Usimwamini Mwanamke asiye mama yako

Yaani unapelekwa puta na kitoto cha form 4??
Hivi vitoto saivi si vinamaliza four na miaka 15.

Mtoto kama huyo hahitaji ndoa anahitaji starehe, ndoa ataitala tu mwenyewe umri wake ukifika. Wewe hutakiwi kumlazimishia ndoa bado ni mdogo kabisa huyo.
 
Kwa hiyo ulikuwa na underage......

Siku hizi form.four ni miaka 16


Unategemea utimize ahadi na mtoto wa miaka 16.....

Then miaka 3 baadae...akiwa 19 umuoe

Mjomba???!!!!!
 
Kama mwanamke uliyemuoa umepangiwa na Mungu, ni sehemu ya mwili yako, amebeba maisha yako, hivyo unabidi uwe na Imani nae.
 
Unapima upendo kwa kitoto cha form four?

Alikuwa hajakuwa tu huyo, kwa sasa amekuwa kapata wa size yake.

Mwisho, acha
kusingizia wanawake wote eti kasoro mama mzazi. Wapo wadada wanaojielewa
Siyo kukua.
Hata huyo mkeo ukimsomesha atakuja kukuambia yeye siyo size yake.
 
Habar za leo wana JF,

Mwenzenu nimepata changamoto ambayo asilimia kubwa ya sisi vijana tunaipitia haswa kwenye ishu ya mahusiano.

Kuna mdada tulipendana nae mwaka 2020, tunapendana kama mbwa na mkia wake, na kipindi hiko alikuwa amehitimu kidato cha nne. Tuliweka malengo na akawa sehemu kubwa sana ya kila hatua nayoipiga kuyakimbilia mafanikio.

Matokeo yalipotoka alienda mbali na mimi na kwa kuwa mimi nilimpenda nikahamisha biashara na makazi yangu mahali karibu.

Tuliweka malengo ya kuoana ifikapo 2023 lakini kadri siku zilivyozidi kusogea kwenye ratiba alibadilika na kila anapoambiwa kuhusu suala la kuoa anakuwa mkali, mwisho wa siku kaishia kunidanganya ya kuwa wazazi wake wamekataaa.

Namshukuru Mungu na kumshukuru huyu binti kwa sababu nimejifunza maisha ambayo sikutegemea kama ningejifunza mahali pengine popote zaidi ya kupitia haya nilioyapitia.

Hawa madada tuwapende ila tusisahau.

Songoroka.
umeshajaza fomu za bodi ya mikopo ya elimu ya juu?? Nenda chuo ukasome. Binti wa kidato cha nne bado ni mtoto, she is still growing up na unajitafutia kifungo cha maisha.
 
Sisomesh ila nilipaswa kumsubiri amalize masomo
Akili ya mwanamke iko hivi.
Mwanamke kadri anavyozidi kupata mafanikio hutafuta mtu mwenye mafanikio makubwa zaidi. Tamaa yake inazidi kuongezeka zaidi na zaidi.
Ukiwa na gari la kawaida, hutamani apate mtu mwenye benzi.
Ukiwa na elimu ya form 4 au form 6, ukamsomesha huyu mwanamke mpk akafika chuo. Hutakuja umuoe abadani. Atatafuta mtu mwenye elimu sawa na yake au zaidi
 
Akili ya mwanamke iko hivi.
Mwanamke kadri anavyozidi kupata mafanikio hutafuta mtu mwenye mafanikio makubwa zaidi. Tamaa yake inazidi kuongezeka zaidi na zaidi.
Ukiwa na gari la kawaida, hutamani apate mtu mwenye benzi.
Ukiwa na elimu ya form 4 au form 6, ukamsomesha huyu mwanamke mpk akafika chuo. Hutakuja umuoe abadani. Atatafuta mtu mwenye elimu sawa na yake au zaidi
Kiuhalisia mm nina elimu kumshinda, na wakati nipo nae nilikuwa sijapata kazi ila kwa sasa nina kazi ila kama ulivyosema tamaa ndy inawaandama hawa wenzetu wa kushoto
 
Back
Top Bottom