Ni kwa njia ya posta mkuu (ingawa sijawahi kuagiza nikiwa Bongo). Halafu kuna wanunuzi wengine wanakupa option ya kuchagua kampuni za kusafirisha vifurisha kama DHL, EMS nk. lakini inabidi ulipie gharama zake amabzo ni kubwa kidogo. Lakini wengi unakuta wanatoa service ya ''free international delivery''. Cha muhimu kabla huja-confirm manunuzi, unaona na kuchagua delivery method na gharama inaonyeshwa. Hakuna longolongo wala ujanja ujanja. Nadhani kuna members wengi wameshaagiza wakiwa Bongo hivyo watakuelewesha watakapochangia huu uzi. Halafu mwisho cheki kama Bongo mizigo huwa inafika salama na mambo ta custom tax yakoje usije kuagiza mzigo ukapotea au wakakutoza kodi kubwa!