usalama kwanza
JF-Expert Member
- Oct 3, 2012
- 386
- 158
- Thread starter
- #21
Hakuna biashara ya kijinga kama ya hisa hasa kwa nchi kama Tanzania, ununue hisa 850, uanze kuomba Mungu ifikie 1600 ili uuuze, una uhakika gani hizo hisa kama hazitaporomoka? je itachukua muda gani kufikia hapo 1600, hizo dividends zinagaiwa kutokana na hela ulizo nazo na ni pesa ndogo sana ila kama ni mvivu na haujui lesa upeleke wapi au ufanyie nini nunua hisa...
Biashara ya kununua hisa nchi hii ni ya kuhatarisha hela yako tu, kama hela yenyewe ndio unategemea ni bora ufanye kitu kingine, nakumbuka mwaka 2009 mzazi wangu alinishauri ninunue hisa za UTT nikamwambia hapana akanipa darasa weee kwa kuwa yeye ni mchumi alisoma enzi za mkoloni akawa anajiona yupo sahihi kweli kuwa italipa sana, nikamwambia sitaki akaniona fala sana, hela hiyo hiyo nikaenda kununua kijishamba nje ya jiji la Arusha Nduruma karibu na Nelson Mandela university, sasa hivi kijishamba kina thamani mara 100 ya hizo hisa zake huko UTT., wanunue tu wanaopenda faida wakiwa wamekaa kwenye stuli ndefu., mimi sinunui ng'oo potelea mbali nitaendelea kuwaungisha vocha tu.
mara ya mwisho hisa za DSE zilipanda kutoka 500 mpaka 1200 , ndani ya muda mchache chini ya miezi miwili tangia iingie kwenye secondary market , sasa kwa hapo ni kwa waliouza hisa inamaana walipata mara mbili ya bei waliyonunulia. Fikiria umenunua hisa za 10M ndani ya miezi miwili una 20M.Hakuna biashara ya kijinga kama ya hisa hasa kwa nchi kama Tanzania, ununue hisa 850, uanze kuomba Mungu ifikie 1600 ili uuuze, una uhakika gani hizo hisa kama hazitaporomoka? je itachukua muda gani kufikia hapo 1600, hizo dividends zinagaiwa kutokana na hela ulizo nazo na ni pesa ndogo sana ila kama ni mvivu na haujui lesa upeleke wapi au ufanyie nini nunua hisa...