Ummesh
JF-Expert Member
- Dec 20, 2015
- 2,077
- 1,142
Nilijua tu. Hizi nyuzi zinazotumwa za kutooa wanawake wasomi lazima zilete madhara makubwa sana kwenye jamii.Mimi ni binti....nilikuwa kwenye uhusiano na mpenz wangu kwa miaka minne toka yeye akiwa first year Chuo flan hivi
Mimi kielimu Ninamalizia certificate ya lab tech mwaka huu ikiwa yeye amemaliza na ameajiriwa tayari ....
Tulikuwa vizuri Tu ki ukweli sikuwahi kucheat hata siku moja toka Niko nae tumeendelea hivyo huku kila mmoja akimuombea mwenzie mwisho Wa siku tufunge pingu za maisha ...,
Pamoja na kupitia changamoto katika mahusiano na maisha magumu wakati mwingine lakini nilikuwa mstari Wa mbele kuyavumilia na kumpa moyo na kuendelea mbele,
Tatizo wiki iliyopita alinitumia meseji tuachane kwa sababu yeye mipango yake hawezi kuoa mwanamke aliyeenda shule
Ki ukweli niliwaza sana na mpka sasa Nina mawazo ambayo Sijui niamue vipi
Ilinibidi nimkubalie japo ndani ya moyo wangu naumia sana hasa vile nilivyomzoea alikuwa kama baba yangu
Nilionelea nipime ili nijielewe afya yangu ki ujumla maana niliwaza sana labda huenda alikuwa na MTU wake nje mimi Sijui na niliwaza jinsi magonjwa yalivyo mengi sahivi ,nilipima HIV nikakuta Niko safi nikapima na mkojo nikakuta Nina ujauzito
TATIZO
Nawaza sana kuotoa mimba hii ila nawaza nitaenda kujibu nini siku nikifa.,
Nawaza endapo nikikubali kukaa nao mtoto wangu nitakae mzaa kumlea peke yangu
Nawaza jinsi ya kuwaeleza wazazi wangu juu ya hali yangu ya uhusiano na hii mimba Tena
Jamani naombeni ushauri wenu Niko kwenye kipindi kigumu sana nisaidie .