USHAURI: Niliacha kazi Serikalini kutokana na mazingira magumu ya kazi miaka miwili imepita, baada ya mambo yangu kutengemaa nataka kurudi

sontable

JF-Expert Member
Apr 13, 2018
261
535
Hello habari za majukumu!

Niliajiriwa serikalini (kama mwalimu)miaka miwili iliyopita lakini baada ya miezi 6 nikaacha kazi si kwa kupenda ila kutokana na mazingira magumu ya kazi na kujikuta mshahara wote unaishia kwenye pango la nyumba, nauli ya kwenda na kurudi kazini. Maana shule haikuwa jirani na nyumba za kupanga Wala Haina nyumba za walimu

Hivyo niliwasilisha lalamiko langu kwenye ofisi husika lakini wakawa wananiambia hata sisi tulianza hivyohivyo daah nikaona sio case hivyo nikaamua kuacha kazi na kuendelea na maisha mengine

Sasa kwa saivi baada ya uhakika wa KIPATO takribani mara mbili ya mshahara nataka nirudi mzigoni

Hapa utaratibu ukoje wakuu ,naweza kukubaliwa ? Japo nimefanya mawasiliano na TSD kwamba inabidi niende nikajieleze Ili waangalie utaratibu kama wakurudishwa kazini upo

Sasa kwa walio experience hali kama hii au Kuna mtu unajua ashawahi kupitia kipindi kama changu ALIWEZAJE kupenya? Je Ili niweze kupenya nitumie mbinu gani ?

Maana saivi nipo dar es salaam lakini kituo changu Cha kazi ni rukwa nahofia kuondoka na kuuza vitu vyangu kwa hasara kuwa naenda kazini afu nikafika huko nikakataliwa si msaala huu
 
Sasa kwa sasa hivi baada ya uhakika wa KIPATO takriban mara mbili ya mshahara nataka nirudi mzigoni
Je hicho kipato ni endelevu.!???

If Yes, Unataka kurudi kazini kufanya nini badala upambane hicho kipato unachopata kiongezeke hata mara 4+....

Kama Mshahara ulikuwa hautoshi.. Maana yake sasa hivi unaenda kutumia hicho kipato chako kujazia hilo gape ambalo Mshahara ulikuwa unafeli kukamilisha(Nauli, Kodi),,, Yaani unaenda kuishi kwa HASARA...
Unatumia Faida yako ya nje kuendesha Maisha ya kazi...
 
Hello habari za majukumu!

Niliajiriwa serikalini (kama mwalimu)miaka miwili iliyopita lakini baada ya miezi 6 nikaacha kazi si kwa kupenda ila kutokana na mazingira magumu ya kazi na kujikuta mshahara wote unaishia kwenye pango la nyumba, nauli ya kwenda na kurudi kazini. Maana shule haikuwa jirani na nyumba za kupanga Wala Haina nyumba za walimu

Hivyo niliwasilisha lalamiko langu kwenye ofisi husika lakini wakawa wananiambia hata sisi tulianza hivyohivyo daah nikaona sio case hivyo nikaamua kuacha kazi na kuendelea na maisha mengine

Sasa kwa sasa hivi baada ya uhakika wa KIPATO takriban mara mbili ya mshahara nataka nirudi mzigoni

Hapa utaratibu ukoje wakuu ,naweza kukubaliwa ? Japo nimefanya mawasiliano na TSD kwamba inabidi niende nikajieleze Ili waangalie utaratibu kama wakurudishwa kazini upo

Sasa kwa walio experience hali kama hii au Kuna mtu unajua ashawahi kupitia kipindi kama changu ALIWEZAJE kupenya? Je Ili niweze kupenya nitumie mbinu gani ?

Maana sasa hivi nipo Dar es Salaam lakini kituo changu cha kazi ni Rukwa, nahofia kuondoka na kuuza vitu vyangu kwa hasara kuwa naenda kazini halafu nikafika huko nikakataliwa si msala huu
Una matatizo ya akili.

Unaongea vitu indirectly proportional.

Yaani una kipato mara 2 halfu urudi bush.

Mjinga mmoja wewe usiyetaka kushauriwa.
 
Pole mwalimu pole sana ushauri ni kuwa huwezi kurudi kazini mfumo ushakutena na gape lako tayali limejazwa na ajira mpya za mwaka juzi, mwaka jana, na mwaka huu pole kwa ugumu wa maisha ya mtaani watu wazima tumejua maisha yamekupiga unatamani uwalimu tena si kipato kimekuwa

MY TAKE
Vijana msikimbilie kuacha kazi kisa mazingira magumu pigana kuondoa hayo mazingira hakuna kisicho wezekana chini ya jua ni maamuzi tu
 
Kuacha kazi ya umma unadhani ni sawa na unaposafiri safari ya mbali na kurudi? Punguani tu ndiye anayeweza kufikiria hivyo, kuna thousands of unemployed professionals and yet you're thinking of being preserved and reserved after quitting the job?!

Labda wewe ni mwalimu wa level ya shule za chini.

Kingine tunafanya kazi kukuza vipato, wewe unapata kipato kikubwa mara mbili ya ulichokuwa ukipata na sasa unataka kurudi kwenye ajira yenye kipato kidogo. Only a goat will understand you bagoosha!
 
Je hicho kipato ni endelevu.!???

If Yes, Unataka kurudi kazini kufanya nini badala upambane hiko kipato unachopata kiongezeke hata mara 4+....

Kama Mshahara ulikuwa hautoshi.. Maana yake unaenda sasa hivi kutumia hiko kipato chako kujazia hilo gape ambalo Mshahara ulikuwa unafeli kukamilisha(Nauli, Kodi),,, Yaani unaenda kuishi kwa HASARA...
Unatumia Faida yako ya nje kuendesha Maisha ya kazi...
Full madness
 
sasa kama uliacha kazi na sasa mambo yako mazuri unataka urudi kwenye kazi uliyoiacha ili iweje? acha uboya kuwa serikalini kama wewe hauko kwenye chanel ya kula rushwa ni kufa masikini, shukuru kama unaweza kupiga mishe zako na maisha yanakwenda usijaribu kurudi maana hata hicho kidogo ulicho nacho kitapukutika watu mnaangamia kwa kukosa maarifa , kwahiyo bado unatamani uitwe mfanyakazi wa serikali ambao hata mia mfukoni wanaitafutiza hasa nyie walimu.DONT BE STUPID
 
Possible kabisa unaweza kurudishwa nenda kajieleze vzr , kwanz ata hizo sababu ni za msing kbsa kikubwa ziboresh

Usiuz vitu hvyo nend kapambanie kesi iishi then ndio uamue
 
Back
Top Bottom