Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,618
- Thread starter
- #21
Nimekuwa nikiweka mafuta mara nyingi sana kwenye hiko kituo cha mafuta kilichopo njia ya Kutoka Mbezi kuelekea Goba, kwa kipindi cha nyuma sikuwahi kuona tatizo.
Kama wiki 2 zimepita niliweka mafuta asubuhi ya sh 10,000/- ambayo kwa kawaida ninaendesha kama 50 km kama hakuna foleni, bahati mbaya sana gari ilizima baada ya kama km 29. Nikajua labda hesabu zangu siyo.
Sasa nielewe kuwa hili limeanza kama wiki mbili tatu hadi sasa.
Kwa mfano niliweka mafuta vituo tofauti katika kata ninayoishi nikagundua ni kama wameambizana kupunguza ujanzo.
Mkuu ukinisoma juu pale kwenye thread nimeandika kwamba tatizo limejitokeza ndani ya wiki 2 hizi, kwa kweli sikuwahi kuona tatizo siku za nyuma.