econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,564
- 30,271
Habari Wana JF.
Kwanza nielezee masikitiko yangu kwa kauli ya Jana ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Mbowe kwamba anajuta kumwamini Rais Samia
Mheshimiwa Mbowe alipigiwa kelele sana kuhusu kuingia maridhiano na CCM hakusikia kabisa. Nakumbuka kwenye mkutano wa CHADEMA Mwanza, tarehe 21/1/2023, Mbowe alidai hatamsema vibaya mama Samia. Leo inakuwaje ndio anashtuka muda umeenda? na kudai anajuta kumwamini Mama Samiah?.
Pia nakumbuka kwenye mkutano wake na diaspora wa Marekani tarehe 11/12/2022, Mh Mbowe alidai kuwa hatarudi nyuma kwenye mazungumzo, na kudai anaweka maslahi ya nchi mbele na sio CHADEMA, Leo inakuwaje anajutia kumwamini Rais Samiah.
Mbowe anajua yaliyotokea Zanzibar na alitakiwa kuchukua Kama fundisho. Kwamba pamoja na maridhiano, CCM wakaiweka CUF ya maalim kwenye mtego mpaka leo imekuwa historia. Mwishoni maalim ikabidi akimbilie ACT baada ya Msajili kutumika kumfustrate. Hii ilitosha kumfundisha Mbowe aache kujikomba kwa Mh Samiah na CCM yake. Ilitakiwa ajifunze kutoka kwa Maalim. Kwamba pamoja na Maalim kujishusha na kukubali maridhiano , CCM wakakivunja chama chake Cha CUF na pia kumfanyia unyama 2020.
Sasa Kutokana na kauli ya Mbowe ya Jana, Naomba nishauri yafuatayo:
1. Kwakuwa Mbowe alilazimisha Maridhiano na yeye kujiweka mbele Kama kiongozi wa maridhiano, basi kwa kuwa maridhiano yameshindikana, nashauri aachie ngazi mara moja. Maana kashindwa kutimiza hayo maridhiano aliyo lazimisha.
2. Kwa kuwa Mh. Mbowe alidharau sauti za wanachama wa CHADEMA kumkataza kuendelea na hayo maridhiano, na kwa kuwa hakufanikiwa na hayo maridhiano aombe Radhi wanachama kwa maamuzi hayo ambayo hayakufanikiwa na yaliyoiweka CHADEMA rehani.
3. Kwa kuwa Mh. Mbowe ameshindwa kutimiza approach yake ya diplomacy , itakuwa ujinga akiendelea kuongoza approach nyingine dhidi ya serikali au CCM maana haaminiki Tena. Hivyo ajiuzulu kupisha uchaguzi wa mwenyekiti mpya ambaye atatumia approach nyingine kabisa kuliko ya Mbowe.
4. Kwamba, kwakuwa imeonekana maridhiano sio njia sahihi ya kutatua malalamiko ya CHADEMA kutokana na kiburi Cha CCM na serikali yake, nashauri CHADEMA waachane na approach ya maridhiano watafute approach nyingine.
5. Kwa kuwa inaonekana maoni ya CHADEMA kwenye mswada ya sheria yamekataliwa na Kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria, nashauri CHADEMA watangaze rasmi kutoshiriki chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
Naomba kuwasilisha.