Ushauri wa lazima: Mbowe muombe Zitto awe Naibu Kiongozi wa upinzani

Sawa, ni ushauri zuri ila tatizo woga wa kufunikwa na kupoteza uenyekiti kimekuwa chanzo kikubwa cha mbowe kutomtaka ZZK katika muungano huo - Ni kweli sasa hivi chadema inabidi ijikite ktk matukio badala ya mipango endelevu (Kutoka kwa ZZK na Slaa katika chama kumeweaken sana siasa za CHADEMA)

siasa kwa upande mwingine hazina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu - hv sasa ni muda mzuri wa kujenga upinzania wenye nguvu bila kubaguana.
Awe mwenyekiti mara ngapi si ana chama? subirini miaka mitano ya ACT ndio mje na comment kama mtu wenu anafaa kuwa mwenyekiti au la? kila mmoja anafaa pale alipo ni sawa na kumlazimisha back awe striker
 
Kuna watu walitaburi mengi mno kwa Zitto ikiwemo na kupotea kisiasa

Lkn kinachotokea wanashindwa kuamini maana amekuwa mtamu kama mcharo huku akiwaacha wale wanaowaamini wakibaki kwny ngonjera zisizo na mantiki. Zitto ni mwanasiasa wa kweli wala mbabaishaji kama Mbowe
Zote zilikuwa ni siasa mfu za kungojea mkono udondoke kama fisi.
 
Hakuna shaka kuwa ufahamu wa Zitto ni mkubwa. Angekuwa mwaminifu angeweza sana kuwa msaada kwa nchi yetu ikiwa ni pamoja na Bungeni. LAKINI hakuna shaka kuwa huyu Mh. Zitto ni msaliti au tuseme alifanya usaliti wakati akiwa CHADEMA kwa maslahi binafsi. Kosa la usaliti ni dhambi kubwa sana. Sio la kusamehewa au kusahauliwa. Kwa serikali hii ambayo inaonekana haikon tayari kumuajiri na kumlipa mtu eti atoe siri za chama kingine kweli Zitti ana hali mbaya. Alipokea mapesa wakati huo sasa hayapo na haaminiki. Ndio maana atahangaika sana lakini kwa wapinzani serious hawawezi kumwamini japo atapigiwa debe na mawakala wake kama kwenye hii thread. Majuto siku zote ni mjukuu.
Ndivyo mnavyokaririshwa hivyo na mbowe?? Tumia akili ya kuzaliwa wewe
 
Zitto ana akili nyingi kuliko Mbowe lakini haaminiki hata kidogo. Once bitten twice shy
 
Amani iwe kwenu.

Sasa imebidi Mbowe aelewe bila kificho kuwa amepwaya kuwa KUB. Imefika wakati lazima ajue KUB ni mtumishi wa umma kama mawaziri hivyo tunalazimika kumwambia ukweli kwa manufaa ya taifa.

mbowe.jpg


Hivi sasa upinzani bungeni umejigawa katika pande mbili; wanaojiita Ukawa chini ya Mbowe na ACT Wazalendo chini ya mbunge pekee Zitto Kabwe. Imedhihirika dhahiri shahiri wabunge wa "ukawa" michango yao imejikita kwenye kushambulia watu na sio hoja ukilinganisha na Zitto ambaye michango yake imejikita kuleta fikra mbadala katika kuharakisha maendeleo ya wananchi.

KUB Mbowe anahitaji "back up" ambayo Zitto alimpa bunge la 10 iliyoficha mapungufu yake lukuki ikiwemo kiueledi. Kushirikiana na Zitto sio tu itamwezesha kutumia kipaji chake bali itaziba ombwe la uongozi kambi ya upinzani. Amethibisha uwezo wa kushawishi kambi zote bungeni kuacha itikadi na kusimamia serikali ambapo mara kadhaa mawaziri waliwajibika.

Zitto-Kabwe-na-Mbowe-Feb-3-2016.jpg


Mbowe wabunge wengi ulionao ni mizigo waliojaa ubishi na uongo.

Pia nawaeleza wabunge kuwa vijembe, bunge live na matusi havileti maji, barabara, madawa nk kwa wananchi hivyo mjikite kwenye mijadala yenye tija.

Hoja hii ni ya ushauri wa lazima japo una hiyari ya kuchukua ama kuacha, ila muda ndio jibu.

Nawasilisha.
Umekuwa walazima tena, ina maana asipo afiki kuna hatua gani zitafuata?
 
Ninaona hoja yako umeianza vizuri ila unahaributu unaposema wabunge wa upinzani ni waongo na watoa vijembe.
Kama lengo nikutaka Zitto aungane na UKAWA ili kuongeza nguvu ni hoja nzuri inayojadilika bali kama unataka aende akasaidie kwakua kuna watoa vijembe na uongo ninaona hakuna hoja ya kujadili

Naomba nikuulize mleta mada kwamba,hivi Milinga na Marwa nao ni UKAWA?Au unadhani kutukana ni itikadi ya chama fulani?

Kama Zito ni muarobaini wa vijembe,washauri hata upande mwingine wamchukue

Ninachukia wabunge wote wazomeaji,watukanaji bila kujali itikadi zao.Mshauri Spika asiyumbishwe hakutakua na vijembe,matusi wala uzushi.
 
Mmempokea Lowassa na majipu yake itakuwa ZZK mwenye chunusi za plastics?

CHADEMA na wakuu wake wanalijua sana hilo. ZZK sawa na wapinzani wote mle pamoja na nusu ya wabunge wa CCM.
Hakuna shaka kuwa ufahamu wa Zitto ni mkubwa. Angekuwa mwaminifu angeweza sana kuwa msaada kwa nchi yetu ikiwa ni pamoja na Bungeni. LAKINI hakuna shaka kuwa huyu Mh. Zitto ni msaliti au tuseme alifanya usaliti wakati akiwa CHADEMA kwa maslahi binafsi. Kosa la usaliti ni dhambi kubwa sana. Sio la kusamehewa au kusahauliwa. Kwa serikali hii ambayo inaonekana haikon tayari kumuajiri na kumlipa mtu eti atoe siri za chama kingine kweli Zitti ana hali mbaya. Alipokea mapesa wakati huo sasa hayapo na haaminiki. Ndio maana atahangaika sana lakini kwa wapinzani serious hawawezi kumwamini japo atapigiwa debe na mawakala wake kama kwenye hii thread. Majuto siku zote ni mjukuu.
 
Back
Top Bottom