SoC04 Ushiriki wa wananchi katika maandalizi ya bajeti ya nchi: Njia bora kwa maendeleo endelevu

Tanzania Tuitakayo competition threads
Nov 23, 2022
57
63
Kila mwaka wa fedha, serikali huandaa na kuweka wazi makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha unaofuata. Licha ya umuhimu wake, swali kubwa linabaki kuwa ni kwa kiasi gani wananchi wanashiriki katika mchakato mzima wa maandalizi ya bajeti hizi? Bila shaka, upo umuhimu mkubwa wa ushiriki wa wananchi katika maandalizi ya bajeti ili kupata maoni yao, kufahamu mahitaji yao na hivyo itasaidia kufahamu vipaumbele vya wananchi.

Katika muktadha huu, ni wakati sasa wa serikali kuona umuhimu wa maoni ya wananchi na kuandaa hatua thabiti ili kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika mchakato huu muhimu. Zipo njia mbalimbali ambazo zinawesa kutumika ili kupata maoni ya wananchi katika maandalizi ya bajeti, njia hizo ni pamoja na;

Mikutano na midahalo ya maendeleo.

Kupitia mikutano na midahalo mbalimbali ya maendeleo, wananchi watapata nafasi ya kutoa maoni yao, mapendekezo pamoja vipaumbele vyao kuelekea mwaka wa fedha unaofuata. Mikutano hii inaweza kufanyika katika ngazi za kata ili kuwapa nafasi wananchi wa kawaida kupaza sauti zao juu ya nini wanatamani kifanyike katika mwaka wa fedha unaofuata.

Kwa uapande mwingine, Midahalo inaweza kuhusisha wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile watumishi wa umma/binafsi, wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu, mashirika ya umma na sekta binafsi. Hawa ni wadau muhimu wenye mawazo chanya kuhusu taifa lao. Kupitia mikutano na midahalo ya maendeleo, serikali itapata nafasi ya kuhamu vipaumbele na mahitaji ya wananchi. Midahalo itatoa nafasi ya ushiriki wa moja kwa moja kati ya wananchi na wawakilishi wa serikali au wataalamu wa masuala ya bajeti ili kuwafanya wananchi washiriki kikamilifu katika mchakato wa bajeti.

Katika hatua nyingine, midahalo ya maendeleo inatoa nafasi ya kupatikana kwa mawazo mapya na ubunifu kuhusu maandalizi na matumizi ya bajeti. Wananchi wanaweza kuleta mapendekezo yenye sura ya kipekee na yenye malengo chanya ambayo huenda yasifikiriwe na wataalamu wenyewe na hivyo kuboresha mipango ya bajeti.

Matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

Mifumo ya kielektiloniki na mitandao ya kijamii inaweza kuwa njia rahisi na ya uhakika katika kukusanya maoni na mapendekezo ya wananchi katika maandalizi ya bajeti. Mifumo ya ujumbe mfupi (SMS) inaweza kutumika ikiwa ni pamoja na matumizi ya “SSD CODE” yenye maelekezo kuhusu utoaji wa maoni. Kupitia mifumo hii, serikali itapokea maoni ya wananchi moja kwa moja na kuyafanyia uchambuzi ili kupata vipaumbele vya wananchi pamoja na mahitaji yao.

Kwa upande mwingine, serikali kupitia wizara ya fedha iangalie uwezekano wa kutengeneza programu (software) maalumu ambayo jukumu lake kubwa ni kukusanya maoni ya wananchi kuhusu maandalizi ya bajeti. Mfumo huu unaweza kuwa na sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mfumo wa uelewa wa bajeti (budget literacy system), jukwaa la kutoa maoni (feedback platforms), jukwaa la uchambuzi wa bajeti (budget analysis platforms) pamoja na jukwaa la mjadala wa umma (public debate platforms). Majukwaa haya ndani ya programu hii yatatoa nafasi kwa wananchi kukuza uelewa wao kuhusu mchakato wa bajeti, nafasi ya kutoa maoni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa bajeti katika kipindi husika.

Wakati gani wananchi watatoa maoni yao?

Mfumo huu wa utoaji maoni kutoka kwa wananchi unatakiwa kuwa endelevu ili kuwapa nafasi wananchi kufuatilia utekelezaji wa bajeti katika mwaka wa fedha husika huku wakitoa maoni nyao kuhusu nini wanatamani serikali ifanye kuelekea mwaka wa fedha unaofuata.

Utoaji wa maoni na mapendekezo kutoka kwa wananchi unaweza kuanza katika nusu ya mwaka wa fedha ikiwa ni muda wa miezi sita (6) kabla ya kuanza mwaka mwingine wa fedha. Kwa Tanzania, mwaka wa fedha huanza mwezi wa saba, hivyo ukusanyaji wa maoni kuhusu bajeti mpya unaweza kuanza mwezi wa kumi na mbili (12) ili kutoa nafasi kwa wizara na waandaaji wa bajeti kuchambua maoni ya wananchi na kupata vipaumbele vyao.

Umuhimu wa maoni ya wananchi katika mchakato wa bajeti.

  • Kutambua mahitaji ya msingi ya wananchi. Wananchi wanajua mahitaji yao ya msingi kuliko mtu mwingine yeyote. Hivyo ushiriki wao katika maandalizi ya bajeti utaisaidia serikali kupata ufahamu wa moja kwa moja kuhusu mahitaji na vipaumbele vya wananchi na inaweza kuisaidia serikali kuweka bajeti inayolingana na mahitaji halisi ya jamii.

The Citizen.JPG

kielelezo 1. 1 Mfano wa vipaumbele vya wananchi. Chanzo; The citizen

  • Ushiriki wa wananchi utasaidia kuimarisha uwazi na uwajibikaji. Kama ilivyoelezwa katika mfumo unaopendekezwa, ushiriki wa wananchi utasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya mali za umma pamoja na rasilimali zake. Wananchi wanaweza kufuatilia jinsi fedha zinavyotumika na kutoa maoni yao ili kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji wa serikali katika matumizi ya fedha za umma.
  • Ushiriki wa wananchi utasaidia kukuza ubunifu katika utekelezaji wa miradi. Maoni ya wananchi yanaweza kusaidia kuongeza ubunifu na mawazo mapya kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Wananchi watapata nafasi ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradi, na kutoa ushauri juu ya namna bora miradi hiyo inaweza kutekelezwa. Wananchi hawa wana ufahamu wa juu kuhusu changamoto za kila siku katika jamii hivyo wanaweza kutoa suluhisho bora zaidi kulingana na matatizo yanayoikabili jamii.
  • Ushiriki wa wananchi ni sehemu muhimu ya kuimarisha demokrasia katika nchi. Nafasi hii inawapa wananchi nafasi ya kupaza sauti zao kuhusu matumizi ya rasilimali za umma na kutoa maoni kuhusu namna bora ya kulijenga taifa kwa pamoja.
Hitimisho.

Kama ilivyoelezwa katika andiko hili, ushiriki wa wananchi katika mchakato wa maandalizi ya bajeti ya nchi ni muhimu sana ili kuimarisha uwazi, uwajibikaji, na ufanisi wa matumizi ya mali za umma. Programu maalumu za TEHAMA, mikutano na midahalo ya maendeleo ni baadhi ya njia zinazoweza kusaidia kuongeza ushiriki wa wananchi katika mchakato wa bajeti ya nchi. Ni wakati sahihi wa serikali kulitazama suala hili kwa upana wa aina yake kwa kuwekeza zaidi katika kuendeleza mifumo tajwa awali na mikakati ambayo itawezesha ushiriki wa wananchi katika maandalizi ya bajeti ya nchi ili kuhakikisha kuwa inaakisi mahitaji halisi na kukuza ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
 

Attachments

  • The Citizen.JPG
    The Citizen.JPG
    210.5 KB · Views: 16
The nonsense is beyond me.

Didn’t the ancient Greeks try that kind of democracy whereby each citizens can contribute and figured it doesn’t work (due wide variation of priorities) we need representatives to debate those matters.

Hivi unadhani ukienda huko Ruvuma vijijini wananchi watataka nini zaidi ya ruzuku ya Mbolea na ukienda Dar wananchi watataka nini zaidi ya serikali kukuza uzalishaji maana yake kupunguza kodi ili watu washawishike.

Sasa hizo mbolea utanunua na ruzuku gani kama walipa kodi wanataka zishushwe.

Ndio msingi wa wa somo la uchumi kuangalia njia sahihi ya kutumia limited financial resources ya nchi ku-maximise utility.

Budget yenyewe ina sources kwanza za income then you figure out expenditures.

Ujinga mtupu, gosh to think of the practicality challenges of deducing such information to make sense to decisions makers. Have you ever done or understand the challenges of sorting information to make sense in a primary interview research (and those are structured) interview. I can’t imagine challenges when people are allowed to free flow nationwide.

Kabisa una likes humu wakati kiwangi cha ujinga ulioanxika dah.
Naona unafanya doria sana kwenye hizi siredi za mashindano :D
Wapeleke polepole, unawapiga kata funua na combative arguments mwanzo mwisho
Jaribu kuwajibu na constructive alternative ya mawazo yao bila ya kuwa dismissive
 
Naona unafanya doria sana kwenye hizi siredi za mashindano :D
Wapeleke polepole, unawapiga kata funua na combative arguments mwanzo mwisho
Jaribu kuwajibu na constructive alternative ya mawazo yao bila ya kuwa dismissive
Kiongozi humu napita pita nikipata wasaa.

Naelewa criticism zangu haziwezi kuwa popular and harsh, lakini lazima tuambizane ukweli.

Imagine gharama za kukusanya watu watoe mawazo, idadi ya watu utakao hitaji ku-deduce maelezo ya wananchi.

Sasa hawa watu wanaotakiwa kuandika kwenye ili shindano ni wasomi ambao washaandika dissertation/s either za undergraduate and some post-graduate.

Wanajua ugumu wa research na wakachagua methodology zao ili kuandika walichoabdika.

Serikali pia inafanya research kwenye maamuzi yake. Hata hayo mapendekezo ya mleta ili yatumiwe kwenye budget ni kama research ya unstructured interview. Mwisho wa siku lazima kuwe na watu wa ku analyse mapendekezo na kujua vipaumbele vya watanzania.

Sasa huko shule lazima kafundishwa primary research kama hiyo ni expensive na inachukua muda hata kwa watu 10.000 inaweza kuwa kazi ya miaka miwili mitatu (ndio maana ni rare). Research nyingi za wananchi ni questionnaires tena ili iwe rahisi ku analyse ni structured questions na sample size ya watu 5000 mtihani kuhutimisha.

Sasa mtu ambae atapendekeza watu million 46 wasikilizwe kabla ya budget kupitishwa. Kuna sababu ya ku-encourage ujinga wake zaidi ya kumwambia ukweli that’s not possible.

Najua maono yangu sio popular humu, ingekuwa jukwaa la siasa unaacha. Lakini mtu ambae andiko lake anali nasibu kuwa la kisomi anastahili pia strong criticisms

Msomi gani anaweza kuwa na wazo la hovyo kama ili na watu wanasifia ujinga wake. Someone has to step in.

Kwa hizo mbinu zake za text messaging na online survey, walau ange-mention mambo ya AI, big data and data analytics kusaidia ningeelewa. Ila mtu ana rumble ujinga mwanzo mwisho umsifie ndio maana tupo hapa kama nchi sababu ya kusifiana ujinga.
 
Hakika, nchi inahitaji uwajibikaji, sio wa viongozi tu bali na wananchi katika kuchangia maendeleo endelevu ya taifa.
 
Back
Top Bottom