saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,522
- 7,030
Tuambie majina yako halisi, rabon ndio niniSalaam, Shalom!!
Kwanza nianze Kwa kuweka wazi kuwa, Mimi Si mwanachama wa chama chochote Cha siasa, na ikiwa Kuna yeyote mwenye ushahidi wa Rabbon kuwa mwanachama wa chama chochote Cha siasa, auweke hapa. Nimesema hayo Ili Ushauri wangu uwe ushauri binafsi, usio na mashinikizo ya kichama, ninashauri tu kama Mtanzania mwenye Nia njema ya USTAWI wa DEMOKRASIA ya vyama nchini.
Naungana na viongozi wengi wenye BUSARA waliotumia muda wao Kutoa angalizo juu ya chaguzi zinazoendelea katika vyama vya siasa, usifanyike mlango wa kuleta sintofahamu kuelekea uchaguzi mkuu. Mchungaji Mwamakula ni MMOJA wa watu hao muhimu waliotahadharisha jambo Hilo nyeti.
Nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha DEMOKRASIA na Maendeleo ( CHADEMA) imekuwa na kelele nyingi sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.
Nashauri CHADEMA kujifunza BUSARA Kutoka Kwa Mwalimu Nyerere juu ya kuruhusu Rais aliyestaafu kuendelea kuwa Mwenyekiti Kwa mwaka mmoja baada ya kufanyika uchaguzi mkuu, Kisha baada ya muda huo kupita, Rais aliyeko madarakani anakabidhi Rasmi.
Utaratibu huo ni mzuri na umechangia Kwa namna Fulani kuzuia mtafaruku wakati wa uchaguzi na baada ya Uchaguzi.
Turudi Kwa CHADEMA, Muheshimiwa Mbowe, ni dhahiri uongozi wako Kwa nafasi ya Mwenyekiti unafikia mwisho, na ingekuwa vyema Ukatoka hadharani na kusema hadharani kuwa HUTAGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti kama ambavyo uliwahi kusema kabla. Ukivushe chama katika wakati huu wa uchaguzi ndani ya chama na uchaguzi wa Serikalini za mitaa 2024 na u haguzi mkuu 2025.
CHADEMA iingie katika chaguzi zijazo ndani na nje ya chama wakiwa wamoja na wakijua fika kuwa baada ya Uchaguzi mkuu 2025, nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA itakuwa wazi Kwa yeyote atakayeonekana kutosha Kwa nafasi hiyo achaguliwe na kuendelea alipoishia mkt Mbowe.
Narudia tena kuishauri CHADEMA, uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti ifanyike baada ya Octoba 2025 sawasawa na mipango mtakayojiwekea.
Mh Mbowe aandike barua ya kutogombea nafasi ya Mwenyekiti wakati huu na aikabidhi hadharani Kila mtu aione kusubiri uchaguzi huo baada ya October 2025.
Ushauri huu pia usipofaa machoni penu, UPUUZWE!!!, Lakini ikiwa utapata kibali machoni penu, UCHUKUENI, Maana Kwa wakati tuliopo, kuiangusha CCM iliyokwisha jichokea, mnahitaji UMOJA na NGUVU MOJA Si malumbano yanayoendelea hivi sasa.
Mungu ibariki CHADEMA,
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Amen. Karibuni🙏