Ushauri kwa TBC 1 juu ya usomaji wa Taarifa ya Habari

Hujanielewa kabisa asee!!
Alafu soma paragraph yangu ya mwisho kwenye post ilopita.

Mie sio mnazi wa tbc lkn sio kweli kwamba wanatimua camera moja, hakuna kitu km hicho, labda uje twende tukawatembelee.
Sasa unakuta camera yenyewe ni moja, na hawatumii visogezi (camera inaratibiwa kwa mikono "manually operated") halafu utegemee mchanganya picha afanye yatakiwayo! Hapana, haiwezekani na ni ajabu saaana, kupata matokeo chanya. Hicho kitu wanachokifanya walitakiwa waandae vyema studio yao ili tuweze kuona vitu vizuri. Ndio maana wanachokifanya sisi tunaona kituko. Hapa watasingizia uhaba wa fedha, hivi ni pesa kiasi gani wanatengewa kila mwaka, hapa utakuta hawana mikakati ya kulikamata soko, wapo wapo tu, wanasubiri mwisho wa mwezi ATM iteme.
 
Hujanielewa kabisa asee!!
Alafu soma paragraph yangu ya mwisho kwenye post ilopita.

Mie sio mnazi wa tbc lkn sio kweli kwamba wanatimua camera moja, hakuna kitu km hicho, labda uje twende tukawatembelee.
Hapo kwenye bold sielewi ulikuwa uamaanisha nini, ila kwa ufupi kama wanatumia camera nyingi basi huyo mchanganya picha ana matatizo saana, mbona anashindwa kuitumikia vema kazi yake?
Bahati mbaya mimi ni mnazi wa habari, na hua napenda kusikiliza habari na sina ubaguzi wa vituo vya utangazaji. Pia nashukuru kwa mualiko wako natumai tafuta wasaa mujaribu tuikonge roho kwa kuwatembelea.
 
Haya mambo ya kuangalia tv kwenye ving'amuzi ni kero sasa,unacho lakini tv zingine hazipo,sasa uwe na ving'amuzi vingapi ndani?!
 
Haya mambo ya kuangalia tv kwenye ving'amuzi ni kero sasa,unacho lakini tv zingine hazipo,sasa uwe na ving'amuzi vingapi ndani?!
 
Hata sipotezi muda kucheki huo mchanel hovyo kabisa! King'amuzi kikikata ni heri kuzima tv na kulala loh!
Halafu ulikuwa wa kwanza kulalamika kuangalia bunge live inayorushwa na hiyo hiyo tbccm. Watu mnaunafikimpaka shetani anaogopa. Khaaaa
 
Wanatakiwa maboresho ya kila sekta kuanzia studio zao za mikoani ambazo nyingi ni kama nyumba za kuishi za kawaida mengine ni kama magofu...wanatakiwa waboreshe systems za kurusha matangazo yao kuendana na teknolojia ya sasa...wanatakiwa waangalie vyema kwenye suala la recruitments yale mambo ya internal vacancy na kupandishana vyeo ndo yana haribu tasnia nzima ya utendaji ktk sekta ya IT...

Kwa kuwapongeza tu ni tbc wapo vizuri kwenye kuelimisha na kuburudisha especially kwenye upande wa redio zao hasahasa hii tbc taifa

Naamini watayapata haya maoni.
 
Ila ulikuwa wa kwanza kulalamika kuangalia bunge live inayorushwa na hiyo hiyo tbccm. Watu mnaunafiki mpaka shetani anaogopa. Khaaaa
Hapa tunazungumzia Taarifa ya Habari.Wewe unazungumzia Bunge.
 
Habari Jf!!!

Kutokana na dhoruba ya Azam TV kupandisha vifurushi vyake pamoja na kukata local channels zote na kuacha TBC pekee na ile ya kwao extra, sasa nimekuwa mfuatiliaj mzuri wa TBC 1, hususani taarifa ya habari saa mbili usiku.

Iko hivi, taarifa ile ya habari husomwa na wasomaji wawili ambapo mara nyingi huwa ni jinsia mbili tofauti yaani KE na ME, sasa Hawa wasomaji,(watangazaji) husoma taarifa moja wote kwa kupokezana kwa wakati mmoja na wakati mwingne husubiriana kwa Muda yaani kila mmoja kujichanganya kumsubiria mwenzake, kama hiyo haitoshi cameraman huweza kutokea kumchukua ambaye hasomi taarifa kwa wakati huo na kumuonesha kwa sekunde kadhaa, kama hiyo haitoshi wakati mwingne hujadiliana wao kwa wao kuhusu taarifa fulani

Athari ambazo husababishwa na watu wawili Kusoma taarifa moja ni

1) Inapoteza Muda taarifa mbili kusomwa na watu wawili, kumbuka Kuna dk 30 za kusoma habari za kitaifa.

2) Inapoteza concentration ya watazamajj wa habari sababu huyu hajamaliza kusoma kadakia mwingine.

3) Wakati mwingne humchanganya cameraman kujua ni yupi ataongea.

4) Hupelekea kuwepo kwa taarifa chache zinazoripotiwa

Mnaweza kujifunza kwa wengine ambao husoma mtu mmoja na taarifa inakuwa nzuri yenye kuvutia Zaidi.

Ni hayo tu.

NAWASILISHA WAKUU....
Sawa lakini hata wale wa ITV baadhi yao wana vituko. Kwa mfano bwana mmoja huwa hatulii, Mara kashika kalamu Mara kageukia wapi sijuwi, yeye hatuli na mikono yake haitulii! Mbwembwe nyingi na maneno mengine hayatamki vizuri kwa haraka zake. Wengine wanamuiga yule wa BBC hadi wanatu-bore na kutupotezea umakini. Presenters wa wenzenu huwa wanatulia ili ku-capture atention ya mtazamaji, na si lazima uchekecheke nk.
 
tbc vipindi vyao havieleweki wanakatisha tu ovyo. ile tamthilia ya mao doudou wameishia kati na hawajaonesha tena...hawa jamaa wanaboa kweli.

kinachowapa jeuri TBC ni kutofanya biashara ndo maana taarifa zao au vipind vyao haviendani sambamba na soko la laeo
hivi tbc ipo kweli?
 
Sawa lakini hata wale wa ITV baadhi yao wana vituko. Kwa mfano bwana mmoja huwa hatulii, Mara kashika kalamu Mara kageukia wapi sijuwi, yeye hatuli na mikono yake haitulii! Mbwembwe nyingi na maneno mengine hayatamki vizuri kwa haraka zake. Wengine wanamuiga yule wa BBC hadi wanatu-bore na kutupotezea umakini. Presenters wa wenzenu huwa wanatulia ili ku-capture atention ya mtazamaji, na si lazima uchekecheke nk.
Mkuu yeye kazungumzia USOMAJI WA TAARIFA YA HABARI kwa watu wawili sio kuhusu vituko, bora ITV hata km hatulii lkn yupo mmoja.
 
Back
Top Bottom