Serikali ifikirie juu ya usafiri kwa wanafunzi wa shule za serikali ili kutatua changamoto wanayopata wanafunzi katika miji mikubwa.
Wanafunzi wamekuwa wakikaa katika vituo hadi saa tatu usiku jambo ambalo ni hatarishi kwa wanafunzi hao.
Serikali itenge bajeti ya kununua mabasi ya shule katika miji mikubwa kama vile Dar es salaam, Arusha, Mwanza n.k ambayo yatatumika kubeba wanafunzi hao kwa utaratibu maalumu na kuwasambaza katika shule zao na kuwarudisha jioni katika vituo elekezi.
Hii itasaidia wanafunzi ambao shule ziko mbali na makazi yao. Serikali ifanye uchunguzi zaidi kuhusu jambo hili.