Usitafute Uhuru, maana Uhuru wa kweli Upo kaburini

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,960
18,515
Maana ya Uhuru, huisha baada ya utambuzi,
Baada ya kutambua kuwa uhuru si maamuzi,
Maana kifungo na mipaka vinafanana,
Aliyekuambia kuna uhuru, Utaupata Kakudanganya.

Kuna asili inayofanya,Mwili wako mashine,
Kufanya ugongwa uwe jela,halafu afya ni jela nyingine,

Mjamaa amemwaga damu tayari,Awe huru ili akawe,Mtumwa kwa mabenpari

Chagua kufa ukiona waja,Hawaliipi wema,
Kufa wokovu kilichokufa hakifii tena,
Kufa ni uhuru kamili tabu ni nini?
Haupo huru sasa,Uhuru wa kweli ni kaburini.

Unakumbatia uhuru wa kuambiwa?
Wakati unaishi Na haukuchagua kuzaliwa...

Uhuru hautafutwi Msafiri, pumzika kubali Chai
Hauwezi kuwa huru ungalI hai,

Uhuru si halisi jamaa Badili umbo,
Uhuru sio jibu hata Usikariri fumbo
Uhuru ni falsafa Ya vitabu, iliyoandikwa Na mababu,
Tutaisoma na mwisho itabaki huko..

Anayehitaji uhuru Aelewe..
Kuogopa kufa ni utumwa Kwa maana Kufa Ndio uhuru wenyewe..,
Hata uwe mfalme ambaye Anatoa idhini Huwezi kuwa huru..Uhuru wa kweli ni kaburini

Ukikumbatia mwanga Jua utaificha nuru,
Uhuru si kwa Mwafrika Kumkimbiza mkaburu,
Kuutaka uhuru sana jamaa Si dalili njema,
Ka' upo hai na Unajisikia uko huru Fikiri tena,

Cheo huleta nuru Pahala nuru haipiti,
Na pesa ndio njia Ya uhuru ukiimiliki,
Pesa na cheo hupita Kote hakuingii,
Alisema mlevi mmoja Ambaye pombe tu imemdhibiti..
Mwathirika ambaye dawa Za kulevya zimemfunga,
Na anahisi yuko huru Mara baada tu ya kuvuta,

Labda si kweli Haupo huru ukijiongezea,
Maana ukishaujua uhuru Tayari ushapoteza,
Je, utaniona chizi au mwizi Ama mshenzi au pumbavu Ninayeongea vituko,

Au utaamua kukaa Chini utafakari kisha ukakubali, Ndoa, ajira Navyo pia vifungo,

Aliye huru ni nani Nieleze,
Mtoto anayeenda Kwa viboko?

Au mlokoke mtenda mema Baada ya kutishiwa moto?

Au msomi ambaye elimu, Mpaka chuo Kihakiki


I swear...Kama uhuru ndio huo Siuafiki,
Anayejisikia yuko huru Pita mbele
Piga kelele

Hata Mungu wako Bado hayuko huru
Hawezi kubadilisha mipango
Hawezi kumuumba Mungu mwingine Mkubwa kupita yeye,

Unayetafuta uhuru Wa kweli utateseka,
Utapoteza damu Utatoa machozi Na utakesha,

Hauwezi kuupata Maana hakuna ulipoiweka,
Uhuru haupatikani kwa Fedha
Uhuru is priceless

Kwa kuwa si bidhaa Halisi

Utaniangusha sana Ukishindea kuamini..,
Upo Uhuru Ila Uhuru wa kweli ni Kaburini..

CC: Mdogo wangu Dizasta Vina
 
Back
Top Bottom