Ushauri: Naona kama huu ni utumwa!

Yaani umepanga Kwa laki 2 kwa Mwezi au?

Basi Umasikini Upo Akilini Mwako Tu.. Ili Uwe Tajiri Jaribu kuwa Mbahili Hata Mwaka Basi halafu Fanya Kitu Cha Maana

Maana Naona Kuna Chakula Kazini 100000 Na Chakula Tena 250000 Wakati Kwa Mtu wa Kawaida Tsh 150000 inatosha Kabisa Kwa Mwezi kama Upo Mwenyewe

jukwaa La Uchumi nq Biashara Lipo Humu mbona Pitia Thread Za Ujasiriamali La Sivyo utagonga 30 hujafanya La Maana
Kumbuka niko ana familia sometimes wanakuja wageni niliamua kupanga vyumba viwili na sebule, labda kama una ufahamu wa maeneo yenye rent ndogo hapa daa nizamie huko as startup strategy
 
Asalamu wakuu!
Ni imani yangu mnaendelea na majukumu yenu ya kujitafutia chochote kitu maisha yasonge.

Back to topic!
Mimi ni kijana muajiliwa hapa mjini Dar kwa takribani miaka miwili sasa. mshahara wangu si hapa mana take home ni kama Tshs. 980,000/= per month.

SHIDA YANGU! kwa takribani muda huu wote wa miaka miwili sijafanya lolote la maana zaidi ya kula, kunywa na kuvaa yaani kuna muda nafuria hata hela ya kula nakuwa sina.

Nikaamua nijaribu kufanya analysis ya expenditure zangu per month nione gap iko wapi! on average (3 month average) ikaonyesha matumizi yangu kwa mwezi ni kama ifuatavyo!

1. Kodi ya nyumba-200,000
2. Maji na umeme-40,000
3. Chakula (mwezi)-250,000
4. Hela ya emergency-100,000
5. Suport fund (ndg)-100,000
6. Vocha na nauli kazini-40,000
7. Ada ya dogo (Form 4)-100,00
8. Chakula kazini (Posta)-100,000
9. Mengineyo* -50,0000

*Nguo, viatu n.k
JUMLA ni Tshs. 980,000.

Yaani kwa mwendo huu nimefungwa kwenye hiyo circle (utumwa). Natamani hata lije dili la kontena lakini wapi. Kwangu mimi naona hii kazi ni utumwa na sitaweza kuendelea kwa kuendekeza huu upuuzi.

katika kuondokana na hili janga nimeonelea kuwa nirudi tu mkoani nikalime na nikajiajili kuliko kukaa hapa mjini bila ramani.

Naombeni wazoefu wanaolima mikoani na mnaoweza kumiliki hata ka vitz kwa hii mishahara tupeane mawazo maana mimi sometimes namchukia hadi wife kwani naona kama tuliwahi kuoana na ndio chanzo cha matatizo.

NB. Nimeoa, nina mtoto (3).
Funga chakula kutoka home, punguza baadhi ya misaada isiyo ya lazima kwa ndugu, mengineyo futa baki na emergency inatosha.

Michango ya birthday, sijui michango ya kwenda beach ondoa

Pole sana ila hiyo hela ni kubwa sana mkuu
 
Chukua mkopo mkubwa hapo unapofanya kazi weka kitega uchumi kikubwa mkeo aendelee kukisimamia.

Hela utakayokatwa kazini itakufanya uadjust matumizi yako.
 
Chukua mkopo mkubwa hapo unapofanya kazi weka kitega uchumi kikubwa mkeo aendelee kukisimamia.

Hela utakayokatwa kazini itakufanya uadjust matumizi yako.
sawa mkuu.. nitalifanyia upembuzi wa kina hili suala la mkopo
 
una matumizi makubwa sana .. fanya hivi ukichukua hiyo 980,000 chukua 1/3 yake usave ambayo ni sawa na 327,000 kila mwezi .. halafu hiyo 653,000 ndiyo ukaingiza kwenye matumizi yako huwezi kuwa na expenditure kubwa hivyo.... make sure unasave 1/3 ya mshahara wako na unao bakia ndiyo sasa jibane uwezavyo matumizi yaagukie huko......
 
aisee hili nalo ni wazo nafikiri nahitaji kurefocus mana mji utanishinda
unaonaje ukienda kupanga vyumba viwili uswazi kodi haitozidi laki, unaonaje mchana ukishuka huko ghorofani unakofanya kazi ukaenda kula na watu wa kawaida kabisa kwa bajeti isiyozidi 2000 kwa mlo, nakuapia hautokuwa wa kawaida, unachokosea hauna nidhamu na hela, nenda sokoni kusanya mazaga yasiyoharibika kirahisi weka ndani, punguza anasa nunua package moja ambayo itakufanya uwe nyumbani uwe unaangalia movie na mpira badala ya pombe, nina mengi ya kukwambia lakini zingatia hayo kwanza, kuna watu wanalipa laki mbili mji huu wana watoto wawili wote wanasoma na wanasurvive tena vizuri tu, kuwa na nidhamu na hela!
 
una matumizi makubwa sana .. fanya hivi ukichukua hiyo 980,000 chukua 1/3 yake usave ambayo ni sawa na 327,000 kila mwezi .. halafu hiyo 653,000 ndiyo ukaingiza kwenye matumizi yako huwezi kuwa na expenditure kubwa hivyo.... make sure unasave 1/3 ya mshahara wako na unao bakia ndiyo sasa jibane uwezavyo matumizi yaagukie huko......
Thanks miss chagga, kwa kweli huu mwezi Austerity measures nitayoifanya itanipa mwelekeo.
 
Kuna gharama ambazo unaweza kuziepuka 1.Kodi ya nyumba unaweza pata ya laki moja ''family size'' 2. Automatically sehem zenye nyumba gharama nafuu na vyakula pia gharama zake ziko chini + maji na umeme waweza ku control kwa kufunga bulb fluorescent na kuepuka radio masaa yote na TV. 3. HELA ya emergency huwezi tenga laki kila mwezi na si lazima upate dharura kila mwezi kiasi kwamba inaweza kuji accumulate ukapata ka mtaji.5 support fund huo ni ujinga wako mambo ya michango ya harusi na upuuzi mwingine ni mwiko kwa mtafutaji...labda msiba na si lazima ufiwe kila mwezi.......huyo dogo wa form 4 kila mwezi laki? mtafutie shule ya bei nafuuu,...9...Chakula kazini jaribu kula kwa mantilie...##@*^hiyo mengineyo...kuna gesti za bei nafuu au buguruni waweza maliza kwa buku 2.
N>B<
Shemeji ana fanya kazi gani? kama ni Golikipa mfungulie genge anza na mkaa na aish krimu.
 
Asalamu wakuu!
Ni imani yangu mnaendelea na majukumu yenu ya kujitafutia chochote kitu maisha yasonge.

Back to topic!
Mimi ni kijana muajiliwa hapa mjini Dar kwa takribani miaka miwili sasa. mshahara wangu si haba mana take home ni kama Tshs. 980,000/= per month.

SHIDA YANGU! kwa takribani muda huu wote wa miaka miwili sijafanya lolote la maana zaidi ya kula, kunywa na kuvaa yaani kuna muda nafuria hata hela ya kula nakuwa sina.

Nikaamua nijaribu kufanya analysis ya expenditure zangu per month nione gap iko wapi! on average (3 month average) ikaonyesha matumizi yangu kwa mwezi ni kama ifuatavyo!

1. Kodi ya nyumba-200,000
2. Maji na umeme-40,000
3. Chakula (mwezi)-250,000
4. Hela ya emergency-100,000
5. Suport fund (ndg)-100,000
6. Vocha na nauli kazini-40,000
7. Ada ya dogo (Form 4)-100,00
8. Chakula kazini (Posta)-100,000
9. Mengineyo* -50,0000
*Nguo, viatu n.k
JUMLA ni Tshs. 980,000.

Yaani kwa mwendo huu nimefungwa kwenye hiyo circle (utumwa). Natamani hata lije dili la kontena lakini wapi. Kwangu mimi naona hii kazi ni utumwa na sitaweza kuendelea kwa kuendekeza huu upuuzi.

katika kuondokana na hili janga nimeonelea kuwa nirudi tu mkoani nikalime na nikajiajili kuliko kukaa hapa mjini bila ramani.

Naombeni wazoefu wanaolima mikoani na mnaoweza kumiliki hata ka vitz kwa hii mishahara tupeane mawazo maana mimi sometimes namchukia hadi wife kwani naona kama tuliwahi kuoana na ndio chanzo cha matatizo.

NB. Nimeoa, nina mtoto (3).
kwenye chakula elfu tano kwa mlo mmoja.save kwa kwenda kula pale ifm wali wa buku na maji ya mia sita.hakuna namna
 
Back
Top Bottom