Usisome kozi ya clinical medicine (clinical officer) kabla ya kusoma thread hii

msafi WCB

Member
Jan 2, 2020
36
99
Kijana uliemaliza kidato cha nne au cha sita.. kabla ya kufanya maamuzi ya kusoma Diploma in clinical medicine yajue haya.

Clinical medicine ni kozi ya diploma ya utabibu (udaktari) ukisoma hii kozi utaweza kutibu baadhi ya magonjwa na kufanya upasuaji mdogo mdogo, kozi hii ni ya miaka mi 3. Kozi hii kwasasa inatolewa na vyuo zaidi ya 82 nchini.

Malengo makubwa mawili huwa yanafanya watu kusoma clinical medicine aidha kupata ajira wakiamini kua afya ina ajira nyingi na pili kujiendeleza kusoma udaktari wa binadamu (kwa ukubwa) au kozi zingine.

Hivi vyuo 82 vimekua viki dahili wanafunzi zaid ya 50 vingine 100 mpk 150 kwa mwaka. Sasa tuchukulie katika kila chuo kati ya hvyo 82 wahitimu clinical officers 50 (wastani) ina maana ni zaidi ya clinical officers 4100 wanazalishwa kila mwaka.
Kwa malengo ya kupata ajira za serikalini, serikali haijawahi kuajiri zaid ya clinical officer 2500 kwa mwaka tangu 2020 na kila mwaka idadi ya kuwaajir clinical officer inazid kushuka.

Kwa lengo la kusoma udaktari kwa ngazi ya digrii .. kwanza watambue vyuo vinavyoa digrii ya udaktar hapa nchini vipo 11. Na kila chuo kina idadi maalumu ya watahiniwa kutoka clinical medicine watakao jiunga. Vyuo hivo vya serikali ni vi nne 1.Muhas 2.Udom 3.Udsm- mchas mbeya 4. Suza zanzibar hivi vya serikali ada ni nafuu 1.8 million mpk 3.1 million (kwa suza). Nafac kwenye hivi vyuo zina badirika kutokana na mwaka husika (TCU guide book huonesha number of sits) lakin hazi zidi nafasi 70 kwa vyuo vyote kwa ujumla. Kwa hiyo ww clinical officer ulihitim jua kua unagombania nafasi zisizo zidi 70 kupata nafasi ya kusoma udaktari kwenye chuo cha serikali ... Hapa lazima ume na GPA kuanzia 4.8 mpaka 5.0 na matokeo ya kidato cha nne yawe mazuri kupata nafasi.

Vyuo vya private na ada zake kwenye mabano 1.Sfuchas ifakara (4.5 million) 2.St joseph boko (6.1 million) 3. Mwanza university (6.7 million) 4.Bugando (5.4 million) 5. Kcmuco (5.4 million) 6.kampala (6.7 million) 7.habert kairuki(6.7 million) . Huku kwa ujumla nafasi hufika mpka 200 kutegemeana na mwaka (TCU guide book number of sits) kwaio kwa upande wa private jua unagombania nafasi 200 au pungufu na clinical officer wenzio kupata nafac ya kusoma udaktari lkn Ada huku ndo kikwazo kingine kwa watoto wa maskini. KWA UJUMLA KWA SASA NAFASI ZA CLINICAL OFFICER KUSOMA MD HAPA NCHINI HAZIFIKI 300.

Habar njema ni kua kuna kozi zingine kama 15 hutegemeana na guidebook ya mwaka husika 1. Clinical nutrition Udom 2. Health information sciences Udom 3. Bsc general nutrition open university 4. Bsc human nutrition SUA 5. Law moshi ushirika 6. Microbiology udsm 7. Biotechnology udsm 8.sociology 9.health management systems mzumbe 10. Family and consumer science SUA 11.physiotherapy 12.public health Zanzibar 13. Counseling and psychology 14. Dental surgery suza na n.k

Swala la kujiajiri .. cheti cha clinical officer hakiwezi kutumika kufungua chochote iwe zahanati, duka la dawa au maabara. Zahanati ni kuanzia ngazi ya AMO ndio unaweza fungua.

Fursa nyingine iliopo ni kuajiriwa private ambapo kwa sasa wamekua wanalipa watakavyo unakata CO analipwa 150k au 200k kama anafanya kazi za ndani. Inaudhi sana.

Sku hzi kwenye kila watu 100 hukosi clinical officer mmoja wamekua wengi sana. Wengine wamekua madaktari TIKTOK sasa ni mwendo wa live tu

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Serikali imeharibu hzi kozi za CO kwa kuruhusu udahili wa uwe alama D ...yahn serious mtu anaenda kusomea utabibu kwa kupata alama D.Nina experiences ya kufundisha mtu anayepata D huwa na uwezo mdogo sana wa kureason mambo na wengi huwa wanapata divisions 3.ukimpata mtu anasoma CO kwa selection ya alama D halafu kapata division 1 nimekaa pale.
 
Kikubwa hugongwi na gari ukivuka barabara hiyo inatosha
 
Serikali imeharibu hzi kozi za CO kwa kuruhusu udahili wa uwe alama D ...yahn serious mtu anaenda kusomea utabibu kwa kupata alama D.Nina experiences ya kufundisha mtu anayepata D huwa na uwezo mdogo sana wa kureason mambo na wengi huwa wanapata divisions 3.ukimpata mtu anasoma CO kwa selection ya alama D halafu kapata division 1 nimekaa pale.
Ndugu, usidharau hizo D, hawa husoma na kupata uzoefu kisha huendelea. Wewe utamkataa kwa vile unamjua. Ila hiwa ni waoga kufanya makosa.

Kuna jamaa naowafahamu leo mmoja ni specialist anamalizia mafunzo amezunguka hizo njia ndefu.

Muhimu ni kuhakikisha hivi vyuo vinakuwa sio vingi ili kulinda ubora wao.
 
Mkuu quality ya D ya 2015 kushuka chini......ni tofauti na quality ya D hzi za miaka hii....miaka hii ya one za saba kama njugu ukipata D sawa na hamna kitu
 
Back
Top Bottom