Ushauri: Anataka kuwa na mimi muda wote wakati ameniacha

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 26.

Nilikuwa na mpenzi tuliyedumu naye kwa takribani miaka miwili na miezi kadhaa sasa. Ni wiki iliyopita tu alitoka kuniambia kuwa mimi na yeye mapenzi yetu yameishia hapo. Nikimuuliza kitu gani nilichokosea, anajibu kuwa hakuna kibaya nilichofanya na ataendelea kuwa msaada kwangu muda wowote nitakapomuhitaji.

Kikubwa ni yeye anataka kujenga maisha yake.Binafsi sioni kama kweli kujenga maisha kunaweza kumsababishia yeye kuniacha. Nilikubali kuwa naye kwa hali yoyote aliyokuwa nayo. Sikuwahi kumbugudhi aninunulie chochote cha gharama ama kunipa pesa ya matumizi. Nilijua mfuko wake vema.

Nikakubali aondoke kishingo upande ingawa nilijaribu kuomba msamaha na kuahidi nitajirekebisha pale anapoona nakosea alikataa kata kata kuwa nami.Kitu cha ajabu kinachonishangaza, ni ile tabia yake ya kutaka kuwa nami muda wote pamoja na kuwa ameshaniacha.

Sielewi wana JamiiForum. Sijui ana malengo ya kuumiza moyo wangu tu ama bado ananipenda?
Muda aawote huo hamkuoana, mwache na wewe inawezekana Mwenyezi Mungu anakuepusha kitu kibaya!!
 
Anataka kukuacha ila hataki mtu mwingine akupate ndiyo maana... Ni mbinafsi tu...
 
Back
Top Bottom