Ushauri: Mke wangu hataki tukaishi kwa wazazi wangu ili tubane matumizi tujenge

Kakupa kama kukukopesha au kakukabidhi kabisa kua ni mali yako?

Either way ata mimi ningekataa!!! Nisingejisikia kua niko kwangu bali niko kwenu!! Yaani niishi wakwe na kaka yako wapo karibu kiasi hicho???
 
Utamnyima mkeo uhuru wa ndoa yake!!! Kama uko tayari kumfanya ajihisi mtumwa basi hamia!
Ni hii generation ya sasa ndio imebadirika na kusikia maneno ya watu ooo usikubali sijui ooo watakutawala basi tu kuvuruga family , zamani nyumba moja family kama mbili tatu hivi hata siku moja kusikia ugonvi wala mamneno .
 
Nakubaliana na mkeo,,, yuko sahihi sana!
Anyway siwezi nika conclude maana sijui the other side of the story! Ila in one way or another mkeo yuko sahihi!
Your the only know your parents and your relatives in a positive way! Lait ungeweza kujivua u-wewe ukauweka pembeni kidogo alafu uwaangalie nduguzo ungemuelewa mkeo sana!
 
kaka mbon
Utamnyima mkeo uhuru wa ndoa yake!!! Kama uko tayari kumfanya ajihisi mtumwa basi hamia!

Mkuu elewa kuwa kwanini kuna point ya kuishi hata chumba kimoja cha kupanga na mkeo na baadae Mungu awajaalie mjenge yenu.

Hapo kwa wazazi ni nyumbani kwa wazazi kumbuka hapo ni nyumani kwa wazazi na ni hivyo hivyo mkeo hatokuwa na uhuru ni muhimu kuwa na kwako wewe na inapendeza ukiwa na kwako hata kama umepanga au umejenga chumba hata kimoja ni kwako.

Mali ya mzazi ni ya mzazi sio yako tafuta yakwenu ishi kwenu na si kwa mzazi kuna mengi ya kuongea kwanini namuunga mkono mkeo hoja yake ila nisingependa kufunguka ila mwisho wa siku wewe ni mtoto wa kiume jitegemee sasa mambo ya kuishi nyumba ya wazazi haileti heshima especially kwenye maisha ya ndoa ungekuwa bachelor sawa.
Kapange hata room moja au jenga hata room mmoja naomba nisiendelee kufunguka kwani ningefunguka madhila atakayopata mkeo na wewe mwenyewe na familia yako wewe mwenyewe i mean kwako kwa mkeo na mtoto/watoto wako

Kumbuka mali ya baba niya baba si yako Jitegemee
 
Vipi mambo wakuu,

Wazazi wangu ni watu wazuri saana sio kama nawasifia ni watu wenye kupenda watu sana kupita kiasi na wala hawana issues na mtu yoyote wala hawana mpango na issues. Hata ndugu zangu ni watu wazuri vile vile hawana matatizo na mtu yoyote yule.

Brother wangu kanipa flat ili nikaishi pale bure, chini wanaishi wazee wangu mimi nimepewa juu ni flat ya kutosha na my brother yuko upande wa pili na family yake.

Sasa wife wangu hataki tukaishi pale kila nikifungua hii topic hataki hata kusikia kila nikimuuliza hanipi jibu namwambia twende tukaishi pale kwa mda ili tuweze ku save pesa ili tujenge nyumba yetu yote hayo hataki.

Naomba ushauri wenu wakuu bila jokes please.
Mwambie arudi kwao, akiwa tayari kukaa na wazazi wako aje
 
Nina maswali kidogo naomba unijibu kabla sijachangia

- Wewe na mkeo mna umri gani na ndoa ina umri gani?
- Mkeo ni kabila gani?
- Mnapo kaa sasa hivi Wazazi na ndugu zako wanawatembelea? yaani wako free kuja?
- Wewe ni mtoto wa ngapi kwenu kuzaliwa?

Asante
 
mtoa mada mkeo ana akili sana ameona kitu ambacho wewe kamwe huwezi kukiona mpaka muda upite. Fuata ushauri wa mkeo maana ukishakuwa mtu mzima utakiwi kuishi karibu na ndugu hasa wazazi hata wawe wazuri kiasi gani yatatokea tu makwazo kwa kuwa watataka muishi kama watakavyo wao na sio mtavyo nyie. Kuna msemo unasema mtegemea cha ndugu ufa masikini, wewe unaonekana unategemea sana ndugu wakati mkeo ana uhakika mnaweza kujitegemea wenyewe. Hivi wote wanaojenga uwa wanaishi kwa ndugu ili wajenge? Jiongeze kidogo ndugu yangu usipende sana mteremko katika haya maisha. Hebu jitahidi ujenge sio mpaka ndugu wakubebe bebe utadhani ndio walikuolea mke bwana.
 
ni mjinga tu huyo achana nae.kwani ndugu zako wana ubaya gani.wangapi wameolewa wanaishi kwa wakwe? sembuse nyie mnaishi kila mtu na jiko lake.ana matatizo huyo .wanaokushauri umsikilize mkeo ni watoto tu hawajui maisha.
 
Mkeo yupo sahihi mkuu.

Tafuta sehemu ya gharama nafuu halafu upangishe na uendelee kuweka akiba ya kuweza kujenga.
 
Kakupa kama kukukopesha au kakukabidhi kabisa kua ni mali yako?

Either way ata mimi ningekataa!!! Nisingejisikia kua niko kwangu bali niko kwenu!! Yaani niishi wakwe na kaka yako wapo karibu kiasi hicho???
kwani kuna ubaya gani shosti kumbuaka hataishi na wakwe ni majirani tu kila mtu na hamsini zake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom