Ushauri wa haraka kwa CHADEMA

Huyo dada YEHODAYA hayuko sawa upstairs. Bado ana athari kubwa za kutimuliwa CHADEMA.
Kumbe ni dada?!, mimi nawapendaga sana watu wa aina hii wenye matatizo, kwa sababu specialization yangu ni kutatua matatizo ya watu, nitampataje nimsaidie?. Kama anataka kupiga pesa msibani, basi tatizo lake kubwa nimeishalijua na liko ndani ya uwezo wangu!.

P.
 
Jamani, nini sasa hii, watu mnajitoa ufaham, matusi meengi.
Natoa pelo sana kwa wafiwa wahusika, wengine nyie aaah mtakuwa mnajifanya kuhuzunika huku mnaangalia wapi pa kupata moto na baridi.
Ila mnachonikera wachaga mnapenda kukaa sana na maiti. Mnaweza kukaa nayo wiki nzima, sijui kwa nini,
Apumzike kwa amani mzee wetu
 
Kuna taarifa kuwa aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Phillemon Ndesamburo amefariki dunia. Kila mmoja, mwanachama na asiye mwanachama wa CHADEMA atakubaliana nami kuwa Ndesamburo alikuwa mzizi mkuu na ngome ya CHADEMA mkoani Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini kwa ujumla.

Ndesamburo alikuwa mpigania chama, mjenga chama, mfadhili wa chama na kioo cha CHADEMA. Ndesamburo ndiye aliyekuwa kielelezo cha CHADEMA kwa kauli na matendo yake. Wananchi wa huko Kilimanjaro na Kaskazini kwa ujumla walivutiwa hadi kujiunga na CHADEMA na matendo na maneno ya Ndesamburo ndani na nje ya Bunge.

Nje ya maisha ya kisiasa, Ndesamburo alikuwa mlezi, mzazi, mnyenyekevu, mcheshi, muungwana, mwenye roho isiyo na inda wala mawaa na mtu mkweli. Aliwapenda waliompenda na hata wasiompenda. Alipendwa kwakuwa alikuwa akiendana na mazingira aliyokuwamo. Ndesamburo alisaidia panapohitajika na kubuni kwa kuwapeleka wananchi wa Tanzania mbele.

Kutokana na umuhimu wake ndani ya CHADEMA na kwa demokrasia ya nchi kwa ujumla, naishauri CHADEMA iahirishe shughuli zake zote na kujihusisha na msiba huo wa Hayati Ndesamburo. Hayo yatakuwa ni malipo yake stahiki kama mwanachama wao, mlezi wao, mpiganaji/kamanda wao, mfadhili wao, kivutio chao na wakujivunia wao.

Najua, Moshi Mjini, Kilimanjaro na Kaskazini yote itatikisika kwa maombolezo. Hakika, Ndesamburo ni nembo ya CHADEMA Bungeni na nje ya Bunge katika siasa za vyama vingi hapa nchini. Rest in peace the late Phillemon Ndesamburo aka Ndesapesa!

Ninadhani Ndesamburo ni kati ya wale tunaowaita inborn leaders,kabla hajafanya kila mtu anamuona kama anafaa kuwa kiongozi.
 
Hotuba haziziki mtu mselewa na akina mayala na wengineo mnaojitia mna uchungu sana na kifo cha ndesamburo na mnakuja na mapendekezo kibao mnachangia shilingi ngapi Ili ndesamburo azikwe kwa heshima zote mnazopendekeza?
Mkuu Yehodaya, nimeelezwa wewe ni she!, kwanza pole kwa sababu una matatizo fulani bila kujijua!. Mtu sio ndugu yako, heshima na uwezo wake unajulikana, ndugu jamaa na marafiki zake wanafahamika na uwezo wao kiuchumi unajulikana, kitendo cha wewe kuja humu jf na kuanza kuhamasisha michanga ili Ndesa azikwe kwa heshima, ni kumdhalilisha na kuidhalilisha familia ya Ndesa, please stop hili la michango!.

Pili nimejitolea kukusaidia, hivyo nitakupandia in box tupange jinsi ya kukuona na nitakusaidia sana, kwa sababu nimesaidia wengi wenye matatizo kama yako.

RIP Ndesa Pesa.

Paskali
 
Huyu alikuwa ni miongoni mwa watanzania wachache wenye uchungu na nchi yao na ambao hawakupenda kabisa hata rangi tu ya magamba. R.I.P our grandfather
 
Naunga mkono hoja. Hata kama Chadema wenyewe waliishapanga kufanya hivyo, maandamu hakuna anayejua walipanga nini hivyo ushauri huu ni muhimu sana kuuzingatia, na sio tuu kwa heshima ya Marehemu, bali pia kwa mustakabali mwema wa majaaliwa ya Chadema mbele ya safari, kwa kuzingatia sana Tanzania tuna makabila na makabila, mila na mila na imani na imani, miongoni mwa vitu vinavyoheshimiwa sana Kanda ya Kaskazini ni misiba, hivyo ni kweli Chadema isimamishe kila kitu, na kama wanawasombaga watu kwa mabasi na malori kuwapeleka kushiriki maandamano, sasa wawahamasishe kujitokeza kwa wingi kushiriki msiba huu mzito, hata mimi japo sio Chadema lakini nitashiriki kwa sababu kila nikienda Moshi, hufikia hotelini kwa Ndesa na nina special discount, sasa sijui kama itaendelea.

Mzee Ndesa na Prof. Beregu ndio viongozi pekee wa Chadema, wenye kuonyesha ukomavu na busara za hali juu, ambao sikupata kuwaona au kuwasikia wakichangia ujinga ujinga, au akishiriki kwenye mambo ya kiajabuajabu na kiuanaharakati ya Chadema ambayo lengo huwa ni ku attract tuu attention lakini hayana maslahi yoyote kwa chama wala taifa, he was cool, mature, sensible na very wise.

RIP Ndesa Pesa.

P.
Tutakutana MOSHI Paschal. Nimeumia sana aisee. Napanga safari fasta
 
Mchango wako wa mawazo umekaa KIUNAA UNAA Pasco, ila nakuacha kwa sasa kwani sio wakati mzuri wa kuleta majibishano ambayo wewe umelenga kuyaanzisha.
Naomba hata hiyo discount uliyokuwa unapewa pale Hotelini waisitishe kabisa.
 
    1. Kada wa CHADEMA JF-Expert Member
      [HASHTAG]#234[/HASHTAG]
      51 minutes ago

      Joined: Feb 27, 2016
      Messages: 287
      Likes Received: 582
      Trophy Points: 180
    1. Kuna leadings ambazo zinatia shaka juu ya kifo cha mzee wetu Ndesamburo.

    2. Aligombea uenyekiti wa CHADEMA kanda ya Kaskazini huku akikabiliwa na shutuma kuwa anakipasua chama.
    3. Mbunge wa Moshi Mjini Jaffar Michael alikuwa na ugomvi mkubwa na Mzee Ndesamburo na inashangaza alikuwa na mahaba naye kuanzia wiki moja iliyopita.
    4. Safari ya Kalist Lazaro kwenda kuchukua Fedha za Rambirambi kwa Mzee Ndesamburo imekuwa na wingu nene kwani kabla hajaenda kwa mzee Ndesamburo, alipitia nyumbani kwa Jaffar Michael haijajulikana alienda kufanya nini.
    5. Kalist Lazaro alipoenda kwa Mzee Ndesamburo alikuwa na hofu kubwa inayotiliwa shaka.
    6. Akina Lazaro walimkuta Mzee Ndesamburo anakunywa chai. Alipoingia chumbani kuchukua Check ili aandike kiasi cha fedha kuna uwezekano kuna something iliwekwa kwenye chai na ndio imesababisha umauti wake. Lazaro anajua.
    7. Inadaiwa kuwa Mzee Ndesamburo alikusudia kutoa hundi ya milioni 10 kwa jina la Kalist Lazaro lakini aliandika milioni 100. Alipogundua kuwa amekosea wakati tayari amemkabidhi Lazaro, alimtaka airejeshe ili arekebishe, Kalist akajifanya anaenda kwenye gari kuchukua simu. Akaondoka na cheki hiyo na hakurudi tena. Huku nyuma mzee Ndesamburo hali ilibadilika na ndipo alipokimbizwa hospitali.
    8. Baada ya kifo cha Mzee Ndesamburo, akina Malisa na Ali Bananga wanatumika kusambaza propaganda kuwa Mzee Ndesamburo alikuwa hajaandika Cheque. Uongo mtupu.
    9. Kuna taarifa kuwa fedha hizo Kalist Lazaro alienda kuzitoa kwenye Benki ya CRDB Moshi Mjini kabla ya taarifa ya kifo cha Mzee Ndesamburo kusambaa.
    10. Ndugu wa Mzee Ndesamburo msiharakishe kumzika mzee wenu mpaka uchunguzi juu ya kifo chake ufanyike. Kwani kuna utata umegubikwa hasa kuhusu

Hii tabia ya uzushi na uchochezi ikiachwa kuendelea italeta maafa siku moja. @MODS chukueni hatua kwa hii ngurumbili.
 
Mkuu Yehodaya, nimeelezwa wewe ni she!, kwanza pole kwa sababu una matatizo fulani bila kujijua!. Mtu sio ndugu yako, heshima na uwezo wake unajulikana, ndugu jamaa na marafiki zake wanafahamika na uwezo wao kiuchumi unajulikana, kitendo cha wewe kuja humu jf na kuanza kuhamasisha michanga ili Ndesa azikwe kwa heshima, ni kumdhalilisha na kuidhalilisha familia ya Ndesa, please stop hili la michango!.

Pili nimejitolea kukusaidia, hivyo nitakupandia in box tupange jinsi ya kukuona na nitakusaidia sana, kwa sababu nimesaidia wengi wenye matatizo kama yako.

RIP Ndesa Pesa.

Paskali
Mkuu misiba Ya wachaga na wajaluo huwezi kwenda tu kutungua kilio kama wasukuma kuwa rafiki yako mpendwa na ndugu yako na mheshimiwa wako kafa watakuona mjinga tu unachotakiwa kufanya unaenda na burungutu la pesa unakabidhi wafiwa ukishawapa ndio unatungua kilio kuwa marehehemu rafiki yako kafa kaacha pengo na utapata waliaji wa kukuunga mkono kibao. Misiba Ya wasukuma na makabila mengine ni tofauti. Nauliza tena Pascal Mayala na wakili Mselewa mnachangia shilingi ngapi? Maneno yenu Ya pole Na maskitiko hayawezi nunua sanda wala jeneza mnachangia shilingi Ngapi? Maneno matupu ya maskitiko hayachongi jeneza wala kununua sanda
 
Back
Top Bottom