Ushauri wangu kwa Wasafi Media

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
449
826
Assalam wanajamvi!

Niende moja kwa moja kwenye hoja, kwa wiki kadhaa sasa nimekua nikifuatilia media ya Wasafi hasa TV kiukweli bado vipindi vyao havijakaa sawa.

Mwanzo walipokuja watangazaji nguli nilijua content za pale zitabadilika, lakini kumbe na mimi nilikuwa na mawazo ambayo hayakuwa sahihi kama kwa aliekuja na wazo la kuwachukua watangazaji hao.

Ushauri wangu ni huu, lazima tukubali kuwa ulimwengu wa sasa umebadilika, si ulimwengu ule wa miaka minne mitano ya nyuma, usikidharau kizazi cha sasa, wapo vijana wenye content nzuri, na wapo mtaani tuu wanafanya shughuli zao tofauti na walizosomea, bila undugu wala urafiki itisha interview kusaka vijana wa kukuongozea jahazi, mishahara yao haitakuwa mikubwa sana, wape kazi! nenda nao taratibu, wape semina za mara kwa mara kuhusu jinsi ya kutoa content za maana!! hakika utatoboa, lakini vinginevyo hivi hakuna ubunifu, kwa siku kuna baadhi ya nyimbo zinapigwa karibia mara 10, ni majanga!!

Kila la kheri!!
 
Bado wanaangalia umaarufu wa Instagram wa mtu ndo unapewa kazi pale , ni Jambo Jema ili kuifanya media ifatiliwe , Ila hao watu maarufu Sana Sana hawana content na ubunifu , ni kupayuka tuuu na memes zao za instagram , hvyo wanatakiwa wapewe backup na watu wenye taaluma zao na wenye vipaji pia ....!!! Ushauri mzur
 
Kwa issue ya content ni channels nyingi tu hasa hizi za vijana hapa nchini hazina maudhui. Na ndio maana muda mwingi wanapiga music.

Ingawa kwa sasa inahitajika nguvu ya ziada kumfanya mtu akae aangalie kipindi cha TV. Na ndio maana wanachukua watu wenye ushawishi ambao bahati mbaya nao katika ubunifu wanakwama.
 
Back
Top Bottom