Ushauri wangu kwa Basata ni huu kazi za wasanii sio za Tanzania pekee na hamuwezi kukaa vikao bila kuelewa hilo. Usanii ni biashara ambayo serikali inanufaika kwa ubunifu sasa cha ajabu ni watu kuwa katikati na kutaka kuwaeleza wabunifu etu wabuni vipi!. Dhana ya hiki chama ni kusaidia kusiwepo na ubaguzi wa dini, jinsia, ukabila na kukokuwa na matusi. Mambo mengine kama wabunifu wanaimba kwa mafumbo ya kimapenzi au kisiasa waachwe wafanye kazi.
Lakini kikubwa ni kwamba kazi yao sio ya Tanzania pekee na hatuwezi kuwabana kiasi kwamba wasanii wetu washidwe kushindana na wenzao maana wenzao hawana sheria za watu eti kusoma mashairi yao kabla hayajatoka!. Hebu jiulizeni hizi rap za bongo flava na taarabu tofauti yake ni nini wote wanaweka mafumbo kwenye sanaa hizi.
Ukiangalia vizuri muziki wa Nigeria, US, South Africa na Congo hauna BASATA hivyo mkibana wasanii wetu kila siku tutakuwa watu wa kusikiliza miziki ya wenzetu. Tusishangae kwanini wasanii wetu wanaimba kwa lugha za kiingereza siku hizi sababu moja wapo wapo zaidi huru kusema lolote bila kufungiwa au kupigwa faini za kijinga lakini ukiangalia vizuri kama ni matusi kwenye kiingereza ni mara 100 ya kiswahili. Hivyo mnafanya wasanii wetu waanze kukimbia kutumia kiswahili kwenye nyimbo za budget kubwa.
Michael Jackson kwenye nyimbo yake BAD mstari wa kwanza anasema "Your Butt Is Mine" sasa je hii ina maana gani? mbona nyimbo haijafungiwa?