Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,314
Mtumishi hongera sana kwa ujumbe wako lakini sio leo wala Jana suala la mapenzi na mwanaume kudumu na mwanamke mmoja limekuwa "impossible".
Kwenye maandiko Mungu alimwinua Daudi kuwa mfalme wa wayahudi, akatenda yaliyo MEMA mbele za Mungu na Watu lakini ni Daudi huyu huyu alipora mke wa mtu kwa kumuua mumewe.
Mungu alimwinua Sulemani na kuwa mfalme wa Israel na zaidi ya yote akampa "Hekima na busara" kushinda watu wote. Mungu akamwonya asioe wanawake wa "mataifa" lakini hadi anakufa alikuwa na mahusiano na wanawake zaidi ya elfu moja akiwamo "Malkia wa Sheba", mwanamke wa nguvu kutoka Ethiopia.
Kumbuka pia ya Samson na Derila. Nadhani ni vizuri uinjilishaji ukaweka mkazo katika kuwahamasisha watu wafanye kazi kwa juhudi kubwa na maarifa. Tatizo ktk jamii zetu waafrika sio zinaa wala ngono. Tatizo ni UMASKINI wa kipato na fikra. Hilo mkilikazania hata Zaka na Sadaka zitaongezeka mara dufu malangoni pa Yahweh.
"Bwana kama wewe ungalihesabu makosa ni nani angesimama? Lakini kwako Kuna msamaha ili wewe uogopwe "