Usiyoyajua kuhusu kupotea kwa 'Submarine' ya Titan

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
399
Naamini utakuwa umepata kusikia tetesi nyingi juu ya hii taarifa ambayo imeteka sana vichwa vya habari kuhusu kupotea kwa manowari ndogo iliyokuwa imebaba watalii baadhi waliotaka kujaribu kwenda chini ya bahari kuangalia mabaki ya Meli kubwa ya Titanic iliyozama mwaka 1912.

Baada ya ajali kubwa ya kuzama kwa meli ya Titanic takribani miaka 111 iliyopita, hatimae Juni 18 mwaka huu 2023 kuna safari mpya ya watu watano ambao waliamua kuchukua chombo kidogo cha usafiri kilichopewa jina la Titan Submarine ambacho kilitengenezwa chini ya kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya usafiri wa majini, kampuni hiyo inaitwa OceanGate Expedition

Safari hiyo ilianza siku ya jumapili, na hadi hivi sasa hakuna hata mmoja aliyepona wote wakisemekana kuwa wamefariki dunia. Miongoni mwa watu hao watano waliokufa ni pamoja na tajiri mwenye asili ya Pakistani anaeitwa Shahzada Dawood aliyekuwa akikadiriwa kuwa na utajiri wa shilingi USD million 350 (sawa na zaidi ya trillion 1.4 za kitanzania). Tajiri huyo alikuwa ameambatana na mwanae Suleman Dawood mwanachuo aliyekuwa akisomea masomo ya biashara mwenye umri wa miaka 19 aliyetoka kuhitimu mwaka wa kwanza wa masomo katika chuo cha Glasgow, Scotland. Watatu katika safari hiyo ni Hamish Harding, wanne ni Paul-Henri Nargeolet na watano ni Stockton Rush huyu ndie CEO wa OceanGate (kampuni iliyotengeneza manowari hiyo).

Sasa utamu unaanzia hapa:
Kampuni ya OceanGate Expedition, haikuwa mara ya kwanza kutengeneza manowari hii ambayo imezama hivi sasa. Waliwahi kufanya hivyo takribani mara tatu na walifanikiwa kuwapeleka watalii zaidi ya 200 chini ya kina kirefu cha maji katika bahari ya Pacific, Atlantic na Gulf of Mexico. Lakini katika safari hizo zote, hii manowari iliyozama ndio safari ndefu kuliko hizo zote zilizofanyika maana ilitakiwa kwenda chini kina cha mita 4000 sawa sawa na futi 13000 ili kuweza kuona masalia ya meli hiyo ya Titanic.

... Itaendelea sehemu ya pili .. 27%
Wako katika kalamu AMANI DIMILE
#amanidimile
InShot_20230623_195942710.jpg


Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Hiv meter 3000 au fut 13000 ni sawa na kilometer ngapi au umbali wa kuanzia dar es salaam mpaka wapi iki nijue umbali wa kima cha hayo maji.
Kwa makadirio ya viwanja vya mpira wa miguu 37 kutoka goli hadi goli ukiwa umeviunganisha, David Lochridge aliwahi kusema ni kweli mlima Everest ni mrefu kuliko yote duniani lakini kina cha meli ya Titanic ilipozama mlima Everest unaingia wote

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
😂😂😂😂😂😂😂😂
Itaendelea kuzama
Big bang implosion

Bahari ni lidubwasha kubwa sana la hatari haswa kwenye vina vya chini.

Ile submersible vessel ilichofanywa na kina cha bahari ni sawa na kuchukua jinyundo kubwa na kubonda pipi ya ivory kwa hasira zote.

Hata waliokwepo mule ndani hawawezi pata maumivu yoyote maana ni tukio linalotokea chini ya sekunde moja.
 

Itaendelea kuzama
Big bang implosion

Bahari ni lidubwasha kubwa sana la hatari haswa kwenye vina vya chini.

Ile submersible vessel ilichofanywa na kina cha bahari ni sawa na kuchukua jinyundo kubwa na kubonda pipi ya ivory kwa hasira zote.

Hata waliokwepo mule ndani hawawezi pata maumivu yoyote maana ni tukio linalotokea chini ya sekunde moja.


Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom