Ushauri kwa serikali ili kudhibiti ufichwaji wa sukari unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa

Pamoja na hili wazo zuri,mimi nashauri waziri wa viwanda
atoke hadharani atueleze ni kitu gani kimetokea
viwanda vya sukari nchini vimeshindwa kutengeneza sukari
ya kutoshereza mahitaji ya hapa nchini?

Unaweza kuta hao hao wenye viwanda
hawatengenezi sukari bali wananunua nje
sukari mbovu kwa mgongo wa wafanya biashara
wa sukari na wanaiingiza kwenye soko kwa kujifanya
wamezalisha wao.
Niliwahi kusoma makala ya wakulima wa miwa
Morogoro wanalalamikia miwa yao kuharibikia shambani
bila wenye kiwanda kuinunua.Nikiunganisha dots
serikali kupiga marufuku uagizwaji wa sukari ili kulinda viwanda
vyetu na mara ghafla sukari inaisha sokoni napata jibu hapa.

Ni Muhimu waziri mwenye dhamani atupatie majibu.
kama hana majibu anamtegemea Mh.rais afanye kila kitu
ni heri atumbuliwa maana atakuwa jipu.

Sishauri viwanda vipewe jukumu la kuagiza sukari
tukifanya hivyo tutalia wakulima wa miwa hawatauza miwa hata kidogo
wenye viwanda wataingiza sukari na kufanya kazi ya packing.
Badala yake wenye viwanda wasio na maelezo ya kutosha
ni kwa nini hwazalishi sukari kutosheleza soko
wasalimishe viwanda hivyo kwa serikali ambaye ndo alikuwa mmiliki
kabla ya viwanda hivyo kubinafsishwa.
 
ishu sio uagizaji, ishu ni kua wanaagiza sukari iliyo expire kwa bei ndogo afu wanauza kwa.bei.kubwa
 
h

uko ni kufikiri kijamaa! kwani hao wenye viwanda siyo wafanyabiashara? ni wafanyabiashara walewale na wote wanataka faida kubwa tu.Kuna mfanyabiashara anataka faida ndogo?
Maana ya ubepari siyo kuharibu mifumo ya masoko....huu ni ufisadi na hata huko kwenye ubepari mambo ya jinsi hii penalties zake ni kubwa.
 
Acha akurupuke kama wale samaki aone atalipa mabilioni mangapi! Sio kila kitu ubabe tu! Kuna busara za kawaida sana zinaweza kutumika
 
Pamoja na hili wazo zuri,mimi nashauri waziri wa viwanda
atoke hadharani atueleze ni kitu gani kimetokea
viwanda vya sukari nchini vimeshindwa kutengeneza sukari
ya kutoshereza mahitaji ya hapa nchini?

Unaweza kuta hao hao wenye viwanda
hawatengenezi sukari bali wananunua nje
sukari mbovu kwa mgongo wa wafanya biashara
wa sukari na wanaiingiza kwenye soko kwa kujifanya
wamezalisha wao.
Niliwahi kusoma makala ya wakulima wa miwa
Morogoro wanalalamikia miwa yao kuharibikia shambani
bila wenye kiwanda kuinunua.Nikiunganisha dots
serikali kupiga marufuku uagizwaji wa sukari ili kulinda viwanda
vyetu na mara ghafla sukari inaisha sokoni napata jibu hapa.

Ni Muhimu waziri mwenye dhamani atupatie majibu.
kama hana majibu anamtegemea Mh.rais afanye kila kitu
ni heri atumbuliwa maana atakuwa jipu.

Sishauri viwanda vipewe jukumu la kuagiza sukari
tukifanya hivyo tutalia wakulima wa miwa hawatauza miwa hata kidogo
wenye viwanda wataingiza sukari na kufanya kazi ya packing.
Badala yake wenye viwanda wasio na maelezo ya kutosha
ni kwa nini hwazalishi sukari kutosheleza soko
wasalimishe viwanda hivyo kwa serikali ambaye ndo alikuwa mmiliki
kabla ya viwanda hivyo kubinafsishwa.

Haswa na ndivyo ilivyo...yaani watu hao hao ndiyo walihusika ama moja kwa moja au indirect kwenye ubinafsishaji, then hao hao wakaingia ubia na hao wawekezaji kwakuwa walikuwa kwenye nafasi nzuri za kufanya hivyo, kisha ndiyo walikuwa waamuzi wa sera zetu za maendeleo na sasa haohao ndiyo wanatuhujumu.....sijui tutafute azimio lingine?

Mbaya zaidi wengi wao ukute ubia wao ni only 1% ofcourse at household level wanapata faida lakini what about 99% ambao wamekuwa replaced kwenye uzalishaji nakubakia kuwa masoko tena kwa bei wanayotupangia na mabeberu.....hii ndiyo kusema ukoloni unafanywa ki science na technology ya kisasa na wanyampara ndiyo hao wenzetu wenye 1% kwenye huo uwekezaji....Mh. Rais tusaidie wala usiogope kama ulivyosema Mungu yupo pamoja na wewe.
 
ishu sio uagizaji, ishu ni kua wanaagiza sukari iliyo expire kwa bei ndogo afu wanauza kwa.bei.kubwa

wewe ni ndezi kabisa! za kuwambiwa changanya na zako! unadanganya kidogo tu basi nawe unajaa upepo kwani tz hakuna mamlaka za kukagua hizo sukari? kama nchi hii ina watu kama nyie sukari utauziwa 1000000 kwa kudanganywa kuwa hii haijaexpire.
 
h

uko ni kufikiri kijamaa! kwani hao wenye viwanda siyo wafanyabiashara? ni wafanyabiashara walewale na wote wanataka faida kubwa tu.Kuna mfanyabiashara anataka faida ndogo?
Ni kweli mkuu,
Ukisoma vizuri nimeshaur vibali vitolewe kwakuratibiwa kwani upungufu wa sukar nchini unafahamika.
Lakini pia lengo ni kupata namna nzur yuku regulate sukar nchini hivyo yeyote anaweza shaur ni namna gani itakua bora ile kuondokana na hii kadhia
 
Serikali inahujumiwa na ili ikomeshe na hii tabia na isije kutohujumiwa tena siku za usoni serikali ikubali kuingia hasara, na ifanye moja kati ya hizi mbili:
1. Serikali inunue sukari kutoka viwandani-mtibwa ama kagera na kuweka kwenye magodauni yake kama inavyofanya kwenye mahindi. Na kama hii haiwezekani basi ifanye option ya pili

2. Serikali, flood the sugar market. Serikali kubalini mpate hasara, mui import sukari kutoka kokote harafu do the-market-flood constantly for six months wakati mtibwa na kagera sugar watakuwa tayari wamejipanga na wapata capacity ya kutosha mahitaji kwa kipindi kijacho baada ya miezi sita.

Serikali iki flood soko la sukari kwa miezi sita, walioficha sukari wataitoa wenyewe tu maana namna nyingine itawaozea na watakuja kuuza kwa bei ya chini sana. Hivyo, siku nyingine mfanyabiashara hatakuja kufanya mchezo wa kuficha bidhaa.
 
Napenda kutoa ushauri wangu wa MWAROBAINI YA SUKARI kama ifuatavyo:-
  • Serikali itangaze tenda kwa wafanyabishara wanaopenda kuleta sukari nchini kutoka nje na waombe.
  • Waonyeshe bei yao ya kuwauzia wauzaji wa jumla pindi sukari itakapofika nchini wakiwa tayari wameweka kodi zote.
  • Wauzaji wa jumla kwa kila Kanda pia waombe kazi hiyo kwa Serikali na wajulikane kwa majina na wapewe bei elekezi.
  • Wauzaji wa jumla kwa kila Mkoa pia waombe kazi hiyo kutoka Serikalini nao wapewe bei elekezi.
  • Wauzaji wa jumla kwa kila Wilaya waombe kazi hiyo kutoka Serikalini nao wapewe bei elekezi.
Utaratibu huu uwe kama ule wa mafuta ambapo waagizaji wanaomba tenda pindi wanapoagiza mafuta na vivyo hivyo iwe kwenye sukari. Kwa utaratibu huu bei ya kilo moja ya sukari inaweza kuwa hata Tshs.1,000. Hebu tujaribu utaratibu huu.

NAWASILISHA
 
Back
Top Bottom