benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,186
Je ngao/nembo ya Taifa imebadilishwa?
Ni moja kati ya maswali ambayo yanaulizwa sana na wadau wengi wakitaka kufahamu kuhusu nembo inayoonekana kwenye mimbari (podium) ya Rais wa Jamhuri ya Muungano katika siku za karibuni
Kimsingi ile si ngao ya taifa bali ni alama ya bendera ya Rais au kwa Kingereza inaitwa Presidential Standard.
Bendera ya Rais ni tofauti na Ngao ya Taifa. Ngao ya taifa imeelezwa kwenye Sheria Namba 15 ya bendera ya Taifa na Ngao ya Taifa ya mwaka 1971.
Bendera ya Rais ni mali ya Rais husika ndiyo maana Rais akimaliza muda wake hukabidhiwa bendera hiyo (Rais husika anaweza kuibadili atakavyo bendera hiyo pasina kuhojiwa kwa sababu ni suala la utashi wake).
Ieleweke kwamba, tofauti na Nembo ya Taifa, nembo ya Rais haina Bibi na Bwana, haina Mlima Kilimanjaro, lakini pia haina mazao ya Pamba na Karafuu
Kwa mfano, Marais walioongoza nchi ya Kenya wote wamebadili bendera ya Rais kutoka kwa mtawala wa kwanza mpaka Rais wa sasa William Ruto.
Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta bendera yake ilikuwa na bluu iliyokolea sana (navy blue), ikiwa na ngao, mikuki miwili na jogoo wa njano kwa pembeni.
Alipoingia Rais Daniel Arap Moi alibadili rangi ya bluu iliyokolea na kuweka kijani huku jogoo akiwa wa rangi nyekundu.
Rais Mwai Kibaki yeye bendera yake ilikuwa nyeupe ikiwa na mikuki lakini ikiwa na majani kama ngano yakizunguka ngao.
Alipoingia Rais Uhuru Kenyatta yeye bendera yake ilikuwa na rangi ya bluu iliyokoza kidogo (air force blue) huku pembeni ikiwa na njiwa anaruka.
Rais wa sasa Mhe. William Samoei Ruto yeye bendera yake ina rangi ya chungwa na kitoroli kwa pembeni.
Kwa kawaida bendera za Marais hubeba kauli mbiu za Marais husika kwa wakati husika. Kwa mfano, Rais wa sasa wa Kenya bendera yake ina kitoroli kwa kuhanikiza ile kauli mbiu yake ya Hustler.
Bahati nzuri kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marais wote wamekuwa wakiheshimu bendera ya Rais wa kwanza Hayati Julius Kambarage Nyerere mpaka sasa hivyo haina mabadiliko kama ilivyo kwa Kenya.
Kwa upande wa Zanzibar, mimbari ya Rais huwa na nembo ya bendera ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ikiwa na visiwa vya Unguja na Pemba na herufu kubwa 'R' ikimaanisha Rais.
Asili ya bendera ya Rais ilianza zamani wakati wa enzi za kabla ya Vita vya Westphalia ambapo wafalme walikuwa wakienda kwenye vita au safari mbalimbali wakiwa wamebeba bendera zao.
Kwa wale wanaotazama filamu ya Ottoman wanaweza kuona namna viongozi walivyokuwa wakitembea na bendera zao.
Baada ya Vita vya Westphalia mwaka 1648 na kuzaliwa kwa aina ya nchi tulizonazo sasa, utaratibu wa bendera ya Mfalme ulirithiwa kwa marais ambapo bendera hizo huwekwa Ikulu au sehemu yoyote ambapo Rais yupo.
Bendera ya Rais huweza kuwekwa Ikulu, kwenye gari au pahala atakapofika kwa tukio.
Bendera hiyo huwa haishushwi pindi nchi ikiwa kwenye vita au ikiwa kuna janga kubwa ambalo litamkutanisha Rais na Kamati ya Usalama ya Taifa hata kama ikiwa saa nane usiku.
Mnaweza kufuatilia vema matangazo ya Ikulu Mawasiliano au Ikulu habari Zanzibar kuona uhalisia wa hayo niliyoainisha hapo juu.
Sehemu kubwa ya andiko hili imetokana na andiko la Ndugu Abbas Mwalimu
Tazama meza ndogo
Tazama meza
Tazama Kiti alichoketi Mhe Rais