Ushauri: Lowassa pumzika siasa, ni hatari kwako

Nakushauri kwa umri ulionao na pilikapilika hizi za kisiasa sidhani kama unastahili na unaweza kuzimudu. Naomba nitumie jukwaa hili kushauri kiungwana na kistaarabu tu kuwa ni vema mheshimiwa sana ukastaafu siasa. Hii ni rejea ya kukamatwa kwako jana ukiwa Geita ukitokea Bukoba si mwengine bali ni ndugu yangu E.N.Lowasa.

Hivi huku huu ujumbe wako ataupataje huyu mjamaa?
 
Anawapa taabu sana? Mnafikiri akastaafu 2020 mtapata nafuu siyo? Tangu lini mkatoa ushauri wenye tija kwa upinzani? What is the motive behind?
 
Wazee Kingunge, Sumaye, Lowasa, Mgeja ndio tumaini jipya la chadema!!!!

Yani waliofanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30 , leo ndio wenye akili mpya na waleta mabadiliko wa chadema.!!!

Cc
Nyumbuz & Malofazi
Sijawahi kujua kama uko hivi
 
Nakushauri kwa umri ulionao na pilikapilika hizi za kisiasa sidhani kama unastahili na unaweza kuzimudu. Naomba nitumie jukwaa hili kushauri kiungwana na kistaarabu tu kuwa ni vema mheshimiwa sana ukastaafu siasa. Hii ni rejea ya kukamatwa kwako jana ukiwa Geita ukitokea Bukoba si mwengine bali ni ndugu yangu E.N.Lowasa.
Labda tumshauri Mbowe amrudishie kwanza billion moja
 
Uloho wamadalaka

Kweli nadhani ni "uloho wa madalaka" wala si uroho. Yaan maccm hakuna zaidi yao. Mwenye huo "Uloho" Ni nani zaidi ya aliyeshindwa kubaki kung'ang'ania madarakani. Twaweza kuwa wote makengeza lakini usidhani wote vipofu.
 
N
Wazee Kingunge, Sumaye, Lowasa, Mgeja ndio tumaini jipya la chadema!!!!

Yani waliofanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30 , leo ndio wenye akili mpya na waleta mabadiliko wa chadema.!!!

Cc
Nyumbuz & Malofazi
Ndugu yangu CDM wanatufanya hatuna akili sijui! Makapi yaliyoachwa na CCM eti ndio yalete mabadiliko! Mzaha gani huu jamani!!
 
Wazee Kingunge, Sumaye, Lowasa, Mgeja ndio tumaini jipya la chadema!!!!

Yani waliofanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30 , leo ndio wenye akili mpya na waleta mabadiliko wa chadema.!!!

Cc
Nyumbuz & Malofazi

Mkuu mbona Kinana alistaafu siasa na bado akarejea kwenye siasa tena za majitaka. Nipe tofauti Kiumri na Lowassa.
Cc: m2020
 
Lowasa apumzike siasa ! Mbona ww kibaraka wa ccm hupumziki mdomo ?kila Leo kusakama upinzani mkiwekwa kwe kona ?.ss mmeiona kona ya Lowasa ilipowafikisha,unachonga.umati unaotaka kumuona Lowasa co umati unaomuona magufuli ! Napamoja na kuwa wanalazimishwa na watawala wenu wa vijijini,lakini wanaomkusanyikia Lowasa tena bila taarifa ni wengi kiac kwamba mnapata aibu na kukamata watu bila kosa llte! Huyo uvccm wa "uloho" hasemi Lowasa alitawala lini,anataka aongze kutawala kwa "uloho" ? Tawaleni fikra zenu kabla ya kufungua midomo yenu !.
 
Jamani, kwenye maisha siyo kila unachotaka utakipata, tamaa mbaya

- Mtu kachuma tangu utoto, kakwiba, lakini bado anakomaa tu

- Tamaa Mbaya Mzee Pumzika

Wakati ' ukimpovukia ' Lowassa anataka nini katika Siasa na nchi hii pia usisahau kutuulizia kwa Mzee wetu nae Steven Wassira kwamba kuna nini bado anakitaka katika Siasa za nchi hii mpaka hii leo bado ' anakomaa ' tu na Kesi za Kupinga ushindi wa halali na haki wa Mbunge wa Bunda Esther Bulaya? Kumbuka huyu Lowassa ameanza kuingia na kusikika katika Siasa zetu hizi in late 80's lakini kwa Mzee Wassira naambiwa tokea siku moja tu nchi hii kupata Uhuru alikuwepo ' Madarakani ' tena katika Awamu zote nne ( 4 )
 
Niliwahi shauri humu khs Lowassa nikatukanwa sana. Huyu mzee tunampenda ni vyema angelustaafu siasa za majukwaani akabaki mshauri wa kisiasa na mengineyo yenye tija kwa Taifa.
 
Back
Top Bottom