwetu tunaita Serikari
2. Legislature = Bunge
3. Judiciary = Mahakama

Mkuu wa Gorvernment ni Rais wa Jamhuri ya muungana

Huu hapa mchoro unaonesha Three Pillars of the Givernement

View attachment 3131274
Pascal Mayalla Ukiusoma mchoro huu na kuuelewa hautakuwa na shida sana. Mkuu wa nchi yeye ndiye kiongozi wa Serikali. Lakini Bunge na Mahakama zipo chini yake. Bams
Kumbe serikali siyo mimi, wewe, yule na huyu nilie nae.

Tuna hitaji neno zuri zaidi la kutuwakilisha sisi ni nani, kwa mfumo huo kumbe tumepumbazwa muda mrefu kwamba serikali ni mimi na wewe

Wapiga kelele huambiwa tumieni wawakilishi wenu ambao ni wabunge na hao wabunge wakikengeuka
Kifuatacho ni kubung'aa

Wawakilishi kwa sasa ni bunge la CCM
 
Kuna kitu watu nadhani wanakichanganya sana. Kufanya Tafsiri ya Kingereza ya neno Governement kuwa ni Serikali

Governement ipo na Pillars tatu:
1. Executive = Kwetu tunaita Serikari
2. Legislature = Bunge
3. Judiciary = Mahakama

Mkuu wa Gorvernment ni Rais wa Jamhuri ya muungana

Huu hapa mchoro unaonesha Three Pillars of the Givernement

View attachment 3131274
Pascal Mayalla Ukiusoma mchoro huu na kuuelewa hautakuwa na shida sana. Mkuu wa nchi yeye ndiye kiongozi wa Serikali. Lakini Bunge na Mahakama zipo chini yake. Bams
asante kwa elimu hii

Ni duniani kote ndo utaratibu,au ni hapa kwetu?
Na kama ni duniani kote mbona Kenya wamumuwajibisha,makamu wa rais?
Na marekani kipindi cha Monica na rais wa zamani Bil Clinton
mbona rais aliponea padogo kuwa impiched?
 
Dunia ipo na nchi zaidi ya 150. Wewe unakodolea macho Marekani na Kenya tu. Je, nikikuita wewe mbumbumbu nitakuwa nimekosea? Yaani Tanzania ianze kuiga vitu vya failed state kama kenya!!? Ebo!!
 
Sawasawa, endelea kugala gala kwenye vumbi ukushukuru kazi iliyofanywa na kodi uliyoitoa,huo ndio usomi si ndio?
Je,nikiuliza kuna haja gani ya kusoma hadi ngazi ya upro-pesa alafu ukaishi jalalani mpaka aje mtu kukuokota na kukupa cheo(A.K.A ulaji)
huo usomi binafsi siuhitaji,ni heri niendelee kulima ilimradi nalipa kodi mnakula.
 
Maelezo yako hayahusiani na topic tunayoongelea
 
Ukipewa nafasi ya uongozi iwe kwa kuchaguliwa, kuteuliwa au kwa kudra za Mwenyezi Mungu, inatoa nafasi nzuri na halisia ya watu unaowaongoza kukufahamu kiuhalisia wewe ni mtu wa namna gani. Nafasi utakayokuwa nayo inaweza kukuinua au kukuporomosha.

Tukirudi kwa kilichotokea baada ya Spika Ndugai kujiuzulu, na kisha wabunge kumchagua mwenzao mmoja, Dr. Tulia kuwa Spika, matarajio ya wengi ilikuwa pengine mabadiliko haya ya kumleta spika mpya, pamoja na Bunge kujaa wabunge wengi batili kwa mujibu wa katiba na sheria, kulikuwa na matarajio kuwa huenda Dr. Tulia angekuwa bora zaidi kuliko mtangulizi wake, kwa maana binadamu siku zote, kwenye mabadiliko, hutarajia kupata kilicho bora zaidi.

Bahati mbaya, nchi ilikuwa kwenye ubaya, kisha ikaenda kwenye ubaya zaidi.

Dr. Tulia, akiwa spika akatangaza wazi kuwa Bunge linapofanya kazi ni lazima lifuate matakwa ya Serikali. Na akatamka wazi kuwa Rais na Serikali ndiyo maboss wa Bunge.

Kama vile ilikuwa imepangwa, naye Jaji mkuu akawaambia majaji kuwa wakati wote wanapotoa hukumu wazingatie matakwa ya Serikali. Kauli hizi za wakubwa wa mihimili miwili, zikaufanya mhimili wa mahakama na mhimili wa Bunge kuwa idara za Serikali.

Kilichofuatia wote tumeshuhudia kazi ya Bunge na kazi ya kila mbunge akiwa bungeni ikawa ni kumsifu tu Rais na Serikali. Serikali na Rais iwe wametenda mema au mambo ya hovyo, Bunge chini ya Dr. Tulia kazi yake kubwa ikawa ni kusifu na kupitisha kila kitu kinacholetwa na Serikali Bungeni; na Dr. Tulia akizuia hoja zinazoonekana zinahoji utendaji wa Serikali. Wananchi wanakumbuka jinsi Spika Tulia, hivi karibuni, wakati watu wakitekwa na kupotezwa, alivyozuia Bunge lisijadili jambo hilo.

Na hiyo ilifuatia baada ya Rais Samia kudai kuwa utekaji haupo, na wanaotekwa ni drama. Hivyo Dr. Tulia kama mtu ambaye kazi yake ni kulifanya Bunge kuwa kama idara tu Serikali, alichokifanya ni kuisistiza kauli ya mkuu wake, hivyo naye akarudia maneno ya mkuu wake kwa lugha tofauti kuwa, kusiwe na hisia kuwa kila anayepotea ametekwa na Serikali. Baada ya kauli hiyo akazuia mjadala juu ya Watanzania wanaoikosoa serikali kutekwa na kupotezwa.

Lakini hayo yalifuatia tukio baya kabisa kwenye historia ya nchi yetu ambapo, Bunge chini ya Tulia, lilipitisha mkataba wa hovyo kabisa wa IGA unaopora sovereignity ya nchi. Mkataba ambao hata mtu asiyejua sheria, aliona wazi kabisa ni mkataba mbaya.

Mkataba huo ambao taasisi mbalimbali independent kuanzia TLS, watu binafsi wataalam waliobobea katika masuala ya kisheria na mikataba, taasisi za dini, baadhi ya viongozi wa kitaifa wastaafu, wote walitamka kwa uwazi kuwa IGA ile ilikuwa ya hovyo kabisa. Lakini Tulia, bila ya kujali maoni ya na hisia za wananchi, alihakikisha mkataba huo unapita, na mpaka sasa ni janga ambalo Taifa linaisha nalo, kwa sababu IGA hiyo haijabadilishwa hata nukta moja.

Walichofanya ni kwenda kutengeneza HIGA ambayo inaweza kumpumbaza mtu kuona mambo ni mazuri, wakati IGA imesimama vile vile, na wakati wowote DPW inaweza kuitumia. Kufuatia IGA hiyo, kuna kila dalili, huko mbeleni, Tanzania ikapatwa na yale yaliyoipata nchi ya Djibout, ambayo viongozi wake baada ya kupewa rushwa, nchi ikaingia kwenye mkataba wa kishenzi na DPW, baadaye wazalendo wakachachamaa, wakaamua kuvunja mkataba, DPW wakaenda mahakama za UK, kulingana na mkataba waliousaini, Djibout ikahukumiwa kuilipa DPW zaidi ya dola za Marekani milioni 700.

Hata sisi kwa ubaya wa IGA iliyopo, kuna siku tutafika huko. Na hilo likitokea, mmoja wa wahusika muhimu watakaokuwa wameliletea hasara hiyo Taifa, ni Spika wa Bunge Dr. Tulia.

Matukio haya mabaya, ambayo yamelifanya Bunge kuwa chawa wa Rais na Serikali, yametupatia nafsi ya kufahamu kwa ukaribu na usahihi kuwa tuna Spika wa Bunge wa namna gani.

Na kwa haya aliyoyafanya Spika kwa Taifa hili, kuna haja kweli kuendelea na mtu huyu kwenye nafasi hiyo? Au kwa vile anaoenda sana kazi ya upambe, ingefaa akawa huku ikulu ambako kazi yake kubwa ingekuwa ni kumteyea Rais na Serikali?

Pia soma: Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin
Hapo kwenye suala la IGA umeharibu uhondo mzima wa mtiririko wa andiko lako. IGA imewapa haki DPW kuwekeza pale bandarini, lakini uwekezaji huo unazuia vipi wawekezaji wengine kuja na uwekezaji wao katika bandari zetu zilizobakia pamoja na kwenye magati mengine ya hapo hapo TPA?.

IGA ingekuwa na huo ubaya unaousema kiasi cha kupora uhuru wa Tanzania, huyo mwekezaji mwingine adani angeweza vipi kuwekeza hapo hapo TPA?. Siasa ni nyingi na zinapata mashiko kwa sababu ya uelewa wetu wa masuala ya sheria za kimataifa kuwa mdogo.
 
Back
Top Bottom