Ushauri: Kafaulu lakini anataka kuolewa

Wewe unamdekeza. Unalea kizungu.

Chapa sana.. peleka shule kinguvu
 
Hahahaha hapana, atakosea zaidi. Aitwe mwanaume awekwe kati aelezwe vizuri, wataelewa tu

Jamaa hapo juu kuna mahali anasema katumia kila mbinu lakini imeshindikana...

Sasa jinsi anavyoendelea kuchelea mwana kulia, siku si nyingi atalia yeye...

Watoto kama hao unatimua kwa kauli mbiu moja, "Ondoka nyumbani kwangu nenda kamtafute baba yako utayemsikiliza"
 
Akiolewa ndoa ikimshinda atarudi kwako na kuwa mzigo kwako so chafuanya ni kumkazania aendelee na shule, full stop
 
Mungu atusaidie aiseeeee
 
Akiolewa ndoa ikimshinda atarudi kwako na kuwa mzigo kwako so chafuanya ni kumkazania aendelee na shule, full stop
Hilo haliwezi tokea ndoa ikimshinda atapambana na hali
 
Fata taratibu za kimila/kidini muozeshe then aombe nafasi chuo aendelee na masomo kama kawaa...

Utakuwa umemsaidia pakubwa..
 
Huyo mwanaume ana umri gani na anafanya mishe gani?!
Mwanaume ana 28, na anajihusisha na biashara. Kuhusu kumtunza sina shaka naye hilo ataliweza vyema..! Ila wasi wasi ni serikali hawawezi kuleta shida kwa kuruhusu binti aliyefaulu kuolewa?
 
Una wakati mgumu kama mzazi pole sana kwa mtihani. kuhusu serikali sidhani kama wanasumbuka na mtu aliyemaliza kidato cha nne akaamua kufuata mlengo mwingine wa maisha. miaka 18 kisheria ni mtu mzima. mshauri yeye pamoja na kijana kwamba aendelee kusoma hata ikibidi kuanza chuo certificate itamsaidia huko mbeleni.
 
Mwanaume ana 28, na anajihusisha na biashara. Kuhusu kumtunza sina shaka naye hilo ataliweza vyema..! Ila wasi wasi ni serikali hawawezi kuleta shida kwa kuruhusu binti aliyefaulu kuolewa?
Binafsi sina jibu la hilo swali, ila humu tuna wataalamu wa kila fani.....hata mimi nasubiri jibu la hilo swali.
Tukirudi kwa binti yako kama ameelekeza moyo wake wote kwenye ndoa, na kama huyo mwanaume ni mtu anayemfaa.....sioni njia nyingine.
Muhimu: ujue sheria ikoje kuhusiana na hilo.
 
Ahsante kwa ushauri wako
 
Wakuu habari za wakati.....!

Unaambiwa kwa mwenzako sikia ila omba yasikukute, Mimi yamenikuta na ni kitu ambacho sikuwaza.....! Iko hivi
Pole sana hapo plan b nikuongea na mkweo.kuwa airishe ndoa kwanza na amuache mwanao asome.tumia hata mkwara kwake utafanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…