yas-mic
JF-Expert Member
- May 25, 2016
- 472
- 728
Ushauri mzuri lakini bila kuwa mnafiki naamini kwa sasa nadhani hauna msaada sana ....Mawazo ya kuwa na shauku ya kutajirika tu bila kumtafuta Mungu ni upotofu wa Wanadamu na kumuasi Mungu. Ni mawazo mapotofu ya tamaa za macho na mwili. Ukishatoka kimaisha na huna Mungu what next ?? Simaanishi ukae tu bila kufanya kazi ila inavyoonekana hapa ni as if haupo tayari kwa lingine bali kutaka kutoka tu kimaisha.
BIBLIA inasema "Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu". Nikuulize ndugu, Je, umejihangaisha kwa kiwango gani kuzishika sheria za BWANA .?
Inaendelea kusema "Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya Mwanadamu"
Kumbe ni dhahiri kwamba, ukifuata na kutii taratibu (Sheria za Mungu) atakupatia ufahamu wa namna ya kufanya au kuenenda ili kujipatia riziki(Mkate) wako.
Zaidi inasema, "Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atanyosha mapito yako". Kumbe kabla ya kuja hapa JF kupata ushauri wa jinsi gani utoke unatakiwa kumtegemea Mungu na kumkabidhi mahitaji yako na yeye atatenda kwa kadiri ya mapenzi yake na si kutimiza ndoto zako kama unavyopenda mwenyewe.
MWISHO; Uhusiano wa nilichokiandika na mada yako ni kuwa, hutakiwi kusumbua akili zako zaidi juu ya jinsi gani ufanye ili utoke kimaisha, bali jishughulishe zaidi kumtafuta Mungu. Ukiwa na Mungu yeye atakuongoza kadiri ya mapenzi yake na si kwa matakwa yako binafsi kutokana na tamaa za macho na mwili za kujipatia mali nyingi hapa Duniani ili uishi maisha ya anasa.
Zingatia kuwa simaanishi ukae tu bila ya kufanya kazi. Bali umtumaini Mungu kwa akili na Moyo wako zaidi kisha yeye atanyoosha mapito yako. Kipaumbele chako kisiwe namna ya kutoka kimaisha, bali kumtafuta Mungu kwanza. Kuwa na Mungu moyoni mwako ni zaidi ya kutoka kimaisha kupitia utajiri wa mali za Dunia hii.
Nashukuru kwa mawazo yako mkuu! Kiuhalisia ni ngumu kupata mkopo kama huna tangible assets! Ila nimewaza kama tukiwa na propasal ya kilimo cha umwagiliaji (hasa kwa value crops) kama group alafu tukaomba funds! Bado tatizo litabaki where can we get funds??