Ushauri: Uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA ufanyike baada ya Oktoba 2025

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,199
31,832
Salaam, Shalom!!

Kwanza nianze Kwa kuweka wazi kuwa, Mimi Si mwanachama wa chama chochote Cha siasa, na ikiwa Kuna yeyote mwenye ushahidi wa Rabbon kuwa mwanachama wa chama chochote Cha siasa, auweke hapa. Nimesema hayo Ili Ushauri wangu uwe ushauri binafsi, usio na mashinikizo ya kichama, ninashauri tu kama Mtanzania mwenye Nia njema ya USTAWI wa DEMOKRASIA ya vyama nchini.

Naungana na viongozi wengi wenye BUSARA waliotumia muda wao Kutoa angalizo juu ya chaguzi zinazoendelea katika vyama vya siasa, usifanyike mlango wa kuleta sintofahamu kuelekea uchaguzi mkuu. Mchungaji Mwamakula ni MMOJA wa watu hao muhimu waliotahadharisha jambo Hilo nyeti.

Nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha DEMOKRASIA na Maendeleo ( CHADEMA) imekuwa na kelele nyingi sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.

Nashauri CHADEMA kujifunza BUSARA Kutoka Kwa Mwalimu Nyerere juu ya kuruhusu Rais aliyestaafu kuendelea kuwa Mwenyekiti Kwa mwaka mmoja baada ya kufanyika uchaguzi mkuu, Kisha baada ya muda huo kupita, Rais aliyeko madarakani anakabidhi Rasmi.

Utaratibu huo ni mzuri na umechangia Kwa namna Fulani kuzuia mtafaruku wakati wa uchaguzi na baada ya Uchaguzi.

Turudi Kwa CHADEMA, Muheshimiwa Mbowe, ni dhahiri uongozi wako Kwa nafasi ya Mwenyekiti unafikia mwisho, na ingekuwa vyema Ukatoka hadharani na kusema hadharani kuwa HUTAGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti kama ambavyo uliwahi kusema kabla. Ukivushe chama katika wakati huu wa uchaguzi ndani ya chama na uchaguzi wa Serikalini za mitaa 2024 na u haguzi mkuu 2025.

CHADEMA iingie katika chaguzi zijazo ndani na nje ya chama wakiwa wamoja na wakijua fika kuwa baada ya Uchaguzi mkuu 2025, nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA itakuwa wazi Kwa yeyote atakayeonekana kutosha Kwa nafasi hiyo achaguliwe na kuendelea alipoishia mkt Mbowe.

Narudia tena kuishauri CHADEMA, uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti ifanyike baada ya Octoba 2025 sawasawa na mipango mtakayojiwekea.

Mh Mbowe aandike barua ya kutogombea nafasi ya Mwenyekiti wakati huu na aikabidhi hadharani Kila mtu aione kusubiri uchaguzi huo baada ya October 2025.

Ushauri huu pia usipofaa machoni penu, UPUUZWE!!!, Lakini ikiwa utapata kibali machoni penu, UCHUKUENI, Maana Kwa wakati tuliopo, kuiangusha CCM iliyokwisha jichokea, mnahitaji UMOJA na NGUVU MOJA Si malumbano yanayoendelea hivi sasa.

Mungu ibariki CHADEMA,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen. Karibuni🙏
 
Mbowe ndio Putin wetu, mitano tena, swali katiba ya Chadema inamruhusu kugombea au vipi?

Uenyekiti wa Chadema siyo ajira, hapo anatakiwa mtu wa kuongoza mapambano na mwenye ushawishi wa kuyafurusha madarakani maccm.

Wanaotaka ajira wasubili kugombea ubunge hizo ndio ajira zenye pesa nyingi.
 
Wewe Si mwana CHADEMA ukumbuke.
 
Mbowe ndio Putin wetu, mitano tena, swali katiba ya Chadema inamruhusu kugombea au vipi?

Uenyekiti wa Chadema siyo ajira, hapo anatakiwa mtu wa kuongoza mapambano na mwenye ushawishi wa kuyafurusha madarakani maccm.

Wanaotaka ajira wasubili kugombea ubunge hizo ndio ajira zenye pesa nyingi.
Kama sio ajira kwanini unapiganiwa?
 
Mbowe ndio Putin wetu, mitano tena, swali katiba ya Chadema inamruhusu kugombea au vipi?

Uenyekiti wa Chadema siyo ajira, hapo anatakiwa mtu wa kuongoza mapambano na mwenye ushawishi wa kuyafurusha madarakani maccm.

Wanaotaka ajira wasubili kugombea ubunge hizo ndio ajira zenye pesa nyingi.
🤣🤣🤣 Ngoja na CCM iwaoneshe Uputin Sasa ila muache maigizo ya Katiba mpya
 
Mbowe apambane vita ya mwisho, ahakikishe CHADEMA inashika Dola 2025, Kisha amkabidhi mwingine na kubaki kama Mzee mshauri wa chama.
 
Umeonyesha wazi namna chama hili la CHADEMA lilivyo Dhaifu na dhoofu mpaka kushindwa kuhimili presha za uchaguzi na kuogopa kusambaratika kwa sababu ya uchaguzi .chama gani kinashindwa kusimamia hata uchaguzi tu wa ndani? Kwani kinachoendesha na kuongoza uchaguzi si ni katiba ya chama? Je katiba ya CHADEMA imekwenda wapi? Ipo kwenye mfuko wa nani? Kwamba hamjuwi kanuni za uchaguzi zinasema nini na taratibu zake zipo je? Kwamba hamfahamu mshindi anapatikana vipi na wajumbe ni akina nani?

Kwa mantiki hiyo hakuna hata sababu ya CHADEMA kushiriki uchaguzi wa aina yoyote ile maana hakina akili ya kuweza kuendesha uchaguzi bila kuacha mgawanyiko. Yaani li CHADEMA linazidiwa na ACT wazalendo walioweza kufanya uchaguzi wake wa ndani na kumaliza kwa amani? Kweli CHADEMA ni genge la wasaka Tonge kwa ajili ya matumbo yao. Kwamba mwakani uchaguzi ukifanyika ndio halitaleta taharuki na migogoro?
 
Mwanangu Lucas, Unaweza kukumbuka ni nani aliyeharibu Ile kura Moja, Mwezi December Uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Chama CCM Taifa?

Tuanzie hapo!!
 
Wachaga achieni chama kwa wengine. Hiki chama mtu mmoja aongoze miaka 40 kisa haonekani mbadala wake kisa chama cha familia ya kimangi meza toka machame watu wamestuka wanataka chama kiwe cha jamii zote sio kaskazin tu. Yan uchaguzi wa kusini mkampeleka john mrema akasimamie kulinda maslahi ya uchagani nani atawapa nchi kama chama tu hamuamini makabila mengine kuongoza
 
Unamkumbuka Sir Bob Makani wewe?

HOJA ya ukabila ni duni mno!!
 
Back
Top Bottom