SoC01 Ushauri wangu kwa Serikali kupitia TRA

Stories of Change - 2021 Competition

guojr

Member
Dec 4, 2015
62
95
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Nianze na angalizo kuhusu andiko langu hili kuwa sio la kielemu wala kitaalam ni mawazo yangu binafsi ninavyotamani kuona kama yanaweza kuonesha njia ya mabadiliko kwenye ukusanyaji wa mapato nchini. Nikirejea motto wa mamlaka ya mapato Tanzania unaosema pamoja tunajenga taifa letu na ukisisitiza ukinunua dai risiti na unapouza toa risiti. Ni ukweli usiopingika kuwa Serikali inaonekana imekosa kabisa vyanzo vipya vya kukusanya mapato kiasi ambacho inaona hakuna namna nyingine zaidi ya kuendelea kumkamua mwananchi kwa kile kidogo alichonacho hasa kwenye maeneo ambayo Serikali inajua kabisa Mwananchi hawezi kukwepa.

Binafsi niangazie eneo moja tu ambalo kwa maoni yangu kama Serikali ingeamua kulifanyiakazi huenda basi ingekusanya pesa nyingi na matokeo yake ingepunguza mzigo kwa wananachi masikini. Ni ukweli usiopingika kuwa wafanyabiashara wengi hukwepa kodi na hii inatokana na kodi zisizo na uhalisia, kutokua na muongozo mzuri wa kudhibiti ukadiriaji kodi kwa wafanyabiashara, yaani ofisa wa TRA anakupangia kuwa utalipa kiasi flani cha kodi na namna hii ya utendaji huchochea vitendo vya rushwa.

Ukimpa chochote afisa huyu basi atakukadiria kiwango kidogo cha kodi ikilinganishwa na biashara yako hivyo serikali inapoteza pesa nyingi hapa. Kwenye upande wa risiti za EFD wafanyabishara wengi wanalikwepa hili na ukienda kununua kitu dukani basi hatokosa sababu ya kutotoa risiti ilimradi Serikali ikose mapato yake kupitia VAT.

Ningetamani Serikali ifanye hivi, inaweza kuchukua sehemu inayofanywa biashara sana kama vile kariakoo na kuifanya liwe ni eneo la cashless zone kwa maana miamala yote kwenye eneo hilo ifanyike kimtandao na ili serikali ione miamala yote wanaweza kumtengenezea kila mfanyabiashara aliyepo pale namba ya malipo ili kurahisisha miamala hiyo, huku mifumo ya TRA ikiunganishwa na namba hizo ili kurahisisha visibility ya ukusanyaji kwa upande wa serikali.

Kwakufanya hivyo serikali itaweza kujua kila mfanyabiashara anauza kiasi gani kwa siku na kiasi gani cha VAT wamekusanya pia itaweza kukadiria kodi stahiki kwakila mfanyabiashara. Ili isiwaumize wafanyabiashara serikali ipunguze KODI na VAT kwenye eneo hilo kwani naamini itakusanywa pesa nyingi sana kwenye mfumo huu.

Kinachoniamisha mfumo huu utafanyakazi ni kuwa tumeona kwenye baadhi ya maeneo kama vile madini udhibiti ulipowekewa mkazo tumeona mapato na uzalishaji umeongezeka sio kwa sababu watu wanachimba sana la hasha bali wamedhibitiwa hakuna namna ya kukwepa. Serikali ifanye hivyo kwa muda hata mwaka mmoja halafu wafanye tathmini na ikiona kuna manufaa basi ipelekwe nchi nzima.

Kila mwananchi lazima awe na namba ya mlipa kodi na ikiwezekana namba hiyo iwe ni miongoni mwa taarifa zilizopo kwenye kitambulisho cha taifa. Namba ya mlipakodi ni taarifa itakayojumuishwa mtu anaponunua bidhaa au kitu chochote, hii itafanya kodi yetu wananchi tunayolipa inaenda sehemu stahiki. Lakini pia kama TRA wanavyofanya kwa wafanyabiashara kukagua kama ametoa risiti, wanaweza kufanya hivyo kwa mwananchi kama wana mashaka na mali anayomiki kama ameinunua kihalali, wanaweza kuingiza namba ya mlipakodi ya aliyetiliwa mashaka na kuona kwenye mfumo iwapo namba hiyo ilinunua hiyo bidhaa.

Hii itafanya mwananchi kulazimika kununua bidhaa kwa mfumo huu akijua kama nitabainika nitachukuliwa hatua za kisheria. Kwa mantiki hiyo basi hakutokua na mashine zinazotoa risiti za karatasi bali wanaingiza namba ya mlipakodi anaenunua, namba ya simu, bidhaa husika na kiasi halafu atatumiwa risiti yake kwa sms kama wanavyofanya GEPG ili kuondokana na kasumba ya kununua mashine za EFD hapa watakua wanatumia App ya TRA kwenye simu zao.

Nawasilisha.
 
I like this place JF. Watu mnamawazo positive sana.

Nimependa hapo kuhusu wazo la kidigitali katika ukusanyaji kodi.

Kiukweli nchi inatakiwa ibadilike katika matumizi ya mtadao kwamana dunia ya sasa imesha ingia huko toka siku nyingi. Mtandaoni kuficha tarifa mda mwingine inakuwa ni mgumu sana kwahiyo kila swala linaonekana wazi wazi.
 
Ndiyo hili linawezakana na linatendeka.

Mwandishi hongera.

Shuhudia na wewe utendaji unavyoghairi ghairi mambo ama kukosa ubunifu... Japo tunaishi nyakati za kuhitaji kujaribu jaribu upesi, kusoma mifumo na kusahihisha mifumo... Miundo mbinu kama ya TEHAMA inaweza kurahisisha hili wakati wote.

Hata mimi naungana na wewe, eneo fulani dogo likitumika kufanya majaribio linaweza kuibua ukweli hata wa kushangaza kuhusiana na 'manunuzi na mapato' baina ya wafanyabiashara na wateja.

Tunachelewa na tumechelewa kutokana na dosari la kimfumo, mazoea na uzito utokanao na kuyaogopa mabadiliko.

Sambamba na hili, siku zijazo tutahitaji wataalam wa kuisoma na kuitathmini mifumo kwa haraka na ustadi wa juu -- Mwandishi unazosifa kuingia kwenye shughuli hii na hata unaonesha uwezekano wa kupokea mafunzo na kujiboresha.

Moja ya mazingira muhimu ya kustawisha viwanda/tasnia ni kuwa na rasilimali watu inayojengewa uwezo wakati wote na kulingana na mabadiliko ya tekinolojia na umahiri katika kazi/shughuli. Hapa Tanzania haya yanajulikana lakini shughuli hii haina kasi ya kuendana na uhitaji wa biashara na maendeleo katika ulimwengu wa utandawazi. Jukumu hili kwa mfano, kiserikali na taifa wamepewa wakala walio ni COSTECH, TIRDO na SIDO... Lakini suala zima la kuvumbua vipaji na kuvitia katika nguvu kazi ya ujenzi wa Taifa halina misingi, utaratibu, makusudi na nguvu ya kutosha katika muktadha na mwelekeo wa kukuza viwanda/tasnia ili kuwezesha maendeleo ya kiuchumi-jamii tunayoazmia kuyapata.

Kodi ni muhimu sana kwa maendeleo na ustawi na nchi. Zipo hata namna mbadala za kuibua mtindo wa ukusanyaji wa kodi wa hiari ambapo hata wanazuoni na watendaji waliokatika utumishi wakiambiwa ama kushauriwa wanaweza kusitasita... Hii ni kuwa mafunzo yao na akili zao bado vipo kwenye paradaimu inayokata pumzi--mifumo dume ya kiuchumi... Hata hili la 'uchangiaji' kupitia makato katika miamala ya simu ni mojawapo ya mengine mengi. Kwanza, pongezi kubwa kwa Serikali na Wizara husika kwa kulifanyia kazi hili na sisi wadau wa fikra mbadala tunaelewa fika jukumu linalofuata ni kuwajibika na kujifunza, kuitathmini mifumo mipya na kujitathmini huku tukihusisha wadau wote wa maendeleo kwa uwazi.

Labda bado tuna mapungufu katika 'kununua ushauri' kutoka katika sekta binafsi hasa linapokuja suala la 'suluhu' -- suluhu kwa ajili ya kubuni na kuimarisha miundo mbinu ya utawala na ufanisi kazini... Hata hivyo shukrani kwa Jamii Forums na ubunifu huu wa kuboresha maudhui na michango kwa msaada wa jukwaa hili la TEHAMA... Siku za mbele inawezekana kabisa kubuni utaratibu namna gani wabunifu na waendeleza miradi watakutana na kusuka mikakati ya kubadili sura ya mambo kwa ajili ya maendeleo ya umma, jamii na taifa kwa ujumla.

Tena kwa kumalizia, heko sana mwandishi wa kwanza.

Shukrani
 
Unajua shida inaanzia wapi?

Shida inaanzia kwenye kodi kuwa kubwa sana nchini, hili linatengeneza kama chain fulani ambayo mwisho wa siku ndo inasababisha issues za wafanyabiashara kutokupenda kutoa risiti za EFS ili ku-underestimate mauzo yao. Nitakupa mfano.

Ukiingiza mzigo wa kontena mfano la bidhaa ambazo umeagiza kutoka nje tuseme mzigo ambao thamani yake ni milioni 200, kodi ya halali ya huo mzigo ni milioni 100. Kwa hiyo, ukilipa kodi halali thamani halisi ya mzigo wako ni milioni 300 (hapo sijaongezea charges za hapa na pale katika kutoa mzigo wako bandarini).

Lakini, ukiongea "kibingwa" na wale jamaa wakati unatoa mzigo wako, utalipa kodi ya milioni 25-40 kwa kadri ya maongezi yenu yatakavyokwenda. Ila sasa, ukiongea na hao jamaa "kibingwa" maana yake lazima uwahonge, so kwenye kuwahonga lazima utoe kati ya milioni 10-20 kulingana na maongezi yenu pia yatakavyokwenda.

Lakini, kumbuka ili uweze kulipa kibingwa, hiyo milioni 20 badala ya kodi halali milioni 100, ni lazima wale maafisa pale wa-underestimate mzigo wako, so lazima waseme labda thamani ya mzigo wako ni milioni 100. So, kwenye makaratasi, thamani ya mzigo wako itakua ni milioni 100 + milioni 20 ya kodi=milioni 120.

Tuseme huu mzigo ukiuuza kihalali kabisa kwa kutoa risiti za EFD kwa kila anaehitaji unakuja kupata revenue ya milioni 350. Kwa hiyo, wakija maafisa wa TRA ina maana wao watasema faida yako ni milioni 350 -(milioni 120 + operation costs kama mishahara). So, kodi ambayo utatakiwa kulipa hapo itakua juu sana.

So, wafanyabishara ili kudeal na hilo sasa, kinachofanyika ni ku-minimize utoaji wa risiti za EFD as much as possible katika mzigo anaouza ili mwisho wa siku asije kuonekana ana revenue kubwa sana na anatengeneza faida kubwa, kumbe thamani ya mzigo ilikua underestimated tangu mwanzo mzigo unaingia.

Nini kifanyike?
Kupunguza kodikwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje hasa zile ambazo hazizalishwi hapa nchini...!!At least iwe a reasonable amount, maana mtu yoyote mwenye akili anaona kabisa kuna kodi mfanaybiashara akisema alipe tu kama ilivyo hatoboi sokoni, na hili hata wale staff wa bandarini wanalijua, hili likishafanyika sasa, ndo mengine yafuatie, naamini bila hili kufanyiwa kazi, itakua ni ngumu sana kufanya wafanyabiashara wawe wanatoa EFD receipts kwa uaminifu!
 
Unajua shida inaanzia wapi?
Shida inaanzia kwenye kodi kuwa kubwa sana nchini, hili linatengeneza kama chain fulani ambayo mwisho wa siku ndo inasababisha issues za wafanyabiashara kutokupenda kutoa risiti za EFS ili ku-underestimate mauzo yao. Nitakupa mfano.
Ukiingiza mzigo wa kontena mfano la bidhaa ambazo umeagiza kutoka nje tuseme mzigo ambao thamani yake ni milioni 200, kodi ya halali ya huo mzigo ni milioni 100. Kwa hiyo, ukilipa kodi halali thamani halisi ya mzigo wako ni milioni 300 (hapo sijaongezea charges za hapa na pale katika kutoa mzigo wako bandarini).
Lakini, ukiongea "kibingwa" na wale jamaa wakati unatoa mzigo wako, utalipa kodi ya milioni 25-40 kwa kadri ya maongezi yenu yatakavyokwenda. Ila sasa, ukiongea na hao jamaa "kibingwa" maana yake lazima uwahonge, so kwenye kuwahonga lazima utoe kati ya milioni 10-20 kulingana na maongezi yenu pia yatakavyokwenda.
Lakini, kumbuka ili uweze kulipa kibingwa, hiyo milioni 20 badala ya kodi halali milioni 100, ni lazima wale maafisa pale wa-underestimate mzigo wako, so lazima waseme labda thamani ya mzigo wako ni milioni 100. So, kwenye makaratasi, thamani ya mzigo wako itakua ni milioni 100 + milioni 20 ya kodi=milioni 120.
Tuseme huu mzigo ukiuuza kihalali kabisa kwa kutoa risiti za EFD kwa kila anaehitaji unakuja kupata revenue ya milioni 350. Kwa hiyo, wakija maafisa wa TRA ina maana wao watasema faida yako ni milioni 350 -(milioni 120 + operation costs kama mishahara). So, kodi ambayo utatakiwa kulipa hapo itakua juu sana.
So, wafanyabishara ili kudeal na hilo sasa, kinachofanyika ni ku-minimize utoaji wa risiti za EFD as much as possible katika mzigo anaouza ili mwisho wa siku asije kuonekana ana revenue kubwa sana na anatengeneza faida kubwa, kumbe thamani ya mzigo ilikua underestimated tangu mwanzo mzigo unaingia.

Nini kifanyike?
Kupunguza kodikwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje hasa zile ambazo hazizalishwi hapa nchini...!!At least iwe a reasonable amount, maana mtu yoyote mwenye akili anaona kabisa kuna kodi mfanaybiashara akisema alipe tu kama ilivyo hatoboi sokoni, na hili hata wale staff wa bandarini wanalijua, hili likishafanyika sasa, ndo mengine yafuatie, naamini bila hili kufanyiwa kazi, itakua ni ngumu sana kufanya wafanyabiashara wawe wanatoa EFD receipts kwa uaminifu!
Kama nilivyosema kwenye andiko langu, ili mfumo huu niliyoupendekeza usiwaumize wafanyabiasha sababu tunajua kodi zipo juu basi serikali iamue kushusha kodi pamoja na VAT ili wafanyabiashara wasiwe na sababu ya kukwepa mfumo na hapo serikali itakusanya mapato ya kutosha.
 
Mchakato wa kuifanya Kariakoo ya sasa iliyojaa wamachinga waliojaza bidhaa chini na vibanda visivyo rasmi kila kona kuwa Cashless Zone ni wa kinadharia zaidi,Labda tuanze kwa kuondoa wamachinga wote na vibanda yabaki maduka rasmi yaliyosajiriwa.Tuje kwa wananchi wenyewe kuwalazimisha wafanye online transactions via debit/credit card or online Money tranfer.Kimsingi mawazo yako ni mazuri ila siyo kwa mazingira yetu ya sasa.
 
Kwa kutumia mtandao ya simu, hapo unamuongezea mnunuzi makato na usumbufu.
Hapana kufanya malipo na kutuma pesa ni vitu viwili tofauti, hapa mimi nazungumzia kufanya malipo ya manunuzi nikama vile unapofanya malipo ya LUKU au King'amuzi charges ni negligible.
 
Sawa.

MABADILIKO, UTANDAWAZI NA MITEGO YA SARAFU-KRIPTO

Hebu tulitanue shauri la Mwandishi wa kwanza ili kujipatia mwangaza bora kwa mabadiliko -- na tuende hata mbali sana...

Pendekezo la Mwandishi wa kwanza linajikita kwenye kuhimiza mabadiliko ya kimfumo katika ukusanyaji wa kodi, kwa TRA, na huku makusudi ya serikali katika kutekeleza azma yake ya maendeleo kwa umma kuzingatiwa. Mwandishi wa kwanza ananyooshea kidole mifumo ya kidijitali kama jukwaa la majaribio, na ikifaa, kwanini basi isiwe ndiyo suluhu?

Mwandishi amefafanua baadhi ya manufaa yanayoweza kupatikana, kuzingatia faida zake za kimfumo kuwa na hadhi ya 'mjumuisho wa taarifa na habari' juu ya miamala ya biashara. Hili linaonekana kuwa ndiyo muafaka katika kubaini uhalali wa kodi, katika muktadha wa biashara na mgawanyo kwa serikali. Mwandishi ametaja ubunifu wa kuwa na 'Ukanda wa Pasipesa', yeye kusema 'cashless zone', ambavyo huduma za kibiashara zitaendelea bila matumizi ya pesa halisi na badala yake 'mifumo ya kidijitali' itumike.

Kwanza kabisa, namna hii ya suluhu imeanza kutumika katika serikali hii ya Awamu ya Sita, kwa mara ya kwanza -- utaratibu wa kodi/tozo ya uzalendo--ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa malipo yote ya mtandaoni. Kwa hivyo, kiufundi, ulilolipendekeza linatekelezeka; na miundo mbinu kwa mtandao, kwa ajili ya utaratibu wa 'malipo na rajisi', ni suala la kuuongezea uwezo na kuuboresha...

KIMSINGI, ugumu wa kufanikisha jambo hili kwa mapana yote ya utumikivu, ni nasibu ya 'changamoto ya kimabadiliko ya kiutendaji' na tena katika mazingira yanayobadilika.

Mara tu Mwandishi wa kwanza alipoyazungumzia masuala ya 'miamala ya kidijitali', tupende ama tusipende wote tunalazimika kutafakari mapelekeo ya kuhama kutoka kwenye mazingira yalizoeleka ya matumizi ya fedha halisi, kwenda kwenye matumizi ya 'fedha-mtandao'...

Itaonwa hata kwenye huu uzi jambo hili lishaanza kuvutia migongano...

Kiuchumi, pesa -- iwe 'fedha halisi' ama 'fedha-mtandao' ni sarafu.

Japo, kitekinolojia inaweza kuonekana ‘fedha-mtandao’ kwa maana ‘malipo ya kiditali’ bado si ‘sarafu’ kwa namna fulani, kuzingatia dhana nzima ya ‘uzungukaji na thamani ya kimabadilishano’ – kimatumizi yake na kwa fasaha yake kimfumo(kasi fedha, uhitaji wake katika mzunguko); Maarifa ya kumalizana na ‘pengo hili la maarifa’ ni jambo la ‘uonivu wa kialama’ na ‘umodelishi wa kihisabati’ ambao unaweza usiwe bayana.

Hili pia lina mapelekeo ya kuingiliana na sera nyingine kama vile sera za mawasiliano, mtandao na uchukuzi. Fedha na ‘uhimilifu wa uchumi’ ni suala mtambuka.

Sarafu inanamna yake ya kutazamwa linapokuja jambo la 'kuuza na kununua'; sarafu ni rasilimali kwa mabadilishano ya jamii yanayoweza kupelekea 'usawa' ama 'kuzidiana nguvu', kwa mujibu wa sura za kiuchumi na biashara; na tena, kwa mapana yake hutuletea 'Ulali wa Malipo' yaani mizania kwa hesabu za 'kilichotoka' na 'kilichoingia' ndani ya kipindi maalum cha tathmini. Hili linahusika sana katika ngazi ya nchi na msimamo wake kiuchumi. Na ikumbukwe, katika ulimwengu wa biashara za kimataifa na utandawazi, nchi si kisiwa... Nchi nayo ni sehemu ya mfumo mpana wa
kiuchumi, jamii, siasa, Utamaduni na mazingira asili...

Hapo tulipo, inatupasa tutathmini na kujitathmini ni wapi tulipotoka na ni wapi tunakwenda.... Ufunguo kwa mabadiliko upo katika umahiri wetu wa kuisoma na kuitathmini mifumo kwa mbinu za kawaida na hata zisizokuwa za kawaida.
Sera yetu ya fedha, ikiwa ‘tunaelekea kujitambua’, inahitaji ‘kuzaliwa upya’. Hili litafika kwa kadri ya ukomaa kwetu kitaasisi na mifumo inayokadirisha ‘uwezo’ na ‘utendaji’ mpya. Hili litaingiliana na mabadiliko zaidi, hata ya sera nyingine nyingi za nchi.

Kwa hivyo kwa kutangulia yote, jawabu la hitaji kwa mabadiliko yote ni umahiri katika jambo tutaloliita sasa rasmi kwa Kiswahili, ‘Uonaji Mfumo’ na pia ‘Ufikirifu Mifumo’. Wenye kuzungumza lugha ya Kiingereza wangalihusisha haya kwa kutaja ‘System View’ na ‘System Thinking’... Ni haya mawili yanaweza kutupatia ujuzi na ufundi kwa ‘alama oanifu’ za kusukia ‘mifumo mipya’... Na kwa kuwandaa wataalam wa mambo haya ipasavyo, washaurike tu kuelewa vitu vyote ni ‘ishara’ na ‘alama’; ukiwa na ujuzi na ufundi wa kuzing’amua alama basi waweza kupitiliza ufahamu rahisi wa mambo na kuelekea kwenye umahiri wa kubuni modeli za kihisabati zisizoishia kwenye ‘milinganyo sahili’; hili liwe wazi, kupitia visomo vilivyozoeleka na maarifa ya ‘kukopa’ na ‘kuigiza’ bado haya ya maarifa ya ‘uelewaji wa ki-bluprinti’ na ‘mbegu mifumo’‘hatujaletewa’--isibidi kwa wataalam wetu wa fedha kuwa wajanja wajanja wa kuvizia ‘fikra’ za wanazuoni wa magharibi na ‘majukwaa ya uchumi kimataifa’, halitatokea!

Media ifuatayo itengeneze njia.


Yatupasa kujikumbusha kwamba ulimwengu wa leo upo katika hatua ya nne ya mapinduzi ya viwanda. Hatua hii ya nne ni matokeo ya maendeleo makubwa ya kitekinolojia na hasa hasa katika ugani wa 'tekinolojia ya habari na mawasiliano'. Kwa nguvu ya sayansi na maarifa, sasa tumeingia katika ya kizazi cha pili cha muoano wa 'uelektronishi' na 'TEHAMA' ilivyo ni 'Sibanetia na/ya Akili Bandia'... Japo ni vigumu kuchora mpaka wa mapinduzi ya tatu na ya nne, lakini hayo ya tatu yanaonekana yalipata kuanza mnamo mwaka 1969--ndiyo yaliyotuletea 'ngamuzi na mfumo wa intaneti' kwa sekta za biashara, huduma za jamii na matumizi ya nyumbani...

Mapinduzi ya viwanda huwa na mapelekeo ya kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi, jamii, siasa, utamaduni na mazingira... Mapinduzi ya Nne ya Viwanda ni ya mwisho, na yanatuleta uzuri na mastaajabu makubwa ambayo yanaweza kubariki sana ustawi wa mwanadamu, kwa kututia wepesi wa kiutendaji, ama 'kuumeza ustawi huo' na basi ubinadamu kama tunavyoujua leo kutoweka.

Hapa tulipo, matumizi ya fedha-mtandao ni kabila moja na 'sarafu-kripto' -- ambayo ni zao la maendeleo ya leo ya 'uchukuzi wa vinasaba' vya kimtandao vinavyowezeshwa na mifumo inayojitegema -- yenye asili ya daraja fulani katika domaini ya Akili Bandia.

Basi kufika hapa, inafaa kusema na kupendekeza, matumizi ya fedha-mtandao na hatua bora na salama kuhamia kwenye 'mazingira bandia ya ulimwengu wa uchukuzi na mawasiliano' kwa kuwa domaini yake ni yauenyeji; na tena, tukiufaulushia ukati wa udhibiti basi tunaweza kukadirishia 'ulali wa malipo' unaoweza kuendana na ulimwengu wa biashara za kimataifa, na tena kulingana na sura halisi ya mifumo inayotawala.

Kwa upande mwingine, sarafu-kripto ni mtego; jamii nzima ya walimwengu leo hii wananaswa na ulimbo wa sarafu-kripto kwa kuona hii inaleta 'wepesi na uhuru' wa kufanya miamala hata inayovuka mipaka za nchi zao. Wao wanaona sarafu-kripto ni kama kielelezo kwa 'uhuru fulani'...

Kuna namna, si rahisi kwa wengi kutambua, sarafu-kripto ni kama Farasi wa Trojani... Hii ni kwa kuwa: kama vile lilivyotatizo la UVIKO19, badala ya watu kudadisi hivi virusi vilikujaje, wao wanakubali tu 'kuchezeshwa Ngoma Ukae'... Siku moja, labda itakuja kufahamika vizuri...

Waliobuni na kuanzisha sarafu-kripto ni 'watu wasiojulikana' -- na sarafu-kripto ni mbadala tukuhamishia nguvu zao kwenye domaini za 'mazingira bandia ya ulimwengu wa uchukuzi na mawasiliano'... Basi, labda chanzo chochote utakachopata kusikia kinahusika na tekinolojia kama 'block chain', usiamini moja moja kuwa ndiyo mwanzo halisi wa sarafu-kripto... Katika nchi zilizoendelea, kuna 'Vinyago vya Mpapure' vya kutosha -- linapokuja suala la tekinolojia na
ubunifu...


SERA JUU YA 'MAZINGIRA BANDIA YA UCHUKUZI NA MAWASILIANO' -- MASHAURI YA AWALI

Hapa tulipo, ni vema tukawa na macho ya kuona: ulimwengu wa mtandao unatufikisha njia panda... Tunahitaji namna ya utawala ambayo maamuzi yake yatanukie na kwenye 'mazingira bandia ya uchukuzi na mawasiliano' na si kuegemea kwenye mbinu na taratibu za utendaji, unaokomea kwenye domaini ya kawaida tu.

Pia, kwa sura ya kipekee, tupate kumaizi kwamba tuna fursa ya kuweza kutumia rasilimali 'fedha-mtandao' kama sarafu inayotuletea suluhu dhidi ya mifumo dume ya tawala na uchumi.

Tukumbuke ule Wimbo Mzuri sana wa zamani wa bendi ya Simba wa Nyika: "Shilingi Yaua, tena
Maua"...

Sarafu ni 'kisicho kibaya' wala 'kizuri' lakini kwa mifumo yetu na tabia zetu, tunaishi na sarafu kama 'maua' na hapo hapo 'inatuua' -- 'inatuua' si kwa kukusudia bali kwa matokeo ya vitendo vyetu vya kuhalalisha haramu, sambamba na halali... Kwa vitu kama vile 'faida' na 'riba'... Haijalishi tunapata elimu hadi ya PhD ama D.Lit... Kama tunanunulika kwenye paradaimu za 'kupata na kukosa' bila kujishtukia mahala wote kwa pamoja kusema itoshe, hebu tusogee kivingine basi tujue fika hakuna mungu wala masihi wa kuingilia kati vilio vyetu... Hali itaendelea kuwa kama ilivyo
kwa kuwa hatudhubutu kufikiria vinginevyo -- na kumbe, kuna wakati, kweli zipo namna...

Tatizo la Kodi na ukadiriaji wake linamapungufu ya kiufundi, maadili na haki -- japo sisi watu kwa werevu wetu unajua kuvikana ngozi za kondoo ama mbuzi ili siku zisogee... Kwa sehemu kubwa mapungufu yake ni athari ya mfumo wenyewe mzima, na tena mbovu, wa kiuchumi unaoitwa uliberali wa kileo... Kwa hivyo tabu, shida na kilio juu ya shughuli ya kodi haiko Tanzania tu... Hata kule Amerika na IRS yao, suala la kodi ni mwiba sana...Uchumi wa kileo wa Dunia ni kielelezo cha Mfume Dume. Unasifa za hulka za kujilimbikizia na kuhodhi bila ukomo... Amerika walau ilifika mahala, baadhi yao wakaanzisha harakati zenye mlengo wa kukabiliana na ghiriba za kikoporeti kupitia jithada za 'AntiTrust Initiatives'.

Hata ukisema watu wawili wakae na kuzungumza juu ya muafaka wa kulipa-aje kodi, si jambo rahisi... Upande wa serikali wasipokuwa wakali, wataonewa kwa kudanganywa, vivyo hivyo serikali ikileta utemi sana itaumiza watu wake na kusabibisha manung'uniko. Kodi ya Uzalendo ni hatua nzuri sana ya kuboresha makusanyo kwa serikali, kikubwa ni juhudi zaidi za kuwa wawazi; na kuleta hesabu kwa umma juu ya mwenendo wa makusanyo, malengo yanayofikiwa na matumizi kadri ilivyodhamiriwa.

Tukienda mbele kidogo, kuna uwezekano tukaja kubaini sarafu ya kidijitali inawezo mkubwa wa kusapoti ubunifu, usimamizi/uendeshaji wa viwanda vidogo kwa vikubwa, na mtanuko wake, huku ikitatua moja kwa moja adha za 'mfumuko wa bei' katika uchumi. Hili litawezekana kupitia na 'mifumo ya mumo kwa mumo' ya makato, hifadhi, kodi na mahitaji -- ambayo inaweza kubuniwa kwa kutangulia kama mpango wa shughuli/biashara, kuakisi ukubwa wa shughuli yenyewe na mapana yake ya 'ukubwa' na 'muda'. Siku sijazo, kila shughuli itaanzishwa kwa marefu na mapana--muda ukifika, kila shughuli lazima igawanyike na kuwa mbili... Kulingana na mpangilio wa menejimenti na wanaoperesheni kazi, ipo namna tatizo la ajira linaweza kutatuliwa 100%...

Utendaji wa namna hii ni namna ya Uchumi wa Kazi; kwa sasa duniani kote hatuna uchumi wa kazi hasa, bali tuna uchumi wa biashara. Uchumi wa Kazi, unafanania kuitwa ni 'Usanisi wa Ujasiriamali wa Kijamii'. Hii ni kwa kuwa huu ni biashara na maendeleo ya jamii kwa wakati mmoja. Si kwamba mmoja akutangulie halafu akumegee ili na wewe kama serikali eti ndiyo ulete ama kustawisha maendeleo ya umma... Wakati uchumi wa biashara ni kilele cha maslahi binafsi halafu taifa, ama taifa kutetea maslahi yake kupitia mashirika koporeti; Uchumi wa Kazi ni Uchumi Mama ambapo shughuli zote za jamii zinaratibiwa kwa misingi ya utawala bora wa 'shughuli za uzalishaji mali na 'shughuli za utoaji huduma' kwa modeli maalum...

Kuna uwezekano, tukitambua ya kwamba kupanga ni kuchagua, ndani ya vizazi viwili -- kipindi cha takribani miaka 30-50, Afrika itakuwa ni bara lenye maendeleo makubwa na kupendekeza, nchi nyingi duniani itawapasa 'wajipange na kujipangua' ili kuendana na modeli zetu za Uchumi Mama...

Na hili napenda liwashangaze wengi, na wajiulize, na kudadisi -- eti kweli Afrika itakuja kuwa bara la mfano siku moja? Na wahakikishia--Afrika itapata maendeleo ya kiuchumi-jamii, utamaduni, mazingira 'asili na bandia' kupita China na Amerika... Na 'bora uamini' -- ukiambiwa sehemu kubwa la chimbuko la hayo maendeleo, inaendelea hapa Tanzania; kunako siku za mbele, kwa ushirika na nchi jirani...

Serikali ya Awamu ya Sita imeanza kuonesha njia kwa 'Maendeleo kupitia Kuchangia'... Hii ndiyo roho hasa ya ile kaulimbiu: 'HARAMBEE'... Afrika itajengwa na wenye moyo, itasonga kwa 'Liberiti na Harambee'-- Watu kusonga mbele Kuunganisha nguvukazi, Utangamano, Kutoyumbayumba Kijamii na Pendo Moja... Lakini mabadiliko kwa tabia za watu jambo linalohitaji saburi na ujuzi wa mawasiliano na umma. Kwa haya yote kutimia, lipo hitaji la Sera Kuu ya mazingira na Utendaji inayotangamanisha 'mazingira asili' na 'mazingira bandia'...

Hapa tulipo, baadhi wa watu kutoka kwenye umma wetu wa Watanzania wanapasa sauti juu ya 'Kutaka Katiba Mpya'... Si ajabu wengi wetu tunaangalia sura ya Taifa na Nchi kiupande upande... Tunakosa kule kuona na kubaini Nchi inaweza kutazamwa vizuri kwa mapana ya pembe-tatu-sawa zinazowakilisha 'Siasa za Nchi', 'Mipango ya Utumishi' na 'Uwezo wa Jamii'...

'Siasa za Nchi' ni shughuli ya vipindi vifupi vifupi ambapo kupitia michakato ya demokrasia za kiliberali, kikundi cha watu wachache kinaingia madarakani kupitia utaratibu wa uchaguzi na matokeo ya kura. Demokrasia za kiliberali zinatuletea taasisi za demokrasia ambazo msingi wake ni uwakilishi -- hapa kwetu Tanzania uwakilishi unafungamana kuwa mwanachama wa chama cha Kisiasa, kunadi Ilani ya chama, kushiriki katika uchaguzi, kuchaguliwa na kushika hatamu.

Kudumu kwa chama katika hatamu ni zao la kukubalika na kupewa nafasi ya kuendelea kuongoza. Mhimili wake wa imani hunyooka kati ya 'Uono' na 'Ontolojia ya Taasisi'. Kusema 'Ontolojia ya Taasisi' kunapelekea maana, taasisi huja na sura yake ilivyo ni zao la 'muundo wa kujitengenea', 'ushawishi' na 'Kujisikia'... Taasisi yoyote ni zao la fikra na hisia na kujitengenea. Chama cha Kisiasa kwa mfano ni taasisi kwa kuwa kina muundo rasmi wa kijumuiya, itikadi yake na katiba. Kinapotaka kujipambanua katika uchaguzi basi kinakuwa na Ilani yake...

'Mipango ya Utumishi' ndiyo sehemu nyeti kwa maendeleo na ustawi na taifa kwa kuwa hii ni shughuli ya kudumu. Dhamira na Miongozo yote ya kiutendaji na utumishi hulalia upande huu wa tawala ya nchi. 'Siasa za Nchi' na ' Mipango ya Utumishi' vinakutana katika kitovu kimoja, pembe ya 'Uono'. Mhimili wa Imani kwa upande huu hunyooka kati ya 'Uono' na 'Sura na Mienendo ya Jamii'. Chama kinachoshika hatamu 'Itikadi yake' haina budi kufanania na 'dhamira' tena 'Ilani' yake kuwa sambamba na 'Miongozo' iliyopo katika ulali huu wa 'Mipango na Utumishi wa Umma'.
Mipango na Utumishi ipo kwa ajili ya kutumika kimfumo ili kuinasibu jamii na sura fulani ya tawala, hadhi na huduma.

Mfumo katika lugha rahisi ni zao la taasisi na wakati; Chama cha Siasa kishikapo hatamu huwa na muda maalum wa kuweza kufanya hivyo na basi utaratibu wa chama kuingia na kutoka madarakani ni mfumo, japo 'Mipango na mtumishi' nayo hukadirika kwa mifumo...

Chama cha Siasa kinaweza kufanya vizuri ikiwa malengo yake ya kimadaraka yanavaana mifumo ya kudumu ya 'Mipango ya Utumishi'. Na hapa moja la kujifunza kwa umakini: Japo demokrasia ya kiliberali inaleta shauri kuwa ushindani na kugombea madaraka vina tija katika suala zima 'utawala bora' hii ni 'kweli' na 'si kweli' kwa wakati mmoja... Kwa kuwa hili linategemeana na vigezo mbalimbali, ikiwamo kwa ujumla, kama: 'elimu bora na ya kutosha ya uraia na maarifa ya jamii miongoni mwa wanajamii', 'tabia njema/mbaya ya wanajamii' na 'kujitambua ndani ya mtu mmoja mmoja'. Hili ndilo lafanya kwa nini upande ulali wa kisiasa za nchi ni jumla ya 'vina vya tafsiri' na 'kujisikia'...

Ni rahisi chama cha kisiasa kuingia madarakani kwa 'kuchezea akili za wengi', ikiwa hao raia urazini wao 'ni wa juu juu' na tena hisia zao zinasombwa na 'upepo wa maoni' kirahisi...Kwa sifa hizo hizo za kimfumo, wanaoingia madarakani wanaweza kujikuta kule 'kuomba kura', 'kupata kura' na 'kuingia madarakani' ni jambo moja; lakini 'muziki' wa kuwa madarakani ni 'mnene' -- ni jambo jingine... Miaka Mitano haitoshi... Labda hata miaka kumi haitoshi... Wengine kwa tabia zao mbaya huanza kutamani 'kuichokonoa katiba' ili wakwepe 'uchaguzi' -- waendelee kutawala kinyemela...

Hapa pia tunapata fundisho: Siyo tu kwa sababu tuna Katiba inayotamka kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa, halafu kwa kuwa kila binadamu huwa ana njozi fulani 'ya kuwa juu, juu zaidi' basi utafsiri unaweza kuwa 'Kiongozi'--uongozi kama 'alama ya ushindi' dhidi ya 'maadui wako' ama wengine 'walio chini ya uwezo' wako. Usidanganyike na siasa; Siasa inasema 'Kiongozi ni mtu mwenye madaraka katika jamii'... Lakini Je, unafahamu? 'Kiti' hakikufanyi kiongozi... 'Upeo wako wa kiakili' na 'utashi' ndivyo daima vya kufanya wewe uwe kiongozi...

Uongozi ni 'kufanya Maamuzi' na 'kuongozea njia'... Walau hili ni dhahiri kwenye upande wa 'Mipango na Utumishi' kwa kuwa huku inafahamika fika: Kupanga ni Kuchagua... 'Mtu anayejitambua' ana mwangaza kwa mapito yake mwenyewe, akijiongeza kuwa ni 'mwenye kujali' basi huyu huwa 'Mtumishi'... Tukihama kutoka kwenye mfumo dume, hili linakuwa kanuni ya kawaida kabisa inakayotuletea tutakachokiita 'Meritokrasia'... Upendo hutumikia, anayejifikiri yuko juu zaidi aweza kuwa ndiye wa chini kabisa... Aliyejuu Zaidi kiukweli ataitika wito kutumikia wengine, na katika hili yeye 'haitaji madaraka' wala 'maslahi binafsi', daima ataitafuta njia yake kudhihirisha nuru yake, yeye kupata kuwa 'mfano wa kuigwa' kwa namna moja ama nyingine...

Leo hii tuna matatizo lukuki hata kwenye daftari zetu za utumishi kwa kuwa ajira hizi ndani ya mfumo dume si lolote bali 'viti'... Tabia mbaya ni kama 'pembe la ng'ombe'... Kuinua mabega... 'Utumishi ni wito', kadri vile hata 'itikadi ni Imani'... Tanzania tuna bahati sana Muasisi wa Taifa letu, Mwl Nyerere, alijitahidi juu chini kuijenga nchi yetu kisiasa, yeye ni mfano halisi wa 'Kiongozi' na si mtu wa madaraka tu... Ukipitia vizuri historia ya Chama cha Mapinduzi kama taasisi, utastaajabu uzuri wa msuko kwa 'itikadi na maadili' ya chama... Kwa nini sasa, hata kwa kipindi kirefu, bado tunasuasua 'kutoboa'? Watu ...

Sasa mifumo yote kwa asili huwa na sifa kukinza mabadiliko; kwa sehemu, hili huponza walioko madarakani kwa kipindi cha kifupi -- pale wanapofikiria kutoka nje ya mpaka kiutendaji na majukumu... Mifumo ya kudumu itawabana, na ikiwa wataendelea kuwa ni 'kitisho', wanaweza kujikuta 'nje ya mfumo' kwa utaratibu rasmi ama hata usiokuwa rasmi. Upande rasmi ni ule uliobayananishwa Kikatiba, usio rasmi ni mapinduzi--ya wazi ama kificho... Kwa kuwa afanyaye mapinduzi, akishindwa, kubainika na kushikwa huwa ni 'mhaini'... Lakini akifaulu... Chama chetu utawala ni 'Chama cha Mapinduzi'; Si lazima, mabadiliko yaje kwa 'matumizi ya nguvu': Akili na mikakati-- 'sawa'; uchochezi na ghiriba-- 'si sawa'... Japo kimsingi, ulimwengu wa Siasa ni uwanja wa 'vituko'; na hata 'hila' pia 'husda'... Hivi vikiachiwa sana huleta usumbufu usio wa lazima. Kwa hivi, kufikiri 'Katiba Mpya' ndiyo kama mwarobaini utarajiwao, suala muafaka, kwa matatizo ya 'kiutawala, utumishi na utendaji', kwa namna fulani jambo hili si la kweli. Hii inaweza kuwa, kwa sehemu kubwa, ni 'ghiriba katika ulingo wa minyukano ya kisiasa' -- fimbo ya 'kuwatishia nyau' watawala kupitia 'maoni yanayoweza kuratibiwa kimkakati' na makundi ya kisiasa na kwa maslahi yaliyojificha...

Hapa tulipo, ni vema kutambua, ujenzi wa taifa ni jukumu la raia wote, 'walioko madarakani' na 'wasioko madarakani'... Pamoja na kwamba tuna Katiba yenye kutupatia misingi ya haki, utawala na kujiamulia mambo yetu, siasa zetu hazina budi kuwa safi. Kwa kuwa usafi wa kisiasa, kiufundi, ni muhari -- kutokana na ukweli kwamba: asili ya makusudi yetu kibinadamu ni yenye kuharibikaupesi, basi tunapohimizana juu ya kuvumuliana na kupeana nafasi ni busara hasa juu ya jambo lenyewe. Siasa ni 'Si-hasa'... Tusiwachokoe walioko madarakani na hata kuweza kuwaponza na wao kufichua makucha yao... Kufanya hivyo kunaweza kufanya nchi isitawalike na kukwamisha maendeleo.

Labda hili litafanya kukumbuka na kutafakari mambo mawili matatu kuhusiana na serikali ya Awamu ya Tano... Hayati Magufuli alikuwa ni mfano wa Kiongozi wa kipekee sana kwa taifa letu la Tanzania, hii ni kwa kuwa yeye alikuwa ni kielelezo hasa cha ulalo wa 'Mipango na Utumishi'...

Mipango kwa asili huvuta na kukusanya wataalam, wa kada mahsusi za mipango, na nyingine zote za maarifa na weledi ili kuimarisha nguvu kazi kwa mikakati iliyopo -- kuisimamia na kuingalia kwa ukaribu katika kuhakikisha inatekelezwa kwa wakati na kuzaa matunda yaliyokusudiwa.

Mikakati ni sehemu ya mipango, na mipango ni mzunguko endelevu wa:-

'kubaini shida, adha, masuala ama uhitaji',
'kulibaini tatizo kwa ushahidi wa utafiti',
'kuweka malengo yanayojibu/kidhi hitaji',
'kuchagua njia ama mbadala mmoja dhidi ya mingine kulingana na uwezo na rasilimali -- ya kuizidi
adha iliyofanyiwa kisomo; na kufanyiwa mkakati',
'kutekeleza mikakati',
'kutazama kwa ukaribu michakato yote na kuitathmini' ili kujifunza zaidi na kupanga zaidi kadri
ifaavyo.

Kwa sifa hizi, ndiyo maana Hayati alikuwa na teuzi nyingi za watendaji wenye madaraja ya juu ya visomo, yaani shahada za uzamivu, katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Umma. Urazini kwa hili ni kwa kuwa, mipango huhitaji 'akili kubwa'... na pia, 'Uangalizi na Tathmni' zake vile vile zinahitaji umahiri... Hadhi na sifa ya 'Uangalizi na Tathmini' ndiyo 'Jicho la Mfumo' wowote...

Hivyo, ile kaulimbiu 'Hapa Kazi Tu' ni mjumuisho wa 'vina vya tafsiri', 'mfumo', 'Nia' na 'Vitendo' ili kukadirisha 'Mchakato wa Maendeleo'... Japo yeye alikuwa kimkakati--'maendeleo ya vitu' ni 1/3 ya 'Mpango Mzima'... Lakini busara yake juu ya agenda ya maendeleo ya nchi ina haki yake; yeye alikusudia kukaza nia katika 'kukazanisha mwendo' wa watumishi ili watekeleze ipasavyo majukumu yao na kukumbuka dhana na dhamira ya utumishi wa umma.

Utumishi serikalini unaongozwa na sera; mipango yote ya kiserikali nayo hutekelezwa kwa misingi sera na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Dira yetu ya Taifa inamalengo ya 'kuibadili jamii kiuchumi, siasa, utamaduni' kuja kuendana na ulimwengu wa leo wa utandawazi na ushindani... Na ndani yake ndiyo huja lile shauri la 'maendeleo ya viwanda' kwa kuwa viwanda hufanya jamii kuwa na maisha tajiri, yakuridhisha, marefu ya kuishi, yaliyojaa fursa na sura anuai za mambo... Ujenzi na Upanuzi wa Miundo Mbinuni hatua za kimkakati zinazotuletea kutangamanisha fursa kwa Maendeleo ya Mjini na Vijijini...

Ujenzi wa Vituo vya Afya, Kuimarisha Huduma za upatikanaji wa Elimu, Maji na Nishati, Masoko na Mambo mengine kama huduma za kimahakama, sanaa, burudani na michezo si tu hutuletea msingi wa 'Maendeleo ya Kibinadamu' lakini yanajenga mizizi kwa ustawi wetu juu ya nchi na mazingira yake. Hili linafanya leo suala la maendeleo ya nchi lazima lijumuishe ulinzi na uhifadhi wa mazingira kwa kuwa sisi wanadamu tunaishi tukiyategemea mazingira, na hali, harakati zetu za kiuchumi na viwanda zaweza kuwa si salama kwa mazingira; na basi kutishia usalama wa vizazi
vya kesho...

Kwa kuwa sasa tumefikia kuzungumiza mazingira, ni vema tukumbuke -- mapinduzi ya nne ya viwanda yamekaribisha namna nyingine ya mazingira tunayojinasibu nayo -- mazingira bandia ya 'uwepo wetu' katika 'mifumo uchukuzi na mawasiliano kimtandao'. Kadri vile sera ni kiungo cha 'Mahusiano ya Nguvu' na 'Mwongozo kwa Utumishi', sera ya kuongoza 'uwepo bandia wa watawala' na 'uwepo bandia wa watawaliwa' katika mifumo ya uchukuzi na mawasiliano kimtandao ni hitaji lisilopingika...

Tuite sera ya mazingira bandia: 'Sera ya Uvichuali'...

Vichuali ni mambo yote yanatendeka na kuendelea katika mazingira bandia, na basi ni muktadha wa uhalisia wetu Uvichualini.

Usuli kwa sura, jamii, biashara, uchukuzi na mawasiliano dunia ya leo


Maendeleo ya kidijitali kwa namna za mtandao, katika stawi za leo, zinatunasibu na jambo kama vile haki sawa katika ufikiaji habari na mawasiliano. Hili linaathiri 'jiografia ya uchumi' uliodumu tangia siku za renasansi -- kati ya karne ya 15 na 16, huko Uropa; ambapo mabadiliko makubwa ya 'kijamii' na 'Ujenzi' yalikuwa sura kutokana na vichochezi vya fikra kana: 'Mtu ndicho kipimo cha Kila kitu'...

Fikra za namna hii zilikuwa ni muamko wa mawazo kutoka Rumi ya Zamani, ambako pia tunapata mawazo juu ya Liberta na Liberiti, Mwenge wa Uhuru na Tabula Ansata.

Sanamu ya Liberiti, iliyojengwa Liberty Island Manhattan, New York iliwekwa pale kama alama ya ukaribisho kwa watu kutoka ng'ambo ya bahari, waje katika nchi ambayo 'watu wote ni huru'... Na maandishi katika daftali la sanamu hii, tabula ansata, ni tarehe ambayo Taifa la Marekani lilijitangazia Uhuru wake, Julai 4, 1776 -- Japo tarehe hasa ilikuwa Julai 2 ya mwaka huo.

Japo mapinduzi ya viwanda yalianzia Uropa, Marekani ni zao vuguvugu za kisiasa na mapinduzi huko Uropa na hasa mapinduzi ya Ufaransa. Misingi ya leo ya demokrasia ya kiliberali ilichipukia Ufaransa, na iliiona 'nuru ya asubuhi kule Marekani.

Awali, Marekani ilikuwa ni koloni la Monaki ya Kibritishi, chini ya Mfalme George wa Tatu, na ili kujitangazia Uhuru wake; Wawakilishi kutoka Majimbo 13 ya awali ya Amerika Kaskazini, walitia sahihi kupitisha Tamko la Uhuru, lililoandaliwa na Thomas Jefferson na kamati yake ya watu watano. Tamko la Uhuru la Marekani ni kati ya hati za kipekee sana katika historia ya dunia ya leo. Hata kwa mataifa mengi yaliyokuja kufanyika siku za mbeleni, Taifa letu la Tanzania kujumuishwa, yamekopa maudhui kwa ajili ya hati zake za 'Katiba' na 'Muundo wa Serikali'. Pia, wakati akina Jefferson, wakiandika tamko hili, walikopa mawazo kutoka kwa wafikirifu wa Uropa, siku zile za renasansi -- mawazo kama ya John Locke juu ya kusema: 'Utawala wa dola ni Mkataba kati ya watawala na watawaliwa kwa ridhaa' -- kule kusema : “their just Powers from the consent of the people.”

Fikirio hili kwa siku za leo ndilo kwa upande mmoja linashinikiza umuhimu wa demokrasia ya kiliberali ambapo serikali yaingia madarakani kupitia sanduku la kura na itaondoka madarakani kwa muda husika kama inaelekezwa kwenye katiba ya nchi. Wenye madaraka wote wabanwa na kuwajibishwa na mwongozo huu wa kikatiba ambapo ikiwa watataka kuendelea kuwa madarakani basi yawabidi kupata ridhaa ya watu kupitia sanduku la kura. Demokrasia ya Kiliberali ni fanusi ya michakato ya siasa za uwakilishi; mgombea hutafuta kuwakilisha jimbo lake la uchaguzi ili akifaulu apate 'kiti' katika 'baraza kuu la kutunga sheria' na kuisimamia serikali iliyoko madarakani.

Tanzania tuna mbunge moja lakini nchi nyingine wana mabunge mawili, ngazi ya chini na ngazi ya shirikisho -- japo shughuli ni zile zile.

Katika kuipambanua misingi ya hali kwa 'kuishi, liberiti na Udhamirifu wa furaha' -- kusema 'inalienable rights to life, liberty and the pursuit of hapiness', siku za awali za ujenzi wa serikali ya shirikisho la nchi za Amerika (Marekani), sera na mipango ya nchi ilisigana kati ya fikra za Thomas Jefferson na Alexander Hamilton. Hamilton alikuwa mtu wa ikulu(Hazina), mwanasiasa, mwanazuoni wa sheria, amiri jeshi, mwanasheria, mwanabenki, na mchumi. Alikuwa ni mmoja wa Waasisi wa Umoja wa Nchi za Merika(Marekani). Wakati wa kampeni ya Urais, Barack Obama
alipata kuhutibia hivi:

“...there was one thing that Jefferson and Hamilton agreed on: that economic growth depended
upon the talent and ingenuity of American People; that in order to harness that talent, opportunity
had to remain open to all; and that through education in particular, every American could climb the
ladder of social and economic mobility and achieve the American dream. In the more than two
centuries since then, we've struggled to balance the same forces that confronted Hamilton and
Jefferson: Self interest and community, markets and democracy, the concentration of wealth and
power and the necessity of transparency and opportunity for each and every citizen.”

"... kuna jambo moja ambalo Jefferson na Hamilton waliunga mkono: kwamba ukuaji wa uchumi

unategemea talanta na ubunifu wa Wamarekani; kwamba ili kuvuna matunda ya hizo talanta, fursa
haina budi kuwa wazi kwa wote; na kwamba kupitia hasa elimu, kila Mmarekani angaliweza
kukwea ngazi ya ujongeaji wa kijamii na uchumi na kuifikia Ndoto Amerika. Katika kipindi cha
zaidi ya karne mbili tangu hapo, tumekuwa kwenye harakati za kumizanisha nguvu zile zile ambazo
Hamilton na Jefferson walikabiliana nazo: maslahi binafsi na jamii, masoko na demokrasia,

'kukoleza utajiri na nguvu' na 'ulazimu kwa uwazi na fursa kwa kila raia mmoja'."
Barack Obama, on Renewing the American Economy. Speech at Cooper Union in New York, March 27, 2008.

Kusema hivi, kuna kuja kutokana ukweli kwamba: Jefferson hakupenda 'mfumo wa mabenki', utaratibu wa ukopeshaji na riba... Alitamani serikali iwe na namna nyingine ya kuchochea uchumi na kusimamia uchumi lakini si kuacha sekta ya fedha 'waachiwe walanguzi' -- hata kwa 'jina' ama 'sifa' ya 'serikali kuu'. Hamilton alikuwa anataka nchi 'ifunguliwe' kwa serikali kujenga miundo mbinu ya ardhini na kusimamia maendeleo na ustawi jamii lakini raia wa Marekani waachiwe kiujasiriamali na biashara, panapo ushindani na masoko, mwenye ubunifu, jitahada na nidhamu atafaulu kuifikia 'Ndoto Amerika' na si serikali 'kuwapatia' raia zake 'Ndoto Amerika' kwa 'dezo dezo' -- walau kuwezesha umma kupitia miundo mbinu na serikali kukusanya kodi...

Shauri la Mgongano kati ya Jefferson na Hamilton, linaasili ya harakati za maisha, mifumo, matatizo na 'kutingishwa kwa dola na mamlaka' hususani Ufaransa. Vuguvugu na fukuto la machafuko nchini Ufaransa lilianza kadri idadi ya watu ilipoanza kuongeza kwa kasi kati ya mwaka 1700 hadi 1789 ambapo idadi ilitoka takriban watu milioni 18 hadi 26. Matatizo ya ukosefu wa chakula cha kutosha kutokana na mavuno mabaya, chakula kupatikana kwa bei juu na ukosefu wa ajira. Aidha, mifumo ya ukabaila na ubwanyenye 'iliwashiwa moto' na raia kwa kudai kwamba hiyo ndiyo chanzo cha kukosekana na usawa katika jamii. Muingiliano wa dini na siasa nao ulionekana ni nuksi, na watu walianza kudai huo 'uondoke'; na pia 'komeshwa utumwa wa namna zote'.

Maneno ya Kifaransa kama Liberté, égalité, fraternité, yaliazmia ukombozi kwa umma kwa mapelekeo ya liberiti, usawa na udugu wa wanadamu wote... Kwa hivi liberiti si tu ni uhuru, liberiti katika mtu ni 'uhuru juu ya nchi' na pia juu ya 'hatma ya nafsi yake yeye mwenyewe' -- si kwa kufungwa na dini wala siasa. Hatma hii ya uhuru wa kujiamulia mambo yako mwenyewe, ikiwa katika tamko la nchi -- nchi kujitamkia uhuru wake, basi ndiyo hufanya muktadha wa 'Usovereini' wa nchi.

Na hapa ndipo mahala sahihi pakuzungumzia sera ni jambo gani...

Uwezo wa jamii, ndiyo ulalo unaounganisha 'Ontolojia ya Taasisi' na 'Sura na Mienendo ya Jamii'. Tathmini kwa mabadiliko ya Kijamii ni muktadha wa fanusi ya utendaji wa mifumo yote katika jamii. Kriteria ya tathmini yaweza kuwa mapana ya uchumi, siasa, jamii, utamaduni na mazingira.

Kwenye mazingira kuna wakati, basi zao la taasisi na wakati ni mfumo ambapo taasisi ni namna jamii inavyojitengenea kimuundo, ushawishi na vitendo. Hili kwa mfano wa Ufaransa, tunaona kulikuwa na shida katika utawala unaochanganya 'dini na siasa' kuhalisha miliki za Kifalme na utwaaji wa ardhi, miongoni mwa koo za kifalme na washirika wachache kiukitirimba wa madaraka na mamlaka. Watu wachache waliishia kuwa mabwanyenye
wenye ukwasi kwa gharama ya 'vibarua wanyonge' na utumishi wa 'watu wa daraja la kati'. Kukosekana kwa sauti ya wanyonge juu ya maamuzi na hatma ya maisha yao ilileta vuguvugu la machafuko kadri hali ilivyozidi kuwa mbaya kwa raia wengi waliokuwa wahanga wa mfumo mzima wa nchi na tawala. Vuguvugu hili ndiyo fukuto kwa mabadiliko ya kitaasisi, ambapo mahusiano ya kijamii yanaelekea kwenye kujipangua na kujipangua... Ikiwa hakuna mapango
mahususi wa kugema fukuto la mabadiliko, jamii huelekea kwenye 'anakia' -- machafuko na kutotawalika. Ndivyo basi ontolojia ndiyo kisomo juu ya jambo: jinsi gani taasisi hutungika, kutoka katika 'usikitu' kuwa 'kitu'... Kwa kuwa taasisi ni vishikisho vya muundo wa jamii na mpangiko wake wote mzima.

Dola, Bunge na Mahakama kwa mfano ni taasisi; vivyo hivyo kaya ya Mama, Baba na Watoto ni taasisi. Shule zote ni Taasisi kadri vile Mashirika ya Umma na Biashara ni Taasisi. Kwenye taasisi kuna watu, mahusiano ya kinguvu za ushawishi kwa wajibu na majukumu yake. Na basi, ontolojia ya Taasisi hupelekea vitendo vinavyokadirisha 'Sura na Mwenendo wa Jamii' husika. Sura ya jamii inaweza kuwa kisiasa, uchumi, jamii na mazingira ambavyo tunaweza kubaini 'Mabadiliko' ama 'Mambo kama Ilivyo' kwa hali ya 'maridhiano ama kushinikizana'-- kwa wenye kuzungumza lugha ya kiingereza wangalisema: 'Status Quo'...

Jamii inaishi katika ulimwengu wenye wakati. Wakati huja kwa majira, mabadiliko na muitikio wa jamii. Moja ya kusudi la msingi la jamii kudumu ni jitihada za pamoja kutafuta muafaka na changamoto za kiwakati na yachukuayo nafasi, kutumia rasilimali zao za pamoja, kujipanga ili kujitafutia uhakika wa mustakabli wao. Kwa mfano Ufaransa, siku za kuelekea mapinduzi kamili ziliambatana na uongozeko la watu na basi kadhia muambata. Watu hawakuridhika na hali zao, kadhia zao zilizaa kutoaminia kati ya watawala na watawaliwa -- hasa hasa miongoni mwa makundi ya wenyenacho na wasionacho; ambapo rasilimali mama kama ardhi kwa ajili ya mashamba na uzalishaji zilikuwa miliki za vibopa wachache. Watu wanapokosa mahitaji yao kimsingi, uvumilivu wao ni jambo la mapana ya wakati -- ikiwa hakuna suluhu ama muafaka, jamii inaweza kuingia kwenye mgogoro wa kiuchumi na siasa. Ufaransa, mageuzi yalikuja kwa mapinduzi kwa kuwa, kwa bahati nzuri, kulikuwa na vikundi vya wazi na kificho vyenye kubeba maono na fikra mpya. Hiki ndicho kilichosaidia machafuko yaishie kuwa ni mapinduzi...

Kiufundi, mapinduzi daima huwa si suluhu kamili...

Hii ni kwa kuwa mfumo mmoja unaweza kubadilishwa kuwa mfumo mwingine na hali 'mfumo' ni 'mfumo'. Sifa kuu ya mfumo wowote ni kuwa na vitu vitatu: mpaka, elementi za vitendo vinavyohusiana na kujilinda kimpaka. Hii ina maana mifumo yote yenye kadiri ya kushawishika na usifa akili hukinza mabadiliko. Pia ni kwa kuwa mfumo hutafuta hatima iliyo ni uhakika kwa maslahi ya taasisi. Epitomi ya mfumo ni paradaimu; na hii ni namna 'maneno juu ya jambo' yanavyotengenezewa 'vina vya tafsiri' na 'dhamiri' kwa 'mahusiano ya kivitendo' na 'nidhamu ama uthamani' kuathiri 'utendaji ama kujichukulia' kwa mtu mmoja mmoja ama hata vikundi--hata 'jamii', 'chama' na 'serikali kama taifa la watu'.Neno 'fanusi' lina msingi wa hisabati; kwamba jambo moja linauhusiano la lingine ambavyo jambo A linaweza kubadilika kisura, ukubwa ama hadhi kutengemeana na mchakato wa jambo B. Kwa mfano, ikiwa twataka kutathmini jambo A ambavyo hili linauhusiano wa moja kwa moja na jambo B kana vile Jambo B lafafanuliwa kwa mlinganyo 'y=X + c' ambavyo X ni 'kipandashuka' katika mlinganyo; basi tunaweza kusema kwa maneno: Uhusiano baina ya A na B ni kuwa kwamba jambo A ni sawa B ambavyo B ni fanusi ya X. Hii sawa na kusema, sura, ukubwa ama hadhi ya jambo A ni fanusi ya kipandashuka X...

Katika ulimwengu wa leo sayansi na tathmini, uhusiano wa mambo huenda sambamba na ukadirishaji. Kwa vivyo hata kule kwetu kupima mashauri na ukweli wa jambo hutubidi kuwa na vishikizo kwa hoja na tafsiri. Katika mfano wa Ufaransa, tunaweza kudai kuna uhusiano kati ya 'kusambaratika kwa jamii' na 'ongozeko la matatizo ya kijamii'; Suala linakuja, je tunaweza kutengeneza 'mlinganyo' ama 'modeli ya kihisabati kuthibitisha hili? Kusambaritika kwa kiasi gani, kivipi na kwa kutambuaje? Matatizo ya jamii ni namna ya fanusi mbalimbali, kujikusanyia pamoja, za vipandashuka; kwa wenye kuzungumza kwa lugha ya kiingereza wangeita 'Variables'--sisi wazungumzaji wa lugha ya kiswahili labda tunaweza kurasimisha neno 'varaya' kwenye istilahi za visomo vya hisabati -- ila kwa humu, tuendelee kutumia 'kipandashuka/vipandashuka'... Sasa, kwenye maarifa ya sayansi ya leo ya jamii, kuna shida juu ya 'ugumu na ukadirishaji' wa mambo ya jamii, hisabati zote ni namna moja kati tatu (1/3) -- katika kubainisha sura na mienendo ya jamii.

Mashauri haya ni sehemu ya kuandaa umma na 'hadhi ya pili ya kubayanisha' mapana na mahusiano ya jamii: 'Jeometria ya Utendekavyo wa Maamuzi Jamii'... Zaidi, tunajinasibu na lugha ya alama kuhusiana na mambo yatendekayo...

Sera ni mwongozo kwa mabadiliko yanayotakiwa ama kutarajiwa.

'Mapungufu ama kujiweza' kwa jamii yoyote ndiyo mwanzo hitaji kwa sera kupambanua muktadha wa mabadiliko katika kuelekea kwenye 'sura bora ' ama 'kutengemaa' kwa mambo yake. Sera huongoza utendaji, kwa kauli na maelekezo kwa vyombo husika -- ilivyo ni muktadha wake kwa 'taasisi' na 'instrumenti/nyenzo' --kwa ufanisi wa shughuli yake.

Sera huwa na wakati wa kuanza kutumika kutawala utendaji na pia huwa na wakati kwa hitaji katazamwa upya ili kubaini lolote la kupitiwa upya mara baada ya mapana fulani ya utumikivu wake. Sera za jamii hulenga kuleta majawabu katika kuipatia jamii usawa, kwa manufaa ya utekelezaji wake wa huduma za msingi kama vile maji, nishati, barabara, mipango ya makazi na matumizi ya ardhi, mazingira, ushirika, elimu n.k; na basi haki zote za watu na jamii huwa na misingi serikali kuwa na dhamira ya kweli na wazi kuwatumikia raia wake pasi ubaguzi wa aina yoyote ama kukosa kutambua makundi ya uhitaji maalum katika jamii.

Katika mfano wetu wa Ufaransa, tunaweza kubaini bado miundo ya kiutendaji ya serikali haikuwa imeshupaa na kwa sehemu kuwa utawala ulikuwa ni 'siasa mbovu za kikabaila'. Shauri la haki, japo hutajwa kwenye katiba lakini ukweli wa jambo lake ni kutokana na dhana ya serikali kuwa taasisi ya utumishi wa umma, kuwakilisha maslahi ya umma. Daima taifa, na stawi yake huwa na 'sifa ya mama' kukaa mahala pa serikali -- ndiyo maana hata Liberta, alikuwa ni mungu mke kwa Warumi na wakati mwingine alama yake huwa mtu mke mshika mizani upande mmoja wa mkono na mwingine kuinua upanga huku akiwa kafumbwa macho... Hii ilikuwa ni ishara ya haki mbele ya watu pasipo kumtazama mtu ni nani mbele sheria. Liberté, égalité, fraternité, ni kwa jamiiinayotafuta kuyafaida matunda ya stawi zao, sawa kwa sawa, na kama ndugu moja -- haki ni 'tunda la dhamiri ya usawa na kugawana mema/mabaya kupitia makusudi ya maridhiano fulani ya kijamii'.

Jambo la 'sawa kwa sawa' ndilo hadi leo lina utata; kwa baadhi ya watu huona hilo ni mapelekeo ya 'ukomunisti'. Katika jamii ya kibepari, 'sawa kwa sawa' ni sawa na kusema 'kile cha kufukuziwa lakini kamwe kushikwa'. Kwa mfano wa Amerika, Jefferson alihofia 'udhalimu' serikali ikishikilia njia kuu za uchumi--kama ilivyokuwa kwa mabwanyenye wa uropa na serikali za vikundi vya watu wachache. Hamilton alihofia 'anakia' kwa kufikiria jambo juu ya mpangiko wa mambo -- kinga dhidi ya watu kuja kuona wamebanwa kiuhuru wao kiuchumi na stawi juu ya nchi. Kimsingi,
hakuna awezaye kuwatumikia mabwana wawili--wa kujilimbikizia mali na wa kugawanyisha mali, Marekani kwa nje 'walisulubisha msalabani' jambo la 'sawa kwa sawa' ya matunda ya fanaka na ustawi wa nchi ndiyo maana ni jambo kawaida kuwakuta mabilionea na mamilionea wakiwamo taifa moja na watu wasiokuwa na mahala pa kuishi -- watu wanaolala barabarani.

Kivielelezo vya nchi-taifa, kuna wakati kwa mfano, nadhiri ya imani kwa Bendera ya Nchi(Kielelezo kwa uzalendo,
usovereini na ushindi dhidi ya vita ya wenyewe kwa wenyewe) na Nchi ya Marekani, ilikuwa ikisemwa:

We give our heads and hearts to God and our country; one country, one language, one flag!
(Utunzi wa Col. George T Balch, 1887)

Twatoa vichwa na mioyo yetu kwa Mungu na nchi yetu, nchi moja, lugha moja, bendera moja!
Mnamo mwaka 1895, Mchungaji Francis Bellamy, akaifanyia marekebisho ili iseme:
I pledge allegiance to my Flag and the Republic for which it stands, one nation, indivisible, with
liberty and justice for all
Ninatia nia ya upande mmoja na bendera yangu na Jamuhuri isimamiayo, nchi moja,
isiyogawanyika, yenye liberiti na kutendewa-haki sawa kwa wote
.
Mwaka 1945, maneno 'under God--chini ya Mungu...', Kuibainisha kifikra kati ya Marekani na Nchi za ki-Marxist-Lenin, yaliongezwa na kwenye dhamiri hii ya uzalendo; kwa rejea kwamba aliyepata kwa Rais wa Marekani, Abrahamu Lincoln alipata kusema:
"Taifa chini ya Mungu, litapata kuzaliwa upya..." Na hivi tangia hapo, Mashuleni vijana hufundishwa kuimarisha dhamiri zao kwa kusema:
Ninatia nia ya upande mmoja na bendera yangu na Jamuhuri isimamiayo, nchi moja, chini ya Mungu isiyogawanyika, yenye liberiti na kutendewa-haki sawa kwa wote.
Basi Mchungaji Bellamy, akiwa ni msoshalisti, alisita kuyaweka maneno 'Equality and Fraternity-Usawa na udugu wa Wanadamu' kwa kuhofu kuwakwaza wasimamizi wa jitihada za uamisho wa hamasa ya kitaifa kwa kuwa wengi wao kipindi kile walikuwa kinyume na 'haki za wanawake' na pia 'haki kwa Wamarekani weusi'.

Haya yote basi yamekuwa mashauri kwa 'vina vya tafsiri' za katiba, kuliko sera...

Kudhania Katiba ndiyo italeta 'mabadiliko ya kweli' ni kujidanganya... Kuna vitu vitatu vinavyokazia muktadha wa mabadiliko, (1) dhamira safi ya kisiasa, (2) mipango kwa mujibu wa sera bora zinazotekelezeka na (3) uwezo wa kijamii unaoendelea kutengemaa kiakili, hisia na utamaduni. Kwa hivyo, kuna namna dhamira ya kisiasa inaweza kushinikizwa kwa advokasi ambapo mkakati kabambe unaweza kutumika kufikisha 'vilio' vya watu wahanga wa sera
zinazoumiza hapa na pale ama kupunja mategemeo -- kufikisha 'vilio vyao' kwa 'wafanya maamuzi'.

Pia mipango ya nchi katika ngazi mbalimbali inaweza kuwekwa kwa namna za 'ushikirishwaji'. Tanzania kwa mfano, suala la mipango kwa ushirikishwaji lipo kisera na utekelezwaji lakini labda kwa sehemu kubwa wananchi aidha 'hawana habari' ama 'ushiriki wao ni hafifu' kila mara nafasi inapotolewa ili washiriki katika tathmini za gurudumu la mipango.

Kwa hivyo kiufundi, Mtendaji Mkuu serikalini akisihi tuvumiliane ili mambo ya 'kujengea jamii uwezo' yachukue nafasi na pia kwamba jitihada za mkondo huo ziendelee; ni wajibu wa kila raia mwenye mapenzi mema kujifikiria na kujitahidi kuelewa mambo. Sera na Mipango havipaswi kuachiwa kikundi cha watu wachache, jamii inawajibu kufuatilia utendaji wa watumishi katika utekelezaji hivyo; na pia, kutafuta yale ya kuboresha mikakati na miradi ya maendeleo iliyopo.

Viwili hivi vinadumu zaidi kuliko hatamu za kimadaraka ya kisiasa. Ikitokea hata jamii kutokujali na kutilia mkazo hili, wanasiasa wanaweza kuvuruga mipango na mikakati ya maendeleo ili watengeneze umaarufu wa chapu chapu kwa ajili ya kutafuta kushinda uchaguzi.

Ikiwa Jamii bado haina uwezo wa kutosha kubaini walau matatizo na mapungufu katika utungaji wa sera za ustawi wa jamii na utekelezaji wake; basi hata suala la Katiba mpya haliwezi kuahidi na kutimiliza chochote. Vivyo hivyo, kama jamii haishiriki vyakutosha katika mipango ya maendeleo kwa ngazi mbalimbali... Kwa kuwa ni watu wale wale wanaoshindwa kujitambua kwa nafasi zao --wenye wajibu na majukumu yao ya kila siku -- wanataka kivingine, kujinasibisha na Katiba mpya.

Katiba si kisomo useme kitawatia watu mwangaza. Katiba ni kama lugha kwa mabadiliko ya muundo mzima wa dola kama taasisi ndani ya taasisi lakini si uhakika wa mapito. Hii ni kwa kuwa 'tabia' na 'utayari' wa watu vinaweza kumudiwa vizuri na sera kuliko Katiba. Watu wasiojitambua vya kutosha kisiasa, uchumi na utamaduni ni wahanga wa siasa chafu, wakiruhusu kuchezewa ni michezo yake. Walau ndivyo kusema, anayeshiriki katika shughuli za moja kwa moja za maendeleo sambamba na majukumu yake ya ajira, kujiajiri, biashara ama huduma, huyu si tu anajenga nchi,
bali anajijenga na utu wake.

Kufika hapa, tuhitimishe kwa chukuo --moja, uwezo wa jamii kuyamudu mabadiliko ni jambo la sanaa, ufundi na mikakati -- yenye kuongozwa nusu na jitahada za kawaida, lakini kwa mara ya kwanza, itajwe -- kwa 'mkono wa asiyeonekana'... Tumetumia mfano wa Amerika na Ufaransa, lakini hatajuingia kubaini upande wa 'gizani' wa mambo.

Nchi zote duniani leo hii zinasimama kwa misingi ya 'sera za wazi' na 'sera za gizani'... Katika ulimwengu wa mifumo dume, nchi huendeshwa kwa siri za kiutendaji ambazo zinamanufaa yake na pia mapungufu yake. Busara ya usiri ni rahisi tu kubaini misingi yake -- kwa sisi Wabantu tuna kitendawili... 'Kitendawili... Tega... Tega nikutege... Mwiba...'

Maana ya kitendawili hichi ni kwamba, kuna namna ikiwa njia yako iko bayana hata kwa
jambo nyeti ambalo usingalipenda kabisa lijekuwekewa vizingiti basi utalificha jambo hilo kama sehemu ya wewe kuwajibika kulilinda jambo lako. Utalificha hadi pale matunda yake yake yatakapokamilika...

Katika Mifumo Mama, paradaimu ambayo sasa hivi tupo kwenye kipindi cha mpito kuelekea kukata shauri kuikumbatia, usiri wa mambo ni sanaa rasmi na ina busara yake. Tofauti na mifumo dume ambapo mambo hufanywa siri ili tu kuepukana na 'tega nikutege'... Kwa Mifumo mama jambo huwa la chini chini ama kimya kimya kwa kuwa tu mabadiliko si 'fimbo' ya kuja kuchapia wengine ama kutambia wengine. Mifume dume inatambua mipango na mikakati ikiwa na sura nyoofu ni rahisi mwingine akakutangulia kwa mbele na kuja kukuzingua mapito yako ikiwa
anakuona wewe unakwenda 'kucheza karata dume ya shupaza'; labda iwe kwa kwamba wewe ni mjanja -- una njia zaidi ya moja, ila hiyo 'unayouza' kwa umma inaweza kuwa ni ya ukweli ama 'danganya toto...'

Mifumo dume inagharama kubwa kwa umma ili ijidumishe na idumishe 'hali ilivyo'. Kwa sehemu kubwa michezo yake huishia kufaidisha wachache--Watemi na Malkia wa nguvu. Hawa, kwa mujibu wa 'nadharia ya mchezo', wanaweza kutumia 'Wajanja' wa mchezo kufaulisha utawala wa mchezo. Wenye kuzungumza lugha ya kiingereza wangaliwaaita hawa 'Jackals'...

Wajanja ni watu wa weledi ambao pia ni mafundi wa mipango na hadaa kwa ajili maslahi ya Watemi na Malkia wa nguvu. Wajanja katika ulimwengu halisi ndiyo wasomi -- labda hata wabobezi wa uchumi, tiba, sayansi, tekinolojia n.k. Wanaweza kuwa ni watu wa nyadhifa za juu juu huku na kule ambao kimsingi: ni werevu kwa nje nje lakini kiuhalisia ni 'wachumia matumbo' na 'wajasiriamali-mifumo'. 'Wajanja kutoka nje' wanapohusiana kivitendo na 'watendaji wanaolengwa wa ndani' basi wa ndani wanaweza kuhadaiwa kama vile 'karata shupaza' inavyopiku 'Karata Galasa'...

Magalasa, Watu ambao ukiondoa pazia la mifumo, hukutwa ni binadamu wenzetu wenye udhaifu wa utegemezi mifumo, wenye makusudi yenye kuharibika upesi, na kusema pasi simile--ni watu wa tabia mbaya. Jamii ina mwelekeo mzuri ikiwa walau 'Wajanja wa ndani' ni watu wa 'tabia njema' -- vinginevyo, kama wajanja wa mfumoni 'wanajichanganya', mwanakulikoroga mwana... ndiyo huzaa mapinduzi kama ilivyopata kuwa katika ule mfano wetu wa Ufaransa...

Hufika wakati, umma hauna budi 'kupewa dawa'...Ikiwa umma unapewa mbinu za kufikiri na kubaini asili na mienendo ya mambo, pasipo hadaa ya utumikivu wa vyombo vya habari, basi tunaweza kuepusha michezo isiyokuwa ya lazima.

Jamii yahitaji uwezo wa jicho lenye kubaini 'mali' ama 'galasa' katika mchezo. Ufikirifu kwa ufaktali wa utatusho ni jambo ambalo kwa muda mrefu imekuwa 'karata ya shupaza ya Wajanja'... Mashauri ya humu yote yameongozwa na ujuzi na ufundi wa ufraktali katika uwezo na ubainifu wa mambo...

Hili, kwa kipindi hichi, likizingatiwa na wengi wenye nia ya kujinasua na michezo isiyo ya lazima, basi watakuwa na ujuzi wa kuzungumza kwa lugha -- na basi kuwa na mawasiliano yenye ufanisi wa hali ya juu kuhusu jambo lolote, tukio lolote na maarifa yoyote. Kushiriki maarifa haya kwa sasa na hapa ni kwa ajili ya kuuandaa na kuujenga umma wa waTanzania na watu wote wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili -- na ulimwengu shujaa wa kesho ambao kwa wengine unaweza kuwa ni leo, hapa na sasa.

Vinasaba kinavyokadirisha 'miundo' na 'vitendo' vinavyopelekea kubadilisha sura, hadhi, sifa na hadhi ya jamii ndivyo hufanyiwa kazi hata kupitia sera na sheria ili kugema mazuri ya mfumo na tena kwa maridhiano ya kheri ya pamoja. Kwa misingi ya namna hii hii hata matukio yanaweza kuhandisiwa kwenye jamii ili kushinikiza mabadiliko ya 'sera' na 'sheria' kwa umma, kokote duniani kwa kulenga 'vinasaba' vya watu, jamii na taasisi zinazolengwa. Vitu kama 'hofu' na 'uhisi wa vitisho' zinaweza kuwa zana za kuthibiti vitendo ama kuwachorea watu uelekeo wa kusombwa na mabadiliko yanayohandisiwa. Dialekti ya Hegeli ni mfano wa jambo hili. Linaweza kusukwa jambo kwa ufundi mkubwa ambapo mawazo, fikra na maoni ya watu vitachezeshwa shere... Kabla ya watu kutambua wanachezeshwa 'ngoma ya ukae', kambi mbili zinazopingana 'kimaoni' kuhusu mapekeleo ya maamuzi ya kuchukua, hawa wanakuwa tayari wameshaandaliwa la tatu ambalo limeshategeshwa 'kukubalika'... Suala la Uviko19 ni moja ya matukio ya hivi karibuni ambayo yanaonesha dalili zote za 'mchezo'... Humu katika jamii forums, mashauri la angalizo kwa mchezo
huu yameshapata kuwekwa humu...

Ni vema umma ukajengewa uwezo wa kufikiri na kubaini sura na mienendo ya mambo. Isiwe tena 'tegemezi' kwa 'matamko'... Tuyayumbishana sana na tutababaishana sana tukibakia na hulka na tabia hizi. Kuna hatua za kuchukuliwa na serikali, na kuna uwajibikaji wa sisi raia 'kuvunja ukimya'. Vigugumizi vipo, lakini isiwe sababu ya watu kusakamana. Wabantu tunamsemo, usione kobe kainama kimya...

Wengi wetu, kwa kukosa moyo wa kujali, tunaziba masikio hata kutozingatia busara ya kawaida ya mambo. Mtawala anapowaasa watumishi wenzake wasijisahau kwenye 'viti'; kuna neno... Anapowaasa waache 'kupandisha mabega'; kuna neno... Anaposema wawe waadilifu; kuna neno...

Ndiyo, siyo lazima kujikombakomba kwa mkuu ama kuwa na misimamo inayoyumbayumba; siyo lazima kuimba mapambio na kumbe ni namna ya kutetea unga wako. Simamia maadili ya kazi lakini usisahau na akili ya kujiongeza. Jua la kusema na usiogope kupingwa -- wala usitafute kuwa mshindi eti oh mimi wazo langu ni bora kuliko mengine... Tabia mbaya ya watu ama watumishi kupenda kuonekana 'wako sahihi pasi kupingika' kwa kuonesha msimamo huu ama ule mbele ya halaiki iliyo kwenye sintofahamu inaleta matatizo katika jamii yetu yasiyo ya lazima...

Ambacho hawa wa namna hiyo wanakosa busara ya jambo ni kwamba, kila msimamo una gharama yake... Usitake msimamo mkali wakati gharama yake hauiwezi, na wala usitake misimamo nyoronyoro ili tu 'uuze ama kununua kambi'. Ipo namna na ufundi wa kujenga na kutetea misimamo ambayo yahitajika sana katika mifumo ya leo ya uwazi na uwajibikaji... Kaka Mkubwa Ndugai aliposema, na kwa kupangilia upya maneno, tumeshapitisha suala la tozo la kizalendo mtandaoni na sasa ni sheria... Ikiwa mtu anadhani hilo halifai basi atumbie tungalifanyaje vinginevyo ili tusonge? Kulikuwa na neno...

Kiongozi wa awamu ya Tano alituacha imara na Tanzania salama; bado tunayonafasi ya kujijenga na kujiimarisha zaidi. Na kama shukrani kwa ujasiri wake siku za mwisho, hatuna budi kushirikiana kwa pamoja kuijenga misingi ya nchi yenye maendeleo ya ukweli na inayokamia kujitegemea kwa kiasi kikubwa. Kama ilivyo ada, tutajifunza lugha ya uwazi tu na si tena kuendekezakana kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa. Yeye 'aliyetutangulia' shughuli yake ilikuwa katika ulali wa 'mipango na maendeleo'; na alikuwa akiitendea haki 'signali' ya 'kuelekea kuijenga Afrika Mpya'...
Awamu ya tano, Kiongozi alikuwa na sifa za kipekee kwa 'shughuli' hiyo... tuliita 'kunyooshwa'...

Awamu ya sita ina nasibu ya ulali 'kujengea Jamii Uwezo'... Kwa hivi, ikiwa tunajicho la kubaini haya, badala ya kuendekeza 'politiki' ni vema tukashirikiana kwenye kuhakikisha taifa hili linakuwa na sera bora na zinazotekelezeka... 'Politiki' haikuwa nzuri kwa awamu ya tano, na wala si nzuri kwa Awamu hii ya sita... Anayeshika hatamu awamu hii, anaasili ya shughuli za 'utetezi wa umma'...

Ikiwa wengi watataka kuwa ni wa msaada kwa gurudumu la maendeleo linalozunguruka sasa basi ni vema waelewe: 'Uwezo wa Kijamii' ni jambo lenye vinasaba vya 'Tabia Njema'... Ni vizuri watu kwa jamii na taasisi zao wawe na adabu, kujiheshimu na kuelekezana kadri ifaavyo. Si lazima ubabe, lakini unafiki ni mbaya...

Hmmm
 
Ilo la Kodi bhana, tumwachie mungu aingilie Kati maana Kodi kubwa ndiyo inawahusu wenye vipato vya chini tu
 
Back
Top Bottom