mamitod
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 914
- 385
Msengerema ni msengerema tu ht iweje. Acha kupindisha maneno ili kupotosha watu
Kwa Mujibu wa waziri Mwakyembe
Vita ya madawa ya kulevya ni ngumu sana
Kuna kijana anaitwa NJINGU huyu alikuwa pale Airport Dar kitengo cha usalama ndiye aliyemsaidia Mwakyembe kukamata madawa ya kulevya pale uwanjani
Huyu kijana baada ya kujulikana kuwa yeye ndio mfanya mipango ya kukamata madawa, wauza madawa na mitandao yao wakamtega NJINGU na akategeka. Leo hii yupo gerezani hata Mwakyembe alishindwa kumtoa huyu kijana kwa sababu kila alichokuwa anafanya kinashindikana kutokana na nguvu kubwa ya pesa na mtandao mkubwa wa wauza madawa
Huwezi kupingana na hii vita iwe hadharani au kimya kimya alafu ukapona hilo haliwezekani. Yupo wapi Amina chifupa? Baada ya kusema tu kuwa atawataja hadharani wauza ngada kila mtu alijua kilichomtokea Amina
Leo hii lazima watanzania wenye mapenzi ya dhati na nchi yetu tujiulize sana kuhusu mambo yanayotokea baada ya makonda kuthubutu kupambana na hii biashara haramu duniani
Tumeona ushirikiano mkubwa sana kati ya vituo vya habari vyenye upinzani mkubwa sana hapa Tanzania ambapo siku za nyuma walikuwa wanatupiana maneno ya vijembe kupitia watangazaji wao
Efm wameitupia sana vijembe clouds pamoja na kuwachukua watangazi wake kwa kigezo cha kusema kule kuna unyonyaji
Clouds imetupiwa sana lawama kuwa inawanyonya wasanii kwenye show na sababu kubwa ya wasanii kutumia madawa ni unyonyaji unaofanywa wa kazi zao na clouds, Haya maneno yapo mitaani siku nyingi tu yanasemwa
Kwa mara ya kwanza namuona mzee Mengi anakwenda clouds media, Hakuna asiyejua kuwa vituo vya mzee huyu vina ugomvi mkubwa sana hasa katika malipo ya wasanii sasa leo hii tunajiuliza urafiki huu umetoka wapi?. Hivi kosa ni Rc kwenda na walinzi wake kuchukua flash yake? Hakuna asiyejua kuwa Makonda ameongezewa ulinzi mkubwa sana baada ya hii vita yake sasa mtu kwenda na walinzi wake ni kosa?
Urafiki wa clouds na efm umeanza lini? Kwanini efm wanamshambulia sana makonda? Na kwanini wamshambulie baada ya boss wao kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.? Mara ngapi Mange kimambi anamtaja wazi wazi Majizo mmiliki wa efm kuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa madawa? Mbona efm hawajawahi kumsema mange kama wanavyomsema Rc.? Au kwa kuwa mange kimambi mpo nae timu moja kwa sasa? Nadhani sasa ule msemo umekamilika sasa kwa ushirikiano unaofanyika sasa, ENEMY OF YOUR ENEMY IS YOUR FRIEND
Hii vita ni kubwa sana na kamwe mkuu wa nchi hawezi kuingia kwenye huo mtego wenu maana haiwezekani wapinzani wako wakupangie majukumu tena ya uteuzi, Kawaida kizuri chochote huwa kinapigwa vita tumeona vingi sana uko nyuma vikipigwa vita. Alichofanyiwa Prof Muhongo kwenye serikali iliyopita hakuna asiyekumbuka, Msimamo wake wa kitaalamu kuhusu vibali vya vitalu vya mafuta ulileta ugomvi mkubwa sana kati yake yeye na wawekezaji wazawa ambao hawakuwa na uwezo wa kumiliki vitalu vya mafuta. Uwekezaji katika mafuta unaitaji mtaji mkubwa sana na dunia nzima kuna makampuni saba tu yanayojihusisha na uchimbaji wa mafuta na hakuna hata moja kutoka Afrika
Kulitokea ugomvi mkubwa sana kati yake na wale wafanyabiashara na wote tunawajua na mmoja wao jana alienda clouds kuwapa pole
Wafanyabiashara hao wakahakikisha kuwa huyu Prof Muhongo habaki serikalini kwa kupitia wanasiasa wetu wanaojari matumbo yao binafsi kwenye saga la escrow walifanikiwa kumtoa huyu mzee na wakafanya sherehe kubwa sana
Nani asiyejua kuwa swala la escrow lilisukwa mahususi ili Prof atoke hapo?
Waulizeni watetezi wenu kati ya makampuni yote yanayozalisha umeme hapa Tanzania ni kampuni ipi ina capacity charges ndogo?Kwanini kampuni zenye capacity charges kubwa hawazisemi? Fedha walizokula za standard chartered na za wale wafanyabiashara zitawatesa sana
Urafiki wa Nape na vituo vya habari umeanza lini?. Huyu huyu Nape aliyezuia matangazo live ya bunge.? Huyu huyu Nape aliyetetea mswada wa habari?
Kwanini wamiliki wa vyombo vya habari hawakuungana kama sasa hivi siku Nape anazuia matangazo live ya bunge.?
Kwa nini hawakuungana kipindi Nape anapeleka muswada wa habari bungeni?
Kwanini hawakuungana kipindi sheria ya mitandao ya kijamii inapitishwa bungeni?
Wabunge wetu wa vyama vya upinzani wameungana kwa sababu ya kumtoa Makonda hapo Dar lakini hawa hawa wameshindwa kuungana kuhakikisha Ben saanane anapatikana na walishindwa kuungana kipindi cha ule msemo wa gori la mkono, ni lazima kwa pamoja tuwe na ukakasi katika akili zetu
Watanzania wanaungana kwenye mambo yasiokuwa na economic impact kabisa na wanaacha kuungana kwa mambo yenye tija kwa taifa
Vijana mmeshindwa kuungana kuhusu wanachuo kukosa mikopo, mnashindwa kuungana kwenye maswala ya ongezeko la makato mmekuja kuungana kwenye vita ya kumtoa Makonda dar inayoratibiwa na wauza madawa ya kulevya
Rafa lukindo
0765499321