SoC01 Usikate tamaa (never give up)

Stories of Change - 2021 Competition

Eng_Mwakibuti

Member
Sep 14, 2021
6
7
inbound2103759028300199539.jpg

Habari.

Hii ni kwavijana na wapambanaji wenzangu. Hizo picha happy juu Ni safari ya mafanikio ya maisha yangu.

Mimi Ni kijana niliye zaliwa kwenye familia masikini, nikasoma katika shule za selikari kwa shida sana.

Hatabaada ya kumaliza masomo, sijawai pata kazi ya kuajiriwa. Nimelelewa na mama yangu akiwa na watoto 6. Hatukuwajua baba zetu.

Mama yetu alikuwa ni mama ntilie, akipika vyakula mbalimbali huko Mbagara Kiburugwa, eneo linaitwa Kona bar (Dar es Salaam). Asubui alikuwa akiuza vitumbua, wakati mwingine chapati na maharage. Mchana akiuza chakula na jioni akiuza supu ya makongoro.

Alijituma mchana na usiku ilikutupatia chakula na alitamani sana watoto wake tusome na kupata kazi nzuri.

Kwa taabu sana alifanikiwa kutupeleka watoto wake wote 5 shule ya msingi. Mdogo wetu mmoja alifariki akiwa mchanga.

Mama yetu alifariki tukiwa bado tu wadogo, mi nilikuwa dalasa la pili 2002, nikiwa naiaka 12. Ndoto ya mama yetu kuona wanae tunasoma na kuwa na kazinzuri ikazimika, akapumzika.

Watoto tukatawanyika wengine kwa ndugu, na wengine tukawasaka baba zetu. Mimi nikampata Baba yangu mkoani Arusha. Baba yangu alikuwa ameoa na anamtoto mmoja.

Maisha ya kuwa na mama mwingine hayakuwa rahisi kwangu. Kwa taabu na misukosuko nikafanikiwa kumaliza elimu ya msingi.

Kutokana na sababu mbalimbali sikuweza kuenda secondary, hivyo nilitafuta kujifunza fani mbalimbali na kuanza kujiajiri.

Kwenye picha ya kwanza hapo juu, nilikuwa nikifanyia kazi zangu ndani kwangu. Nilianza kwa kupika vitafunwa na kuuza kwenye shule za mzingi. Huku nikichezesha Game kwa watoto sebureni kwangu.

Nilijichanga mpaka nikapata hicho kibanda kwenye picha ya pili happy juu. Hivyo kazi zikaamia kwa kibanda. Niliendelea na kazi zangu za upishi huku nikitengeneza simu na vifaa vya umeme.

Nikiwa naendelea na kazi zangu kibandani, nilijifunza kupamba (kanisani) hivyo nilianza kupata kazi za kupamba ndogo ndogo. Hii ilinisaidia kukuza mtaji wangu.

Kupitia kazi ya kupamba niliamua kujaribu kutimiza ndoto ya mama ya kusoma na kupata kazi nzuri (yenye mshahara mzuri). Hivyo niliamua kusoma.

Nilienda kujiandikisha kusoma masomo ya QT mwaka 2012 nikafanya mtiani wa form 4 na kuambulia D nne. Ambazo zilinisaidia kujiunga chuo cha ufundi (KILIMANJARO INTERNATIONAL INSTITUTES FOR TELECOMMUNICATIONS ELECTRONICS AND COMPUTER). Ambako ilikuwa Ni ndoto yangu kusoma hapo. Nilia apply 2014 nikakosa nafasi, sikukata tamaa. Mwaka uliofuata 2015 nilifanikiwa kujiunga na Diploma.

Nilisoma kwa miaka 3, nikijisomesha mwenyewe kupitia kibanda changu na kazi za kupamba. Haikuwa rahisi maana chuoni (KIITEC) tulikuwa tunaingia asubui saa mbili na kutoka saa kumi na moja jioni.

Hivyo muda wa kufanya kazi zangu ni baada ya kutoka chuo na siku za jumamosi na juma pili.

Mwaka 2018 nilifanikiwa kumaliza masomo yangu
inbound9058513855616024148.jpg

Nilipo kuwa chuoni tulipewa uhakika mkubwa sana wa kupata ajira. Hukutuki oneshwa mifano kwa waliosoma happy chuoni na kupata kazi nzuri. Hii ilitufanya kuamini kwamba tukimaliza chuo kazi ipo.

Mara baada ya kumaliza masomo, niliingia kutafuta ajira. Nilizunguka huku na huko bila mafanikio. Niliamua kurudi kitaa na kupambana kama zamani, nikipiak mikate na vitafunzwa vibgine.

Huku nikiuza bidhaa mbalimbali Kariakoo. Nilifanya hivyo maana kibanda nilishakigawa kwa kuamini naenda kuajiriwa na kupata mshahara mkubwa.

Tenda za kupamba nazo zilipotea maana niliama mkoa (kutoka Arusha kwenda Dar), hivyo nikapoteza wateja.

Nilipambana kukuza mtaji ili nifungue ofisi ya ufundi Computer. Maana ndicho nilichosomea na nilikuwa napenda ufundi zaidi. Nilifanikiwa kuungana na jamaa mmoja huko dar nikwa nafanyia kazi zangu za ufundi ofisini kwake (Manzese Tip-Top).

Baada ya mwaka mmoja kupita 2019 niliamua kurudi Arusha. Maana maisha ya kupambana Dar yalikuwa siyo rahisi.

Nilirudi Arusha na kufungua ofisi ya ufundi Computer, Umeme na simu
inbound5704819457226796113.jpg

Kupitia ofisi hii ambayo ilianza kazi 2020, nimeweza kuinua kipato changu kwa zaidi ya 75% ya kipato nilichokuwa nakipata mwanzo.

Pia siyo kwangu tu kupitia ofisi hii imetoa ajira kwa vijana waliojifunza kazi chini yangu zaidi ya wanna.

NINI NATAKA UJIFUNZE KUPITIA HISTORIA HII YA MAISHA YANGU?

1. USIKATE TAMAA
2. HAIJARISHI UMESOMA AU LAA, UKIAMUA UNAWEZA KUFIKA MBALI
3. HATAKAMA UMESOMA USICHAGUE KAZI.
4. USIKATETAMAA KUIPAMBANIA NDOTO YAKO.

Pamoja na mengii niliyo pitia sijakata tamaa, sijakata tamaa ya kutafuta pesa, sijakata tamaa ya kujiendeleza kielimu.

Nilipofika siyo mwisho Nina ndoto za kutika mbalizaidi ya hapanilipo.

USIKATE TAMAA PAMBANA.......
 
View attachment 1945256

View attachment 1945293

View attachment 1945308

Kupitia ofisi hii ambayo ilianza kazi 2020, nimeweza kuinua kipato changu kwa zaidi ya 75% ya kipato nilichokuwa nakipata mwanzo.

Pia siyo kwangu tu kupitia ofisi hii imetoa ajira kwa vijana waliojifunza kazi chini yangu zaidi ya wanna.

NINI NATAKA UJIFUNZE KUPITIA HISTORIA HII YA MAISHA YANGU?

1. USIKATE TAMAA
2. HAIJARISHI UMESOMA AU LAA, UKIAMUA UNAWEZA KUFIKA MBALI
3. HATAKAMA UMESOMA USICHAGUE KAZI.
4. USIKATETAMAA KUIPAMBANIA NDOTO YAKO.

Pamoja na mengii niliyo pitia sijakata tamaa, sijakata tamaa ya kutafuta pesa, sijakata tamaa ya kujiendeleza kielimu.

Nilipofika siyo mwisho Nina ndoto za kutika mbalizaidi ya hapanilipo.

USIKATE TAMAA PAMBANA.......
Hakuna kukata tamaa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hivi msiosoma mbona mnakuwa na inferiority complex, nani kakuambia kufanikiwa ni kusoma. Kufanikiwa ni ujanja wako wa kupata information Ili upate maarifa. Kufanikiwa sio vyeti tu ni zaidi ya vyeti. Mbio za mafanikio hazichagui wewe ni nani.
 
Back
Top Bottom