Usipodai risiti jela miaka mitatu au faini ya shilingi milioni 3

Atakuwa alipitisha yule mbunge aliyeporwa balaghashia yake. Hata anayetunga Sheria kama hiyo na kuipeleka bungeni ni kutilia shaka. Au ndio mambo ya kutumia ubabe kila kona utanyimwa ushirikiano mahakamani maana huwezi kutumia ubabe kupata mashahidi kuthibitisha mtu amegoma kudai risiti na Sheria nzima itaonekana Ni wastage of time and resources
 
Bora umeliona hilo. Kuna watu akili zao zipo likizo

Risiti hainunuliwi: ukishalipia bidhaa zako dai risiti

Ukiwa na akili timamu utabaini kuwa muanzisha mada alikusudia tu KUDAI RISITI, lakini kwa kuwa ubongo ni wa rangi ya kijani basi huwezi ku-connect dots. Bora akili iliyoenda likizo baadaye itarudi kuliko ubongo uliokufa.
 
Mimi nimenunua chapati kutoka kwa mama lishe mtaani.....risiti anatoa wapi? analipa kodi ya genge kwa serikali ya mtaa....unga wa ngano na mafuta ananunua kwa kulipia kodi ndani yake...hajui kitu inaitwa risiti.

sheria inatakiwa kusema wananchi watake risiti za TRA kwenye bidhaa ........zitajwe. sio nikinunua bamia nidai risiti.
 
Watakuwa wanapita majumbani kukagua bidhaa zilizonunuliwa kwa siku hiyo? Watakuwa wanasimamisha watu barabarani kukagua mifuko yao kuangalia bidhaa na kuuliza risiti au watakuwa wamejipanga kwenye maduka yote nchini kukagua wateja wanunuapo bidhaa? Sio lazima kila siku watoke na matamko hata wakikaa kimya tunajua wao ndio watawala, yamezidi sasa.
 
Sheria hiyo bado haijapitishwa na Bunge. Itajadiliwa na kupitishwa katika kikao hiki cha bunge. Hata hivyo, naipongeza sana Serikali kwa kupeleka muswada wa sheria hiyo
unaipongeza serikali kwa kupeleka muswada wa sheria hiyo............................
 
Kwa majitu majinga yaliyozoea ku-bargain Bei na wenye maduka yatapinga hii hatua.

unakuta mwenye duka anakwambia " Ukitaka na risit ya EFD Bei ni 30000 Ukitaka bila risit ya EFD ni 15000,
 
Rais hajui nchi inapoelekea... Kiranga ni uongo?
I am sure even if you ask him. He will never deliver the concrete answer... He doesnt have any plan... Kama ni kodi anazikisanya kutoka kwa nani? Biashara zinafungwa hakuna pesa, purchasing power ya watu imepungua sana, bar na restaurant zinafungwa mapema sana.
Where is he going to collect taxes? From cigarettes?
***
hapo penye bold hapana million 7 kweli?.
 
Wameangalia kuhusu Network maana unaweza kudai risiti muuzaji anamuambia network inasumbua
je atasubiri mpaka saa ngapi..!?
 
Rais hajui nchi inapoelekea... Kiranga ni uongo?
I am sure even if you ask him. He will never deliver the concrete answer... He doesnt have any plan... Kama ni kodi anazikisanya kutoka kwa nani? Biashara zinafungwa hakuna pesa, purchasing power ya watu imepungua sana, bar na restaurant zinafungwa mapema sana.
Where is he going to collect taxes? From cigarettes?

Kujua kiingereza siyo uthibitisho wa hoja inayojadiliwa.Niambie rais amepunguzaje uwezo wa wananchi kununua? Je turuhusu kila aina ya biashara ifanywe kihuni ili serikali iweze kukusanya mapato zaidi kirahisi? Turuhusu gongo,bangi,ukahaba, ushoga,mirungi,Cocaine,mandrax nk maana vitawawezesha baadhi yetu wapate fedha zaidi?
 
Back
Top Bottom