Usalama wa manunuzi ya online Amazon na eBay

Kama niliandika post nyingine... everything should be through eBay. Au kama unatumia paypal nayo ni nzuri.
Najau usalama pia upo kote maana pana jamaa juzi alinunua simu toka ebay muuzaji akiwa honkong baafa ya siku moja ikatumwa email ndani ebay kwamba hawezi tuma mzigo tanzania sababu ya matukio ya kupotea kwa vitu ktk posta zetu.. ..so pesa ikarudishwa!!

Nao wanaogopa bad reviews
 
Naitumia sana eBay na sijawahi kukutana na tatizo lolote. Kuna vitu vingi ambavyo bei yake ni nzuri kulinganisha na bei za madukani. Kwa mfano ukienda sehemu kama Ulaya utakuta lile kasha la kuwekea simu kama Iphone 7 ni euro 30 lakini ukiingia eBay unalinunua kwa euro 2 na uasafirishaji ni bure. Kuna vitu vingi sana unavyoweza kununua kwa bei nzuri na ni salama. Ila siku zote nunua through eBay na usikubali kuwasiliana na huyo muuzaji moja kwa moja.
Mkuu naomba unielezee jinsi gani wanakutumia vitu vyako.. Unatumia posta au njia gani?
 
Ni kwa njia ya posta mkuu (ingawa sijawahi kuagiza nikiwa Bongo). Halafu kuna wanunuzi wengine wanakupa option ya kuchagua kampuni za kusafirisha vifurisha kama DHL, EMS nk. lakini inabidi ulipie gharama zake amabzo ni kubwa kidogo. Lakini wengi unakuta wanatoa service ya ''free international delivery''. Cha muhimu kabla huja-confirm manunuzi, unaona na kuchagua delivery method na gharama inaonyeshwa. Hakuna longolongo wala ujanja ujanja. Nadhani kuna members wengi wameshaagiza wakiwa Bongo hivyo watakuelewesha watakapochangia huu uzi. Halafu mwisho cheki kama Bongo mizigo huwa inafika salama na mambo ta custom tax yakoje usije kuagiza mzigo ukapotea au wakakutoza kodi kubwa!
 
Sawa mkuu.. Nafikiri wajuzi wengine watatueleza
 
Back
Top Bottom